Sura ya 3: Uvuvio wa Biblia

Ufafanuzi kuhusu uvuvio wa Biblia

1. Uvuvio maana yake ni nini?

  • Kamusi ya Webster inafafanua uvuvio kama: kitendo chochote cha kupumlia.
  • Neno Uvuvio linatokana na Neno la kiingereza inspiration ambalo kwa kilatini ni in spiro maana yake ‘pumulia ndani’.
  • Neno hilo kwa maana yake halisi enye pumzi ya Mungu.
  • 2 Tim. 3:16— Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, la faa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadabisha katika haki.

    Maneno katika taarifa ya kuwa na pumzi ya Mungu ni tafsiri kutoka katika neno moja la Kiyunani: theopneustos, ambalo limetolewa katika neno  Theos  - Mungu na  pneuma – Roho Mtakatifu.  Pneuma limetolewa kutoka neno lenye maana ya pumzi. Tafsiri halisi ya maneno haya (iliyotolewa kwa pumzi ya Mungu) ni: ILIYO PUMULIWA NA MUNGU  

     

     

    II Petro 1:21—Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

     

    Unabii katika maandiko haya yanahusiana na aya ya 20 inayosema: Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Aya hizi zinahusu unabii ulioko katika Maandiko. Maandiko hayakuletwa kwetu na mwanadamu.  Wale wanadamu walisukumwa na Roho Mtakatifu. Kitendo hiki Kitukufu cha Mungu.  

    Je tumeshapata Neno lenye pumzi ya Mungu? Ndiyo, tumeshapata! Haitoshi kujibu ndiyo peke yake swali kama hili, kila muamini anapaswa kufahamu bila shaka yeyote kwamba Biblia siyo kitu kingine zaidi ya pumzi ya Mwenyezi Mungu.

    2. Mawazo Potofu kuhusu Uvuvio wa Biblia

    Biblia ilipatikana kwa uvuvio wa asili.

    Wazo hili la uwongo hushikilia kwamba Biblia ni tunda la mtu mmoja mwerevu wa hali ya juu, ila siyo mwenye nguvu za ajabu au za Utukufu. Hii ni aina ya msukumo ambao umeoneshwa katika maandishi ya Milton, Shakespeare au Confusius. Hakuna binadamu mwenye kipaji hata kiwe cha namna gani, ambaye akisoma alichoandika Shakespeare kisha akaisoma Biblia atashindwa kuona tofauti kati ya mambo haya mawili kuwa ni kubwa sana. Kitabu kinaweza kuwa na uvuvio bila kuwa na pumzi. Biblia inavipita kwa mbali vitabu vya wanadamu.

    Mungu alitumia ngazi mbalimbali za msukumo kutupatia Biblia.

    Wazo hili la uongo hudai kwamba Mungu alitumia ngazi mbalimbali za udhibiti kwa vipindi tofauti katika mchakato wa msukumo. Wazo hili linatetewa zaidi kwamba Mungu alitumia utukufu wake na wakati mwingine, alitoa tu mapendekezo au alianzisha jambo kwa maagizo. Hii ni kinyume kabisa na msukumo wa kweli wa Biblia.

    Mungu alitoa pendekezo au maoni kwa wanadamu ambao waliiandika Biblia.

    Wale wanaoshabikia wazo hili la uongo wanasema kwamba mapendekezo au mawazo hayo yalipewa uvuvio. Msimamo huu unawapa wanadamu nafasi ya kutumia maneno yao katika taarifa hizo kutoka akili mwao. Hii ni kinyume na maana halisi ya uvuvio wa kweli wa Biblia.

    Sehemu chache tu za Biblia zimepumuliwa.

    Haya ni mafundisho ya uongo ambayo ni hatari kuzungumzia sehemu tu kuwa na pumzi. Msimamo huu unatamka kwamba Biblia inalo Neno la Mungu lakini siyo maandiko yote yamepumuliwa. Ni nani basi wa kuamua nini ndiyo na kipi hakijapumuliwa? Nadharia ya namna hiyo inamuacha mwanadamu katika hali tata na hatari ya kutokuwa na uhakika.

    3. Matangazo ya Uvuvio wa kiBiblia

     

     

    II Tim. 3:16—Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu ……

     

    Wazo kwamba Biblia katika ukamilifu wake inayo pumzi ya Mungu huitwa uvuvio kwa mamlaka. Mamlaka maana yake kamili au timia. Biblia kamili huanzia mwanzo mpaka ufunuo ni Neno la Mungu lenye uvuvio. Maandiko yote yamepumliwa sawasawa.

    Kwa kuwa imepumuliwa na Mungu Biblia haiwezi kuwa na kosa. Haiwezi kuwa na kosa maana yake imetenganishwa kabisa na uwezekano wa kukosewa. Maneno hayo huhusishwa na Mungu ambaye hawezi kufanya kosa au kughafilika. Katika matumizi yake kuihusu Biblia kutokuwa na kosa kunahusu Utukufu wa Mwandishi wa Maandiko. Muandishi huyu Mtukufu hafanyi makosa na kwa hiyo Neno lake haliwezi kuwa na kosa.

     

    Mara kwa mara tena tunaweza kupata maelezo yafuatayo katika Agano la Kale:

     

    “Neno la Bwana”         “Mungu akaamuru” “Mungu akasema /akaonge

    “Bwana akasema”   “Mungu akatokea”    “Asema Bwana”

     

    Maelezo kama haya yanadhibitisha uvuvio wa Agano la Kale. Uthibitisho wa madai haya uko wazi kutokana na umakini wa kila neno la taarifa na majina, nyakati na mahali ambako watendaji walikamilisha ujumbe wao na, ukamilifu wa kutimia kwa unabii wao.

     

    Matendo 28:25—Na walipokuwa hawapatani wao kwa wao, wakaenda zao, Paulo alipokwisha kusema neno hili moja, ya kwamba, Roho Mtakatifu alinena vyema na baba zetu, kwa kinywa cha nabii Isaya,

     

    2 Petro 1:21—Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

     

    Waebrania 1:1—Mungu ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi.

     

    Kumb.18:18-22—v. 22 Atakaponena nabii kwa jina la Bwana, lisifuate jambo lile wala kutimia hilo ndilo neno asilonena Bwana; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimuogope.

     

    Waandishi wa Agano Jipya wanadai kuwa uvuvio kwa waandishi wa Agano la Kale  unawahusu wao pia:

    Matendo 1:16—…ilipasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daudi kwa habari za Yuda aliyewaongoza wao waliomkamata Yesu....,

    Maandiko yanatamka kwamba watu watakatifu wa Mungu waliongea kama walivyosukumwa na Roho Mtakatifu. – 2 Petro 1:Mungu aliwavuvia Neno lake watu ambao walikuwa ni vyombo vya kibinadamu kuandika Biblia. Kauli za Manabii kutoka kwa Mungu zilitumiwa na Mungu kuwasiliana na watu Wake. Bwana aliwaagiza wengi wa watu hao kuandika Maneno Yake. Watu hao walivuviwa na kuagizwa na Mungu kuwapatia watu wake Neno lake.

     

    E. Yale Maneno Yalivuviwa

     

    Yuda 17—Bali ninyi, wapenzi, yakumbukeni maneno yaliyonenwa zamani na mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo;

    2 Petro 3:2—Mpate kuyakumbuka yale maneno yaliyonenwa zamani na manabii watakatifu, na ile amri ya Bwana na Mokozi iliyoletwa na mitume wenu.

    Yohana 12:48—Yeye anikataaye mimi,asiye yakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.

     

    Zile herufi za maneno ya Biblia zimevuviwa kwa Utukufu wa Mungu. Kwa mfano, hebu tuangalie mafundisho ya “punje moja na siyo nyingi” kwa njia ya Kristo ambao ilidhibitishwa kwa matumizi ya herufi: ‘u.’

     

    Wagalatia 3:16—Basi ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu kwa mzao wake. Hasemi, kwa wazao kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni  mmoja, Kwa mzao wako, yaani, Kristo. (linganisha na Mwanzo. 22:16-18)

     

    Herufi ‘u’ katika aya hii inaweka tofauti KUBWA.  Herufi ‘u’ inaweka tofauti kati ya umoja na wingi na muhimu zaidi tofauti ya kutamka kwamba kuna msuluhishi mmoja au kutamka kwamba wapo wasuluhishi wengi. Iwapo Mungu angesema wazao’ badala ya uzao’ ahadi hizo zingeweza kutolewa kupitia Confucius, Buddha, Mohammed, Papa au mwingine yeyote ambaye amechagua kujitwalia umaarufu huu. Kwa kutumia umoja, Mungu ameufunga mlango kwa manabii wa uongo na kumnyanyua Kristo kama njia PEKEE ya kwenda kwa Mungu. Punje ya Ahadi inaweza kuwa Kristo tu, na siyo Kristo na Buddha au Kristo na Muhammed. Yesu Kristo peke yake alikuwa ndiye punje ya ahadi.

     

    Mathayo 5:18—Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka Mbingu na Nchi zitakapoondoka yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.

     

    Yodi inaweza kulinganishwa na apostrofi (‘) na nukta kulinganishwa na kistari ungio (-).

     

    “Biblia siyo kitu kingine isipokuwa ni sauti Yake yule akaaye katika kiti cha enzi. Kila kitabu chake, kila mlango, kila aya, kila neno, kila silabi, kila herufi, ni tamshi lake Yule Aliye Juu ya Yote.”—Dan Burgon

     

     

     

     

     

    II Kor. 5:17—Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.

    Jedwali lifuatalo ni orodha ya watu wa Mungu ambao waligeuka kupitia sehemu mbalimbali za maandiko. Maandiko haya yalikuwa na matokeo katika maisha ya watu hawa wa Mungu.

    John Calvin

    Isaya 53:5

    C.H. Spurgeon

    Isaya 45:22

    Henry Moorhouse

    Mathayo 1:21

    John Williams

    Marko 8:36

    Sir James Simpson

    Yohana 3:14,15

    W.P. Lockhart

    Yohana 19:30

    David Livingston

    Matendo 16:31

    William Cowper

    Warumi 3:25

    Sir  George Williams

    I Wakorinto 15:1-4

    Martin Luther

    Wagalatia 3:11

    Lord Shaftesbury

    I Petro 3:18

    Hedley Vicars

    I Yohana 1:7

    James Chalmers

    Ufunuo 22:17

    Robert Moffat

    Yohana 3:16

    Duncan Mathieson

    Yohana 3:16

    Richard Weaver

    Yohana 3:16

    Hakuna yeyote aliyewahi kusikia mtu aliyefanywa “kiumbe kipya” kupitia Homer, Shakespeare, Scott, Dickens, Macauley, Huxley, Carlyle, Eliot, Kipling, Wells, au mtu mwingine yeyote? Mamilioni ya watu wamefanywa wapya kwa kusoma na kuiamini Biblia ambayo ni Neno la Mungu.

     

    Biblia huzalisha ukuaji wa Kiroho katika maisha ya Watakatifu wa Mungu. Biblia ni chakula cha roho ya Mkristo na inapaswa kusomwa kila siku ili kupata nguvu na kukua Kikristo.

    Yeremia 15:16—Maneno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ya furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu maana nimeitwa kwa jina lako, Ee BWANA, Mungu wa Majeshi.

    1 Petro 2:2—Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa,ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu:

    Biblia inaweza kuyasafisha maisha ya wanaume na wanawake. Roho Mtakatifu atawahukumu wanadamu kwa Neno. Biblia itaonesha wanadamu kitu kinachopaswa kubadilishwa katika maisha yao. Maji yaliyopo katika Hema ya kukutania ni alama ya Neno la Mungu. Makuhani walipaswa kunawa katika maji hayo kila wakati waendapo kufanya ibada ya Bwana.

    Yohana 15:3—Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu lile neno nililowaambia. (Eph. 5:26)

    Zaburi 119:9—Jinsi kijana aisafisha njia yake? Kwa kutii akilifuata Neno lako.

     

    Kunakuwepo na nguvu na kuwa na moyo katika neno la Mungu. Neno la Mungu litakujenga na kukuweka imara katika wakati mgumu. Wakristo wanaweza kusimama katika mwamba huu imara.

    Warumi 16:25—Sasa na atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara sawasawa na Injili yangu…

    Waefeso 2:20 -22—Mmejengwa  juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe Hekalu Takatifu katika Bwana. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.


    Revision #7
    Created 7 September 2022 15:39:22 by Stephen Reynolds Jr
    Updated 7 September 2022 17:12:00 by Stephen Reynolds Jr