Skip to main content

Sura ya 3: Uvuvio wa Biblia

Ufafanuzi kuhusu uvuvio wa Biblia

1. Uvuvio maana yake ni nini?

  • Kamusi ya Webster inafafanua uvuvio kama: kitendo chochote cha kupumlia.
  • Neno Uvuvio linatokana na Neno la kiingereza inspiration ambalo kwa kilatini ni in spiro maana yake ‘pumulia ndani’.
  • Neno hilo kwa maana yake halisi enye pumzi ya Mungu.
  • 2 Tim. 3:16— Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, la faa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadabisha katika haki.

    Maneno katika taarifa ya kuwa na pumzi ya Mungu ni tafsiri kutoka katika neno moja la Kiyunani: theopneustos, ambalo limetolewa katika neno  Theos  - Mungu na  pneuma – Roho Mtakatifu.  Pneuma limetolewa kutoka neno lenye maana ya pumzi. Tafsiri halisi ya maneno haya (iliyotolewa kwa pumzi ya Mungu) ni: ILIYO PUMULIWA NA MUNGU  

     

    • Neno hili limetumiwa kuhusiana na asili ya Kimungu ya Maandiko. Biblia haikuandikwa na Mwanadamu Roho Mtakatifu alilipumulia Neno kwa watu ambao walikuwa ni vyombo vya kibinadamu vya Mwandishi ambaye ni Mungu.

     

    II Petro 1:21—Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

     

    Unabii katika maandiko haya yanahusiana na aya ya 20 inayosema: Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Aya hizi zinahusu unabii ulioko katika Maandiko. Maandiko hayakuletwa kwetu na mwanadamu.  Wale wanadamu walisukumwa na Roho Mtakatifu. Kitendo hiki Kitukufu cha Mungu.  

    Je tumeshapata Neno lenye pumzi ya Mungu? Ndiyo, tumeshapata! Haitoshi kujibu ndiyo peke yake swali kama hili, kila muamini anapaswa kufahamu bila shaka yeyote kwamba Biblia siyo kitu kingine zaidi ya pumzi ya Mwenyezi Mungu.

    2. Mawazo Potofu kuhusu Uvuvio wa Biblia

    Biblia ilipatikana kwa uvuvio wa asili.

    Wazo hili la uwongo hushikilia kwamba Biblia ni tunda la mtu mmoja mwerevu wa hali ya juu, ila siyo mwenye nguvu za ajabu au za Utukufu. Hii ni aina ya msukumo ambao umeoneshwa katika maandishi ya Milton, Shakespeare au Confusius. Hakuna binadamu mwenye kipaji hata kiwe cha namna gani, ambaye akisoma alichoandika Shakespeare kisha akaisoma Biblia atashindwa kuona tofauti kati ya mambo haya mawili kuwa ni kubwa sana. Kitabu kinaweza kuwa na uvuvio bila kuwa na pumzi. Biblia inavipita kwa mbali vitabu vya wanadamu.

    Mungu alitumia ngazi mbalimbali za msukumo kutupatia Biblia.

    Wazo hili la uongo hudai kwamba Mungu alitumia ngazi mbalimbali za udhibiti kwa vipindi tofauti katika mchakato wa msukumo. Wazo hili linatetewa zaidi kwamba Mungu alitumia utukufu wake na wakati mwingine, alitoa tu mapendekezo au alianzisha jambo kwa maagizo. Hii ni kinyume kabisa na msukumo wa kweli wa Biblia.

    Mungu alitoa pendekezo au maoni kwa wanadamu ambao waliiandika Biblia.

    Wale wanaoshabikia wazo hili la uongo wanasema kwamba mapendekezo au mawazo hayo yalipewa uvuvio. Msimamo huu unawapa wanadamu nafasi ya kutumia maneno yao katika taarifa hizo kutoka akili mwao. Hii ni kinyume na maana halisi ya uvuvio wa kweli wa Biblia.

    Sehemu chache tu za Biblia zimepumuliwa.

    Haya ni mafundisho ya uongo ambayo ni hatari kuzungumzia sehemu tu kuwa na pumzi. Msimamo huu unatamka kwamba Biblia inalo Neno la Mungu lakini siyo maandiko yote yamepumuliwa. Ni nani basi wa kuamua nini ndiyo na kipi hakijapumuliwa? Nadharia ya namna hiyo inamuacha mwanadamu katika hali tata na hatari ya kutokuwa na uhakika.

    • Ni nini uelewa sahihi wa uvuvio wa Biblia?
    • “Uvuvio wa mdomo na wa mamlaka” ndio sahihi. (jambo hili litaelezwa kwa kina baadaye)

    3. Matangazo ya Uvuvio wa kiBiblia

     

    • Biblia nzima inayo pumzi ya Mungu.

     

    II Tim. 3:16—Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu ……

     

    Wazo kwamba Biblia katika ukamilifu wake inayo pumzi ya Mungu huitwa uvuvio kwa mamlaka. Mamlaka maana yake kamili au timia. Biblia kamili huanzia mwanzo mpaka ufunuo ni Neno la Mungu lenye uvuvio. Maandiko yote yamepumliwa sawasawa.

    Kwa kuwa imepumuliwa na Mungu Biblia haiwezi kuwa na kosa. Haiwezi kuwa na kosa maana yake imetenganishwa kabisa na uwezekano wa kukosewa. Maneno hayo huhusishwa na Mungu ambaye hawezi kufanya kosa au kughafilika. Katika matumizi yake kuihusu Biblia kutokuwa na kosa kunahusu Utukufu wa Mwandishi wa Maandiko. Muandishi huyu Mtukufu hafanyi makosa na kwa hiyo Neno lake haliwezi kuwa na kosa.

     

    • Agano la Kale limevuviwa na Mungu.

    Mara kwa mara tena tunaweza kupata maelezo yafuatayo katika Agano la Kale:

     

    “Neno la Bwana”         “Mungu akaamuru” “Mungu akasema /akaonge

    “Bwana akasema”   “Mungu akatokea”    “Asema Bwana”

     

    Maelezo kama haya yanadhibitisha uvuvio wa Agano la Kale. Uthibitisho wa madai haya uko wazi kutokana na umakini wa kila neno la taarifa na majina, nyakati na mahali ambako watendaji walikamilisha ujumbe wao na, ukamilifu wa kutimia kwa unabii wao.

     

    Matendo 28:25—Na walipokuwa hawapatani wao kwa wao, wakaenda zao, Paulo alipokwisha kusema neno hili moja, ya kwamba, Roho Mtakatifu alinena vyema na baba zetu, kwa kinywa cha nabii Isaya,

     

    2 Petro 1:21—Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

     

    Waebrania 1:1—Mungu ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi.

     

    Kumb.18:18-22—v. 22 Atakaponena nabii kwa jina la Bwana, lisifuate jambo lile wala kutimia hilo ndilo neno asilonena Bwana; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimuogope.

     

    • Agano Jipya limevuviwa na Mungu

    Waandishi wa Agano Jipya wanadai kuwa uvuvio kwa waandishi wa Agano la Kale  unawahusu wao pia:

    Matendo 1:16—…ilipasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daudi kwa habari za Yuda aliyewaongoza wao waliomkamata Yesu....,

    • Wale watu walivuviwa

    Maandiko yanatamka kwamba watu watakatifu wa Mungu waliongea kama walivyosukumwa na Roho Mtakatifu. – 2 Petro 1:Mungu aliwavuvia Neno lake watu ambao walikuwa ni vyombo vya kibinadamu kuandika Biblia. Kauli za Manabii kutoka kwa Mungu zilitumiwa na Mungu kuwasiliana na watu Wake. Bwana aliwaagiza wengi wa watu hao kuandika Maneno Yake. Watu hao walivuviwa na kuagizwa na Mungu kuwapatia watu wake Neno lake.

     

    E. Yale Maneno Yalivuviwa

    • Siyo wale watu waliovuviwa na Mungu peke yao, bali uchaguzi wa maneno ulikuja moja kwa moja kutoka katika kiti cha enzi cha Mungu. Mungu alivuvia uchaguzi wa maneno ya Maandiko. Jambo hili hujulikana kama uvuvio wa maneno. Wale waandishi hawakuachwa peke yao katika uchaguzi wa maneno ambayo yatatumika.  Mungu aliongoza katika uchaguzi wa maneno katika Biblia.  

     

    Yuda 17—Bali ninyi, wapenzi, yakumbukeni maneno yaliyonenwa zamani na mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo;

    2 Petro 3:2—Mpate kuyakumbuka yale maneno yaliyonenwa zamani na manabii watakatifu, na ile amri ya Bwana na Mokozi iliyoletwa na mitume wenu.

    Yohana 12:48—Yeye anikataaye mimi,asiye yakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.

     

    • Zile Herufi zilikuwa na uvuvio

    Zile herufi za maneno ya Biblia zimevuviwa kwa Utukufu wa Mungu. Kwa mfano, hebu tuangalie mafundisho ya “punje moja na siyo nyingi” kwa njia ya Kristo ambao ilidhibitishwa kwa matumizi ya herufi: ‘u.’

     

    Wagalatia 3:16—Basi ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu kwa mzao wake. Hasemi, kwa wazao kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni  mmoja, Kwa mzao wako, yaani, Kristo. (linganisha na Mwanzo. 22:16-18)

     

    Herufi ‘u’ katika aya hii inaweka tofauti KUBWA.  Herufi ‘u’ inaweka tofauti kati ya umoja na wingi na muhimu zaidi tofauti ya kutamka kwamba kuna msuluhishi mmoja au kutamka kwamba wapo wasuluhishi wengi. Iwapo Mungu angesema wazao’ badala ya uzao’ ahadi hizo zingeweza kutolewa kupitia Confucius, Buddha, Mohammed, Papa au mwingine yeyote ambaye amechagua kujitwalia umaarufu huu. Kwa kutumia umoja, Mungu ameufunga mlango kwa manabii wa uongo na kumnyanyua Kristo kama njia PEKEE ya kwenda kwa Mungu. Punje ya Ahadi inaweza kuwa Kristo tu, na siyo Kristo na Buddha au Kristo na Muhammed. Yesu Kristo peke yake alikuwa ndiye punje ya ahadi.

     

    • G. Kila chembe Ilivuviwa

    Mathayo 5:18—Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka Mbingu na Nchi zitakapoondoka yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.

     

    Yodi inaweza kulinganishwa na apostrofi (‘) na nukta kulinganishwa na kistari ungio (-).

     

    “Biblia siyo kitu kingine isipokuwa ni sauti Yake yule akaaye katika kiti cha enzi. Kila kitabu chake, kila mlango, kila aya, kila neno, kila silabi, kila herufi, ni tamshi lake Yule Aliye Juu ya Yote.”—Dan Burgon

     

     

     

     

    • Ufafanuzi wa  Uvuvio wa kiBiblia

     

    • Huzalisha watu “waliozaliwa mara ya pili”.

    II Kor. 5:17—Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.

    Jedwali lifuatalo ni orodha ya watu wa Mungu ambao waligeuka kupitia sehemu mbalimbali za maandiko. Maandiko haya yalikuwa na matokeo katika maisha ya watu hawa wa Mungu.

    John Calvin

    Isaya 53:5

    C.H. Spurgeon

    Isaya 45:22

    Henry Moorhouse

    Mathayo 1:21

    John Williams

    Marko 8:36

    Sir James Simpson

    Yohana 3:14,15

    W.P. Lockhart

    Yohana 19:30

    David Livingston

    Matendo 16:31

    William Cowper

    Warumi 3:25

    Sir  George Williams

    I Wakorinto 15:1-4

    Martin Luther

    Wagalatia 3:11

    Lord Shaftesbury

    I Petro 3:18

    Hedley Vicars

    I Yohana 1:7

    James Chalmers

    Ufunuo 22:17

    Robert Moffat

    Yohana 3:16

    Duncan Mathieson

    Yohana 3:16

    Richard Weaver

    Yohana 3:16

    Hakuna yeyote aliyewahi kusikia mtu aliyefanywa “kiumbe kipya” kupitia Homer, Shakespeare, Scott, Dickens, Macauley, Huxley, Carlyle, Eliot, Kipling, Wells, au mtu mwingine yeyote? Mamilioni ya watu wamefanywa wapya kwa kusoma na kuiamini Biblia ambayo ni Neno la Mungu.

     

    • Huzalisha ukuaji wa Kiroho.

    Biblia huzalisha ukuaji wa Kiroho katika maisha ya Watakatifu wa Mungu. Biblia ni chakula cha roho ya Mkristo na inapaswa kusomwa kila siku ili kupata nguvu na kukua Kikristo.

    Yeremia 15:16—Maneno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ya furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu maana nimeitwa kwa jina lako, Ee BWANA, Mungu wa Majeshi.

    1 Petro 2:2—Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa,ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu:

    • Husafisha Maisha.

    Biblia inaweza kuyasafisha maisha ya wanaume na wanawake. Roho Mtakatifu atawahukumu wanadamu kwa Neno. Biblia itaonesha wanadamu kitu kinachopaswa kubadilishwa katika maisha yao. Maji yaliyopo katika Hema ya kukutania ni alama ya Neno la Mungu. Makuhani walipaswa kunawa katika maji hayo kila wakati waendapo kufanya ibada ya Bwana.

    Yohana 15:3—Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu lile neno nililowaambia. (Eph. 5:26)

    Zaburi 119:9—Jinsi kijana aisafisha njia yake? Kwa kutii akilifuata Neno lako.

     

    • Humjenga Aaminiye.

    Kunakuwepo na nguvu na kuwa na moyo katika neno la Mungu. Neno la Mungu litakujenga na kukuweka imara katika wakati mgumu. Wakristo wanaweza kusimama katika mwamba huu imara.

    Warumi 16:25—Sasa na atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara sawasawa na Injili yangu…

    Waefeso 2:20 -22—Mmejengwa  juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe Hekalu Takatifu katika Bwana. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.

    • Hukamilishwa katika utimilifu. (Soma Waefeso 4:11-15)
    • 4. Udhibitisho wa hakika wa uvuvio wa Biblia

      Upo ushahidi ulio wazi wa kudhibitisha uvuvio wa Biblia. Zaidi ya matamko yaliyomo katika maandishi yenyewe, taarifa nyingi za ukweli wa Biblia zinaonyesha kwamba maandiko yalivuviwa kwa utukufu.

      • Haijavunjwa na iko katika utimilifu ulio pamoja.

      Biblia inavyo vitabu 66 vilivyoandikwa kwa lugha 4 na watu 40 ambao walikuwa wakiishi umbali wa zaidi ya maili 1500 katika kipindi cha miaka 1600.  Watu waliotumiwa walitoka katika ngazi mbalimbali za maisha; Baadhi yao walikuwa wafalme, madaktari, manabii, wachungaji, wafanya kazi, wavuvi, na mmoja alikuwa mtoza ushuru.  Pamoja na ukweli huo mtiririko wake haukuvunjika na inao utimilifu ulio na umoja katika Biblia nzima. Hii inaweza kuwa kazi ya Mungu peke yake.  

      • Haiogopi kutoa Unabii

       Biblia husema mapema kuhusu matukio ya miaka au karne nyingi zijazo kabla hayajatokea. Wakati wa kuandikwa kwa unabii ulioko katika Agano la Kale unaweza kuelezwa kwa historia kwa sababu taarifa sahihi za historia kati ya maagano yote mawili imeendelea kuwepo.  Taarifa hii ya kihistoria inathibitisha tarehe ya kuisha kwa Agano la Kale kwa kuweka kipindi cha miaka 400 ambacho Biblia imekuwa kimya kati ya utabiri wa mwisho wa Agano la Kale na ukamilishaji wake kuanza katika Agano Jipya.

      Tarehe ambazo vitabu vya Biblia zimeandikwa zinaweza kupatikana katika historia. Uwepo wa Septuaginti, yaani ile tafsiri ya Kiyunani ya Agano la Kale unaweza kuwekwa kwa usahihi katika miaka 250 kabla ya Kristo. Kwa kuwa Septuaginti ilitafsiriwa kutoka katika maandishi ya Kiebrania ni lazima kulikuwepo na Agano la Kale la Kiebrania angalau miaka 250 kabla ya kuwepo kwa Agano Jipya. Uthibitisho huu ni wa kihistoria kwamba unabii huo uliandikwa miaka 100 kadhaa kabla ya kutokea utimilifu wake katika Agano Jipya. Hakuna uwezekano wa mwanadamu kuweza kutabiri kwa uhakika wa namna hiyo. Huu ni uthibitisho usiokuwa na ubishi ya kwamba Maandiko ya Injili yamevuviwa.

      MIFANO YA UNABII ULIOKAMILISHWA KWA UHAKIKA:

      • Unabii wa Kristo
      • Atakuwa ni wa uzao wa Abraham – Mwanzo. 22:18 – Mathayo. 1:1
      • Atakuwa wa ukoo wa Daudi – Yeremia. 23:5 – Mathayo. 1:1
      • Atatoka katika kabila la Yuda – Mika 5:2 – Mathayo. 1:2, Waebrania. 7:14
      • Atazaliwa katika mji wa Betlehemu – Mika 5:2 – Mathayo. 2:1
      • Kulikuwepo na unabii mara 29 uliotimia katika siku moja katika yale matukio ya kusulubiwa kwa Yesu ambayo utabiri wake ulikuwa na taarifa za kina tangu karne kadhaa kabla ya kifo chake.
      • Kulikuwepo na unabii zaidi ya mia tatu kuhusu Masiha iliyotimia kwa Kristo.

      Mdo. 3:18—Lakini mambo yale aliyohubiri Mungu tangu zamani kwa kinywa cha manabii wake wote, ya kwamba Kristo wake atateswa, ameyatimiza hivyo.

      Kristo alitimiza unabii wote katika Agano la Kale kumhusu yeye pamoja na mashaka yote. Hakuna mwanadamu mwenye uwezo wa kuchagua ukoo wake kabla ya kuzaliwa ingawa Yesu alizaliwa katika ukoo kama ilivyokuwa imetabiriwa na manabii. Walikuwepo watu wengine waliohusika katika ukamilisho wa unabii huo kama askari wa Kirumi ambao waligawana mavazi ya Yesu kati yao na kuipigia kanzu yake kura.  Hata lile giza lililotokea Kristo alipofariki linaweza kuthibitishwa kwa taarifa za historia na nyingine zilizoandikwa.  Nabii Amosi alitabiri giza lile miaka mia 700 hivi iliyopita kabla ya kutokea kwake.  Hakuna mwanadamu anayeweza kuelezea kwa usahihi kutimia kwa utabiri huu wa Kimasiha.  Huu ni uthibitisho ulio wazi wa uvuvio wa Biblia!

       

      • Unabii wa Israel
      • Musa alitabiri maisha ya baadaye ya Israel. – Kumb. 4:23-38.
      • Watawekwa mateka kwa sababu ya dhambi yao. –Isaya. 22:17, Yeremia. 20:6.
      • Watatawanyishwa katika nchi zote. – Kumb. 30:1-3.
      • Watapata mateso. – Lk. 19:41-44.
      • Kabla wa wakati wa kurudi Kristo, Israel itakusanywa tena katika ardhi yake. (Luka 21:29-32; Eze. 36-37) hili lilitimia 14, Mei 1948.

      Ezekieli 36:24—Maana nitawatwaa kati ya mataifa nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe.

      • Mungu alitamka kwamba atawalinda watu wake wa Israeli kama mchungaji (Yeremia 31:10). Chini ya saa 24 baada ya Israeli kutangaza uhuru wake mwaka 1948, nchi zinazoizunguka (Misri, Yordani, Iraq, Syria, na Lebanoni) ziliivamia Israeli kwa mategemeo kwamba wataliondoa Taifa la Kiyahudi na kuweka Taifa la Kiarabu. Nchi hizi ni kubwa kuliko Israeli, lakini Israeli kwa udogo wake iliendelea kuwepo hata baada ya kuwepo vita nyingine mbili kubwa (Vita ya siku 6, 1967 na Vita ya Yom Kippur, 1973).

      • Utabiri wa Mataifa
      • Babeli ilipinduliwa na kuangushwa kama Sodoma kama ilivyotabiriwa (Isaya. 13:19;  Yer. 51:37). Katika Danieli 5 kuna maelezo kuhusu kuhamishwa kwa madaraka kutoka Wamede na Waajemi.
      • Himaya ya Gresi ndio utawala wa tatu wa Shaba ndio utawala wa tatu ulioelezwa katika ndoto ya nabii kwenye kitabu cha Danieli 2:39 Babeli ukiwa ni Ufalme wa kwanza. Aleksanda Mkuu aliushinda ulimwengu kama ilivyo tabiriwa katika unabii huu. (ndoto hii ya Nabii inasomwa kwa kina katika mwaka wa tatu kwenye somo la Utabiri wa Manabii.)
      • Kugawanyika kwa Himaya ya Kirumi kumetabiriwa katika mgawanyiko wa miguu aliouona katika ndoto ni Nebukadneza katika Danieli 2.
      • Ninawi iliharibiwa kwa ya mataifa wahamiaji.  Nahumu (1-3, 3:7) ilitabiriwa kwamba malango yatawekwa wazi kabisa kwa manufaa yaadui zako (3:13).  Mto Tigrisi ulifurika wakati wa mashambulio na kubeba zile kuta pamoja na malango ya mji.

       

      • Mji wa Tiro ulikuwa uharibiwe kama ilivyo katika kitabu cha Ezekieli 26:3-14. Huu ni utabiri mahsusi uliotolewa 588 kabla ya Kristo.  Maandiko yanatamka kwamba mataifa mengi yataupinga mji wa Tiro. Sura ya 3.  

      Mungu alisema atamleta Mfalme wa Babeli kuwapinga. Aya ya 7.  Utabiri huu unasema kwamba yale mawe, mbao na udongo vitatupwa katika maji. Aya ya 12.  Nebukadneza, Mfalme wa Babeli, aliuzingira mji wa Tiro kwa miaka 13.  Aleksanda Mkuu aliuteka mji wa Tiro katika kile kisiwa mwaka 332 Kabla ya Kristo kwa kujenga daraja toka nchi kavu hadi kisiwani. Walitumia mawe, mbao kutoka kwenye majengo yaliyoharibiwa na udongo wakaujaza kutengeneza kinachoitwa bomazuizi (daraja la udongo) katika maji. Wale Askari waliweka mawe, mbao, na udongo majini kama ilivyotabiriwa na manabii. Jambo hili la hakika lililotabiriwa na likatokea siyo kubahatisha kwa binadamu peke yake.  Biblia ni Neno lililovuviwa la Mwenyezi Mungu. Lile Bomazuizi la Aleksanda Mkuu bado liko mahali pale hadi leo.   

      • Yesu alitangulia kuuzungumzia kuharibiwa kwa Hekalu la Yerusalemu. – Mt. 24:1-2, Mk. 13:1-3. Mji wa Yerusalemu uliharibiwa mwaka wa 70 Baada ya Kristo chini ya Jemadari Tito wa Kirumi. Lile Hekalu lilichomwa moto na ile dhahabu iliyokuwemo iliyeyukia katikati ya mawe yake. Wale askari walilivunja lile Hekalu Jiwe kwa Jiwe ili kuitoa dhahabu.  Kwa mara nyingine utabiri wa nabii umekamilika kwa kina kama Yesu alivyosema itakuwa.

       

      4. Unabii wa Siku za mwisho

       

      2 Timotheo 3:1-9—msitari 1 Mambo haya mfahamu pia, kwamba katika zile siku za mwisho…

       

      Yako maelezo mengi ambayo ni sahihi kuhusu siku za mwisho yanayopatikana katika Maandiko. Haya ni baadhi tu ya mambo yaliyotabiriwa ambayo yanaeleza hali ya siku zetu:

      • Kuongezeka kwa maarifa – Danieli 12:4

      Fikiria kuhusu vitu vyote vipya vilivyogunduliwa katika kipindi cha miaka 100.  Wale ndugu wawili wajulikanao kama Wright waliruka kwa ndege kwa mara ya kwanza 1903 na leo usafiri wa anga ni njia ya kawaida ya usafirishaji. Kumekuwa na maendeleo makubwa ya Teknologia katika muda mfupi sana.

      • Manabii wengi wa uongo – Mathayo 24:5,11
      • Vita nyingi na tetesi za vita – Mathayo 24:6
      • Njaa, majanga na matetemeko ya ardhi – Mathayo 24:7
      • Kutokuwepo usawa kumeenea – Mathayo 24:12
      • Injili kuhubiriwa ulimwenguni kote – Mathayo 24:14
      • Kula, kunywa na kuoana – Mathayo 24:38
      • Ni kama ilivyokuwa wakati wa Lutu – Luka 17: 28-29

      (walikunywa, wakauza, wakanunua, wakapanda na wakajenga. Hali hii inasikika sana kama ilivyo kwa watu wa leo. Kuna ongezeko pia la dhambi ya ushoga leo kuliko ilivyokuwa siku za Lutu.)

      • Kuiacha ile Imani – I Timotheo. 4:1

       

      • Usahihi wake Kihistoria

      Akiolojia ni kuhusu mafunzo mambo ya kale kwa kutafuta vitu vilivyotumiwa na watu wa zamani. Vitu hivi vya zamani vinatupatia habari kuwahusu watu ambao walivitumia. Kumesha gunduliwa vitu vingi kudhihirisha usahihi wa kihistoria wa Biblia. Kwa kweli, hakuna chochote cha akiolojia kilichopatikana kinachopinga Biblia.  Wakosoaji wamebisha kwamba Biblia si sahihi kwa historia lakini akiolojia inaendelea kudhihirisha kwamba Biblia ni ya kweli.  

      Makitaba ya Wahiti iligunduliwa huko Uturuki 1906 ikidhibitisha usahihi wa Taarifa ya Biblia kuhusu jamii ya Wahiti.

      Kumekuwep na vionzi vya mfupa vilivyopatikana vya majitu makubwa kudhibitisha maelezo ya majitu iliyoko katika Biblia.

      Masalia ya mtu aliye uawa kwa kusulubiwa yalipatikana Yerusalemu mwaka 1968. Masalia hayo yalikuwa na tundu la msumari katika miguu yake lililopita katika nyayo zote mbili na tundu moja la msumari katika viganja vya mikono. Mtu huyo aliaminika kwamba aliuawa na Warumi wakati wa uasi wa Wayahudi mwaka wa  70 baada ya Kristo.  Hii inathibitisha kwamba kusulubu msalabani ilikuwa ni njia ya kutekeleza hukumu ya kifo iliyotumiwa na Warumi kama ilivyoelezwa katika taarifa za Biblia kuhusu kusulubiwa kwa Yesu.

      Kitabu cha Matendo kimethibitishwa kihistoria kuwa sahihi.

      Michoro imegunduliwa yenye majina ya watu walioelezwa katika Biblia katika maeneo ambamo Biblia imewaweka.

      Zimekuwepo taarifa za kupatikana kwa vifaa vya akiolojia vinavyoendelea kudhibitisha usahihi kihistoria wa Biblia. Huu ni ushahidi zaidi ambao unathibitisha uvuvio wa Neno la Mungu.

       

      • Usahihi wa Kisayansi

       

      Biblia iko sahihi kisayansi.  Yapo mambo kadhaa katika Biblia ambayo wanadamu walioyaandika hawakuwa na uelewa wa kuweza kuyajua.  Mungu ndiye mwandishi wa Maandiko Matakatifu na anafahamu mambo yote.

      Maelezo yaliyoka katika Biblia ni ya kweli na yako sahihi kisayansi.

      Vipimo vya safina ya Nuhu alivyopewa na Mungu vinalingana na meli inayofaa kabisa kwa usafirishaji baharini.  Meli za kisasa zimeundwa kwa uelewa mkubwa wa fizikia na matumizi ya teknologia ya kompyuta na zinatumia vipimo kama alivyotumia Nuhu.  Isingewezekana Nuhu apate elimu hiyo kwa wakati wake.  Ni jambo la busara katika hali kama hiyo kuamini kwamba taarifa kuhusu vipimo vya safina katika Biblia ambavyo Mungu alimpatia Nuhu ni sahihi.

       

      Katika kitabu cha Ayubu kuna taarifa kuhusu kugawanywa kwa mwanga. Ayubu 38:24 Mwanga unaweza kugawanywa katika vipande kwa kutumia mche wa kioo. Hakuna uwezekano wa Ayubu katika kitabu chake ambacho ni cha zamani zaidi kuliko vyote katika Biblia aweze kufahamu kwamba mwanga unaweza kugawanywa.  

      Kitabu cha Mhubiri kinazungumzia mizunguko ya upepo. Kuna mizunguko ya upepo na maumbo yake ambayo imegundulika katika sayansi hivi karibuni kwa matumizi ya setelaiti na kompyuta. Watu katika zama za Agano la Kale wasingeweza kuwa na habari kama hizo japo kwa mara nyingine Biblia inayo taarifa sahihi kuhusu mizunguko ya upepo.

      Mwandishi wa kitabu cha maombolezo angewezaje kujua kwamba mito ilimwagikia baharini. –Mhubiri. 1:7

      Nabii Isaya alizungumza kuhusu Mungu akiwa ameketi katika duara ya dunia.  Isaya. 40:22.  Dunia haikuthibitishwa kuwa duara mpaka Magellani alipoizunguka kwa merikebu miaka ya 1500. Isaya hakuwa na uwezo wa kupata habari hizo. Ili kwa mara nyingine tena ni jambo linalothibitisha uvuvio wa Maandiko.

       

      • Ni Nguvu Isiyotegemea Rika

       

      Warumi 1:16—Kwa maana siionei haua Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao Wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia.

       

      Biblia ni zaidi ya kitabu. Biblia ni neno la Mungu.  Wale ambao wanaisoma Biblia kwa umakini katika imani wanaweza kubadilishwa kwa nguvu ya Mungu. Mungu anaweza kuitumia Biblia kubadilisha maisha ya wanadamu. Maisha ya watu wengi yameshabadilika kwa nguvu za Mungu kwa kuisoma tu Biblia na kuiamini.

      Biblia inanguvu za kuwaokoa watu katika hali zote za maisha: walevi, wabuya unga, malaya, wezi, wauaji, watenda dhambi wote. Wote wanaweza kuokolewa kwa njia ya Yesu Kristo. Tunaweza kupata muongozo katika Neno la Mungu kwa kila tukio la maisha yetu, kwa ushauri usiokuwa na ubaguzi wowote. Biblia inasimama imara juu ya kitabu chochote kile kilichoandikwa bila ushindani wala kupingana. Kwa usahihi Biblia ndio kitabu pekee alichoandika Mungu.