Skip to main content

Archived Swahili Textbook

romans-en

Mwaka la Kwanza

Vitabu vya Kiada

Historia Ya Kanisa

Utangulizi kwa Historia ya Kanisa

Somo hili litamwezesha mwana funzi kuifahamu vizuri historia ya kanisa. Zipo tarehe zitakazotolewa kuhusu matukio ya Historia ya Kanisa. Hutalazimika kukariri matukio wala tarehe nyingi. Lengo la somo hili ni kumpatia mwanafunzi uelewa wa matukio yaliyojiri katika kipindi kizima cha Historia ya Kanisa. Kanisa la Yesu Kristo liko hai. Tutajifunza kuhusu maisha ya baadhi ya watu waliotumiwa na Mungu kama nguzo kuu katika Kanisa.

Ufafanuzi wa Historia ya Kanisa

Kanisa

Neno la Kigiriki la kanisa ni ekklesia lenye maana "wale walioitwa pamoja au wale walioitwa mbele."

Darasa hili litasoma kuhusu kanisa la Yesu Kristo. Neno kanisa kama linavyotumika siku hizi humaanisha majengo ambamo watakatifu walikusanyika ndani yake kwa ajili ya kuabudu lakini nisahihi zaidi kuhusisha watu. Maandiko hutumia neno kanisa kumaanisha kusanyiko katika nyumba mahali au mji fulani (Warumi 16:5; 1 Kor. 16:19; Kol. 4:15). Kanisa ni zaidi ya nyumba au jengo ila ni watakatifu ambao ndio mwili wa Kristo.

Bwana akalizidisha kanisa

Matendo 2:47…Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa walewaliokuwa wakiokolewa.

Baada ya kupata ubatizo mkuu wa Roho Mtakatifu katika chumbacha ghorofani, wanafunzi wake walikuwa na ushawishi mkubwa katika kumshuhudia Kristo. Siku ile roho 3,000 ziliokolewa na kuongezwa katika kusanyiko la mahalipale. Kila siku wengi zaidi walizidi kuongezwa!

Kuna kanisa moja tu la Mungu, na Mungu peke yake anaweza kuongeza wanachama kwa hilo. Wanadamu wana mashirika ya kidini na wanaweza kudhibiti wanachama wao, lakini hakuna mwanadamu anayeweza kusema nani au si mwanachama wa kanisa la Mungu.

Yesu ni kichwa cha kanisa

Waefeso 1:22–23—akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo ndilo mwili wake…

Kanisa katika andiko hili linaelezwa kama mwili wa Kristo. Yesu ni kichwa cha Mwili wake. Katika hali ya kawaida kichwa huuagiza mwili kufanya mambo inayotakiwa na kazi nyinginezo. Katika mwili wa Kristo, Yesu ni Kamanda anayeamrisha Kanisa lake kufanya kazi ya Mungu.

Kanisa lilizaliwa na Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste. Darasa hili litajumlisha somo la kanisa la mwanzo la Matendo hadi Kanisa letu la kipindi hiki cha sasa.

Historia

Neno hili historia linatokana na neno "linalomaanisha kujifunza kwa kufanya uchunguzi."

Kamusi ya Webster inafafanua historia kama "lile tawi la elimu linalohusu matukio fulani katika hii dunia yetu. Somo au uchunguzi wa mambo ya wakati uliokwishapita."

Mwandishi mmoja alisema kwamba "Zamani ni nchi ya kigeni: wanafanya mambo tofauti huko." [1]

Ukristo

Tunajifunza historia ya kanisa la Kikristo. Neno Mkristo lina maana "ya kuwa kama Kristo au mmoja wa Wafuasi" wa Kristo ambapo lilitumika kwa mara ya kwanza huko Antiokia kwenye mwaka wa 40 BK (Matendo 11:26).

Kuzaliwa, maisha, kifo, na ufufuko wake Kristo ndio kiini cha historia ya dunia. Historia imeandikwa kumzunguka Kristo; tarehe huandikwa katika KK (Kabla ya Kristo) na BK (Baada ya Kristo). Historia yote imemweka Kristo katikati yake.

[1] L. P. Hartley, The Go-Between (1953)

Kwanini tujifunze Historia ya kanisa?

Historia ya Kanisa inatusaidia kuelewa kile tunachoamini

Ukiingia kanisa la Kiprotestanti popote ulimwenguni, utasalimiwa na huduma inayofanana na nyingine yeyote uliyowahi kuhudhuria. Kutakuwa na tofauti za mtindo, lakini utatarajia sala ya ufunguzi, wakati wa kuimba, sadaka, na kuhubiri Mara nyingi hizi zitakuwa katika utaratibu sawa. Hakuna mahali popote katika Biblia hutolewa orodha ya jinsi ya kuongoza huduma ya kanisa, sasa imekuwaje wote tumekuwa na mfumo sawa?

Ni kwa sababu mengi ya yale tunayofanya na kuamini kama Wakristo yameumbwa na zaidi ya miaka elfu mbili ya mila, ingawa mara nyingi hatujagundua. Mila mara nyingi huonekana kuwa jambo baya katika makanisa ya Kiprotestanti. Tunapenda kuamini tunafanya mambo sawasawa na Paulo na mitume wengine walifanya katika Agano Jipya, lakini hakuna mahali pa Biblia tunaona kwamba Paulo alikuwa amevaa suti na tai siku ya Jumapili (kwa kweli, Jumapili kufanywa kama siku rasmi kwa wakristo kuabudu imetokana na mila na sio katika Biblia).

Mila ya kanisa inaweza kuwa jambo jema. Watu wengi wamejifunza Biblia, kuomba, na kujadili mafundisho na mawazo mengi kuhusu jinsi kanisa linapaswa kuishi. Hatupaswi "kurejesha gurudumu," na kujifunza masomo haya yote, lakini tunaweza kujifunza kutokana na kile ambacho watu hawa wamepitisha kwa njia ya mila. Hatuamini kwamba mila ni bora zaidi kuliko Maandiko, lakini tunaamini kwamba mila hutusaidia kuelewa Biblia.

Tukisoma historia ya kanisa, tutaelewa mengi kuhusu namna hii mila ilivyoingia. Tujifunze historia au la, tutaathiriwa na historia. Ushawishi utatoka kwenye utamaduni unaotuzunguka sisi, hitimisho tunayofikiria kwa siri, na hadithi ambazo tulisimuliwa. Hatari ni kwamba bila kujifunza kwa ufahamu wa jinsi tulivyokuwa, tunaweza kufikia hitimisho baya.

Kuijenga Imani yetu

Somo la historia ya kanisa linatuwezesha kuutambua urithi wetu. Wanaume wengi na wanawake walikwishajitoa mhanga maisha yao katika jitihada zaokueneza ujumbe wa neno la Mungu. Neno la Mungu limehubiriwa katika mazingira magumu sana na wakati mwingine yanayoogopesha.

Jifunze kuhusu uamsho wa ajabu uliofanyika katika Kanisa

Uwepo wa nguvu za Mungu umeonekana waziwazi katika historia yote ya Kanisa. Ni Roho Mtakatifu aliyewezesha uamsho ule uliopita na ndiye yeye anayefanya mambo yatendeke vizuri leo.

Unaweza kuuona mkono wa Mungu ukiwa juu ya Kanisa lake kila wakati

Historia hujirudiarudia

Mwandishi wa Mhubiri alisema "wala jambo jipya hakuna chini ya jua" (Mhubiri 1:9). Historia huja kwa mizunguko. Kwakuyasoma matukio yaliyokwishapita tunaweza kuelewa vizuri mambo yanayotokeahivi sasa. Tunaweza kujifunza kutokana na makosa yaliyofanywa na watu wengine. Mungu hachambui watu kwa ajili ya kuwaheshimu. Kila kitu alichokitendea kizazi kilichopita anaweza pia akatufanyia sisi iwapo tutamtii kama kizazi hicho cha zamani.

Warumi 2:11—Kwa maana kwa Mungu hakuna upendeleo.

Tunaweza kujifunza kutokana na mafanikio na makosa ya wale ambao wameishi mbele yetu.

Mungu habadili

Mungu huwataka watu wake watende kazi kwa usawa katika vipindi vyote. Mungu alivyowafanyia watu wa kale ni hivyo hivyo atawatendea watu wake leo. Mungu anataka watu waishi maisha matakatifu na hatabadilisha msimamo wake kabisa.

Mungu huwatumia wanadamu wa kawaida kufanya kazi zake

Mungu yule aliyewatumia akina Petro, Yakobo, na Yohane ni huyo atakayekutumia pia wewe. Mungu katika utendaji wake huwatumia watu wa kawaida tu kama wewe au mimi.

Uneemeshaji wa elimu ya mchungaji

Mchungaji wa Injili anapaswa asiwe mjinga, awe mjuzi kwa utajiri wa historia ya kanisa.

Vipindi saba vya historia ya kanisa

KANISA LA KITUME

MWANZO: Tangu siku ya Pentekoste (30 BK)

MWISHO: Hadi kukamilishwa kwa Agano Jipya kwenye (100 BK)

KANISA LA MATESO

MWANZO: Kuanzia kukamilishwa Agano Jipya kwenye (100 BK)

MWISHO: Hadi kutolewakwa Hati ya Konstantino (313 BK)

Hiki ni kipindi cha mateso makuu kwa kanisa. Kanisa liligandamizwa mno chini ya Ufalme wa Kirumi.

KANISA LA KIFALME

MWANZO: Kuanzia kutolewa kwa Hati ya Konstantino (313 BK)

MWISHO: Hadi anguko la Roma (476 BK)

Neno la Ufalme linahusiana na mfalme au mtawala. Hiki ni kipindi ambacho mfalme alikuwa na ushawishi mkubwa sana ndani ya kanisa.

KANISA LA ZAMA ENZI ZA KATI

MWANZO: Tangu anguko la Roma (476 BK)

MWISHO: Hadi anguko la Konstatinopo (1453 BK)

Wakati huu kanisa Katoliki lilikuwa na mamlaka makubwa katika bara la Ulaya.

KANISA LILILOTENGENEZWA

MWANZO: Tangu anguko la Konstantinipo (1453 BK)

MWISHO: Hadi mwisho wa vita vya miaka 30 (1678 BK)

Huu ni wakati ambao Mungu aliwatumia watu kama Martin Luther kusimamia nakupigana na wimbi la ukatoliki na walihubiri kwamba wenye haki wataishi kwa imani yao. Mungu aliamsha wanaume katika eneo lote la Ulaya ili walirudishe Neno la Mungu kanisani.

KANISA LA KISASA

MWANZO: Kuanzia mwisho wa vita ya miaka 30 (1678 BK)

MWISHO: Hadi katika karne ya ishirini (Miaka ya 1950 BK)

Hiki ni kipindi cha uamsho wa hali ya juu na umisionari ulienea sehemu nyingi. Hadi kufikia kipindi hiki kulikuwa hakuna jitihada mahususi zilizofanyika za kuieneza Injili duniani kote. Wakati huu ndio David Livingstone alianzisha vituo vingi vya umisionari katika bara la Afrika.

KANISA LA BAADA YA KISASA

MWANZO: Kwanzia karne ya ishirini (Miaka ya 1950 BK)

MWISHO: Hadi siku yaleo

Tutasoma kila kipindi katika vipindi hivi 7 peke yake. Sura hii ilikuwa ni muhtasari tu wamafunzo yatakayo fundishwa.

Moja: Kanisa la Mitume (30–100 BK)

Kutoka siku ya Penstekoste hadi kukamilishwa Agano Jipya

Maelezo ya kanisa la kwanza

Nguvu za kanisa

Walipokea nguvu siku Roho Mtakatifu alipowashukia (Mdo. 1:8)

Makazi asilia ya Kanisa

Kanisa lilianzia katika mji wa Yerusalemu lakini mateso yalilitawanyia nchi nyingine (Matendo 8:1).

Uanachama katika Kanisa

Wanachama wa mwanzo katika Kanisa walikuwa wote ni Wayahudi. Walikuwa hawajafahamu kwamba injili ni kwa ajiliya mataifa pia.

Serikali ya Kanisa

Wale Mitume kumi nawawili waliongoza kanisa.

Kanuni za Kanisa

Yesu alikuwa ndiye Masia (Mdo. 2:36)

Ufufuko wa Kristo (Mdo. 2:30–32)

Kuja tena kwake Kristo (1 The. 4:15–17)

Wakuu wa Kanisa

Mtume Petro

Katika kanisa la Yerusalemu Mtume alikuwa ndiye msemaji wa mitume wote na msaidizi wake alikuwa ni Yakobo. Historia inasema kwamba Petro alikufa shahidi huko Roma mwaka wa 67 BK.

Stefano

Alikuwa nimmoja kati ya watu saba walioteuliwa kwa ajili ya kutunza mahitaji ya kanisa (Mdo. 6:8) Anasimuliwa kama mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu. Alitumiwa na Mungu kufanya mambo makubwa ya ajabu na miujiza katikati ya watu. Stefano alikufa shahidi wa kwanza (Mdo. 7:55–60).

Philipo

Alianzisha kanisa katika Samaria. Kanisa hili lilitambuliwa na Mitume. Hili lilikuwa kanisa la kwanza nje ya dhehebu la Yuda. Alianzisha pia makanisa huko Gaza, Joppa na Kaesaria (Mdo. 8:40).

Mtume Paulo

Mateso ya Sauli

Sauli aliongoza askari waliowatesa sana Wakristo (Mdo. 8:3). Sauli ndiyea liyeidhinisha Stefano auawe. Mateso hayo yalisaidia kulieneza kwa upana zaidi kanisa (Mdo. 8:4).

Kubadilika kwa Sauli

Yesu alikutana na Sauli katika barabara iendayo Dameski. Akiwa njiani alianguka na akageuka mara akawa mhubiri shupavu kwa Wayahudi na Mataifa mengine (Mdo. 9:19–22). Jina la Sauli lilibadilishwa likawa Paulo. Huyu Paulo akawa mtume mmoja mkakamavu sana kwa mataifa.

Safari za umishonari za Paulo

Paulo alifanya safari nyingi za kueneza injili na alianzisha makanisa huko Filipi, Tesaloniki, Berea, Athene, na Korinto. Aliyaunda yale makanisa saba ya Asia moja kwa moja au kwa njia iliokuwa rasmi (Mdo. 19:10). Makanisa hayo yalianzishwa katika mateso makubwa (2 Kor. 11:23–28).

Alifundisha katika masinagogi na alipokea toka kwa Roho Mtakatifu ujumbe mwingi wa Agano Jipya. Alipokuwa kifungoni Roma aliandika waraka kwa Waefeso, Wafilipi, Wakolosai na kwa Filemoni. Historia inaonesha kwamba Paulo alikufa shahidi mwaka 67 BK.

Yakobo

Yakobo alikuwa mdogo wake Yesu. Huyu anatakiwa asichanganywe na mtume Yakobo ambaye aliuawa na Herode katika Matendo 12. "Na akamuua Yakobo nduguye Yohana kwa upanga" (Mdo. 12:2). Yakobo alikuwa mzee kiongozi au mchungaji wa kanisa la Yerusalemu. Yeye alitambua mataifa mengine kama sehemu ya mwili wa Kristo. Historia inaonesha kwamba Yakobo alikufa shahidi mwaka 62 BK.

Mtume Yohana

Huyu mtume Yohana alikuwa ndiye kijana mdogo kuliko mitume wengine wote. Alinyanyuka baada ya mitume wengine kufa. Alimfundisha injili Inyasi na Polikarpi ambao baadaye waliliongoza kanisa.

Kanisa katika Mataifa

Petro na Kornelio (Mdo. 10)

Petro alihubiri injili katika nyumba ya Kornelio na hapo ndipo Mataifa mengine yalipompokea Roho Mtakatifu (Mdo. 10:44–48).

Taarifa ya Petro kwa wazee (Mdo. 11:1–18)

Baraza la Yerusalemu katika mwaka wa 48 BK (Mdo. 15:5–20)

Mitume waliitisha baraza la wakuu wa watu wakae pamoja kuamua iwapo mataifa mengine walipaswa kufuata sheria ya itifaki ya Musa. Baadhi yao walikuwa wakisisitiza kwamba ni lazima watu wa mataifa watahiriwe (mst. 5). Baraza iliamua kwamba Mataifa hawana haja ya kufuata sheria ya ibada ya Kiyahudi.

Paulo anamkemea Petro (Wagal. 2:11–14)

Anguko la Yerusalemu mwaka wa 70 BK

Wayahudi waliasi dhidi ya utawala wa Warumi mwaka wa 66 BK

Jemadari wa Yerusalemu aliyejulikana kama Tito aliubomoa kabisa mji wa Yerusalem

Mji huo uliwaka moto mkubwa uliosababisha dhahabu iyeyukie katikati ya matofali yaliyoujenga. Askari walilivunja hekalu vipandevipande, tofali kwa tofali kwa lengo la kuondoa ile dhahabu iliyokuwa imeyeyukia katikati. Hili lilitimiza utabiri wa Yesu kuhusu hekalu hilo.

Marko 13:2—Yesu akajibu, akamwambia, Wayaona majengo haya makubwa? Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomolewa.

Sadaka za kuteketeza wanyama zilikoma hekalu lilipobomolewa

Wakati huo Mungu alihitimisha mambo yake na dhehebu la Yuda






Mbili: Kanisa la Mateso (100—313 BK)

Kuanzia kukamilishwa Agano Jipya hadi kutolewa Hati ya Konstantino.

Hii inazindua kipindi ambacho kanisa liligandamizwa chini ya utawala wa kipagani wa Roma. Kinyume na mategemeo hayakutokeza marashi matamu kwa Mungu kwa kuwa katika karne hizo mbili kulikuwa na mashahidi kuuliwa mfululizo. Kutolewa kwa Hati ya Kostantino kutajadiliwa zaidi katika kipindi cha Kanisa la Kifalme.

Tuna kumbukumbu za matukio ya kipindi cha kanisa la kwanza kutoka kwa Biblia, ambayo tunaamini yametutia moyo. Hatuna kumbukumbu za kibiblia za wakati wowote wa kanisa. Hii ina maana kwamba si kila tunachokisoma ni kweli. Watu wawili wanaweza kushuhudia tukio moja na bado wakatoa taarifa tofauti kabisa kuhusu jambo hilo. Historia ni ngumu kwa sababu vyanzo vinaweza kuwa kweli au visiwe kweli. Kuna msemo unasema, "historia imeandikwa na washindi." Hii ni kwa sababu wale walioshindwa vita walishakufa, na hawakuweza kuandika ukweli wao wenyewe wa kile kilichotokea.

Mateso

Huu ulikuwa ni wakati wa mateso makali kwa kanisa. Watu ambao hawakuawa walilazimika kwenda mafichoni na huko walivumilia umaskini na maisha ya taabu.

Yesu aliwaeleza mapema kuhusu kipindi hicho cha mateso. Yesu aliwatia moyo wafuasi wake ili wasikiogope. Huo ulikuwa ni utabiri wa mateso ambayo kanisa lingeyapata kwa kipindi fulani.

Wengi walifungwa kwa sababu za kuhubiri injili katika kipindi hiki. Kuwa Mkristo ilifanywa kuwa ni kosa chini ya sheria ya Kirumi.

Katika mwaka wa 303 BK Mfalme Diocletiani alianzisha kipindi cha mateso makali sana kwa wakristo yaliyojulikana kama "Mateso Makuu." Hili lilikuwa ni jaribio la kuuondoa Ukristo katika uso wa dunia hii. Inasemekana Diocletiani alijenga mnara ulioandikwa: Kwa kumbukumbu ya kufukuzwa ushirikiano unaoitwa Ukristo. Wakristo wengi walichomwa moto wakiwa hai kwa sababu ya ushuhuda wao. Wakristo walitupiwa wanyama wakali ambao waliwararua na kuwala katika viwanja vya michezo.

Sababu zilizofanya kuwepo na mateso chini ya utawala wa kifalme

Ibada za kipagani zilikuwepo kutokana na uwepo miungu wapya wakati ambapo Ukristo ulitambua kuabudiwa kwa Mungu mmoja tu wa kweli tu

Miungu wapya walikubalika chini ya utawala uliotukuza utamaduni wa kuabudu miungu wengi wa Roma. Wakristo walishindwa kuvumilia kuabudiwa kwa miungu wa uongo na walizikataa njia za kipagani.

Ibada za kuabudu sanamu ziliingizwa katika maisha ya jamii

Sanamu zilijengwa katika nyumba nyingi na kutukuzwa. Mapicha yaliabudiwa kama miungu katika sherehe rasmi na shughuli nyingine za jamii. Wakristo ambao hawakukubali kushirikishwa katika ibada hizo za kipagani hawakuishi kwa amani na jamii hiyo ya watu wasioamini Mungu. Kwa sababu Wakristo hawakushiriki katika sherehe ya ibada ya kipagani, watu wengi hawakufikiri kwamba waliabudu wakati wote na kwamba hawakuamini Mungu.

Kuabudu Mfalme

Wakristo hawakubali wazo la kuabudu mfalme. Wakristo walimzungumzia Mfalme mwingine. Wakristo walitazamwa kama waliokosa utii kwa mfalme na wanapanga mapinduzi ya kumwondoa mfalme.

Katika karne ya kwanza dini ya Yuda ilikuwa dhehebu rasmi iliyokuwa imeruhusiwa kuwepo katika himaya ya Kirumi

Ukristo ulihesabiwa kama sehemu ya dini hiyo ya Yuda ambayo ilikuwa imeruhusiwa. Baada ya Yerusalemu kuharibiwa mwaka wa 70 BK, Ukristo ulisimama peke yake bila kulindwa na sheria.

Mikutano ya siri

Wakristo walianza kufanya mikutano yao kwa siri ili kujilinda wasikamatwe. Mikutano hiyo ya siri iliwatia wasiwasi sana watawala. Wakristo walishutumiwa kwamba mikutano yao ya siri ilikuwa ni ya kupanga kuuangusha Ufalme wa Kirumi uliokuwa madarakani. Kwa sababu ya Mlo wa Bwana na kuzungumza juu ya kula mwili wa Kristo, watu wengine walidhani kuwa walikuwa wachanga.

Usawa katika kanisa

Wakristo waliwaona watu wote kuwa sawa, kwa hiyo waliharibu utaratibu wa jamii wa kutukuza sanamu za miungu. Jambo hili lilikuwa ni kinyume na mila za jamii ya Kirumi.

Faida za kibiashara

Kustawi kwa Ukristo kulisababisha biashara iliyokuwa na faida kubwa ya kutengeneza na kuuza sanamu na picha za ibada za kipagani kufa.Watengenezaji wakubwa wa vitu hivyo waliunga mkono kuteswa kwa wakristo (Mdo. 19:23—28).

Mashahidi muhimu na viongozi wa makanisa ya liyoteseka

Inyasi

Inyasi alikuwa asikofu wa Antiokia huko Syria. Huyu alikuwa ni mwanafunzi wa mtume Yohana.

Inyasi alitupiwa wanyama wakali wamrarue katika kiwanja cha Coliseum. Akisimama katika uwanja huo wakati wanyama wakali wanamsogelea, Inyasi alisali ifuatavyo, "Nakushukuru ee Bwana kwa kuwa wewe umenitoa mimi ilinitukuke. Mimi ni punje ya Mungu ambaye nitasagiwa katikati ya meno ya wanyama wakali ili niwe mkate mtakatifu wa Bwana."

Shahidi Yustini

Shahidi Yustini alikuwa mwana falsafa aliyekuwa Mkristo baada ya kukutana na mtu mzee ambaye alielezea jinsi Yesu alivyotimiza unabii wa Agano la Kale. Alikuwa mmoja wa watetezi wa kwanza, ambaye ni mtu aliyetumia sababu na mantiki ili kulinda imani yake. Aliandika vitabu vingi ambavyo vipo hadi leo na vinatupatia taarifa nyingi za kipindi hicho. Mojawapo ya kazi zake muhimu ni Mazungumzo na Trypho maandishi ambayo hufundisha dhidi ya Waebionaiti (Ufunuo 2:9).

Aliandika mara moja, "Unaweza kutuua, lakini huwezi kutudhuru." Yustini shahidi alikatwa kichwa huko Roma mwaka 165 BK. Maneno yake ya mwisho yalikuwa, "Mimi ni Mkristo, nimewekwa huru na Kristo na kwa wema wake Kristo nina pokea pigo hili kwa tumaini moja."

Polikarpi

Polikarpi alikuwa asikofu wa Smirna katika Asia ndogo. Alifundishwa akiwa kijana na Mtume Yohana. Alikuwa mhudumu shupavu katika kizazi chake. Wakati polisi walipokuja kumkamata, aliwapokea kama wageni. Aliwapa chakula na kuomba muda wa lisaa wa kuomba, lakini alitumia masaa mawili.

Walimleta Polycarp kwa mtawala, ambaye alitishia kumchoma akiwa hai kwa moto kama hatamkana Kristo. Polikarpi akajibu, "Miaka themanini na sita nimemtumikia Kristo na hajanitendea kosa lolote; ni kwa nini basi nimkufuru mfalme wangu na ambaye ameniokoa? Unanitishia kwa moto unaowaka kwa saa moja na kuacha; lakini hujui moto wa hukumu ujao, na pia hufahamu moto wa adhabu ya milele. Leta chochote kama utakavyo."

Mtawala huyo alimsihi akisema, "Akae mbali na wasioamini Mungu!" (akimaanisha Wakristo), ili waweze kumruhusu awe huru. Polycarp aliugeukia umati uliokuwa unatazama huku akisema, "Akae mbali na wasioamini Mungu!" Kwa sababu hakuweza kupingana na imani yake ya Kikristo, aliteketezwa akiwa hai huko Smyrna mwaka wa 155 BK. Polycarpi alikuwa kiungo cha mwisho kwa Kanisa la Mitume.

Ireneusi

Ireneusi alikuwa mwanafunzi wa Polikarpi. Baadaye alikuwa askofu wa Lionsi (huko Gaul) mwaka 177 BK. Alisisitiza kanuni za msingi za Ukristo ambazo zilipingwa na Waagnosti. Wagnostiki waliamini "maarifa ya siri" ambayo waamini wachache tu wangepokea, lakini Ireneusi aliwakumbusha kwamba Mitume walifundishwa waziwazi na si kwa siri. Baadhi ya maandiko yake bado yanakuja leo.

Origen (185—254 BK)

Origen alikuwa mwanadolijia, ambayo ina maana kwamba alisoma kutoka kwenye vyanzo vya kidunia, kama vile falsafa ya Kigiriki, na kutumia mawazo yao kwa kufikiria kidini.

Aliamini kwamba kulikuwa na viwango vitatu vya maana ya Kibiblia: halisi, maadili, na ishara.

Tertullian (150—229 BK)

Tertullian alisema "Je, Athene inafanya nini na Yerusalemu?" Alikuwa akisema kuwa mawazo ya falsafa (Athene) hawakuweza kuongeza chochote kwenye mafundisho ya Ukristo (Yerusalemu). Hii ilikuwa shambulio dhidi ya mwanadolijia.

Aliamini kwamba mateso yalitoka kwa Mungu. Alidhani ilikuwa chombo kilichotenganisha waumini wa kweli kutoka kwa waongo.

Simeoni

Simeoni alikuwa kiongozi wa kanisa la Yerusalemu baada ya Yakobo. Alisulubiwa msalabani kwa amri ya Gavana wa Kirumi wa Palestina mwaka 107 BK wakati wa utawala wa Trajani.

Blandina

Blandina alikuwa msichana Mkristo aliyekuwa mtumwa ambaye aliteswa tangu asubuhi hadi usiku kisha akatamka, "mimi ni Mkristo na kat iyetu hakuna uovu unaotendwa."

Perpetua na Felista

Alikuwa ni mwanamke mwadilifu wa Kartago, Perpetua na mtumwa wake Felisita waliuawa na wanyama wakali mwaka 203 BK.

Uundaji wa kanuni za Agano Jipya

Neno kanuni lina maana "ya fimbo, sheria, au kifaa cha kupimia."

Inahusu vitabu vya Biblia ambavyo vinatambuliwa kama vifaa vya utukufu wa Mungu kwa asili yake (vilivyopumuliw ana Mungu) na vikajumlishwa katika Biblia kama sehemu yake.

Hakuna tarehe maalumu ambazo zinatambuliwa kama rasmi ambazo rasimu ya Agano Jipya ilipatikana lakini haiwezi ikawekwa mapema zaidi ya mwaka wa 300 BK.

Mafundisho ya uwongo yalizuka kipindi hiki

Wagnosti

Wagnosti walifundisha kwamba watu wanaweza kuokolewa kwa ujuzi wa siri. Wanapata jina lao kutoka Gnosis, ambayo ni neno la Kigriki limaanishalo "ujuzi." Waliamini kwamba wokovu haukuwa uhuru kutoka dhambini, lakini ilikuwa uhuru kutoka kwa ujinga.

Waliamini kwamba Yehova alikuwa mungu mwovu aliyeumba ulimwengu huu kama gereza kwa roho za wanadamu. Kwao, ulimwengu wa asili ulikuwa uovu, na hivyo roho za wanadamu zinapaswa kuepuka hilo kwa ujuzi huu wa siri. Ujuzi huu hauwezi kuja kutoka ulimwenguni, lakini njia yao ya kupokea ni kwa njia ya kukataa mwenyewe. Hawatashiriki ujuzi huu na watu nje ya kikundi chao.

Waebionaiti

Waebionaiti waliendeleza mila na sheria za Musa na walijaribu kushawishi wengine wafanye vile vile pia. Walikuwa Wayahudi ambao walidhani kwamba Mataifa wanapaswa kubadilika kwa Uyahudi. Wakamkataa Paulo kama mtume. Hawakuamini kwamba Yesu ni uungu. Maandiko pekee ambayo walitumia kutoka Agano Jipya ni sura ya 3-28 ya Injili ya Mathayo. Hawakutumia sura mbili za kwanza za Injili, kwa sababu zinaonyesha Yesu kama Mwana wa Mungu.

Wamarcioni

Walikuwa wafuasi wa Marcioni. Kikundi hiki kilikuwa kinyume cha Waebionaiti. Wao walitaka Wakristo kujitenga kabisa na chochote kinachohusiana na Wayahudi. Marcioni aliunda kanuni ya Biblia ambayo ilikuwa na injili tu ya Luka (ambaye alikuwa mtu wa Mataifa) na nyaraka kumi za Paulo (zilizobadilishwa ili kuondoa kumbukumbu za Uyahudi). Hakupenda Mungu wa Agano la Kale.

Wamontani

Walikuwa wafuasi wa Montanusi (150-170 BK). Hii ilikuwa kundi la kinabii ambalo liliamini kwamba Roho Mtakatifu alizungumza mambo mapya kwa kanisa. Waliamini kwamba wanachama wa Utatu walifanya kazi kwa nyakati tofauti:

  • Baba alifanya kazi katika nyakati za Agano la Kale
  • Mwana alifanya kazi katika nyakati za Agano Jipya
  • Roho Mtakatifu anafanya kazi leo

Wasabelliani (pia inajulikana kama Wamodali)

Kundi hili liliamini kwamba kulikuwa na Mungu mmoja ambaye alikuwa na nafasi tatu (au muundo): Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.

Tatu: Kanisa la Kifalme (313–476 BK)

Tangu kutolewa Hati ya Konstantino mpaka angukola Roma.

Konstantino

Msalaba wa Konstantino

Alipigana vita na Maksentiusi kugombea ufalme katika mapigano ya Daraja la Milviani na mwaka 312 BK. Jeshi lake lilizidiwa nguvu na askari wa Maksentiusi ambaye aliutaka pia ufalme. Mshindi wa vita hii angekuwa mfalme ajaye wa Roma. Konsitantino alidai kuwa na maono ya msalaba ulioandikwa maneno, "katika alama hii shinda vita." Msalaba ulikuwa barua za Kigiriki chi (Χ) na rho (Ρ), ambazo ni barua mbili za kwanza za neno la Kigiriki Christos (ΧΡΙΣΤΟΣ), ambalo tulipata neno letu "Kristo." Konstantino alifanya alama hii ya msalaba kuwa alama ya jeshi lake, na akaiweka katika ngao za askari wake. Konstantino alishinda vita ile na akawa Mfalme wa Warumi.

Konstantini alifanya muafaka wa imani na hii akachukuliwa kama aliyeingia ukristo

Wanahistoria wengi wa kikristo walitilia shaka uaminifu wake.

Hati ya Uvumilivu (Hati ya Konstantini) (313 BK)

Hati ni amri rasmi au waraka maalumu. Hati hii ilitoa uhuru kwa dini zote katika Ufalme wa Kirumi na ikasimamisha mateso yote ya Warumi kwa Wakristo. Mali zote zilizokamatwa wakati wa utawala wa Mfalme Diokletiani zilirudishiwa wenyewe.

Matokeo ya kuvumiliwa kwa kanisa

Mateso kwa Wakristo yalikoma

Ukristo uliostawi katika kipindi cha mateso uligeuka wa kidunia chini ya maelewano na serikali

Makanisa yaliyokamatwa wakati wa mateso yalirudishiwa hadhi yake

Majengo mapya ya kanisa yalijengwa. Kanisa la Roma liitwalo Basilika likawa ndio jengo la mfano wa majengo ya kuvutia ya makanisa. Jengo la Basilika lilikuwa ni mahakama iliyokuwa na umbo la mstatili uliyogawanywa katika safu yanguzo zenye jukwaa lililokuwa nusu mviringo upande mmoja na viti vya maofisa vikiwepo mwishoni mwa upande mmoja. Huu ndio mfumo uliopo bado mpaka leo katika kanisa Katoliki. Mfano wa usanifu wa majengo wa namna hii ni Basilika ya Mtakatifu Petro huko Roma.

Matoleo ya sadaka ambazo ni rasmi yalikoma

Raia wa Roma waliacha kutoa matoleo za sadaka kwa miungu wa kipagani.

Makanisa yalikuwa yakisaidiwa na Dola

Mahekalu ya miungu pia yalikuwa yakipata misaada kutoka katika hazina ya umma. Makanisa na wachungaji wake walipokea fedha kutoka serikalini.

Wachungaji walikuwa wakipewa marupurupu

Makuhani akawa darasa tajiri. Wanaume walipenda nafasi hizi kwa faida ya fedha na nguvu zinazohusiana na nafasi hiyo.

Sehemu zingine za ibada ya kipagani zilikuwa sehemu ya kanisa

Kwa kipindi kirefu, kulikuwa na matendo fulani ya mila za kipagani za Kirumi ambazo zikawa sehemu ya kanisa. Baadhi ya miungu ya kirumi inafanana na watakatifu ambao wakatoliki wanawaomba. Baada ya watu huona ufanano kati ya sanamu ya Maria ikimshikilia mtoto Yesu sanamu za kirumi hufafanua Fortuna na Jupita. Kuna baadhi ya wakristo ambao hawapendi kusherehekea Krismas kwasababu sikukuu hii ina mizizi katika sikukuu za kipagani za kirumi za Satunalia.

Baadhi ya watu watasema Konstantino alianzisha Kanisa la Kikatoliki, lakini lazima ikumbukwe kwamba mapokeo na imani za kile ambacho Kanisa la Kikatoliki liko kwa siku zetu za leo imehusishwa kwa zaidi ya miaka mingi kutoka ile hali ambayo kanisa lilikuwa nayo wakati wa Konstantino.

Kuanguka kwa utawala wa Kirumi wa Magharibi

Mfalme Konstantino alichagua mji wa Ugriki uitwao Baizantiamu kuwa mji wake mkuu na akauita Konstantinopo (330 BK)

Hali hii ilimwongezea ushawishi askofu wa Roma. Sasa mji mkuu ukawa ukombali sana na Roma na ile Himaya ikiwa imeshaporomoka.

Kugawanywa kwa himaya hiyo kulifuatiwa na ujenzi wa mji mkuu mwingine

Mfalme mmoja peke yake hakuweza tena kulitawala eneo lote kwani lilikuwa kubwa mno. Bahari ya Adriati ikawa ndio mpaka wa asili kati ya sehemu mbili za himaya hiyo. Mwaka wa 395 baada ya Kristo himaya ya Kirumi iligawanyika rasmi kuwa Himaya ya Mashariki na Himaya Magharibi.

Himaya ya Magharibi ilimokuwa Roma kama mji wake mkuu iliendelea kuwepo hadi mwaka 476 BK

Himaya ya Mashariki iliyokuwa na Konstantinopo kama mji mkuu ilikuwepo hadi mwaka 1453 BK

Hii ndio baadaye ikageuzwa kuwa Himaya Takatifu ya Roma ya Nyakati za Kati kuanzia mwaka 500 hadi mwaka wa 1500 BK.

Viongozi wakuu wa Kikristo wa kipindi hiki

Atanasi (296–373 BK)

Alikuwa mlinzi wa imani katika ubishani wa Ariani. Aria ambaye aliongoza mafundisho ya uongo hakuamini kanuni ya Biblia ya Utatu. Alikuwa Askofu wa Alexandria tangu mwaka 325 BK. Mnamo 367 BK yeye aliandika barua kutambua kanuni za Agano Jipya ambazo tunatumia leo. Alipelekwa uhamishoni mara tano kwa sababu ya mafundisho yake.

Yohana Krisostomu (345–407 BK)

Huyu anajulikana kama "mdomo wa dhahabu" kwa sababu aliweza kuongea kwa ufasaha wa ajabu. Alikuwa mhubiri shupavu, kiongozi watu na mwenye uwezo mzuri wa kuifafanua Biblia. Alikuwa askofu wa Konstantinopo mwaka 398 BK. Alifukuzwa nchini kutokana na msimamo wake wa kusema ukweli na alifia uhamishoni.

Augustino (354–430 BK)

Augustino alisema, "Mioyo yetu haina pumziko hadi imekupata wewe." Alikuwa Askofu wa Hippo huko Afrika Kaskazini mwaka 395 BK. Yeye ndiye mtetezi Mkuu wa ubishani wa Pelagia. Mafundisho haya ya uongo yalipambwa na Pelagio ambaye hakuamini dhambi ya asili. Augustino alijenga jina lake kama mhubiri, mwalimu na mwandishi. Yeye alijihusisha katika changamoto nyingi za siku zake (mfano wa Udonatismu na Upelagiasmu).

Ambrosi

Ambrosi alikuwa mtawala wa Milani. Wakati askofu wa Milani alipokufa mnamo mwaka BK 374, kutuliza ghasia juu ya nani angekuwa Askofu baadaye. Ambrosi alipiga hatua katika kujaribu kushusha vitu chini, na watu katika kusanyiko walipiga kelele kwamba yeye angekuwa askofu, hata ingawa yeye alikuwa bado haja batizwa yeye alilalamika lakinni mwishowe akaja kuwa askofu.

Wakati mtawala Theodosi kwenye uwanja wa watu waliouawa, Ambrosi aliwasiliana naye. Theodosi alifanya toba kwa kuvaa mavazi ya magunia na kupiga magoti mbele ya askofu akiomba msamaha. Huu ulikuwa mwanzo wa serikali kunyenyekea mbele ya kanisa.

Tunaona maendeleo ya uhusiano wa kanisa na serikali:

  1. Kanisa lilikuwa ndogo kuliko serikali
  2. Kanisa lilikuwa sawa na serikali
  3. Kanisa lilikuwa kubwa kuliko serikali

Yeromi

Yeromi (aliyejulikana kama Eusebio) alitafasiri Biblia kwenda Kilatini mnamo mwaka 405 BK. Na tafasiri hii ikawa inajulikana kama Vulgate kutoka neno la kilatini vulgus, ambalo humaanisha "kawaida."

Patriki (390 BK)

Patriki alikuwa mmishenari kutoka Uingereza kwenda Ireland. Aliuleta ukristo huko Ireland, na kanisa huko Ireland liliendelea kwa nje ya Utaratibu wa kirumi. Ireland haikuwa wakatoliki hadi 1100s.

Matukio ya ufunguo wa kipindi

Mabishano ya Wadonatusi (312 BK)

Wakati wa mateso ya Diocletiani, baadhi ya viongozi wa kanisa walitoa nakala ya Maandiko kwa mamlaka ya serikali. Viongozi hawa wa kanisa walijulikana kama wasaliti kwa sababu walisalitiwa kanisa.

Katika 311 BK mtu mmoja aitwaye Caecilliani alichaguliwa askofu wa Carthage. Caecilliani alikuwa amewekwa wakfu na askofu ambaye alikuwa msaliti. Mtu wa Kaskazini mwa Afrika aliyeitwa Donatusi alijitenga na kanisa mwaka 312 BK kwa sababu hakuamini kuwa Caecilliani lazima kuruhusiwa kuwa askofu, tangu alipaswa kuteuliwa na msaliti.

Baadaye Wadonatusi walibatiza tena Wakristo waliokuwa alikanusha imani yao kwa sababu ya mateso.

Baraza la Nikia (325–460 BK)

Katika Agano Jipya hasa hasa injili ya Yohana, tunaona kuwa Yesu yuko sawa na Baba, lakini hakuna habari za moja kwa moja kuhusu uhusiano wao. Swali lilikuwa kwamba vipi mtu aweza kuabudu wote Yesu na Baba hata sasa bado kuna swali hili kwa (mtu wanaoamini kwa mungu moja na kumwabudu)?

Ario, aliyekuwa ni mzee katika Alexandria, alianza kuhubiri mnamo mwaka 318 BK kwamba Yesu hakuwa Mungu wakati wote, bali alikuwa ni mtumishi mdogo wa Mungu. Hili lilikuwa jibu lake kwa wana monotheism. Alexanda Askofu wa Ario alisema ikiwa Mungu habadiliki, na yeye siku zote amekuwa Baba basi hiyo humaanisha kuwa lazima siku zote awe na Mwana.

Mjadala huu wa kidini ulimpata Konstantino, kwa sababu vurugu zilianza kwa sababu hiyo. Mnamo mwaka 325 BK Konstantino aliita baraza katika Nikia kutatua mjadala ulioibuliwa na Ario. Maasikofu zaidi ya 300 walihudhuria.

Maaskofu walitengeneza maelezo ya imani, ambayo, baada ya nyogeza zingine zilizofanywa kipindi cha Konstantinopo mnamo mwaka 381, ikajulikana kama shahada ya Nikia. Wote walitolewa pamoja na Ario ispokuwa Maaskofu wawili tuu walikataa saini maelezo ya imani. Kifwatacho ni kifungu kamili cha shahada:

Nasadiki kwa Mungu mmoja,
Baba mwenyezi,
Muumba wa mbingu na dunia
na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.
Nasadiki kwa Bwana mmoja, Yesu Kristo,
Mwanae pekee wa Mungu,
aliyezaliwa kwa Baba tangu milele yote.
Mungu aliyetoka kwa Mungu, mwanga kwa mwanga,
Mungu kweli kwa Mungu kweli,
aliyezaliwa, bila kuumbwa, mwenye uungu mmoja na Baba:
ambaye vitu vyote vimeumbwa naye.
Alishuka kutoka mbinguni,
kwa ajili yetu sisi wanadamu, na kwa ajili ya wokovu wetu.
Akatwaa mwili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kwake yeye Bikira Maria,
akawa mwanadamu.
Akasulubiwa kwa ajili yetu sisi, kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato;
akateswa, akafa, akazikwa,
siku ya tatu akafufuka,
kadiri ya Maandiko,
akapaa mbinguni,
amekaa kuume kwa Baba.
Atakuja tena kwa utukufu,
kuwahukumu walio hai na wafu,
nao ufalme wake hautakuwa na mwisho.
Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Bwana mleta uzima:
atokaye kwa Baba na Mwana.
Anayeabudiwa na kutukuzwa, pamoja na Baba na Mwana:
aliyenena kwa vinywa vya manabii.
Nasadiki kwa Kanisa moja, takatifu, katoliki, la Mitume.
Naungama ubatizo mmoja kwa maondoleo ya dhambi.
Nangojea na ufufuko wa wafu,
na uzima wa milele ijayo. Amina.

(https://sw.wikipedia.org/wiki/Kanuni_ya_Imani_ya_Nisea-Konstantinopoli accessed 2018/08/23)

Shahada inasema Yesu ni "Nuru kutoka Nuru." Je unawezaje kutenga nuru na jua? Kwa mfano huo huo je unawezaje kumtenga Mungu (Baba) kutoka Mungu (Mwana)?

Baraza haikujenga wazo la Utatu, tangu Utatu ilikuwa sehemu ya ibada ya kanisa tangu mwanzo (kwa mfano, ilitumika katika ibada ya ubatizo). Kwa Nicea waliunda msamiati kuelezea yale waliyoamini tayari kuhusu Mungu.

Baraza la kwanza huko Efeso (431 BK)

Baraza la Nikia liliamua kwamba Yesu alikuwa Mungu pia mwanadamu lakini kulibakia maswali kuhusu asili ya Yesu. Yeye ni Mungu kwa kiasi gani? Je, Yesu aliwahi kufanya dhambi kwa upande kibinadamu? Je, yeye ana akili mbili? Yesu angeweza kutenda dhambi kwa kuwa alikuwa mwanadamu? Viongozi wa wawili wa kanisa walitoa majibu kuhusu aina hizi za maswali. Walikuwa ni Nestorius na Cyril.

Nestorius

Nestorius alikuwa Asikofu wa Konstantinopo. Ni mwindaji aliye jaribu kuzuia kuenea kwa mafundisho kama Arianism kutoka kueneza.

Nestorius alipokea mawazo ya viongozi wengine wa kanisa wakati alikataa kutumia neno Theotokos, ambalo linamaanisha "Mama wa Mungu." Aliamini kama Mwana wa Mungu alikuwapo kila wakati, basi hakuweza kuzaliwa. Alipenda neno Christotokos, ambalo linamaanisha "Mama wa Kristo." Nestorius pia hakupenda Theotokos kwa sababu ya msisitizo kwamba Apollinarianism kuwekwa juu ya neno hili. Apollinarianism ilifundisha kwamba Yesu hakuwa na roho ya mwanadamu, lakini alikuwa Mungu amevaa katika mwili wa kibinadamu.

Aliamini kwamba Kristo alikuwa na nafsi mbili, lakini alikuwa bado mtu mmoja. Alisisitiza tofauti kati ya nafsi hizi mbili, hasa katika mateso ya Kristo. Alisema kwamba ilikuwa tu nafsi ya kibinadamu ulioteseka wakati Kristo aliteseka, na sio nafsi ya kimungu.

Cyril

Cyril alikuwa askofu wa Alexandria. Wakati Nestorius alisisitiza zaidi nafsi wa mwanadamu wa Kristo, Cyril alisisitiza zaidi ya nafsi yake kwa Mungu. Aliamini kwamba msisitizo wa Nestorius wa nafsi mbili za Kristo ulikuwa unaharibu wazo la umoja wa Kristo. Ikiwa tu mwili wa Kristo unasumbuliwa, basi Kristo hakuwa kuhani mkuu wa wakika, kwani ilikuwa tu kwa mateso ya kimungu ambayo Kristo angeweza kulipa kwa ajili ya dhambi za ubinadamu.

Uamuzi wa baraza

Kwa sababu Nestorius hakutaka kutumia jina Mama wa Mungu kwa Maria, alitunguliwa mashtaka na Cyril kwamba hakuamini kwamba Yesu alikuwa Mungu. Baada ya barua zenye hasira kati yao, baraza la maaskofu liliitwa kutatua mjadala huo.

Baraza lilivutia kwa kiasi kikubwa kwa sababu za kisiasa. Baraza la Pamoja la 381 liltangaza kwamba Askofu wa Konstantinopo atakuwa askofu wa pili pekee wa Roma (papa). Hasira za baadhi za maaskofu wengine, akiwemo Cyril, kwa sababu ilizuia nguvuu wao kama maaskofu. Pamoja na hivyo kulikuwa na maswali kuhusu mafundisho ya Nestorius, baraza pia liliitwa kwasababu ya wivu wa madaraka yake.

Baraza liliamua kinyume cha Nestorius na alikuwa uhamishoni kama mrithi. Pamojana hivyo alihamishwa, watu waliendelea kuamini mafundisho yake na Unestoria bado upo leo kama tawi la Ukristo.

Japokuwa kulikuwa na baadhi ya tofauti ya mafundisho kati ya Cyril na Nestorius, kwa kiasi kidogo hawakukubaliana kw jinsi ya uhamasishaji wa baadhi ya sehemu ya mafundisho ya Kristo na maajabu ya makubaliano yangeweza kuwepo kama wangekaa kuongea pamoja kuhusu mawazo yao. Wote wawili walikuwa na wasiwasi wa kulinda imani dhidi ya mafundisho ya uwongo. Wakati haiwezekani kujua, hatuwezi kushangaa makubaliano gani ambayo wangeweza kuja nao ikiwa walisema pamoja kuhusu mawazo yao.

Ingawa Nestorius mara zote alihusishwa mhamiaji, baraza la Kalsedoni lilifanya maamuzi kuhusu mafundisho ya Kristo ambayo yalikuwa karibu na mawazo ya Nestorius. Nestorius pia alikuwa sahihi kuhusu ni namna gani Mama wa Mungu walimtukuza Maria katika nafasi ambayo ilikuwa ni zaidi ya madai. Kwa miaka mingi, tumeona mila ya Kanisa la Katoliki la Kirumi likimtoa Maria katika nafasi aliyokuwa zaidi wamejihusisha kwa kimungu.

Baraza ya Konstantinople (381 BK)

Watu wengine hawakuamini kwamba Roho Mtakatifu alikuwa Mungu, kwa sababu Yeye hakuzungumza yeye Mwenyewe. Walisema kwamba hakuwa nafsi, bali nguvu ya kiroho. Baraza hii iliitwa ili kuthibitisha uungu wa Roho.

Baraza ya Chalcedon (451 BK)

Hili ndio baraza la mwisho la makanisa yote yaliyokuwa kuhusu asili-mbili za Yesu. Kusudi lake lilikuwa kumaliza mjadala juu ya Utatu. Ndani yake, ilitangazwa kuwa Kristo ni "atambuliwe katika asili mbili, bila kuchanganyikiwa, kugeuzwa, kugawanywa, kutengwa... bali hulka ya kila asili ikihifadhiwa na kukubaliana katika mmoja na katika dutu moja, si kugawanywa au kutengwa kuwa wawili, bali mwana huyo mmoja." Dutu maana "vifaa." Kufuatia ni maandishi kamili ya imani iliyotolewa kwa Chalcedon:

Sisi, basi, tukiwafuata baba zetu watakatifu, sote kwa ridhaa moja, twafunza watu kukiri Mwana yule mmoja, Bwana wetu Yesu Kristo, yeye mkamilifu katika utatu na pia katika ubinadamu; Mungu kweli na binadamu kweli, mwenye roho na mwili zote kamili kawaida; hususan na Baba kulingana na utatu, hususan kama sisi kibinadamu; katika vyote kama sisi, bila dhambi, wa pekee wa Baba kabla ya nyakati kulingana na utatu, na siku hizi za baadaye, kwa ajili yetu na wokovu wetu, mzaliwa wa bikira Maria, mama [wa] Mungu, kibinadamu; Kristo mmoja yule, Mwana, Bwana, wa pekee, atambuliwe katika asili mbili, bila kuchanganyikiwa, kugeuzwa, kugawanywa, kutengwa; tofauti katika asili isiwe nafasi ya kubatilisha hali ya umoja, bali hulka ya kila asili ikihifadhiwa na kukubaliana katika mmoja na katika dutu moja, si kugawanywa au kutengwa kuwa wawili, bali mwana huyo mmoja, pekee, Mungu Neno, Bwana Yesu Kristo; vile manabii tokea mwanzo (wamefunza) kumhusu, na Bwana Yesu Kristo ametufunza, na imani ya baba watakatifu tuliyoachiwa.

(http://www.cprf.co.uk/languages/chalcedon_swahili.html#.W4zxCegzbb1 accessed on 2018/09/03)

Tangu Nikia, kanisa lilikazia kwamba Yesu alishiriki asili na Baba, lakini sasa waliongeza kwa hili jinsi Yesu pia alishiriki asili na mtu.

Ilikuwa ni baraza la kwanza ambalo papa alicheza jukumu kubwa, na ilikuwa baraza la mwisho ambalo Mashariki na Magharibi wote watatambua rasmi.

Nne: Kanisa la Zama za Enzi za Kati (476—1473 BK)

Toka anguko la Roma hadi anguko la Konstatinopo.

Kanisa la Zama za Enzi za Kati lilifunikwa na giza

Isaya 9:19—Kwa sababu ya hasira ya BWANA nchi hii inateketea.

Kipindi cha karne ya 5 mpaka ya 15 huitwa kipindi cha zama za Giza.

Ustaarabu na uvumilivu ulifikia mwisho.

Kulikuwepona maendeleo madogo sana katika fasihi, sanaa na sayansi

Kulikuwa na umaskini na ushirikina ulioijaza nchi. Nchi nyingine walivamia Ulaya na kuua watu wengi. Palitokea pia vifo vilivyotokana na ugonjwa wa mtoki ambao ulienea katika bara lote.

Mazungumzo: Je, Mungu bado hutumia hukumu ili kuwaadhibu watu?

Biblia ilikuwa imezuiliwa kutoka kwa watu

Kanisa lilifundisha kwamba ni wachungaji tu ndio wanaoweza kuitafsiri Biblia. Watu wa kawaida walikatazwa kusoma Biblia, Biblia ilikuwa katika lugha yake ya mwanzo au katika lugha ya Kilatini ambayo ni watu wachache waliokuwa wanaielewa hata kama walitaka kujisomea wenyewe.

Watu waliwekwa gizani

Misa ilifanywa kwa Kilatini ambacho hakukuwepo wengi waliokifahamu. Ukweli na sayansi viligandamizwa na kanisa Katoliki. Galileo, yule mtu aliyegundua darubini alikaribia kuuawa kwa sababu kile alichoona kwa kutumia darubini kilikuwa kinyume na msimamo wa Papa ambaye alifikiriwa kwamba hawezi kukosea.

Viongozi wa kanisa walikuwa na tabia mbaya

Mawazo ya kanisa katika kipindi hiki

Ushirika

Ushirika ulikuwa kitovu ni kitovu cha wakristo kuabudu kwa kipindi hiki. Ibada ilizungumzwa kwa Kilatini, na makuhani wengi wa vijijini walikuwa hawaja elimika, hivyo hawakuweza kutoa hotuba. Viongozi ndio waliruhusiwa kuimba, lakini watu wote hawakuruhusiwa kuimba.

Kujikana

Baadhi ya watu hawakupenda jinsi kanisa lilivyo kua katika utajiri na nguvu. Hawa watu walijitenga wenyewe kutoka ulimwenguni na kuishi katika jamii zao. Walisali mara saba wakati wa mchana na kukaririsha sehemu kubwa ya Maandiko. Wanaume waliitwa watauwa na Wanawake waliitwa masista. Watauwa na masista waliishi katika jamii zilizo jitenga.

kuhamisha wenye dhambi (Purgatori)

Kanisa lilijua kwamba wenye haki walienda mbinguni na wasiohaki walienda Jehanamu,lakini nini ilitokea kwa watu ambao hawakuwa na haki wala wale wenye haki zaidi? Kuhamishwa kwa wenye dhambi (pagatori) kulikuwa endelevu kwa kipindi kile kama jibu kwa wale watu wa kawaida walipokuwa wakienda baada ya kufa.Inasemekana kuwa mahali ambapo mtu kawaida hutolewa kutokana na dhambi gani ambazo walikuwa nazo.

Vyeti vya upatanisho Indulgences

Hizi zilikuwa ni hati ambazo zilitolewa na kanisa kuondoa adhabu kwa wenye dhambi.

Falme za Kikristo

Katika kipndi hiki, hapakuwa na tofauti kati ya dini na kidunia. serikali na kanisa walishirikiana (na mara nyingine walipigana kwa ajili ya) mamlaka. Watu wote waliozaliwa katika nchi za Kikristo walifanywa kuwa Wakristo.

Kuongezeka kwa Upapa

Katika kanisa la kwanza, Askofu wa Roma (aliyejulikana baadaye kama papa) alikuwa ni askofu wa maaskofu. Maaskofu wote walikuwa na nguvu sawa. Lakini mwishoni mwa kipindi hiki, Papa alikuja kuwa ni mtu mwenye nguvu zaidi katika kanisa. Hii ilitokeaje? Ilitokea kwa miaka mingi na ilikuwa kwa sababu ya mawazo ya baadhi ya mapapa.

Leo Mkuu (c. 400–461 BK)

Leo alikuwa Papa kutoka mwaka 440–461 BK.Alisema kwamba nguvu ya upapa alipewa na Petro kutoka kwa Kristo na ile nguvu ilipitishwa kutoka kwa petro hadi kwa warithi wake. [1] Yeye alikuwa papa wa kwanza kutegemea nguvu kutoka kwa petro.Yeye aliwashawishi Wahani (wale ambao walitokea katikati mwa Asia) na Wavandali(wale ambao walitokea Mashariki mwa Ujerumani) sio kuvamia Roma.

Gregori Mkuu (c.540-604 BK)

Gregori alitokea katika familia ya kidini-Babu wa Baba yake alikuwa Papa. Alikuwa na elimu nzuri na alikuwa kiongozi wa serikali. Hakutegemea kufanywa papa mwaka590 BK,na aliendelea kuwa papa hadi kifo chake mwaka 604BK. Alijiita mwenyewe ni "mtumishi wa watumishi wa Mungu."

Kulikuwa na matatizo mengi Roma,na waliwasiliana na mtawala wa mashariki kwa ajili ya kuomba msaada. Mtawala alikuwa na matatizo yake ya kushughulikia,kwahiyo hakupeleka msaada Roma.Gregori aliamua kuyatatua hayo matatizo mwenyewe. Alichukua fedha kwa mhasibu wa kanisa kununua chakula kwa ajili ya watu na kushughulikia mifereji wa maji. Walambadi (ambao walikuwa wajerumani) walitawala sana Ulaya. Gregori alifanya mahusiano ya kidiplomasia na wao na kuwashawishi wasiivamie Roma. Kwa kutenda mambo haya ya serikali, Gregori alikuwa ni moja ya mapapa wa kwanza kuhamasisha nguvu ya kidunia ya upapa.Alisema urithi wa Petro ulimpa yeye nguvu ya kufanya maamuzi ya matatizo ya kimaadili.

Mchango wa Pippini (754 BK)

Walambadi walikuwa wakivamia tena eneo linalo zunguka Roma, na Papa stephano II hakutegemea msaada kutoka Byzantine (Mashariki) Himaya. Alitaka kutafuta kiongozi mpya wa kumsaidia matatizo haya. Aliomba msaada kutoka kwa Pippini mfupi, ambaye alikuwa mfalme wa Wafrenki (ambapo baadae iliitwa Ufaransa). Pippini alimuahidi kuwa atapigana na Walambadi na kurudisha ardhi ambayo waliichukua.

Mchango wa Konstantino

Hii ilikuwa hati ya uongo ambayo ilisemekana kuwa Costantino alimpa Papa Sylivesta aridhi iliyo izunguka Roma. Iliaminika kuwa Papa stephano wa II alitumia hati hii kumshawishi Pippini ili kumsaidia.

Charlemagne

Charlemagne alichukua kiti cha enzi 771 BK. Siku ya Christmas miaka 800, papa alimwita yeye mtawala. Tena alikuwa mtawala wa Wakristo. Bado maswali yalikuwepo juu ya kanisa au serikali ndiyo itakayekuwa na kiongozi mkuu.

Mabishano ya Kusimika (1076 BK)

Huu ulikuwa ni ushindani wa kiutawala kati ya Papa Gregori VII na Mtawala Henry IV. Serikali ilikuwa na mamlaka ya kuteua kiongozi wa Dini, hususani Papa. Henry alipaswa kuwa kiongozi alipokuwa na miaka sita tu, na viongozi wengine katika serikali walimsaidia kufanya maamuzi wakati anakua. Kanisa lilitumia faida kwa wakati huu kurudisha nyuma nguvu ya kuteua vingozi wa dini. Walijua Henry alikuwa mdogo kuwakataza wao. Katika mwaka 1059 waliunda baraza ambalo lilitangaza kuwa sifa hazitakuwa na sehemu katika kuchagua viongozi wa kanisa.

Katika mwaka wa 1075 BK Papa Gregori VII alijumuisha hati ambayo ilisema kuwa papa ana nguvu ya pekee ya kumtaja mtawala. Hivyo kanisa sasa halina nguvu tu ya kuwateua vingozi wao, lakini pia viongozi wa serikali. Kwa wakati huo Henry alikuwa mkubwa na alijibu kwa kusema kuwa Gregori sio papa tena na walifanya uchaguzi kwa ajili ya papa mpya. Gregori kisha alimtenga Henry. Mapigano haya ya nyuma na ya mbele yaliendelea kati hawa wawili kwa kipindi kirefu.

Innosenti III (1160–1216 BK)

Innosenti alipigana na viongozi wa serikali kwa ajili ya madaraka.

Mapantano ya Worms (1122 BK)

Huu ulikuwa mwisho wa ugomvi wa uwekezaji. Serikali na kanisa zilifanya makubaliano kuwa kanisa liteue viongozi wa dini. Kama tu kanisa litakuwa na migogoro kati yao serikali itasaidia kutatua huo mgogoro.

Uchunguzi Rasmi

Mahakama maalumu iliundwa mwaka 1200 kushughulikia waasi. Yoyote aliyepingana na kanisa alihesabiwa kama muasi waasi. Waasi waliwindwa na kufikishwa mahakamani na Viongozi wa viongozi wa kanisa.

Vita takatifu ambavyo pia huitwa vita vya Kidini vilidumu tangu mwaka 1095 hadi 1291 baada ya Kristo

Vita hivi vilikuwa ni jaribio la kanisa kuchukua nchi takatifu kutoka kwa Waislam

Kanisa iliweza kuwashauri watawala wa Ulaya kuongoza vita hivyo vya kidini. Kanisa walikuwa wanataka kuwafukuza Waislam kutoka Yerusalemu na kumpatia Papa mji huo kuumiliki.

Askari walishindwa kuichukua nchi takatifu kutoka udhibiti wa waislam

Mgawanyo wa mashariki-magharibi (1054 BK)

Orodha zifuatazo zinaonyesha baadhi ya tofauti kati ya makanisa ya mashariki na magharibi:

Mashariki Magharibi
Walizungumza Kigiriki Walizungumza Kilatini
Makuhani wao waliweza kuoa Makuhani wao hawakuweza kuolewa
Makuhani wao walikuwa na ndevu Makuhani wao hawakuwa na ndevu
Imani ya Nikia inasema Roho anakuja "kutoka kwa Baba" Ya kuongeza "na Mwana" (Inaitwa "Maneno ya Filioque")
Walikuwa na sherehe tofauti za Misa
Walikuwa na tofauti za Mafundisho

Papa Leo IX alimtaka Michaeli, Askofu Mkuu wa Konstantinopo, kutengana naye. Papa alituma wa wakilishi kwa Konstantinopo, lakini Mikaeli alikataa kukutana naye. Wawakilishi walimkataa Mikaeli kuongea naye na yeye kukataa kuongea nao.

Watu wengine wamejitenga na Kanisa Katoliki

Kulikuwapo na mabaki ya vikundi ambavyo havikuwa sehemu ya Kanisa Katoliki.

Waalbigeni walikuwa wakazi wa Albi huko Ufaransa watu hawa waliamini agano jipya ndilo lililotoa ujumbe na ya imani yao

Walimpinga Papa na kanisa Katoliki. Waalbigeni walipewa mateso makali na Papa Innocent III mwaka 1208 baada ya Kristo.

Waldensi walikuwa wenyeji wa Ufaransa, Italia na Uswisi

Walipata jina lao kumuenzi kiongozi wao aliyeitwa Perto Waldo ambaye alitafsiri Biblia kwa lugha ya watu hao. Waldo alifundisha kwamba maandiko matakatifu ndiyo mamlaka kuu kwa wakristo. Neno lao la wito lilikuwa, "Neno la Mungu linaongea na, ni busara tukitii."

Viongozi wakuu wa kipindi hicho

Bonifasi

Bonifasi alizaliwa katika 680 BK. Jina lake alilozaliwa nayo lilikuwa Winfred. Alifundishwa kama mtauwa wa Benedicto, na alitumia maisha yake mengi kama mmishenari kwa Wajerumani.

Wahenga walisema kwamba ukichukua shoka kuuendea mti uliyesimama kuusulubu kwa ngurumo ya mungu, ile radi itaupiga mti na utaanguka chini.

Anselm

Anselm alizaliwa kati ya 1033 BK. Mwaka 1903 William II, mwana wa William mshindi, alimfanya Anselm kuwa Mkuu wa maaskofu wa Canterbury, lakini alitaka kuweka nguvu kwa kumtaja Clergy. Anselm alikataa kumwachia William mamlaka haya, na yaliyotokea, yeye alitumia muda wake uhamishoni.

Henry I, kaka wa William wa II, alichukua nafasi baada ya kaka yake kufa, na alimwomba Anselm kurudi. Anselm hakuwa kiongozi kwa muda mrefu, angalau, na alienda kuishi uhamishoni tena. Aliweza kuandika mengi kwa kipindi hiki huko uhamishoni.

Thomasi Aquinas

Thomasi Aquinas alizailwa 1225 BK. Yawezekana alikuwa mwanatheolojia mkuu wa zama za kati. Yeye alisema sababu (zilizohusu wana falsafa wa zaman) katika theolojia yake.

Yohane Wykliffe

Yohane Wykliffe (1330—1384) alikuwa mtu wa kwanza kutafsiri Biblia kwa kiingereza. Anakumbukwa kama nyota ya asubuhi wa mageuzi. Alikuwa na wafuasi, waliyekuwa wanaitwa lollards, ikiwa na maana ya "wahubiri maskini." Alipingana sana na Kanisa Katoliki. Zifuatazo ni baadhi ya mambo aliyoyauliza juu ya kanisa:

  • Haki za kanisa kwa wagonjwa na utajiri
  • Kuuza vyeti vya upatanisho
  • Ibada ya Watakatifu na vifaa vilivyo tumika
  • Mamlaka ya papa
  • Kugeuka asili ya mwili na damu ya Yesu katika ushirika Mtakatifu.

Huyu angeuawa na kanisa katoliki kama mabwenyenye wa Uingereza hawakumpatia ulinzi. Mahubiri ya Wykliffe na tafsiri ya Biblia iliandalia njia ya mageuzi. Wakatoliki walimchukia sana Wyklif kiasi kwamba alipokufa waliutoa mwili wake kaburini miaka mingi baada ya kuzikwa na kuudhihaki.

Yohane Huss

Yohane Huss (1369—1415 BK) alikuwa msomi wa maandiko ya Wykliffe, na alikataa kabisa mamlaka ya papa. Alisisitiza kwamba Kristo pekee ndiye alikuwa kichwa cha kanisa na Mungu pekee ndiye asameheaye dhambi. Alipopelekwa mbele ya baraza kwenda kuulizwa maswali kuhusu imani yake, alisema, "Mimi sikuwa mhudumu mkuu, dhahabu hujionyesha kutokana na ukweli." Alihukumiwa kama muasi na alichomwa katika mchi kwa amri ya Baraza la Kanisa Kikatoliki.

Pertro Abelardi

Tano: Kanisa lililotengenezwa upya (1453–1678 BK)

Tangu anguko la Konstantino mpaka mwishoni mwa Vita vya miaka Thelathini.

Hawa ni wale waliokuwa wamebaki wakilipinga kwa ushupavu mafundisho ya uwongo. Hiki kilikuwa ni kipindi ambacho Mungu aliinua wanaume wakang'ara na kufunika lile giza la mafundisho ya uwongo.

Kipindi cha kuchipuka upya (Mvurumko)

Mwanga wa kujifunzia

Mvurumko nineno linaloeleza kuamka kwa Ulaya katika fani za elimu sanaa na sayansi. Haya ni mambo yanayohusiana na ustaarabu.

Mwanga wa neno la Mungu

Neno la Mungu liliiondoa Ulaya kutoka enzi ya giza. Siyo jambo la kushangaza kwamba ustaarabu ulirudi wakati neno la Mungu liliporudishwa kwa wanadamu.

Mashine ya uchapishaji ulivumbuliwa huko Gutenberg mwaka 1456 na kitabu cha kwanza kilichochapishwa ni Biblia (nakala 200 ya Vulgate Kilatini). Kuanzia hapo Biblia ziliweza kuchapishwa kwa wingi na kufikia mikono ya watu wa kawaida kwasababu ya uvumbuzi huu.

Majadiliano: Je, watu wa kawaida wanaweza kuelewa Biblia?

Mwanga wa ukweli

Mashine inayohamishika ya kuchapisha iligeuka chombo muhimu sana katika mageuzo ya kanisa. Wanamageuzi walichapisha vitabu na vitini vya kufundisha kupinga mafandisho ya Kanisa la Katoliki na uukweli kuhusu kuhesabiwa haki kwa imani. Vitini hivi vipya vilipata umaarufu na kusambazwa bara lote la Ulaya. Ilibid ivitabu vinakiliwe kwa mikono na waandishi kabla ya uvumbuzi wa mashine ya uchapishaji na sasa vitabu viliweza kusambazwa kwa haraka. Watu waliweza kusoma na kufanya uamuzi wao wenyewe kwa msingi wa ukweli si tu kwa kile alichosema kuhani.

Mageuzo

Mageuzo maana "yake ni rekebisha, geuza au ongeza ubora." Wanamageuzi walikuwa wakijaribu kuleta mabadiliko katika kanisa. Baadhi ya hao wanamageuzi hawakutambua kwamba Kanisa Katoliki la Katoliki lisingekubali mabadiliko. Walisimama imara na kupinga yale waliyofikiri walikuwa mafundisho ya uongo. Wanamageuzi walikuwa wakiwarudishia watu neno la Mungu kama lilivyo katika Biblia kwa lugha yao. Kanisa la Katoliki lilipinga usomaji wa Bibilia kwa mtu wa kawaida. Watu waliotetea ukweli waliteswa na ndipo wakaanza kufahamu kwamba Kanisa la Katoliki lisingebadilika kamwe. Waprotestanti ni jina walilopewa watu waliokataa mambo ya Kanisa Katoliki.

Mageuzo katika bara la Ulaya

Martini Luther (1483–1546) huko Ujerumani

Martini Luther anachukuliwa kuwa ndiye Baba wa mageuzo.

Aliweka tangazo lenye Hoja 95 katika lango kuu la kanisa la Askofu wa Wittenberg tarehe 31 Oktoba 1517. Hoja hizo zilionesha jinsi anavyopinga kanuni za Kanisa Katoliki. Alikana kile alichokiona kama mafundisho ya kanisa la uwongo na kukataa mamlaka ya papa. Nakala nyingi za tangazo lake hilo zilizochapishwa na zilienea haraka Ulaya na zikasaidia kuwasha moto mkali wa mageuzo.

Aliichoma nembo ya Papa. Nembo ya papa ni lakiri iliyoitwa kwa kilatini Bula. Neno hili la kilatini bula ambalo kwa kiingeraza ni bull linatokanana neno la kilatini lilitumiwa katika hati zote rasmi zilizokuwa na muhuri au lakiri yaani nembo ya papa. Mwaka 1520 papa alimtumia Martini Luther Bula (hati rasmi) ya kumtuhumu kwamba ameasi.

Martini Luther aliitwa kuhudhuria Diete huko mjini Worms. Diete ni baraza la utawala. Mnamo mwezi Juni 1521 Luther aliitwa mbele ya Diete la Mfalme huko Worms nchini Ujerumani. Alihakikishiwa na viongozi wa serikali wa Ujerumani kwamba atasafiri kwa usalama kwenda na kurudi Worms kuhudhuria baraza hilo. Aliamriwa na viongozi wakanisa Katoliki atubu. Luther alijibu ifuatavyo, "Hadi nitakaposhaurika kwa kuona ushahidi katika maandiko matakatifu au kwa sababu zilizo wazi, sitaweza kubadilisha msimamo wangu, kwa kuwa siyo salama au busara kufany akitu chochote kinyume na dhamira. Mungu anisadie. Amina."

Rafiki wa Luther, ambaye alikuwa kiongozi wa serikali, "alimkamata" Luther na kumtia katika Ngome la Wartburg kwa mwaka mmoja. Alifanya hili kulinda Luther kutoka kanisa. Katika mwaka huo, Luther alitafsiri Agano Jipya na sehemu ya Agano la Kale kwa Kijerumani ambayo ni lugha ya watu wake.

Ulrich Zwingli (1484–1531) huko Uswisi

Zwingli akawa mchungaji wa kanisa kuu katika Zurich tarehe 1/1/1519. Alisema atahubiri kupitia Injili ya Mathayo badala ya kutumia mtaala. Mwaka 1522 baadhi ya washirika wake wa kanisa walikula nyama wakati wa kwaresima, na aliwaunga mkono kwa kuhubiri juu ya uhuru. Makuhani waliweza kuoa chini yake, sanamu ziliondolewa kanisani, na ibada ilifanywa kwa huduma rahisi ambazo zilihamasiha mahubiri. Alichapisha kitabu kupinga Wakatoliki. Badala ya kuwa mchungaji, pia yeye alichaguliwa kuwa kiongozi wa jamii. Aliuawa katika vita ya wenyewe kwa wenyewe kisha Yohane Kalvini akaendelea na kazi hiyo ya kuhubiri injli.

Yohane Kalivini (1509–1564) huko Ufaransa na Uswisi

Kuzunguka miaka ya 1533 BK Yohana Kalvini alijitoa kutoka Ukatoliki, aliiacha nchi yake ya Ufaransa, na kuishi Uswisi kama mhamiaji. Mwaka 1536 alichapa toleo la kwanza la Katiba ya Dini ya Kikristo.

Yohane Kalvini alikuwa ni mhubiri aliyekuwaa mwazi na mwandishi ambaye alihubiri ukombozi kwa imani akisisitiza mamlaka ya Injili. Kalivini akafundisha kwamba kufanikiwa ni kwa wateule tu. Alisema, "huwezi kumtenga Mungu au kumweka yeye katika deni lako. Yeye alikuokoa; usingeweza kufanya hinyo mwenyewe." Mafundisho ya Calvin ya Mungu kutujua tangu mwanzo ni ni kuimarika kwa Arminianism, ambaye walijikita juu ya imani ambayo mtu yeyote anaweza kuokolewa kama ataamini.

Kalvinism Arminianism
Kumnyima kamili
Watu wote ni wenye dhambi sana hata hawawezi kumwamini Mungu
Utashi huru
Wanadamu wanaweza kuchagua mema au mabaya
Masharti ya kutochaguliwa (wateule) Masharti kuchagua (kuteuliwa)
Ukombozi kwa wateule Ukombozi kwa wote
Pingamizi kwa neema Roho Mtakatifu anaweza kukuzuia
Huwezi kupoteza wokovu (utakatifu) Waweza kupoteza wokovo

Jakizi Lefeve (1455–1536) huko Ufaransa

Aliandika kitabu kiitwacho Kustahili kwa sababu ya Imani mwaka 1512 na akahubiri ukombozi kwa imani. Alitafsiri Biblia nzima katika Kifaransa. Yeye kamwe hakujitenga rasmi na Kanisa Katoliki.

Uuaji wa Siku ya Bartholomew Mtakatifu (1572)

Waprotestanti ulikua nchini Ufaransa ingawa kulikuwa na upinzani kutoka kwa serikali. Waprotestanti wa Ufaransa waliitwa Wahuguenote. Wahuguenote ziliongozwa na admiral Coligny, na walitaka uhuru wa kidini. Wakatoliki wa Ufaransa waliongozwa na familia ya Guise, ambao waliamini mila ya Kifaransa ya "mfalme moja,imani moja, sheria moja." Katika miaka kumi inayoongoza kwenye mauaji, Ufaransa ilikuwa na vita vitatu vya kidini. Vikundi vyote viwili vilitumia vurugu kujaribu kupata kile walitaka.

Mnamo Agosti 18, 1572, mkuu wa Kiprotestanti, Henri wa Navarre, aliolewa Margaret Mkatoliki wa Valois. Mfalme alitumaini kuwa ndoa italeta amani.

Mnamo Agosti 22 mtu alijaribu na kushindwa kumwua kiongozi wa Huguenot, Coligny. Wahuguenote walikasirika na shambulio hili.

Mnamo Agosti 23 mfalme aliamua kuwa Wahuguenote wote wanapaswa kuuawa, na mnamo Agosti 24 mauaji yalianza kabla ya 4 asubuhi.

Waprotestanti elfu ishirini waliuawa kwa siku hiyo, and hiyo ambayo inakumbukwa kama "Uuaji wa Siku ya Bartholomew Mtakatifu." Viongozi wengi wa Waprostanti waliuawa katika mauaji hayo na Waprotestanti wengine mengi waliikimbia nchi kwa usalama wao.

Waanabaptisti (1525) huko Uswisi

Kujaribu kuzuia mgawanyo, Wajerumani walijigawanya katika nchi za kidini. Baadhi ya nchi zilikuwa Katoliki na zingine zilikuwa Lutherani. Hii ilikuwa ni kwasababu kwa wakati huu, watu walilichukulia kanisa na serikali kama ulikuwa muungano.

Hii pia ilikuwa kweli katika sehemu zingine za Ulaya. Huuko Uswis, kundi la Wakristo hawakuwa na furaha kuwa mamlaka ya Rumi yalichukuliwa na mtawala mwingine wa kidini wa serikali (akiitwa kiongozi wa Zurich). Walitaka udugu badala ya nguvu ya umma. Walizoea demokrasia ya mkusanyiko. Kila moja anaweza kuzungumza kwa Mungu, siyo maaskofu pekee na wanabaraza.

Kundi hili pia lililenga juu ya wokovu binafsi. Januari 21, 1525, kundi hili lilikutana na kubatizana. Hii ilikuwa kinyume cha mafundisho maalum ya kanisa la Zurich, ambayo walisisitiza ubatizo wa watoto. Hawa watu walikuja kujulikana kama Waanabaptisti, wakimaanisha "kubatizwa tena," kwasababu tayari walishabatizwa kama watoto.

Mageuzo huko Uingereza na Uskochi

Sheria ya Ukuu wa Henry VIII (1534)

Mnamo mwaka wa 1521 Henry alishambulia maoni ya Luther juu ya sakramenti, na hivyo papa akampa jina "Mlinzi wa Imani." Ni karibu na kupendeza kwamba papa alimpa jina hili, kwa sababu kwa muda mfupi tu, Henry angeondoka kabisa na shirika ambalo lilimpa jina hilo.

Baada ya kifo cha ndugu yake, Henry alioa shemeji wa kike, Catherine wa Aragon. Hawakuwa na mtoto wa kiume pamoja, na hivyo Henry alitaka kufuta ndoa yake na kuoa Anne Boleyn. Alitumia Mambo ya Walawi 20:21 ili kupatikana kesi yake kwa talaka.

Papa hakumpa talaka, na hivyo Henry alimteua Askofu Mkuu wa Canterbury Thomas Cramner. Askofu Mkuu mpya alimpa talaka aliyokuwa anaitaka. Henry alitangaza kwamba mfalme wa Uingereza alikuwa kichwa cha kanisa.

Henry alikuwa na binti wawili. Maria alikuwa Mkatoliki, na Elizabeth alikuwa Kiprotestanti.

Watakasjiaji na Watawanyishi huko Uingereza

Mfalme Henri wa VIII (1491–1547) iliondoa Kanisa Katoliki huko Uingereza na kuanzisha kanisa la Anglikana. Waliolikataa kanisa hilo la dola waliitwa waasi. Wengi wa waasi hao hasa wachungaji waliofanya kazi yao bila leseni walitupwa magerezani. Kulikuwepo na vikundi viwili vya waasi: Watakasaji na Watawanyishi. Watawanyishi walikuwa ni wale waliotaka kujitenga na kanisa la Anglikana. Watakasaji walikuwa ni wale waliotaka kanisa la Anglikana litakaswe.

Yohane Bunyani (1628–1688) huko Uingereza

Yohane Bunyani alikuwa mhubiri shupavu kati ya waasi. Alihubiri ukombozi kwa neema kwa njia ya imani ndani ya Yesu. Bunyani alifundisha bila idhini ya Serikali na alifungwa kwa miaka 12 kwa sababu ya kuhubiri injili. Aliandika kitabu kiitwacho Safari ya Msafiri ambacho kinaendelea kuchapishwa hadi leo.

Yohane Knoksi (1510–1572) huko Uskochi

Sala yake Knoksi iligeuka kuwa "Nipatie Uskochi au la nife." Alikuwa mwanafunzi wa Kalvini. Alimpinga Malkia Maria wa Uskochi ambaye alikuwa mkatoliki. Vita vya kimwili halisi vilipiganwa kati ya wanaume wa malkia na Waprotestanti. Aliliongoza Bunge kuharamisha misa ya katoliki mwaka 1560. Kanisa la kiprotestanti la Uskochi liitwalo kanisa la Presbaiteriani liligeuzwa kuwa kanisa la dola mnamo mwaka 1567.

Wanamageuzi katika Dunia Mpya (Amerika)

Wasafiri wale waliofika katika Dunia mpya walikuwa ni watawanyishi kutoka Uingereza. Walitia nanga katika Dunia Mpya mwaka 1620. Walifuata uhuru wa kuabudu na kuachana na unyanyasaji wa Kanisa la Anglikana. Walizindua HATI YA MAYFLOWER ambayo ilikuja kuwa ndio hati ya kwanza ya serikali ya ndani ya Dunia Mpya.

Mabadiliko ndaniya Kanisa Katoliki

Baraza la Trenti (1545–1563)

Kusudi kuu la baraza lilikuwa kushughulikia masuala na maswali yaliyotolewa na wafuasi wa Kiprotestanti. Matendo ya wafuasi walilazimika Kanisa Katoliki kutambua kwamba kulikuwa na masuala katika kanisa ambalo lilihitaji kushughulikiwa. Baraza ya Trent ilifanyika katika hatua tatu kati ya 1545 na 1563. Kufuatia ni baadhi ya maamuzi na matokeo kutoka kwa baraza:

  • Walifanya mageuzi kwa wachungaji. Waliamua kuwa maaskofu wangeweza kushikilia ofisi moja tu, ili waweze kuzingatia makutaniko yao.
  • Walisema kwamba Maandiko na mila zina mamlaka sawa.
  • Waliweka nafasi ya "aliongoza utakatifu" kwa haki. Hii ina maana kwamba Mungu anampa mwamini fursa na nguvu ya kuwa nzuri, na ni kwa muumini kujibu.
  • Walithibitisha sakramenti saba, ambazo ni ubatizo, uthibitisho, Ekaristi, uvunjaji, unction kali (upako wa wagonjwa), amri takatifu, na ndoa.
  • Walisema wazi mafundisho ya ibada ya watakatifu. Walisema kwamba sanamu za watakatifu hawakupaswa kuabudu kwao wenyewe, bali kwamba kulikuwa na ukweli wa kiroho zaidi ya vitu vya kimwili.

Wachungaji waliobadilishwa (Wayesuiti)

Wayesuiti ambao mwanzoni walijulikanakama "wachungaji waliobadilishwa" walisafiri na kiongozi wao mkuu Inyasi wa Loyola aliyepatikana kwa uchaguzi hadi Roma ambapo walitoa huduma yao kwa Papa mwezi Oktoba 1534.

Kabla ya kutawanywa sehemu mbalimbali alizowatuma Papa Paulo III aliandika amri yake (Bula) iliyojulikana kama Regimini militalis Ecclesiae (Kwa kilatini maana yake; kwa serikali ya kijeshi ya kanisa) ikiwa ni tangazo lake kwamba amewakubali Wayesuiti ambao wanaendelea na shirika lao hilo hadi leo. Wayesuiti waliongoza mapambano dhidi ya wanamageuzi kuwapinga Waprostestanti.

Majadiliano: Je, lini kuwatenganisha nani na wengine ambao wanaamini tofauti na wewe? Je, tunapaswa kushirikiana na watu ambao wanaamini tofauti kuliko sisi?

Sita: Kanisa la Kisasa (1678–c. 1950 BK)

Kuanzia mwisho wa vita ya miaka thelathini ya mwaka 1678 hadi miaka ya 1950.

Uamsho Mkubwa (wa miaka ya 1700)

Uamsho mkubwa unahusishwa nakuanzishwa upya jitihada za kuieneza injili Uingereza na Marekani.

Georgi Whitefield (1714–1770)

Bwana Whitefield ambaye alikuwa mhubiri shupavu wa injili iliyokuwa katika lugha rahisi tangu akiwa naumri wa miaka 24, alipingwa marufuku kuhubiri katika kanisa la Anglikana. Aliamua kufundisha mitaani na kufanya viwanja vya wazi kuwa mahali pake pa salana akahubiria maelfu ya watu. Huu ulikuwa mwanzo wa uamsho katika maeneo ya Magharibi ya Uingereza. Alihubiri Uingereza na Marekani.

Yohane Wesley (1703–1791)

Dunia ilikuwa ndio parokia yake. Aliwahubiria watu kwa maelfu katika maeneo ya wazi. Alihubiri kote Uingereza na Marekani akianzia katika makanisa kadhaa. Yeye ndiye mwanzilishi wa Kanisa la Methodisti.

Jonathani Edwardi (1703–1758)

Alikuwa mchungaji eneo la Northampton, Massachusetts akiwa na umri wa miaka 17. Mwaka 1741 alisoma hotuba yake maarufu yenye kichwa cha habari "Watenda dhambi wakiwa mikononi mwa Mungu aliyekasirika" mbele ya waumini wake. Imani ya ajabu iliwapata waumini wake kiasi kwamba walihubiri na kuongoza uamsho ulioenea Uingereza yote mpya.

Kuzinduka kwa ajabu kwa mara ya pili (miaka ya 1820)

Huu ulikuwa ni muondoko mwingine wa Mungu wa kuwasha moto wa matumaini uliosambaa hadi Uingereza.

Charles Finney alikuwa mstari wa mbele katika kuwasha moto wa uamsho mkubwa huko Marekani

Katika miaka ya mwanzoni ya 1820 Finney alihubiri katika mikutano ya injili huko New York ambayo iliwasha moto wa uamsho kwa mara ya pili. Finney alikuwa ni mtu wa imani kali na mwinjilishaji shupavu wa neno la Mungu. Finney ameelezewa mara nyingi kama mwinjili anayeongoza wengine wote wa kutoka Amerika.

D. L. Moody

Moody aliitetemesha Marekani na Uingereza kwa ajili ya Mungu. Alihubiri Injili vizuri kwa Lugha ya watu wakawaida. Inakadiriwa kwamba roho za watu milioni moja ziliokolewa katika huduma yake. Alianzisha chuo cha Biblia cha Moody ambacho kinaendelea kuwepo hadi leo.

Charles Spargeoni

Spargeoni alikuwa ni Mwana wa mfalme wa wahubiri na alikuwa mchungaji wa Kanisa la Kibaptisti tubernakulo mjini Londoni. Aliwahubiria zaidi ya watu 5000 kwa saa 40 kila wiki.

Mungu alikuwa anarudisha mahubiri ya msalaba kwa kanisa lake

Mwenendo wa kisasa kwa kazi za misheni

Hiki ni kipindi cha uamsho mkubwa na jitihada nzito za kimisionari. Dunia ilikuwa ni mlango uliokuwa wazi kwa wamisionari.

Marko 16:15—Naye akawambia enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri injili kwa kila kiumbe. (Mathayo 28:19–20)

William Carey (Uhindi)

William Carey (1761–1834) ni baba wa Umisionari wa kisasa. Alikuwa Mwingereza maskini. Kipindi fulani, alitembea kilomita 13 kila Jumapili kuhubiri kanisani. Alijaribu kuwashawishi watu kwenda kuhubiri katika nchi nyingine, lakini wakasema, "Ikiwa Mungu anataka kuokoa wapagani, atafanya hivyo, bila msaada wako au wangu."

Alikwenda kwa Uhindi 1793. Huyu ndiye misionari wa kisasa kwanza aliwasili nchini Uhindi. Huko, hakuona waongofu kwa miaka saba. Hakuwa na muda mwingi akilaani dini ya Hindu, lakini badala yake alitumia wakati wake akizungumza juu ya Yesu, kifo chake, na Ufufuo Wake. Huyu ndiye mmisionari wa kwanza kufika nchini Uhindi. Maneno mazuri yake ni, "Anatarajia mambo makuu kutoka kwa Mungu, jaribu mambo makuu kwa Mungu."

Adoniramu Judsoni (Burma)

Aliowa 5 Februari, 1812, na ndani ya wiki mbili walikuwa katika mashua kuelekea Uhindi kutoka Marekani. Walianza safari ya kufanya kazi kwa Kanisa la Congregational, lakini kwa sababu Adoniram alifikiri kuwa Kanisa la Congregational lilikuwa baya kuhusu ubatizo, alimshawishi mkewe na mshirika mwingine aliyekuwa pamoja nao kuwa Wabatisti. Alipeleka barua ya kujiuzulu walipofika Uhindi. Mshirika huyo alichukua barua hiyo, na akajaribu kuongeza fedha kutoka kwa Wabatisti.

Serikali ya Uhindi haikuwaacha wapate kukaa huko, na William Carey alipendekeza kuwa wanapaswa kwenda Burma. Walipofika Burma, walianza kujifunza lugha, walifungua shule kwa wasichana, na walitafsiri Agano Jipya. Ilikuwa miaka sita kabla ya kuwa na Mkristo wao wa kwanza kubadilisha. Adoniram alitumia miaka miwili jela. Ann, mke wa Adoniram alikufa akiwa na umri wa miaka 36. Judson alianzisha makanisa 63, hasa kati ya kabila la Karen.

Daudi Livingstone (Afrika)

Anaelezwa kama mtafuta njia barani Afrika. Alijitolea kusafiri hadi ndani kabisa ya bara la Afrika ambako hakukuwa na mzungu yeyote aliyekwisha fika huko kabla yake. Alitumikia miongoni mwa watu wa Tswana kwa miaka kumi, lakini aliona mtu mmoja tu aliyebadilishwa. Alifungua vituo vya misheni na alifanya mengi kuinadi injili barani Afrika.

Hadsoni Taylor (Uchina)

Alianzisha kituo cha Misioni ndani ya Uchina na kikundi chake kilihubiri injili hadi katikati ya nchi hiyo. Alikua na ndevu, alikua na nywele zake kwa muda mrefu, na yeye alisuka nywele zake, ambao ulikuwa mtindo wa wanaume nchini China wakati huo. Yeye alisema, "Sio kuuhamisha utaifa wao, bali tunataka wao kuwa Wakristo." Aliwaweka wamisionari 849 vituoni, kuanzisha vituo vya wamisionari 205, na jamii yake ya umishonari ilikuwa na waongofu 125,000 kwa Ukristo.

Majadiliano: Je, wamishonari husaidia au kuumiza watu wa ndani?

Uamsho wa Mtaa wa Azuza (1906)

Kuanza kwa karne ya 20 kulishuhudia mbubujiko wa Roho Mtakatifu huko Los Angeles katika California, Marekani. Mungu alikuwa analirudishia Kanisa Pentekoste upya.

Wahubiri wengine muhimu

Billy Sunday

Billy Sunday alisimama imara kupinga ulevi na alikuwa ni mhubiri shupavu wa injili.

Smith Wigglesworth

Smith Wigglesworth alikuwa Mtume wa Imani ambaye alikuwa na huduma kubwa ya uponyaji.

Uamsho wa Mahemani wa miaka ya 1950

Oral Roberts, A. A. Alan, Jack Coe, na William Branham walizunguka Amerika na mahema makubwa na wakahubiri. Jack Coe alikuwa mtu wa imani kali. Aliweza kuvunja magongo ya walemavu na kutupa mbali mikongojo wakati alipoombea wagonjwa.

Saba: Kanisa la Baada ya Kisasa (1950—leo)

Kuanzia mwaka wa 1950 wa Kristo hadi leo

Kanisa linaendeshwa kwa sanduku la kura

Laodeshia maana yake utawala wa watu wenyewe. Makanisa mengi ya leo yanaendeshwa na watu wenyewe. Jina la kipindi hiki linaelezea serikali ya kisasa. Kanisa haliongozwi tena na Mungu ila linaendeshwa na watu ambao wanafanya mambo kwa njia zao binafsi watakavyo.

Kanisa la karisma

Kuna upako wa mafuta wakilaghai (Mat. 24:5)

Yesu alikwishaonya kwamba watatokea waongo watakaojiita Kristo katika siku za mwisho. Neno Kristo maana yake mpakwa mafuta. Siku hizi wapo wapakwa mafuta wengi wa uongo wasiokuwa na uhusiano wowote na Mungu.

Wapo manabii wa uongo (Mat. 24:11, 24)

Yesu alisema watakuwepo manabii wa uongo ambao watadanganya wengi. Kati ya wanakarismatiki wa siku hizi kuna manabii wengi wa uongo. Wanaondoa tendo la upako wa mafuta unaofanywa na Roho Mtakatifu.

Vuguvugu la ukarismatiki lilianzia ndani ya Kanisa Katoliki

Kanisa la anasa na rushwa

Injili ya mafanikio imeshaiondoa injili ya Yesu Kristo katika makanisa mengi ya kisasa

Wahubiri wengi wa injili wa kisasa wanafundisha mambo ya mafanikio wa kupata fedha na faida nyingine. Watu wanashauriwa kwa maneno kama, "Otesha mbegu yako kwa mategemeo ya kujipatia mavuno makubwa." Wanaambiwa wakitoa watabarikiwa mara mia. Wanaambiwa watamke watakavyo wabarikiwe.