Skip to main content

Sura ya 4: Kanoni za Biblia

 

Kuorodheshwa kwa vitabu vya  Biblia

 

Mchakato wa ukusanyaji wa vitabu vya Biblia katika mfumo wake wa sasa ndio kunakoitwa: kuorodheshwa kwa vitabu vya Biblia. Jambo hii halikufanyika kwa siku moja.  Ikumbukwe kwamba kila kitabu kimoja ilibidi kiandikwe kwa mkono na kwa umakini mkubwa.  Vitabu hivyo vilitumiwa na kusambazwa na viongozi wa dini wa siku hizo.  Kulikuwepo pia vitabu vingine vilivyodai kuwa na uvuvio ambavyo havikuingizwa katika Biblia. Kulikuwepo na vitabu vya dini na historia ambavyo vilikuwa vinasambazwa wakati wa kuamua ni vitabu gani viingizwe katika Orodha hiyo. Mchakato huu wa kutambua vitabu vyenye uvuvio na vipi havina ndio jambo tutakaloangalia katika somo la sehemu hii.  Tutajaribu pia kulijibu swali: Biblia iliwezaje kufikia katika hali iliyo nayo sasa?

 

  • Ufafanuzi Kuhusu Kanoni

 

  • Neno Kanoni linatokana na mzizi wa neno mtete.  
  • Jani la mtete lilitumiwa kama kifaa cha kupimia.  Neno lake la Kingereza ni fimbo (cane) na Kiyunani ni kanuni. Neno kanuni maana yake ufito, rula au kifaa cha kupimia urefu. Kiongozi wa kanisa la karne ya 3 aitwaye Origeni alitumia neno kanuni akimaanisha kipimo cha imani.

 

  • Neno kanuni lilitumiwa kuvihusu vitabu vilivyoamuliwa kuwa na asili ya Mungu.  
  • Kanuni ya Biblia ni vitabu vyenye uvuvio ambavyo vilikusanywa pamoja katika Biblia Takatifu. Kumbuka kwamba neno Biblia maana yake vitabu na Biblia Takatifu ni mkusanyiko wa vitabu Vitakatifu.  Neno kanuni ni neno la kawaida ambalo hutumiwa kuuhusu mkusanyo huu wa vitabu vitakatifu ambavyo tunaviita Biblia ambayo ndilo Neno la Mungu lenye uvuvio.     
  • Kanoni ya Agano la Kale inahusu vitabu vya Agano la Kale ambavyo viliamuliwa kuwa na uvuvio wa Mungu na kuingizwa katika Biblia kama sehemu yake tunayoiita Agano la Kale.
  • Kanoni ya Agano Jipya inahusu vitabu vya Agano Jipya ambavyo viliamuliwa kuwa na uvuvio wa Mungu na kuingizwa katika Biblia kama sehemu yake tunayoiita Agano Jipya.

 

  • Mchakato wa kuorodhesha maandiko kwa kanoni ya Biblia .
  • Mwandishi Mtukufu aliwapa watu Watakatifu wa Mungu Maandiko.  
  • Maandishi ya mkono yalinakiliwa kwa umakini mkubwa.
  • Vitabu vile havikukusanywa pamoja katika mfumo wake wa sasa kwa haraka.
  • Waandishi wa Kiyahudi na viongozi wa dini walivikusanya vile vitabu ambavyo asili yake ilidhihirika kuwa ni Mungu pamoja katika Kanoni ya Agano la Kale.
  • Viongozi wa kale wa kanisa walivikusanya vitabu vile pamoja ambavyo vilithihirika kuwa na asili ya Mungu na kuviweka katika Kanoni ya Agano Jipya.

 

  •  Uwepo wa Kanoni humaanisha ukweli kwamba kitabu kinachohusika kimeshadhihirika kuwa na asili ya Mungu na kuingizwa katika Kanoni.
  • Mfano: uwepo wa Kanoni katika Kitabu cha Isaya ulitambuliwa kwa sababu iliaminika kuwepo na uvuvio wa Mungu.   
  • Uwepo wa Kanoni katika hali kama hii haupaswi kuchanganywa na ule unaotumiwa na Kanisa katoliki ambao huusu utaratibu wa kuwafanya watu waliokufa watakatifu.
  • Namna ya kuamua uwepo wa Kanuni

 

Ni Kigezo gani kilitumika kuamua vitabu gani viingizwe katika Biblia na vitabu vipi visiingizwe katika orodha ya Maandiko Matakatifu?  Hili ni swali muhimu ambalo inabidi lipatiwe majibu na mwanafunzi makini wa Biblia.  Uanapaswa kufahamu bila shaka yeyote kwamba  Biblia katika mfumo wake wa sasa ndio NENO LA MUNGU LENYE UVUVIO

 

 

  • Fikra potofu kuhusu Uamuzi wa vitabu vya Kuorodhesha katika Biblia

 

  • Viongozi wa kidini ndio walioamua orodha ya vitabu vya Biblia.

 

Mabaraza ya dini hayakuamua vitabu vya kuorodheshwa katika Biblia.  Mabaraza ya wanadamu hayawezi kufanya kitabu kuwa Andiko Takatifu ambacho katika asili yake siyo maandiko matakatifu.

 

  • Wakosoaji watasisitiza kwamba ilibidi mwanadamu aamue vitabu vya kuingiza katika orodha ya Biblia hali inayotia shaka kuaminika kwa Biblia.

 

 

  • Kumekuwepo na madai kwamba wanadamu walichagua vile vitabu ambavyo vinawiana na mtizamo wa dini zao ambao waliuorodhesha katika Kanoni.  

 

Hali hii ndio inayosemekana kwamba ni sababu pekee ya umoja na uelewano wa Maandiko Matakatifu. Ubishi ni kwamba wanadamu waliondoa vitabu ambavyo havikukubaliana na maoni yao na kuingiza vile ambavyo vilikubaliana na maoni yao.  Maoni haya ya yongo humuweka mwanadamu katika nafasi ya uamuzi wa orodha ya kanoni.

 

  • Mawazo sahihi kuhusu uamuzi wa orodha ya vitabu vya Biblia.

 

  • Mungu aliamua kanoni ya uorodheshaji wa vitabu vya Biblia.   

Mungu alimpatia mwanadamu vitabu ambavyo alitaka viingizwe katika Biblia.  Mungu alilinda na kuhifadhi vile vitabu alivyovivuvia na kuvitunza hadi wakati wa kuviweka katika orodha ya Biblia.

 

  • Uvuvio wa Kiungu wa kitabu kilicho amliwa kikanoni.

 

Kitabu kiliweza kuingizwa katika Kanoni  kwa sababu ya kutambuliwa kwake kuwa na Uvuvio wa Wakiungu wa Neno la Mungu. Kitabu ambacho kilionekana kutokuwa na Mamlaka ya Kiungu hakikuingizwa katika Biblia kama sehemu ya  kanoni ya Maandiko Matakatifu.

 

  • Maelezo ya Kanuni ya Agano la Kale

 

  • Kanuni ya Agano la Kale iligawanywa katika sehemu tatu.

 

  • Sheria – Maandishi ya Musa.

 

  • Manabii – Maandishi ya watu waliokuwa na cheo cha manabii.

 

  • Maandishi – Ukiondoa Ruthu na Maombolezo maandishi ya watu ambao hawakuwa na cheo cha nabii. Shehemu hii huitwa pia Hagiografa katika taarifa nyingi za Kiyahudi.

 

  • Taarifa za Kimasoreti (TM)

 

  • Neno masoreti maana yake a desturi. Maandishi ya Kimasoreti yanahusu Maandiko yanayokubalika ya Kiebrania. Maandiko ya Kimasoreti mwanzoni yalithibitiwa na kikundi cha Wayahudi wanaojulikana kama Masoreti.

 

  • Maandishi ya Kimasoreti ni taarifa katika vitabu 24 zenye mamlaka vya kanoni ya Kiyahudi (Tanakh au Biblia ya Kiebrania) ambayo ni kamili ikiwa na maelezo, sarufi, matamshi, na herufi zinavyotamkwa na maelezo ya kina kuhusu maandishi. (kwa mfano idadi ya herufi katika ukurasa fulani inaweza kuwekwa pembeni mwa Taarifa ya Masoreti.)
  • Lengo la Masoreti lilikuwa ni kuhifadhi mfumo halisi, maneno na maana ya Maandiko. Upungufu au badiliko lolote halikukubaliwa.

 

  • Maandiko ya Kiebrania yalihifadhiwa na makuhani.
  • Ulikuwa ni wajibu wa Makuhani kuifadhi ufunuo uliokuwa katika Maandishi wa Maandiko. Makuhani walikuwa ndio wateule wa Mungu wa kutunza Sheria yake na kuifundisha.

Kumbukumbu 31:24-26—Basi ikawa hapo Musa alipomaliza kuandika maneno ya Torati hii katika Chuo, hata yakaisha, 25 ndipo Musa akawaamuru Walawi waliokuwa wakilichukua sanduku la Agano la BWANA akawaambia, 26 Twaeni chuo hiki cha Torati, mkiweke kando la agano la BWANA, Mungu wenu, ili kiwepo kama shahidi juu yako.

Sheria iliwekwa kama muongozo kwa Makuhani ili kuitunza pamoja na lile Agano. Makuhani hao waliagizwa kuisoma Sheria kila miaka saba.

 

 

  • Makuhani walisimania matengenezo ya Nakala sahihi za sheria kwa ajili ya matumizi ya wafalme na watawala.
  • Uangalifu Mkubwa ulitumika katika kulinda na kuhifadhi maandishi yaliyovuviwa.

 

  • Kristo alikuwa mwaminifu kwa ahadi yake kwamba Maandiko ya  Agano la Kale hayatapotea.  

 

Mathayo 5:18—Kwa maana Amini, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya Torati haitaondoka, hata yote yatimie.

 

  • Waandishi walitumia mbinu mbalimbali kuhakikisha usahihi wa nakala za maandishi zilizotolewa za taarifa za Kiebrania.  Walitumia majaribio kama ya kuhesabu maumbo ya irabu na kukagua uwekaji wa maneno fulani katika taarifa wakati wa kuthibitisha usahihi wa nakala iliyokamilishwa upya.  Nakala yote nzima ilitupwa kama ikikutwa na kosa lolote.  

 

  •  
  • Tangu mwanzo wa karne ya kwanza mpaka Mageuzo ya kanisa la Protestanti, Agano la Kale la Waebrania lilihifadhiwa na Wayahudi.

  Waandishi wa Kiyahudi walinakili kwa uangalifu mkubwa na kuhifadhi maandishi ya Agano la Kale.  Augustino alisema, waandishi wa Kiyahudi walikuwa ni Wakutubi wa kanisa la Kikristo. Waandishi wa mwanzo kabisa kati ya hawa waliitwa Tannaim (walimu) walinakili maandishi ya Agano la Kale kwa usahihi mkubwa. Watannaim walifuatwa kwa hadhi na kikundi cha waandishi walioitwa Amoraim (wafichuaji). Hawa walikuwa ni wasomi waliofanya kazi siyo kama wa kunakili tu, bali walizalisha pia ile Talmud ambayo ni kitabu kinachoweka hadharani sheria na mila za Wayahudi.

 

  • Zile desturi (Taarifa za Masoreti) zilizoandikwa na kuchapishwa mwishoni mwa enzi za kale. Zaburi zilichapishwa 1477. Katika mwaka 1488 Biblia nzima ya Waebrania ilichapishwa kwa mara ya kwanza.

 

 

  • Kuzikwa kwa Maandiko ya Waebrania.

 

Walimu (Rabi) wa Kiyahudi waliziweka nakala za Maandiko Matakatifu katika heshima ya hadhi ya juu.  Wakati andiko lolote lilipo zeeka au kuchujika na kuonekana halifai kwa matumizi lilipumzishwa kwa heshima kuu.  Iliaminika kwamba ni bora zaidi kuzizika kwa heshima kuliko kuthubutu kuziacha ziangukue mikono isiyofaa au kudharauriwa. Hii ndio sababu ya kuwepo nakala nyingi za Agano la Kale zilizoandikwa.

 

  • Ugawaji wa Maandiko ya Waebrania katika sura na aya mbalimbali.

 

  • Kugawanywa kwa Maandiko katika Aya ni jambo lililofanyika mapema kabisa na familia ya Masoreti ya ben Asheri miaka ya 900 baada ya Kristo.
  • Mfumo huu unagawanya vitabu 39 vya Agano la Kale (kama tunavyoona katika Biblia) katika aya 23,100. Maandiko ya Waebrania yamegawanywa katika ubeti.  
  • Mgawanyiko katika sura ulifanywa kwa mara ya kwanza na Kadinali Hugh wa Mtakatifu Cher mwaka 1244.

 

  • Ugunduzi wa Kanuni ya Agano la Kale

 

  • Uhusiano wa ndani katika taarifa
  •  
  • Hakuna taarifa ya Historia iliyo kamili ya kukubalika kwa kila kitabu cha Agano la Kale, kwa hiyo, maelezo ya Biblia yenyewe ndio taarifa za kihistoria zilizopo ambazo ni bora zaidi.
  • Vitabu vya sheria vilikubaliwa mara moja na Israeli. -Kut. 24: 3-4
  • Yoshua aliandika katika kitabu cha Sheria ya Mungu. –Yoshua 24:26.
  • Kitabu cha Samweli kiliwekwa mbele ya Bwana. –I Samweli 10:25.
  • Kitabu cha Sheria kilianzishwa upya kipindi cha Yosia.  -II Fal 22:8-11,23:1-2
  • Ezra na Nehemia waliwaonya watu kuwa wataiendea torati ya Mungu. –Nehemiah sura ya 8 na 10:28-29
  • Waandishi wa baadaye walitambua maandiko ya mwanzo kama neno la Mungu lenye mamlaka.
  • Danieli alitambua kitabu cha Yeremia kuwa chatoka kwa Bwana. – Danieli. 9:2
  • Vitabu vya Sheria ya Musa vimetajwa katika vitabu vingine vya Agano la Kale. -Yos. 1:8, 8:31, I Fal 2:3, II Fal 14:6, 21:8, 23:25, Dan. 9:11-13, Mal 4:4
  • Maandiko ya Sulemani yanatajwa katika I Wafalme 4:32
  • Yeremia aliutaja unabii wa Mika kuanzia karne moja nyuma. – Yer.26:17-29

  •  Kuijaribu kanoni ya Agano la Kale

 

Yapo majaribio yaliyotumiwa na viongozi wa Wayahudi ili kuamua kanoni ya kitabu misingi hii ilizingatia walichotaka waandishi wa historia ya Biblia na kanisa.  Ulikuwepo mfumo maalumu wa kuangalia utambuzi wa kanoni ya kitabu.  Sehemu hii inataja waandishi wa kanoni za vitabu vya Biblia. Maelekezo haya ni kuhusu ukweli kwamba walikuwa ni vyombo vya kibinadamu  vya mwandishi wa kiungu.

 

  • Iliandikwa na Musa?  

Uandishi wa Musa wa kitabu ulichukuliwa kama jaribio halali la uvuvio na Wayahudi tangu zamani. Musa anatajwa kama nabii mkuu wa Wayahudi. Vitabu ambavyo viliandikwa na Musa vinachukuliwa kama vyenye asili ya Mungu kutoka mwanzoni kabisa mwa taarifa za historia ya Wayahudi.  Ushahidi wa akiolojia wa Palestina unaimarisha sana mtazamo huu wa kitamaduni.  Yesu alithibitisha kwamba Musa ndiye chombo cha kibinadamu kilichopokea ile Sheria. Musa hakuwapa torati? – Yoh. 7:19. Kama tunavyofahamu taarifa iliyoandikwa katika Biblia inaonesha kukubalika mara moja kwa vitabu vya sheria kama vilivyotolewa na Mungu.

 

  • Iliandikwa na nabii wa Mungu anayejulikana?

Iwapo kitabu hicho kiliandikwa na nabii wa Mungu anayejulikana ambaye alifikiriwa kama mwaguzi wa Mungu; kitabu hicho kiliaminiwa kuwa ni Neno la Mungu.

 

  • Mwandishi wake alithibitishwa kwa matendo ya Mungu?

Mwandishi alichukuliwa kuwa mtu wa Mungu iwapo alionesha ushahidi wa nguvu za Mungu katika maisha yake.  Kama mwandishi alichukuliwa kama mtu wa Mungu na maandishi yake pia yaliaminika kwamba yametoka kwa Mungu. Watoto wa manabii walitambua mamlaka ya Elisha walipomuona amechukua nafasi ya Eliya na kuutenganisha mtu Yordani. – II Fal 2:15.

 

  • Inao uelewano na kanuni nyingine za Maandiko?

Ni lazima kuwepo umoja kamili wa Maandiko.  Kanuni katika sehemu moja ya Maandiko ni lazima ielewane na ukweli ulioko katika sehemu nyingine za Maandiko. Kama ilivyokwisha tamkwa wengine watabisha kwamba vitabu vilivyochaguliwa ni vile vinavyopatana na maoni ya viongozi ambao walivichagua.  Hata hivyo kitabu kisingeweza kuhesabika kama cha Kanoni iwapo isingekuwa kinakubaliana na Maandiko mengine yaliyopokelewa.  Kitabu kilitambuliwa kuwa cha Kanoni kwa sababu ya kuwa na uvuvio.  Jambo hili kama tunavyoweza kuona siyo jaribio pekee la kuthibitisha kanoni ya kitabu.  Ni wazi kwamba Kitabu chenye asili ya Mungu hakitapingana na kitabu kingine chenye asili ya Mungu.

   

  • Kinasema ukweli kumhusu Mungu?

Ni lazima kitabu kiwe sahihi katika maelezo yake kumhusu Mungu na kuhusu vitu vya Mungu.  Kitabu hicho kitakaliwa kwa kutokuwa na uvuvio iwapo kutakuwa na makosa kuhusu teolojia.

 

  • Kilikubaliwa na viongozi wa Kiyahudi kama chenye mamlaka ya Maandiko?

Baadhi ya vitabu vilikubaliwa na viongozi wa Wayahudi kama vya kanoni na vingine vilikataliwa.  Huu ni ushahidi kwamba viongozi wa Kiyahudi walitambua vitabu hivyo ambavyo viliingizwa katika Kanoni kama Maandiko yenye mamlaka.

 

  • Ushuhuda  wa Agano Jipya unaohusu Kanuni ya Agano la Kale

 

  • Yesu alithibitisha mamlaka ya Kanoni ya Agano la Kale.

 

  • Yesu alizungumzia sehemu tatu za Kanoni ya Agano la Kale: Sheria, Manabii,
  • na Maandiko.  

Luka 24:44—… ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na

katika Manabii na Zaburi.

  • Ni jambo la kawaida wakati wa Kristo kwa Agano la Kale kuwa katika mgawanyiko wenye sehemu hizo tatu. Kwa kuzitaja sehemu hizo, Yesu alithibitisha mamlaka ya Kanoni ya Agano la Kale kama ilivyogawanywa. Wayahudi wa siku za Yesu wangeweza kuelewa kwamba alikuwa anazungumzia ile Kanuni kamili (ya Agano la Kale) katika tamko hili:
  • Yesu aliwauliza Wayahudi: Musa hakuwapa ile Sheria? –Yoh. 7:19
  • Yesu anatamka ile sheria na wale Manabii. -Mt. 5:17; 22:40.
  • Zaburi kwa kwa ujumla inagusia sehemu ambayo kwa kawaida huitwa Maandiko.
  • Yesu alisoma kutoka kitabu cha Isaya.  Lk.4:17-21. Yesu alizitaja taarifa hizi kama Habari Njema kwa hiyo alithibitisha mamlaka na uvuvio wake.

 

  • Yesu asingetumia taarifa kutoka vitabu vya Agano la Kale kama visingekuwa na uvuvio.

 

  • Agano jipya linathibitisha mamlaka ya Agano la Kale.

 

  • Agano la Kale limetajwa mara 263 katika Agano Jipya. Matumizi ya maandiko haya katika Agano Jipya ni uthibitisho kwamba yalichukuliwa kama yenye Mamlaka katika Neno la Mungu.
  • Paulo ametaja za taarifa za Agano Jipya kama Maandiko.
  • Rum. 10:11; 11:2; Gal. 3:8
  • Maelezo ya Kanuni ya Agano Jipya

 

  • Kanoni ya Agano Jipya imegawanywa katika sehemu tano.
  • InjiliMathayo, Marko, Luka, Yohana
  • Historia Matendo
  • Nyaraka za PauloWarumi, 1&2 Wakorinto, Wagalatia, Waefeso, Wafilipi, Wakolosai, 1&2 Wathesalonike, 1&2 Timotheo, Tito, Filemoni, Waebrania*
  • Nyaraka za Kawaida(Waebrania*) Yakobo, I&2 Petro, 1,2&3 Yohana, Yuda
  • UnabiiUfunuo

 

  • Maandishi yaliyopokelewa (Textus Receptus)
  •  
  • Neno la Kilatini Textus Receptus maana yake maandishi yaliyopokelewa na yanahusu Agano Jipya la Kiyunani kama lilivyo katika maandishi  ambayo yalikubaliwa na Kanisa la mwanzo. Kuna historia inayopatikana ambayo inayo taarifa yenye uvuvio ambayo ilikubaliwa na kanisa la mwanzo.  Mungu alihifadhi neno lake katika vizazi vyote.
  • Asilimia 99 % au zaidi ya maandiko 5,200 ya Agano Jipya la Kigiriki wanakubalina kwamba Toleo la Agano Jipya la Mfalme James (KJV). Agano Jipya la Kiyunani la Erasmo. Chini ya asilimia 1% (.08%) wanakubali kwamba mambo machache yaliyopungua au kubadilika katika TNIV, NIV, ESV, HCSB, NASB, NRSV, NLB, CEV, NCV, NAB, na NJB.
  • Maandishi yaliyopokelewa ndio maandishi yaliyotumiwa na wale Wanamageuzi. Kanisa la Kikristo linatambua vitabu 27 vya maandishi haya kuwa ni kanuni ya Agano Jipya na maandishi mengine yanayobakia yanapingana na yamechanganyika kiasi ambacho ni vigumu kuyafikiria kama yanaweza kuaminika.

 

  • Uchapishaji wa kwanza wa Agano Jipya la Kiyunani

 

  • Erasmo alichapisha Agano Jipya la Kiyunani mwaka 1516. Erasmo alitumia maandishi yote yaliyokuwepo katika kuchapisha hili Agano Jipya la Kigiriki. Alitaja pia mkusanyiko wa Kilatini (Latin Vulgate) ambao aliamini kuwa inazo dosari nyingi na kukosa maadili ili kuhakikisha kwamba ameangalia kila kianzio kilichokuwepo.  Alitegemea kupata taarifa sahihi ambayo ni halisi na inao uvuvio wa Roho Mtakatifu.  Agano Jipya la Kiyunani la Erasmo lilikuwa ni matokeo yenye uelewano na uaminifu wa taarifa za Kiyunani zilizoandikwa kwa mikono ambazo zilitumiwa kabla ya kuwepo mashine za uchapishaji.  Alitumia kila daftari iliyokuwa imeandikwa na akazilinganisha kwa uangalifu mkubwa ili kuhakikisha anapata Agano Jipya la Kiyunani lililo sahihi ambalo litachapishwa na kusambazwa kwa mara ya kwanza.

 

  • Erasmo hakuanzisha  maandishi yaliyopokelewa; alikusanya na kuchapisha. Alikusanya nakala nyingi zilizoandikwa kwa mkono  za Maandiko zilizokuwa katika mzunguko na kwa kulinganisha moja na nyingine alipata msimamo kati yake ambao aliuchapisha kama Agano Jipya.

 “hatupaswi kulionyesha kama ni chimbuko la Erasmo la ‘maandishi yaliyopokelewa’ bali kama muendelezo wa kutoka kwenye maandishi ya mkono iliyozooeleka jinsi ilivyopokelewa kwenda kwenye mfumo wa kuchapisha, ambao uliendelea kuwepo kwa karne tatu.” – Kenneth W. Clark, msomi wa Maandishi ya Kiyunani  (msisitizo umeongezwa)

 

  •    Roho Mtakatifu alizilinda na kuzihifadhi taarifa za kweli za Agano Jipya.

 

  • Neno la Mungu halitapita.

Mathayo 24:35—Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

 I Petro 1:23—Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili si kwa mbegu iharibikayo bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima lidumulo hata milele.

 

  • Roho Mtakatifu aliwafundisha Wakristo ni vitabu vipi vyenye uvuvio.
  • Yohana 14:25-26—Hayo ndiyo niliyowaambia wakati nilipokuwa nikikaa kwenu. Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
  • Roho Mtakatifu aliwaongoza pia Wakristo kutambua ni vitabu gani vilivyokosa uvuvio. Baadhi ya vitabu vilichukuliwa kwa makosa kama vyenye kanoni na baadhi ya Wakristo wa mwanzo.  Kwa mfano Ireneo alichukulia kitabu cha “mchungaji wa Hermesi” kuwa ni kimojawapo chenye uvuvio.  Roho Mtakatifu aliweka kanoni katika hali yake ya sasa kwa vitabu 27 vya agano Jipya.

 

  • Taarifa zilizopokelewa za Agano Jipya zilihifadhiwa na viongozi wa kanisa.

 

  • Mwanzoni kabisa mwa kanisa Mitume waliagiza kanisa ni vitabu vipi vyenye uvuvio na vipi havina. Mkumbuke Yohana, yule mtume wa mwisho kati ya Wafuasi waanzilishi, alikuwa na umuhimu katika kuliagiza kanisa na kulifikishia maandiko ya kweli yenye uvuvio ya Agano Jipya hadi mwaka wa 100 Baada ya Kristo.
  • Viongozi wa kwanza wa kanisa walizifikisha taarifa hizo za Agano Jipya kwa waliowapokea. Inyasi na Polikarpi ambao walikuwa ni viongozi wa kanisa la mwanzo walifundishwa na Mtume Yohane kwa kuwapa maagizo ya kitume moja kwa moja kuhusu elimu ya maandishi yenye uvuvio. Polikarpi alimfundisha Ireneo ambaye baadaye alikuja kuwa kiongozi wa kanisa.  Wale viongozi waliwafundisha warithi wao ukweli wa Neno la Mungu.

 

  • Ugunduzi wa Kanoni ya Agano Jipya

  • Zipo taarifa za Kihistoria kuhusu kukubalika kwa Kanoni ya Agano Jipya.

 

  • Vitabu vya mwanzo vya Agano Jipya vilivyokusanywa pamoja ni nyaraka za Paulo.  Mkusanyo wa nyaraka za Paulo ulikuwepo katika mzunguko mwanzoni mwa karne ya pili.  Inyasi ambaye ni kiongozi wa Karne ya Pili alitaja nyaraka za Paulo kama Injili.  Mkusanyiko wa barua za Paulo ulikuwepo wakati Polikarpi alipowaandikia Wafilipo na wakati Inyasi alipoandika barua zake saba kwa makanisa ya Asia ndogo mwaka 115 Baada ya Kristo.
  • Zile Injili nne zilikusanywa pamoja na kuwekwa katika mfumo muda fulani katika karne ya pili. Tarehe kamili ambapo Injili hizo nne ziliwekwa pamoja haijulikani. Inakubaliwa kwa ujumla kwamba ziliwekwa pamoja na kukubaliwa kabla ya mwaka 170 Baada ya Kristo, kwa sababu injili hizo nne za Kanoni zilitumiwa na Tatiano ambaye alikuwa ni kiongozi wa Kanisa katika kongamano lake la Injili lililoandikwa mwaka wa 170 Baada ya Kristo.  Ireneo,katika kitabu chake "kinyume cha upotofu" (mwaka 182-88 Baada ya Kristo), anazitaja injili hizo nne za Agano Jipya akizisema ni Maandiko.
  • Injili nne zinazotajwa kama Injili na nyaraka za Paulo anayetajwa kama Mtume zilikuwemo katika mzunguko kama mkusanyo tofauti miaka ya mwanzo ya karne ya pili.  Sehemu hizi mbili ziliunganishwa baadaye kwa kitabu cha Matendo ambacho kilizileta pamoja katika mkusanyo mmoja wa vitabu. Hii ilikuwa ni hatua ya mwanzo ya kuvikusanya vitabu vya Agano Jipya katika kanoni moja iliyo kamilika.
  • Kabla ya mwaka 200 Baada ya Kristo nyaraka za Paulo, Injili, Matendo,
  • I Petro na I Yohana zilitambuliwa kama Maandiko na kanisa la Kikristo. Maandishi ya Ireneo, Klementi wa Aleksandria na Tertuliano yanaonyesha kukubaliwa kwa vitabu hivi kama vyenye uvuvio na vilivyo hesabika kuwa na mamlaka sawa na yale yaliyoandikwa katika Agano la Kale.
  • Vitabu saba vilivyobaki, Yohana 2 na 3, Petro 2, Waebrania, Yakobo, Yuda na Ufunuo, vilikubaliwa kama Injili mwaka 300 Baada ya Kristo.

 

  • Ushuhuda uliomo katika Agano Jipya lenyewe.

 

  • Mtume Petro muda mfupi kabla ya kufa kwake, alitaja nyaraka za Paulo kama Maandiko na Injili nyingine zilizobaki kuonyesha kwamba anaziheshimu kazi nyingine katika vitabu vyenye uvuvio vya Injili. – II Petro 3:15-16.
  •  
  • Kitabu cha Ufunuo kinayo taarifa kwamba ni cha unabii. – Ufu. 1:3, 22:18,19.

 

  • Upo ushahidi wa kihistoria wa matumizi ya vitabu vya Agano Jipya uliofanywa na viongozi wa zamani wa kanisa.

 

  • Klementi wa Roma (97-140 BK) aliandika mengi kutokana  na kuhusu Agano Jipya. Klementi wa Roma mwaka 95 Baada ya Kristo aliandika barua kwa jina la Wakristo wa Roma kwa wale walioko Korinto. Katika barua hiyo anatumia taarifa zinazopatikana katika Mathayo na Luka.
  • Inyasi (35-116 BK) inataja maeneo makubwa ya Agano Jipya. Barua za Inyasi (115 BK) zimetumia lugha inayopatikana katika nyaraka zote za mtume Paulo. Waraka kwa Polikarpi unataja sehemu za kitabu cha Wafilipi na kugusia barua tisa kati ya barua za Paulo. Inyasi ananukuu kutoka Mathayo na I Petro na I Yohana pia.
  • Polikarpi (69- 155 BK) amerejea mara nyingi katika maandiko ya Agano Jipya.

 

  • Kunao ushuhuda wa kihistoria wa kukubalika kwa kanuni kwa viongozi wa Kanisa.

 

  • Theofilo (115-188 BK), Askofu wa Antiokia mwaka 168 BK, aliwataja wainjilisti na Maandiko Matakatifu ya Agano Jipya.
  • Klementi wa Aleksandria (115-188 BK) katika kipindi cha pili cha karne ya pili panatajwa ukusanyaji wa Injili nne ambazo zilitambuliwa kama Maandiko.
  • Ireneo (130-200 BK) analitaja Agano Jipya kama Maandiko Maandiko Matakatifu. Ananukuu kutoka kila kitabu cha Agano Jipya isipokuwa Filemoni na IIIYohana. Kanoni ya Agano Jipya inayo tambuliwa na Ireneo inafanana sana na tuliyonayo leo.
  • Tertuliano (160-221 BK) alitumia kwa mara ya kwanza maneno Agano Jipya na anaiita Biblia kamili kama chombo kizima cha Maagano yote mawili.
  • Eusebio (260-340 BK) kwenye mwaka wa 330 BK aligawa vitabu vyote 27 vya Agano Jipya katika mafungu ya vinavyobishaniwa na visivyokuwa na ubishani.
  • Atanasi (298-373), Askofu wa Aleksandria, katika barua yake ya pasaka ya mwaka 367 BK aliorodhesha vile vitabu 27 vya Agano Jipya na akatumia maneno kuwekwa kanoni kuvihusu.

 

  • Majaribio ya uwepo Kanoni katika Agano Jipya

 

Yalikuwepo majaribio ambayo yalitumiwa na kanisa la mwanzo kuamua kuwepo kwa kanoni katika kitabu. Walikuwepo viongozi wa kanisa waliohusika kwa wakati mbalimbali ambao waliamua ni vitabu gani vyenye uvuvio na visivyokuwa nao.  Ifuatayo ni miongozo mnne iliyotumiwa na viongozi hawa katika ugunduzi wao wa kanoni ya Agano Jipya.

 

  • Kitabu hiki kiliandikwa na Mtume?

 

Tunaelewa kwamba Mungu ndiye mwandishi wa Agano Jipya.  wale Mitume walikuwa ni baadhi ya watu watakatifu wa Mungu ambao kwa Utukufu wake Mwandishi aliongea kuwapitia wao.  Kama kitabu kiliweza kuthibitishwa kuandikwa na mmoja wa wale mitume wa mwanzo wa Yesu kilichukuliwa kama chenye asili ya Mungu.  Uzito mkubwa uliwekwa katika ufundishaji na maagizo ya mitume wale wa mwanzo. Maandiko yaliyowahusu wao yalisambazwa kati ya jamii za Kikristo za kwanza kabisa.

  •  
  • Kitabu hiki kiliidhinishwa na Mtume?

 

Iliaminika kwamba wale mitume wa kwanza walifahamu zaidi ni vitabu vipi vyenye uvuvio na ni vipi visivyokuwa nao. Kitabu ambacho hakikuandikwa na mtume ambacho kilikuwa na idhini ya Kitume kilichukuliwa kuwa na asili ya Mungu.  

  •  
  • Kitabu hiki kilipokelewa kimataifa na kanisa la mwanzo mwishoni mwa karne ya nne?

 

Vipo vitabu fulani ambavyo vilikubaliwa haraka na kanisa la mwanzo kuwa Maandiko yenye Utukufu wa Mungu.  Vitabu hivi viliingizwa mara moja katika Kanuni. Kulikuwepo na vitabu vingine ambavyo vilichukua muda kukubaliwa na kanisa kuwekwa katika orodha ya kanoni.

 

  • Kitabu hiki kilisomwa hadharani wakati kanisa la mwanzo lilipokusanyika kwa Karamu ya Bwana?

 

Tunayo taarifa ya kihistoria kutoka kwa viongozi wa mwanzo wa kanisa zinazoonesha kwamba ni vitabu gani vilisomwa katika makusanyiko ya kanisa.  Vitabu hivi vilitumiwa na kanisa kwa sababu vilichukuliwa kama vyenye uvuvio.

 

  • Kitabu hiki kinao uwiyano na vitabu vingine vilivyokubalika vya Maandiko?

 

Kama ilivyokwisha tamkwa kuhusu kukubaliwa kwa Maandiko ya Agano la Kale kwamba ni lazima kitabu kioane vizuri na vitabu vingine vyenye kanoni iliyokwisha kubalika. Pamoja na hayo, vitabu vya Agano Jipya ambavyo vilipokelewa vinapaswa kuwa na uwiano na kanoni ya Agano la Kale na kanoni ya Agani Jipya ya Maandiko Matakatifu.    

  • Vitabu vinavyoitwa Homologoumena na Antilegomena.

 

  • Homologoumena maana yake iliyokubalika na inahusu vitabu vya Agano Jipya ambavyo vilikubalika mara moja.

Vitabu 20 kati ya 27 vya Agano Jipya vilikubalika mara moja na vikapokelewa ulimwenguni pote kuwa asilia na kuitwa Homologoumena.  Vitabu hivi  20  ni zile Injili nne, Matendo, Nyaraka za Paulo (isipokuwa Waebrania), na nyaraka za kwanza za Yohana na Petro.

 

  • Antilegomena maana yake kupinga na inahusu vitabu ambavyo viongozi wa kanisa hawakuvikubali haraka na walichukua muda zaidi kuvikubali katika kanoni ya Maandiko.

Vitabu vile saba vya Waebrania, II Yohana na III, II petro, Yuda, Yakobo, Ufunuo vilipingwa kwa kipindi fulani na kuitwa Antilegomena.  Yalikuwepo maswali kadhaa kuhusu vitabu vilivyoitwa Antilegomena.  Moja ya maswali hayo ni lile la kwamba viliandikwa kweli na wale watu wanaoitwa waandishi wake. Waebrania kilikuwa hakina jina la mwandishi wake na kilitofautiana na mwelekeo wa nyaraka za Paulo uliofahamika; II Petro ilikuwa na tofauti na I Petro; Yakobo na Yuda walijiita watumishi; na siyo mitume; mwandishi wa II Yohana na III Yohana alijiita mzee na siyo mtume. Uandishi wa kitume ulichukuliwa kama kigezo muhimu katika kutambua kanoni ya kitabu. Yalikuwepo maigizo mengi yaliyodai mamlaka ya kitume, kwa hiyo vitabu hivi vilichunguzwa kwa makini kabla ya kuingizwa katika kanoni.

Swali lingine ni kwamba Yuda aliandika taarifa ambazo hazijatajwa mahali pengine katika Maandiko na anamtaja Henoko jambo ambalo lilihusishwa na Apokrifa.  Kitabu cha Ufunuo hakikueleweka kwa viongozi wengi wa kanisa kwa hiyo kikazua maulizo katika akili zao. Vitabu hivi havikukubalika mara moja na kuwekwa mahali pake katika kanoni. Baada ya kuchunguzwa kwa makusudi mwishoni vilipokelewa kama halisi, na ucheleweshaji wake ukathibitisha uchunguzi ambao ulitumika katika mchakato wa kuviweka kanoni. Mwanzoni mwa karne ya nne vilipokelewa katika makanisa mengi na mwishoni mwa karne hiyo vikapokelewa na makanisa yote.

 

  • Vitabu vya Apokrifa
  •  
  • Neno hili Apokraifa hutumiwa kwa vitabu vilivyoko kati ya Agano la Kale na Agano jipya na hujumlishwa kama rejea kwa baadhi ya kanoni.
  • Vitabu hivi vimepata jina lake kutokana na neno la Kiyunani apokruphos, maana yake iliyofichika. Vilipewa jina hili kwa sababu vilifichika na mamlaka yake hayajulikani.
  • Kanisa la Katoliki la Roma linakubali Apokraifa kama sehemu ya kanoni yao ya Maandiko.
  •  Wayahudi wanavitambua kama sehemu muhimu ya historia ya Taifa lao.
  • Vitabu hivi havikufikia kiwango cha msingi wa majaribio ya kuwekwa kanoni. Havikutambuliwa kama vitabu vyenye uvuvio na Wayahudi. Vilipewa sehemu yake vyenyewe katika kitabu hicho kitakatifu vikiwa na maelezo ya kutosha kwamba havihesabiwi kama vyenye mamlaka yaliyosawa na vitabu vyenye kanoni.
  • Baadhi ya viongozi wa kanisa walitumia neno hili kwa vitabu ambavyo havina kanoni.  

 

  • Maandiko yenye maana ndogo

 

  • Maneno haya yalitumika kuvihusu vitabu vilivyoonekana kudai kutambuliwa kuwa na umuhimu au thamani ya kidini.
  • Baadhi ya vitabu vilivyomo katika kundi hili vilionekana kulaghai kwa kudai kuwa na asili ya Kitume kama injili ya Tomaso.
  • Vilikuwepo vitabu vingi vilivyoandikwa ambavyo havikuwa na uvuvio ijapokuwa vilidai aina fulani ya utukufu wa Mungu.  Vitabu vilivyomo katika kundi hili huitwa maandiko yenye maana ndogo. Haya ni maneno ambayo yanatumika katika tahariri nyingi na machapisho ya utafiti.  Mwanafunzi makini wa Biblia anapaswa angalau kuwa na uelewa wa msingi wa kinachofahamika kuhusu maneno haya.

 

  • Orodha ya Kanuni mbalimbali

 

  • Kanuni tofauti zimeorodheshwa na madhehebu mengi ya kidini na viongozi wa kanisa katika historia yote.

 

  • Kanuni ya Kiyahudi

Kanuni ya Kiyahudi inaundwa na vitabu 39 vya Agano la Kale.

 

  • Kanuni ya Kisamaria
  •  
  • Kanuni ya Kisamaria ndiyo Biblia iliyo ndogo kuliko zote duniani na ambayo hutambua vitabu vitano tu vya Pentateukia.

 

  • Kanuni ya Marsiyo

 

Marisiyo ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kutengeneza orodha ya baadhi ya vitabu vya Agano Jipya. Marisiyo alilikataa Agano la kale lote na akamuona Mungu wa Agano la Kale kuwa ni mdogo kwa Yesu.  Kanoni ya Marsiyo iliundwa na vitabu 10 tu ambavyo ni nyaraka za Paulo (ukiondoa ambazo za kichungaji) na injili ya Luka. Vitabu  hivi alivifanyia masahihisho ili vielewane na ufundishaji wake uliokengeuka.

Ingawaje alikuwa muongo kuibuka kwa mafundisho ya uongo kulilifanya kanisa ligundue umuhinu wa kufafanua kanoni ya kweli ya Maandiko.

 

  • Kanuni ya Muratoriano iliyotawanyika

 

Mtawanyiko wa Kanuni Muratoriano unaorodhesha kanoni ya vitabu vya Agano Jipya. Mtawanyiko wa Muratoriano ambao ni maandishi ya kale sana katika miaka ya 200 Baada ya Kristo inayo orodha ya Kanoni kwa vitabu vya Agano Jipya.  Haisomeki yote kwa hiyo inaelezewa kama iliyotawanyika. Inavitambua vitabu vyote isipokuwa Waebrania, Yakobo, II Petro, na III Yohana.  

Lipo pia suala la I Petro ilivyotajwa au hapana. Imejumuisha pia kitabu kimoja kiitwacho Apokalipse cha Petro ambacho kilikataliwa baadaye kwa kutokuwa na Kanuni.

 

  • Kanuni ya Terituliano

Tertuliano (160-221 Baada ya Kristo) anavyo vitabu 22 katika kanoni yake ya Agano Jipya inayohusu Injili nne, Matendo, nyaraka 13 za Paulo, I Petro, I Yohana, Yuda na Ufunuo. Hakukiona kitabu cha Waebrania kama chenye kanoni.

 

  • Kanoni ya Origeni

Origeni (185-254 Baada ya Kristo) alikiri Injili nne zenye kanuni, matendo, Nyaraka za Mtume Paulo na Waebrania, I Petro, I Yohana na Ufunuo kama vitabu visivyokuwa na upinzani.  Origeni alikiri kwamba Waebrania,  II Petro, II na III Yohana, Yakobo na Yuda ni vitabu visivyokuwa na upinzani.

 

  • Kanuni ya Eusebio

 

Eusebio (260-340 Baada ya Kristo) anachukuliwa kama mwanahistoria wa kanisa.  Anatupatia taarifa kamili yenye maelezo ya nafasi ya kanisa kwa upana. Anaonesha tofauti muhimu kati ya homologoumena (vitabu vilivyokubaliwa) na antilegomena (vitabu vilivyopingwa).  Vitabu vilivyo kubaliwa ni zile Injili, Matrndo, Nyaraka za Paulo pamoja na Waebrania, I Petro, I Yohana, na Ufunuo.  Amevigawanya vitabu vilivyopingwa katika mafungu mawili madogo: (1) vile vinavyoelekea kufaa kuingizwa katika Kanoni - Yakobo, Yuda, II Petro, II na III Yohana (2) vile visivyoelekea kufaa kuingizwa katika kanoni — Matendo ya Paulo, Mchungaji wa Herimesi, Apokalipse ya Petro, Didisi, Barnaba.  Alihoji kuingizwa kwa ufunuo kutokana na wasiwasi wa kuhusika Mtume katika Uandishi wake.  Ukiacha kusita huku kwenye Ufunuo kwa Eusebio yeye katika Agano Jipya anafanana na la wakati wetu.

 

  • Kanuni ya Atanasio

 

Atanasio (298-373 Baada ya Kristo), Atanasio amaorodhesha vitabu 27 vya Agano Jipya la wakati wetu.

  • Kanuni ya Katoliki ya Roma

 

Kanisa Katoliki la Roma linaingiza ndani vitabu 66 vya Biblia yetu na kukubali pia vitabu vya Apokraifa kama sehemu ya kanoni yao ya Maandiko. Hii ni kanoni ile ile ya Yerome aliyetengeneza Vulgeti ya Kilatini ambayo ni msingi wa Biblia ya Katoliki ya Roma.

 

  • Kanuni ya kweli inayotambuliwa na kanisa la Kikriso

 

Kanoni ya kweli imeundwa kwa vitabu 39 vya Agano la Kale na vitabu 27 vya Agano Jipya la Biblia.

 

  • Kanuni ya Lutheri

 

Martini Lutheri aliorodhesha vitabu 27 vya Agano Jipya kama lilivyo isipokuwa vitabu vinne alivyoviona kama vyenye utata.  Aliweka Waebrania, Yakobo, Yuda na Ufunuo kwa utenganisho mwishoni mwa Agano Jipya.

Vipindi Saba Maalum katika Maandiko Matakatifu

I

II

III

IV

V

VI

VII

MWANZONI

VIONGOZI

WAKUU

WAFALME

WATAWALA WAGENI

 

UJIO WA KWANZA WA KRISTO

KANISA

UJIO WA PILI WA KRISTO

KUTOKA: Uumbaji

KUTOKA: Musa

KUTOKA: Saulo

KUTOKA: Kutekwa

KUTOKA: Uzalio wa Bikra

KUTOKA: Pentekoste

KUTOKA: Millenia

HADI: Musa

HADI: Paulo

HADI: Kutekwa

HADI: Kristo

HADI: Kupaa

HADI: Mateso

HADI:
Mbingu mpya & Dunia Mpya

VITABU: Mwanzo, Kutoka

VITABU: Kutoka, Walawi, Hesabu, Kumbukumbu, Yoshua, Waamuzi, Ruthu,

I Samweli

VITABU: I & II Samweli,

I & II Wafalme,

I & II Nyakati, Vitabu vya Manabii

VITABU: Ezra, Nehemia, Esta, Danieli, Ezekieli

VITABU: Mathayo, Marko, Luka, Yohana

VITABU:
Matendo Nyaraka

VITABU: Ufunuo