Skip to main content

Sura ya 2: Umoja kamili wa Biblia

Umoja Kamili wa Biblia

  • Ukombozi ni Dhamira moja Kuu ya Biblia.  
  •  
  • Ukombozi ni tendo la kununua au kulipia kwa ukamilifu.

Mwanadamu amekombolewa kwa damu ya Yesu Kristo. Yesu ameshalipa kikamilifu  kwa damu yake iliyomwagwa msalabani bei ya ukombozi wa mwanadamu.  Wokovu kwa Damu ya Yesu ndio dhamira kuu ya Biblia. Dhamira hii inapatikana tangu kitabu cha Mwanzo mpaka Ufunuo. Ahadi ya kwanza ya ukombozi imetolewa katika Mwa. 3:15. Nami nitaweka uadui kati yao na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huu utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.

Huu ni utabiri kwamba Yule Masiha ambaye atakuja kutokana na uzao wa mwanamke siku moja atakiponda kichwa cha nyoka. Mada hii inaendelea mpaka kitabu cha Ufunuo.

 

Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukatukomboa kwenda kwa Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa; - Ufunuo 5:9  Andiko hili linahusu kufufuka kwa Kristo aliyetukomboa kwa Damu Yake.

  • Mkombozi wetu Kristo ndiye Mtu muhimu katika Biblia.

Sadaka za kumwaga damu katika Agano la Kale zilikuwa ni aina inayofanana na Yesu ambaye ni Mwanakondoo aliyechinjwa kabla ya misingi ya ulimwengu. Wakisema kwa sauti kuu, Anastahili Mwana – Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka. (Ufu. 5:12)  Agano la Kale huangalia mbele kwa imani katika msalaba wa Kristo. Injili hii inamuonesha Kristo na Kifo chake juu ya msalaba. Agano Jipya huangalia nyuma katika kazi iliyomaliziwa katika msalaba.  Kristo hujidhihirisha mwenyewe katika Agano la Kale kwa nyakati tofauti na kwa njia mbalimbali.Kristo ameelezwa kwa namna ya kinabii kuwa ni Masiha ajaye.

Tangu Adamu hadi Abrahamu tunaona ______________ mwanzo wa jamii ya mwanadamu. Mwanzo 1:26, 27,  4:1,  5:1-5 ,32;  6:9, 10 ;  7:17-23; 9:1; 11:10, 27.

Kizazi_____ taarifa ya historia ya ukoo wa mtu somo la mtiririko wa familia

 

Tangu Abraham mpaka Kristo tunaona____________ mwanzo wa kabila teule. Taifa la waebrania .

Mwanzo 12:1,2;  22:15-18;   32:9-12;  Yoshua 1:1-3;  Mathayo 1:1, 2, 16 [Taifa hili lilianzishwa na kulelewa na mungu ili kumleta mwanadamu ulimwenguni.]

 

Tangu Kristo na kuendelea tunaona _________ Mwanzo wa kanisa. Mathayo 16:18; matendo 2:47;  11:26

 

Tunapata mwonekano wake katika kila ukurasa, katika maandishi matakatifu yaliyochirwa kwa Nuru, Mkombozi, Nabii, Kuhani.

 

 

II Biblia Haipingani.

  •  
  • Hakuna kosa katika Biblia. Biblia ni Neno la Mungu la hakika. Neno la Mungu halina makosa au mgongano. Biblia ni sahihi na kamili. Biblia ni sahihi kihistoria na kisayansi. Hakuna mgongano kati ya sayansi ya kweli na Biblia. Taarifa ya kweli ya historia na taarifa za ugunduzi zinakubaliana kikamilifu na Biblia.     
  • Kuna utulivu kamili katika Biblia yenyewe. Kilichoandikwa katika sehemu moja ya Biblia kinaoana na kilichoandikwa katika sehemu nyingine ya Biblia. Upo umoja kamilifu ndani ya Biblia yenyewe.  

 

  • III Biblia ina umoja

 

  • Biblia ina umoja katika unabii

 

  • Agano la Kale linao unabii mwingi. Unabii ni tangazo la tukio ambalo litakuja kutokea.  Ni historia ambayo imeandikwa mapema. Utabiri wote huo unakubaliana na kila mmoja wapo. Baadhi ya unabii katika Agano la Kale umeshakamilika katika tarehe za baadaye katika Agano la Kale. Unabii mwingi katika Agano la Kale ulielezea ujio wa Masiha.
  • Agano Jipya limekamilisha mambo mengi yaliyotabiriwa katika Agano la Kale. Unabii huo ulikamilishwa vya kutosha bila upungufu. Msisitizo wa Nabii katika kila kitabu unaoana na kila unabii mwingine.  

 

  • Biblia ni umoja katika mafundisho.

 

  • Mafundisho ni ukweli wa msingi wa Biblia uliopangwa kwa mfumo sahihi. Ukweli wa Biblia umeendelea kuwa ule ule katika Neno la Mungu lote. Kuna uelewano mmoja ulio sahihi kwa Kanuni ya Biblia. Umoja huu umeendelezwa kutoka Agano la Kale hadi katika Agano Jipya. Biblia ni taarifa sahihi iliyofunuliwa kwa mwanadamu ikiwa na uelewano wa kutosha kwa kila mafundisho na ukweli.
  • Biblia ni umoja kamili wa ukweli. Ukweli haubadiliki. Kamusi ya Webster inafafanua ukweli kama: Kukubaliana na hali halisi kwa ukamilifu kwa kuzingatia kitu kilichopo, au kilichokuwepo au kitakachokuwepo.  Ukweli wa Biblia unabakiwa kuwa sawasawa kuanzia kitabu cha Mwanzo mpaka kitabu cha Ufunuo.    

Uwatakase kwa ile kweli; Neno lako ndiyo kweli. - Yohana 17:17

 

  • Biblia ni Umoja kwa Kusudi.

 

  • Kusudi la Biblia ni kuonesha mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu. Biblia inaonesha mpango wa Mungu katika nyakati zote. Neno la Mungu hutoa maagizo na mwongozo kwa roho za wanadamu. Mpango wa ukombozi unaoneshwa kwa mwanadamu katika Biblia.  
  • Kila kitabu cha Biblia hutanguliza lengo moja la Biblia. Mungu ameonyesha mapenzi yake kwa watu mbalimbali katika vipindi tofauti katika Biblia yote. Biblia nzima huongoza wanadamu kwa Kristo na mpango wa ukombozi ambao ni dhamira kuu ya Biblia.

 

 

 

  • Biblia ni Moja kwa Umbile.
  • Kila agano limeundwa kwa sehemu tatu kuu – historia, maagizo, na unabii.
  • Ipo Biblia moja yenye Agano Jipya na Agano la Kale.

           

Jipya liko katika la Kale ndani yake; la Kale limeelezewa katika Jipya;

 Jipya liko katika la Kale linefichwa; la Kale ni katika Jipya limeoneshwa;

Jipya liko katika la Kale limetangulia kuoneshwa; la Kale liko katika Jipya limekomaa.

         “Huu mtungamano wote wa Biblia katika maelezo na mchoro, kwa uelewano wake utulivu na uthibitisho unaoelewana ungekuwa kunaonekana wazi kama ingekuwa umekamilishwa na kikundi cha wasomi waliofanya kazi pamoja wakiwa na mawasiliano ya kudumu ya habari na mawazo. Hata katika hali ya namna hioyo ambapo kila mwandishi angegawiwa sehemu iliyohaririwa na bingwa wa mawazo na ikapitishwa na kikundi kipana umoja uliounganishwa wa maandiko hayo ungekuwa ni mafanikio ya ajabu.  LAKINI, Biblia haikuandikwa kwa njia hiyo!  Iliandaliwa na waandishi 40 au zaidi ambao waliishi katika kipindi kinachozidi miaka 1600 katika nchi 13 tofauti ndani ya mabara 3 ambao waliandika kutoka katika maeneo na ujuzi usiofanana kabisa. Walikuwa wachunga kondoo, wafalme, wanajeshi, wana wa wafalme, makuhani, wavuvi, wasomi, wanahistoria, watalaam na vibarua wa kawaida. Kazi yao ilifanyikia maporini, majangwani, mapangoni, makasri, magerezani, kwenye meli na nyumbani. Waliandika kuhusu mada nyingi kwa mbinu tofauti katika angalao lugha tatu. Hata hivyo pamoja na tofauti za namna hiyo na matatizo yaliyotokana na kazi zao mbalimbali walichofanya kinaoana kwa hakika na ni sare, inayoonekana kuandaliwa moja kwa ajili ya nyingine.”

 

Kristo katika Vitabu 66 vya Biblia

 

Katika Mwanzo, Yeye ni uzao wa mwanamke 3:15

Katika Kutoka, Yeye ni Mwanakondoo  wa Pasaka 12:1-28

Katika Mambo ya Walawi, Yeye ni Sadaka ya upatanisho 1:14

Katika Hesabu, Yeye ni Mwamba, na yule Nyoka wa Shaba 20:8-11; 21:8,9

Katika Kumbukumbu, Yeye ni Nabii ambaye Atakuja 18:15,18,19

Katika Yoshua, Yeye ni Amiri wa jeshi la Bwana 5:13-15

Katika Waamuzi, Yeye ndiye aliyewakomboa watu wa Mungu 2:16,18

Katika Ruthu, Yeye ni  Mkombozi wa jamii 4:1-10

Katika I Samweli, Yeye ni Mpakwa mafuta 16:10-17

Katika II Samweli, Yeye ni Mfalme Aliyetawazwa 5:3-5

Katika I Wafalme, Yeye ni utukufu unaolijaza hekalu 8:10,11

Katika II Wafalme, Yeye ni uzao wa  kifalme aliyeokolewa kutoka kwa mchinjaji 11:1-3

Katika I Mambo ya Nyakati, Yeye ni Mfalme Mtukufu 11:2,3; 14:17

Katika II Mambo ya Nyakati, Yeye ni Bwana aliyemtokea Sulemani 7:12

Katika Ezra, Yeye ni Mtawanyaji Mkuu wa wanadamu ch.10

Katika Nehemia, Yeye ni Mrejezi mpya wa Taifa la Israeli 2:5

Katika Esta, Yeye ni Wakili wa watu wake 7:2-4

Katika Ayubu, Yeye ni Mtetezi aliye hai na sauti katika upepo wa kisulisuli 19:25; 38:1

Katika Zaburi, Yeye ni Mchungaji, ni Mwana, ni Mfalme wa Amani,

ni Mungu wa Majeshi, ni Mwenyezi Mungu       23:1; 2:12; 24

Katika Mithali, Yeye ni Hekima na ni rafiki akaaye karibu kuliko ndugu Mt.8,9; 18:24

Katika Mhubiri, Yeye ni Msingi wa Uhai Mhu.12

Katika Wimbo ulio Bora, Yeye ni Bwana Harusi Mtukufu

Katika Isaya, Yeye ni Imanueli, Mshauri wa Ajabu, Mwenye Nguvu,

Baba wa Milele, Mfalme wa Amani, na Bwana wa Mateso

alichubuliwa kwa maovu yetu 9:6; 53:3-6

Katika Yeremia, Yeye ni mfinyanzi wa Kimungu, Chipukizi la Haki, na

BWANA ambaye ni haki yetu 18:1-6; 23:5; 23:6

Katika Maombolezo, Yeye ni Yehova anayesikitika ambaye huwalea watu wake 1:1-6

Katika Ezekieli, Yeye ni Utukufu wa Bwana na ni yule

  Mfalme atakaye kuja 10:4,18;11:23; 44:4 21:26,27; 37:24

Katika Danieli, Yeye ni Jiwe Lililokatwa bila kazi ya mikono, ndiye Mtu

wa nne katika lile tanuru la moto, katika siku za zamani 2:34; 3:25; 7:22

Katika Hosea, Yeye ni mtoto aliyeitwa toka Misri 11:1

Katika Yoeli, Yeye ni Simba aungurumaye kutoka Sayuni 3:16

Katika Amosi, Yeye ni Hakimu wa Mataifa 9:8

Katika Obadia, Yeye ni Mfalme wa Ufalme utakaokuja 1:21

Katika Yona, Yeye ni mjumbe wa Bwana kwa Mataifa 1:1,2; 3:3-5

Katika Mika, Yeye ni Mtoto wa Betlehemu mtawala wa Israeli 5:2

Katika Nahumu, Yeye ni Ngome katika siku za tabu 1:7

Katika Habakuki, Yeye ni Bwana wa hekalu Lake takatifu 2:20

Katika Sefania, Yeye ni Mfalme wa Israeli 3:15-17

Katika Hagai, Yeye ni Bwana wa majeshi, ni Tamanio la mataifa 2:7

Katika Zekaria, Yeye ni Mfalme aliyepanda mwana punda na

ni Mchungaji Aliyepigwa   9:9; 13:7

Katika Malaki, Yeye ni Mjumbe wa Mungu, na Jua la Uchamungu

linalochomoza kwa uponyaji katika mbawa Zake 3:1; 4:2

katika zile Injili Nne, Yeye ni Mungu – Mtu akifundisha, akiponya, akihubiri,

akifa, na akifufuka tena Yoh.1:14; Mt.9:35; Lk.23:44-46;Mk.16:5,6

Katika Matendo, Yeye ni Bwana Aliyeshuka akiwa kazini ulimwenguni kwa

Roho Yake 1:8,9

Katika Nyaraka, Yeye ni Kristo katika mkono wa kuume wa Baba Mpatanishi

wetu, Kol.3:1; I Tim.2:5; Ebr.7:25; I Yh..2:1

Katika Ufunuo, Yeye ni Mshindi wa dhambi na kifo anayerudi katika utukufu 19:11-16