Utangulizi
- Ukurasa wa Jalada
- Utangulizi kwa Historia ya Kanisa
- Ufafanuzi wa Historia ya Kanisa
- Kwanini tujifunze Historia ya kanisa?
- Utunzaji wa Kimungu
- Vipindi saba vya historia ya kanisa
Ukurasa wa Jalada
Utangulizi kwa Historia ya Kanisa
Somo hili litamwezesha mwana funzi kuifahamu vizuri historia ya kanisa. Zipo tarehe zitakazotolewa kuhusu matukio ya Historia ya Kanisa. Hutalazimika kukariri matukio wala tarehe nyingi. Lengo la somo hili ni kumpatia mwanafunzi uelewa wa matukio yaliyojiri katika kipindi kizima cha Historia ya Kanisa. Kanisa la Yesu Kristo liko hai. Tutajifunza kuhusu maisha ya baadhi ya watu waliotumiwa na Mungu kama nguzo kuu katika Kanisa.
Ufafanuzi wa Historia ya Kanisa
Ufafanuzi wa Historia ya Kanisa
Kanisa
Neno la Kigiriki la kanisa ni ekklesia lenye maana "wale walioitwa pamoja au wale walioitwa mbele."
Darasa hili litasoma kuhusu kanisa la Yesu Kristo. Neno kanisa kama linavyotumika siku hizi humaanisha majengo ambamo watakatifu walikusanyika ndani yake kwa ajili ya kuabudu lakini nisahihi zaidi kuhusisha watu. Maandiko hutumia neno kanisa kumaanisha kusanyiko katika nyumba mahali au mji fulani (Warumi 16:5; 1 Kor. 16:19; Kol. 4:15). Kanisa ni zaidi ya nyumba au jengo ila ni watakatifu ambao ndio mwili wa Kristo.
Bwana akalizidisha kanisa
Matendo 2:47…Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa walewaliokuwa wakiokolewa.
Baada ya kupata ubatizo mkuu wa Roho Mtakatifu katika chumbacha ghorofani, wanafunzi wake walikuwa na ushawishi mkubwa katika kumshuhudia Kristo. Siku ile roho 3,000 ziliokolewa na kuongezwa katika kusanyiko la mahalipale. Kila siku wengi zaidi walizidi kuongezwa!
Kuna kanisa moja tu la Mungu, na Mungu peke yake anaweza kuongeza wanachama kwa hilo. Wanadamu wana mashirika ya kidini na wanaweza kudhibiti wanachama wao, lakini hakuna mwanadamu anayeweza kusema nani au si mwanachama wa kanisa la Mungu.
Yesu ni kichwa cha kanisa
Waefeso 1:22–23—akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo ndilo mwili wake…
Kanisa katika andiko hili linaelezwa kama mwili wa Kristo. Yesu ni kichwa cha Mwili wake. Katika hali ya kawaida kichwa huuagiza mwili kufanya mambo inayotakiwa na kazi nyinginezo. Katika mwili wa Kristo, Yesu ni Kamanda anayeamrisha Kanisa lake kufanya kazi ya Mungu.
Kanisa lilizaliwa na Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste. Darasa hili litajumlisha somo la kanisa la mwanzo la Matendo hadi Kanisa letu la kipindi hiki cha sasa.
Historia
Neno hili historia linatokana na neno "linalomaanisha kujifunza kwa kufanya uchunguzi."
Kamusi ya Webster inafafanua historia kama "lile tawi la elimu linalohusu matukio fulani katika hii dunia yetu. Somo au uchunguzi wa mambo ya wakati uliokwishapita."
Mwandishi mmoja alisema kwamba "Zamani ni nchi ya kigeni: wanafanya mambo tofauti huko." [1]
Ukristo
Tunajifunza historia ya kanisa la Kikristo. Neno Mkristo lina maana "ya kuwa kama Kristo au mmoja wa Wafuasi" wa Kristo ambapo lilitumika kwa mara ya kwanza huko Antiokia kwenye mwaka wa 40 BK (Matendo 11:26).
Kuzaliwa, maisha, kifo, na ufufuko wake Kristo ndio kiini cha historia ya dunia. Historia imeandikwa kumzunguka Kristo; tarehe huandikwa katika KK (Kabla ya Kristo) na BK (Baada ya Kristo). Historia yote imemweka Kristo katikati yake.
[1] L. P. Hartley, The Go-Between (1953)
Kwanini tujifunze Historia ya kanisa?
Kwanini tujifunze Historia ya kanisa?
Historia ya Kanisa inatusaidia kuelewa kile tunachoamini
Ukiingia kanisa la Kiprotestanti popote ulimwenguni, utasalimiwa na huduma inayofanana na nyingine yeyote uliyowahi kuhudhuria. Kutakuwa na tofauti za mtindo, lakini utatarajia sala ya ufunguzi, wakati wa kuimba, sadaka, na kuhubiri Mara nyingi hizi zitakuwa katika utaratibu sawa. Hakuna mahali popote katika Biblia hutolewa orodha ya jinsi ya kuongoza huduma ya kanisa, sasa imekuwaje wote tumekuwa na mfumo sawa?
Ni kwa sababu mengi ya yale tunayofanya na kuamini kama Wakristo yameumbwa na zaidi ya miaka elfu mbili ya mila, ingawa mara nyingi hatujagundua. Mila mara nyingi huonekana kuwa jambo baya katika makanisa ya Kiprotestanti. Tunapenda kuamini tunafanya mambo sawasawa na Paulo na mitume wengine walifanya katika Agano Jipya, lakini hakuna mahali pa Biblia tunaona kwamba Paulo alikuwa amevaa suti na tai siku ya Jumapili (kwa kweli, Jumapili kufanywa kama siku rasmi kwa wakristo kuabudu imetokana na mila na sio katika Biblia).
Mila ya kanisa inaweza kuwa jambo jema. Watu wengi wamejifunza Biblia, kuomba, na kujadili mafundisho na mawazo mengi kuhusu jinsi kanisa linapaswa kuishi. Hatupaswi "kurejesha gurudumu," na kujifunza masomo haya yote, lakini tunaweza kujifunza kutokana na kile ambacho watu hawa wamepitisha kwa njia ya mila. Hatuamini kwamba mila ni bora zaidi kuliko Maandiko, lakini tunaamini kwamba mila hutusaidia kuelewa Biblia.
Tukisoma historia ya kanisa, tutaelewa mengi kuhusu namna hii mila ilivyoingia. Tujifunze historia au la, tutaathiriwa na historia. Ushawishi utatoka kwenye utamaduni unaotuzunguka sisi, hitimisho tunayofikiria kwa siri, na hadithi ambazo tulisimuliwa. Hatari ni kwamba bila kujifunza kwa ufahamu wa jinsi tulivyokuwa, tunaweza kufikia hitimisho baya.
Kuijenga Imani yetu
Somo la historia ya kanisa linatuwezesha kuutambua urithi wetu. Wanaume wengi na wanawake walikwishajitoa mhanga maisha yao katika jitihada zaokueneza ujumbe wa neno la Mungu. Neno la Mungu limehubiriwa katika mazingira magumu sana na wakati mwingine yanayoogopesha.
Jifunze kuhusu uamsho wa ajabu uliofanyika katika Kanisa
Uwepo wa nguvu za Mungu umeonekana waziwazi katika historia yote ya Kanisa. Ni Roho Mtakatifu aliyewezesha uamsho ule uliopita na ndiye yeye anayefanya mambo yatendeke vizuri leo.
Unaweza kuuona mkono wa Mungu ukiwa juu ya Kanisa lake kila wakati
Historia hujirudiarudia
Mwandishi wa Mhubiri alisema "wala jambo jipya hakuna chini ya jua" (Mhubiri 1:9). Historia huja kwa mizunguko. Kwakuyasoma matukio yaliyokwishapita tunaweza kuelewa vizuri mambo yanayotokeahivi sasa. Tunaweza kujifunza kutokana na makosa yaliyofanywa na watu wengine. Mungu hachambui watu kwa ajili ya kuwaheshimu. Kila kitu alichokitendea kizazi kilichopita anaweza pia akatufanyia sisi iwapo tutamtii kama kizazi hicho cha zamani.
Warumi 2:11—Kwa maana kwa Mungu hakuna upendeleo.
Tunaweza kujifunza kutokana na mafanikio na makosa ya wale ambao wameishi mbele yetu.
Mungu habadili
Mungu huwataka watu wake watende kazi kwa usawa katika vipindi vyote. Mungu alivyowafanyia watu wa kale ni hivyo hivyo atawatendea watu wake leo. Mungu anataka watu waishi maisha matakatifu na hatabadilisha msimamo wake kabisa.
Mungu huwatumia wanadamu wa kawaida kufanya kazi zake
Mungu yule aliyewatumia akina Petro, Yakobo, na Yohane ni huyo atakayekutumia pia wewe. Mungu katika utendaji wake huwatumia watu wa kawaida tu kama wewe au mimi.
Uneemeshaji wa elimu ya mchungaji
Mchungaji wa Injili anapaswa asiwe mjinga, awe mjuzi kwa utajiri wa historia ya kanisa.
Utunzaji wa Kimungu
Divine providence. How does God interact with humans? Does He manipulate the course of history? Do men have a choice in what they do? If God controls everything, why is there evil in the world?
- God hardened Pharoah's heart.
- He removes kings and sets up kings
- He moved David to number Israel (2 Sam. 24:1)
- He hates lying (Prov. 12:22), but sends a lying spirit to Ahab (1 Kings 22:23; 2 Chron. 18:21–22)
BUT
- Men have choice
- Choose you this day...
- If any man believe...
Vipindi saba vya historia ya kanisa
Vipindi saba vya historia ya kanisa
KANISA LA KITUME
MWANZO: Tangu siku ya Pentekoste (30 BK)
MWISHO: Hadi kukamilishwa kwa Agano Jipya kwenye (100 BK)
KANISA LA MATESO
MWANZO: Kuanzia kukamilishwa Agano Jipya kwenye (100 BK)
MWISHO: Hadi kutolewakwa Hati ya Konstantino (313 BK)
Hiki ni kipindi cha mateso makuu kwa kanisa. Kanisa liligandamizwa mno chini ya Ufalme wa Kirumi.
KANISA LA KIFALME
MWANZO: Kuanzia kutolewa kwa Hati ya Konstantino (313 BK)
MWISHO: Hadi anguko la Roma (476 BK)
Neno la Ufalme linahusiana na mfalme au mtawala. Hiki ni kipindi ambacho mfalme alikuwa na ushawishi mkubwa sana ndani ya kanisa.
KANISA LA ZAMA ENZI ZA KATI
MWANZO: Tangu anguko la Roma (476 BK)
MWISHO: Hadi anguko la Konstatinopo (1453 BK)
Wakati huu kanisa Katoliki lilikuwa na mamlaka makubwa katika bara la Ulaya.
KANISA LILILOTENGENEZWA
MWANZO: Tangu anguko la Konstantinipo (1453 BK)
MWISHO: Hadi mwisho wa vita vya miaka 30 (1678 BK)
Huu ni wakati ambao Mungu aliwatumia watu kama Martin Luther kusimamia nakupigana na wimbi la ukatoliki na walihubiri kwamba wenye haki wataishi kwa imani yao. Mungu aliamsha wanaume katika eneo lote la Ulaya ili walirudishe Neno la Mungu kanisani.
KANISA LA KISASA
MWANZO: Kuanzia mwisho wa vita ya miaka 30 (1678 BK)
MWISHO: Hadi katika karne ya ishirini (Miaka ya 1950 BK)
Hiki ni kipindi cha uamsho wa hali ya juu na umisionari ulienea sehemu nyingi. Hadi kufikia kipindi hiki kulikuwa hakuna jitihada mahususi zilizofanyika za kuieneza Injili duniani kote. Wakati huu ndio David Livingstone alianzisha vituo vingi vya umisionari katika bara la Afrika.
KANISA LA BAADA YA KISASA
MWANZO: Kwanzia karne ya ishirini (Miaka ya 1950 BK)
MWISHO: Hadi siku yaleo
Tutasoma kila kipindi katika vipindi hivi 7 peke yake. Sura hii ilikuwa ni muhtasari tu wamafunzo yatakayo fundishwa.