Skip to main content

Textbook (before Jacob)

MWAKA WA KWANZA KITABU CHA KIADA

UTANGULIZI WA BIBLIA

Uchunguzi wa Jumla wa Biblia

Utangulizi

MUONEKANO

Utangulizi wa Biblia utakuwa na somo lenye mambo yafuatayo:

  1. Vile vitabu 66 vya Biblia na mambo yaliyomo ndani kwa kifupi.
  2. Wahusika wakuu, maeneo, ukweli na matukio ya Biblia.
  3. Uvuvio wa Biblia.
  4. Kanuni za Biblia.
  5. Neno la Mungu katika nyakati mbalimbali.

Mtiririko wa Mafunzo: Utangulizi wa Biblia Takatifu na sababu zinazotufanya tuamini kwamba haina dosari, kosa, ni safi, na ni neno la Mungu lenye msukumo wake ambalo halina mgongano.

KUFAULU MAFUNZO HAYA

Vigezo vya mafunzo kwa ujumla:

  1. Kuhudhuria kila somo.
  2. Kufanya kazi za kuandika na nadharia.
  3. Kujifunza kwa kukariri:
    1. Maandiko.
    2. Orodha ya majina ya vitabu vya Biblia kama vilivyopangwa.
  4. Kutimiza kazi kwa wakati uliopangwa ikiwa ni pamoja na maswali ya kujifunza na mambo mengine ya kufanyia nyumbani kwa maagizo ya Mwalimu.

Maelezo ya Msingi ya Biblia

BIBLIA NI NINI?

Biblia ni Ufunuo wa Mapenzi ya Mungu kwa wanadamu.

Mungu hakuandika kitabu kingine zaidi ya Biblia. Hakuna ushahidi mwingine wowote wenye maelezo ya kina ya mapenzi ya Mungu na uwezo wake zaidi ya Biblia. Ni kwa kusoma Biblia peke yake ndio tunaweza kuwa na majibu kuhusu maswali mengi yanayomhusu Mungu.

  • Mungu ni nani?
  • Mungu anapenda nini?
  • Mungu anataka nini?
  • Mpango wa Mungu ni nini?
  • Kwa nini Mungu anatenda kile anachotenda?
  • Na, kadhalika.

Katika Biblia Mungu ameandaa maelezo ya habari za mapenzi yake na kuonyesha upendo wake kwa binadamu. Ufunuo mwingine wowote unapaswa kuoana na kitabu hiki cha ajabu. Ni kiwango cha uhai wote—wa muda mfupi na wa milele!

Dhamira kuu ya Biblia ni wokovu kupitia Yesu Kristo

(‘ya katikati’ -> kuu, kiongozi, dhamira ya msingi – mada, kama ya hotuba.)

MAMBO YANAYOIHUSU BIBLIA

Mwanzoni Agano la Kale liliandikwa kwa Kiebrania (na asilimia ndogo kwa Kiarabu.) Agano Jipya liliandikwa kwa lugha ya Kigiriki. Toleo la Kingereza la Mfalme Yakobo ni tafsiri inayotokana na lugha hizi asilia. ‘Kutafsiri’ maana yake ni kubadilisha kutoka lugha moja kwenda katika lugha nyingine.

Biblia ni kitabu kimoja, historia moja, na simulizi moja HISTORIA YAKE (Historia ya Mungu)! Tunaiita Biblia TAKATIFU kwa sababu ni Neno la Mungu na siyo hadithi tu ya wanadamu. Neno TAKATIFU maana yake tukufu, safi, isiyo na lawama, au ya kidini, iliyotengwa. Biblia ni kitabu cha Kimungu ingawaje Mungu aliwatumia watu kuueleza ukweli wake Mtakatifu. Watu watakatifu (asili yake binadamu) waliandika kama walivyo himizwa na Roho Mtakatifu (Utukufu wa asili ya Mungu). Kwa kuwa ni Neno la Mungu hatuwezi tukatimiza wazo kwa kitabu au taarifa moja ya Biblia.

Biblia inavyo vitabu 66. 39 katika Agano la Kale na 27 katika Agano Jipya. Utukufu wa Kimungu umefunuliwa katika Biblia kwa utaratibu kuanzia kitabu cha Mwanzo hadi mwisho wake katika Kitabu cha Ufunuo. Mwanzo ni kitabu kinachoonyesha asili; Ufunuo ni kitahu kinachohusu mwishoni. Vitabu vya Biblia vya katikati ni maneno ya Mungu ya uamsho kutoka katika ulimwengu ulioharibika. Kila kitabu cha Biblia kinao ujumbe wake, hata hivyo kitabu kizima kinakuwa na ujumbe wa wokovu wa mwanadamu ambao unaonekana. Inaweza kusemwa pia kwamba Agano la Kale ni taarifa ya taifa (Israeli) na agano jipya ni taarifa za mwanadamu (Yesu).

MAJINA YA BIBLIA TAKATIFU

Biblia Takatifu

Neno hili Biblia haliko mahali popote katika maandishi ya Biblia. Neno biblia tunalipata katika neno la Kigiriki biblios ambalo maana yake ni “vitabu.” Neno biblios kwa asili yake lilitumiwa kuhusiana na maandishi ya yaliyotumia mafunjo (magombo) katika utengenezaji wa karatasi za kale. Neno la Kingereza biblia maana yake “vitabu.” Biblia Takatifu ni kuhusiana na mkusanyiko wa vitabu Vitakatifu.

Majina ya Biblia kwa yenyewe

Kile Kitabu

Mwanzo 5:1—Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu.

Zaburi 40:7—Ndipo niliposema, Tazama nimekuja, (katika gombo la chuo nimeandikwa, (Ebr. 10:7)

Mathayo 1:1—Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo mwana wa Daudi, Mwana wa Ibrahimu.

Luka 4:17—Akapewa chuo cha Nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa.

Agano

Neno Agano maana yake mkataba au mapatano. Vitabu vya Biblia kwa mapatano ya zamani vinaitwa Agano la Kale na vitabu vya Biblia katika mapatamo mapya vinaitwa Agano Jipya.

II Wakorinto 3:14—Ila fikra zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi, wakati lisomwapo Agano la Kale, utaji uo huo wakaa; yaani, haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo.

II Wakorinto 3:6—Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa Roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.

Andiko

Neno andiko maana yake “maandishi.” Neno hili hutumiwa kuhusiana na maandishi matakatifu, na mara nyingi hutumiwa kwa uhusiano na Biblia. Yesu alizungumzia maandishi ya Nabii Isaya kama maandiko (Lk. 4:21). Yesu aliwauliza wakuu wa makuhani na wazee: “Hamkupata kusoma katika maandiko…” (Mt. 21:42). Kwa mara nyingine tena Yesu alitumia Neno hili alipokuwa akiongea na masadukayo: “mwapotea kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu” (Mt. 22:29). Sehemu nyingine kuhusu maandiko: Lk. 24:27, Rum. 1:2, Rum. 15:4, II Tim. 3:15-16; I Petro 1:20.

Neno la Mungu

Hili ndio muhimu, lenye nguvu na jina kamili la Biblia Takatifu. Biblia ni Neno la Mungu lililoandikwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya mwanadamu. Biblia siyo Neno la mwanadamu. Biblia ni Neno la Mungu. Taarifa muhimu: Mk. 7:13, Rum. 10:17, II Kor. 2:17.

Waebrania 4:12—Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na Roho na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

ULINGANISHO: AGANO LA KALE & AGANO JIPYA

Yote mawili huanza na Uungu

Agano la Kale huanza na Mungu (Mwanzo 1:1).

Agano Jipya huanza na Kristo (Mathayo 1:1).

Yote mawili hushirikiana dhamira moja

Wokovu kwa njia ya Yesu Kristo ni dhamira kwa Maagano yote mawili.

Agano la Kale huangalia mbele kwa imani katika msalaba. Ukombozi kwa damu ya Yesu ulikuwa mpango wa Mungu kwa Agano la Kale na ndio mpango wa Mungu kwa Agano jipya.

Ufunuo 13:8—Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana—Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.

Mpango wa Mungu toka mwanzo wa nyakati ni wa Yesu ambaye ni Kondoo wa Mungu kumwaga Damu Yake Takatifu kwa malipo ya ukombozi wetu.

Agano Jipya huangalia nyuma katika kazi iliyokamilishwa katika msalaba.

Kristo yupo katikati ya yote mawili

Agano la kale limejaa utabiri wa Kristo. Utabiri huu huitwa Utabiri wa Mesia. Agano la kale linavivuli vingi na viashiria vinavyoonesha ujio wa Kristo. Sheria ni mwalimu wa kutupeleka kwa Kristo (Gal. 3:24). Kristo ni utimilifu wa sheria.

Mathayo 5:17—Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; laa, sikuja kutangua bali kutimiliza.

Kristo ndie mtu wa katikati katika Agano Jipya. Kristo ndiye mpatanishi wa Agano Jipya (Ebr. 12:24).

AGANO LA KALE NA AGANO JIPYA: LILIVYO TENGANISHWA

AGANO LA KALE

Historia

  • Yoshua
  • Waamuzi
  • Ruthu
  • 1 Samweli
  • 2 Samweli
  • 1 Wafalme
  • 2 Wafalme
  • 1 Mambo ya Nyalati
  • 2 Mambo ya Nyalati
  • Ezra
  • Nehemia
  • Esta

Ushairi

  • Ayubu
  • Zaburi
  • Mithali
  • Mhubiri
  • Wimbo ulio bora

Manabii Wakuus

  • Isaya
  • Yeremia
  • Maombolezo
  • Ezekieli
  • Danieli

Manabii Wadogo

  • Hosea
  • Yoeli
  • Amosi
  • Obadia
  • Jona
  • Mika
  • Nahumu
  • Habakuki
  • Sefania
  • Hagai
  • Zekaria
  • Malaki

Agano Jipya

Injili

  • Mathayo
  • Marko
  • Luka
  • Yohana

Historia

  • Matendo

Nyaraka za Paulo

  • Warumi
  • 1 Wakorinto
  • 2 Wakorinto
  • Wagalatia
  • Waefeso
  • Wafilipi
  • Wakolosai
  • 1 Wathesalonike
  • 2 Wathesalonike
  • 1 Timotheo
  • 2 Timotheo
  • Tito
  • Filemoni

Mkuu wa nyaraka

  • Waebrania
  • Yakobo
  • 1 Petro
  • 2 Perto
  • 1 Yohana
  • 2 Yohana
  • 3 Yohana
  • Yuda

Unabii

  • Ufunuo

KUSUDI LA BIBLIA

Biblia iliandikwa ili wanadamu wa weze kuamini, kuelewa, kufahamu, kupenda, na kumfuata Kristo.

Kwamba wanadamu wataweza kuamini kuwa Yesu ndiye Kristo.

Dhamira kuu ya Biblia ni ukombozi kwa njia ya Yesu Kristo. Neno Kristo maana yake “aliyepakwa mafuta”, na ni kumhusu Masia. Wanadamu wanapaswa kuamini kwamba Yesu ndiye Mwokozi (Warumi 1:16).

Yohana 20:31—Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, mwana wa Mungu; na kwa kuamini muwe na uzima kwa jina lake.

Kwamba wanadamu wataweza kuelewa Kristo ni nani.

Yesu anajifunua Mwenyewe katika Neno Lake. Biblia inatuambia kwamba Maandiko yanamthibitisha Yesu. Wanadamu wanapaswa kuelewa kwa tafakari ya Neno kwamba Yesu ndiye Masia; Yeye ndiye Mwokozi na njia pekee ya kupata Wokovu.

Yohana 5:39—Mwayachunguza Maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia.

Ili wanadamu waweze kumfahamu Kristo. Biblia huwasaidia wanadamu kumfahamu Kristo.

Mwandishi wa wimbo alitamka, “Ninayo furaha kwa kuwa ninamjua Yesu!” Paulo alitamani kumfahamu Kristo kwa undani zaidi. Wakristo wanaweza kufahamu Yesu ni nani na wanaweza pia kumjua binafsi kwa kushirikiana naye katika masomo.

Yohana 17:3—Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

Ili wanadamu wampende Kristo

Kufuatana na Maandiko, ili mwanadamu ampende Kristo anapaswa kuyashika maneno yake Kristo ambayo yamo katika Biblia. Inatupasa kujifunza Biblia ili tuweze kulitii Neno la Mungu na kumpenda Yesu.

Yohana 14:23—…mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda…

I Yohana 2:5—Lakini yeye alishikaye Neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika…

Ili wanadamu weweze kumfuata Kristo

Neno Mkiristo maana yake “Mtu anayemfuata Kristo.” Biblia imeandikwa ili wanadamu waweze kumfuata Kristo.

Yohana 10:27—Kondo wangu waisikie sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata.

Yohana 12:26—Mtu akinitumikia, na anifuate…

Biblia inaonesha kusudi na mpango wa Mungu

Mambo yanayohusu Wokovu

Biblia inaeleza kwamba wokovu unapokelewa kwa njia ya kumwamini Yesu na inaonyesha jinsi mwanadamu anavyohitaji wokovu.

Yohana 3:16—Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Kulihusu Kanisa

Katika mpango wa Mungu kulihusu kanisa lake ni kwamba ndilo linalopaswa kuwa tukufu, takatifu lisilo na mawaa. Yapo maagizo mengi kwa kanisa katika Biblia.

Waefeso 5:27—Ili apate kujiletea kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.

Kuhusu siku za mwisho

Biblia inaonyesha mpango wa Mungu kwa siku za mwisho. Tunaelewa kwamba Biblia inasema tunaishi katika siku za mwisho naye Mungu alituonya kuhusu matukio yatakayokuja kupita katika siku hizi za mwisho.

II Timotheo 3:1—Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.

Biblia ni andiko la Neno la Mungu kwa mwanadamu

Ni neno la hakika lililotabiriwa na manabii

Bibilia ni Neno la Mungu lisilokuwa na kosa. Siyo kwamba lina neno la Mungu ndani yake bali ni Neno la Mungu. Biblia ni Neno makini katika saa ya giza.

II Petro 1:19-21—Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu. 20. Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. 21. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Ni msingi imara (I Kor. 3:11)

Neno la Mungu ni msingi imara wa imani yetu. Yesu ni mwamba wa wokovu wetu. Yesu ni Neno lililogeuka nyama. Wakati kila kitu kingine kikiwa kinazama; Neno la Mungu halitashindwa.

I Wakorinto 3:11—Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.

Ni Neno lenye nguvu lisilokuwa na kosa

Neno nguvu maana yake “Lenye pumzi ya Mungu.” Kuna uhai katika Neno ambao ni pumzi halisi ya Mungu. Neno la Mungu ni bila makosa au kupingana.

II Tim. 3:16—Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kuwaonya watu makosa yao, na kuwaongoza, na kuwaadibisha katika haki:

Biblia ni mamlaka ya mwisho

Kuhubiri na kufundisha ni lazima msingi wake uwe ni Neno la Mungu (II Tim. 4:2)

Paulo alimwambia Timotheo alihubiri Neno. Neno ni msingi wa imani yetu (Rum. 10:17). Tunachoamini na kukihubiri kinapaswa kuwa na uelewano mzuri na Biblia.

Kila swali linapaswa kutulizwa kwa Neno la Mungu

Ni sharti Biblia iwe mamlaka kuu katika kila eneo la swali katika maisha ya wanadamu. Mamlaka ya Neno la Mungu haipaswi kuwekewa maswali na mtakatifu wa Mungu. Hii ndio sababu inayotufanya tulazimike kufahamu bila mashaka yoyote kwamba tunalo neno la Mungu leo.

Sehemu muhimu katika Biblia

Ifuatayo ni orodha ya sehemu muhimu za Biblia na maelezo mafupi kuhusu kilichotokea katika kila sehemu mojawapo. Kujifunza kwa moyo sehemu hizi na kujua kilichotokea katika kila sehemu mojawapo kutakupatia picha nzuri ya Biblia yote.

SEHEMU MUHIMU KATIKA AGANO LA KALE

MAHALI MAELEZO ANDIKO
Edeni Mungu alimuumba mwanadamu na kumweka katika Bustani ya Edeni. Eneo la anguko la mwanadamu Mwanzo 2:8
Mlima Ararat Mahali safina ya Nuhu ilipokuja kusimama baada ya ile gharika. Mwanzo 8:1-5
Babeli Mnara uliojengwa kuifikia mbingu na Mungu akawafanya wanadamu waongee katika lugha tofauti. Babeli maana yake mkanganyiko Mwanzo 10:10; 11:4
Uri wa Wakaldayo Mahali abrahamu alipoambiwa mwanzoni aende Kanaani. Nchi ambayo baadaye ilikuja kuitwa Babeli. Nehemia 9:7
Kanani Nchi ya ahadi ambayo walimoishi Abrahamu, Isaka na Yakobo. Yoshua aliiteka na kugawia kila kabila sehemu. Mwanzo 12:5
Misri Nchi Yusufu alikouzwa kuwa mtumwa. Israeli ikadumu utumwani miaka 400. Musa aliitoa Israeli kutoka Misri. Mwanzo 12:10
Mlima Sinai Mahali Musa alipoona kichaka kinachowaka moto na baadaye akapokea sheria na agano. Kutoka 19:11
Nyikani Watoto wa Israeli walihangaika jangwani kwa miaka 40 kwa kutoamini kwao. Matendo 7:42
Syria Mateka wa Israeli walipelekwa Syria. 2 Fal. 18:11
Babeli Mateka wa Yuda walipelekwa Babeli. Danieli alikuwa mmoja wao. Danieli 1:1

AGANO JIPYA – MAENEO MUHIMU

MAHALI MAELEZO ANDIKO
Betlehemu Mahali pa asili—Kuzaliwa Kristo katika hori. Luka 2:7
Galilaya Palistina iligawanywa katika mikoa mitatu, Yudea, Samaria, na Galilaya, ambayo ilijumuisha eneo lote la kaskazini la nchi (Mdo. 9:31), ambao ndio mkubwa zaidi. Luka 4:14
Getsemane Mahali pa Kristo pa sala na aliposalitiwa na Yuda. Mat. 26:39
Golgota Mahali Kristo aliposulubiwa. “Mahali pa fuvu la kichwa.” Marko 15:22-28
Yerusalemu Huitwa pia: Salemu, Arieli, Yebusi, "Mji wa Mungu," "mji mtakatifu;" wakati fulani "Mji wa Yuda" Mahali lilipozaliwa kanisa la Agano Jipya. Mdo 1:8 (2:25, 28)
Samaria Samaria mkoa ulioko katikati ya Palestina lakini hauchukuliwi kama nchi takatifu. Umbali kati ya Samaria na Israeli ambayo ni mji mikuu ya falme mbili ni maili 35 tu katika mstari ulionyooka. Yoh. 4:1-5

Watendaji muhimu katika Agano la Kale

  • Mungu—Biblia inatueleza kwamba Mungu ni roho (Yohana 4:24). Mungu ni Roho nao wamuabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli (Strong) Mungu ni zaidi ya mtendaji katika Biblia; Mungu ni chimbuko la kila kiumbe. Biblia inamfunua Mungu kwa mwanadamu.
  • Shetani—Neno shetani maana yake anayeshtaki. Yeye ndiye anayeshtaki kati ya wanaoamini (Ufunuo 12:10). Shetani huitwa pia muovu. Mungu hakumuumba muovu. Mungu alimuumba malaika Lusiferi ambaye alianguka kwa sababu ya dhambi akawa muovu (Isaya 14:12, Lk. 10:18).
  • Adamu—Mungu alimuumba Adamu, mwanadamu wa kwanza, akamuweka katika Bustani ya Edeni. Ni yeye ndiye aliyeingiza dhambi katika jamii ya wanadamu (Rum. 5:12).
  • Eva—Mungu alimuumba Eva, mwanamke wa kwanza, kutokana na ubavu mmoja wa Adamu (Mwanzo 2:21-22).
  • Kaini—Mwanaye Adamu wa kwanza. Alikuwa mkulimaAlimuua nduguye Abeli na kuwa muuaji wa kwanza (Mwa. 4:1).
  • Abeli—Mwanaye Adamu wa pili aliyeuawa na Kaini. Alikuwa mchungaji (Mwa. 4:2).
  • Seti—Mwanae Adamu wa tatu (Mwa. 5:3).
  • Nuhu—Alijenga safina kulinda uhai katika dunia (Mwa. 6:13-22)
  • Abram—Mungu alimwita Abram aondoke nyumbani na kwenda katika nchi isiyojulikana ambako Mungu atamfanya baba wa taifa kubwa, ndio historia ya Wayahudi ikaanza (Mwa. 12:1-3). Mungu alibadili jina lake kutoka Abram Baba Mkubwa kuwa Abrahamu Baba wa Umati (Mwa. 17:5).
  • Isaka—Mwanaye Abrahamu wa agano aliyempata kwa ahadi uzeeni (Mwa. 17:19).
  • Yakobo—Jina lake lilibadilishwa na Mungu likawa Israeli. Wanae 12 ndio waliounda makabila ya taifa la Israeli (Mwa. 32:28).
  • Yusufu—Mwanaye Yakobo ambaye aliuzwa utumwani Misri. Mungu alimpandisha cheo hadi nafasi ya pili katika ufalume na akamtumia kuilinda Misri na Israeli. Yakobo na familia yake walihamia Gosheni wilaya iliyoko Misri (Mwa. 37:36, 42:1-3).
  • Farao—Cheo cha mtawala wa Misri. Watoto wa Israeli walikuwa utumwani Misri kwa miaka 400. Mungu aliufanya moyo wa Farao aliyetawala wakati wa Kutoka kuwa mgumu na akawaondoa Waisraeli kutoka Misri kwa mkono wenye nguvu (Kut. 1:11-14, 6:1).
  • Musa—Mungu alimwinua Musa kwenda kuwatoa utumwani Misri wana wa Israeli. Alipokea amri zake na agano katika mlima Sinai. Aliwaongoza Waisraeli kwa miaka 40 (Kut. 3:10-12).
  • Aroni—Ndugu yake Musa na Kuhani Mkuu kwa utaratibu wa Makuhani (Kut. 28:1-3).
  • Kalebi—Mmojawapo wa wapelelezi aliowatuma Musa wakamletea taarifa nzuri (Nu. 13:30).
  • Yoshua—Aliteuliwa na Mungu kuwa mrithi wa Musa. Yoshua aliwaongoza Waisraeli wakaishinda Kanani (Nu. 27:18-23).
  • Waamuzi—Walikuwepo Waamuzi 15 waliotawala Israeli baada ya kifo cha Yoshua. Hili ni jina la kitabu kimojawapo katika Agano la Kale.
  • Ruthu—Wamoabi ambao walirudi Betlehemu pamoja na Naomi mume wake alifia Moabu kabla Naomi hajarudi Betlehemu. Ruthu aliolewa na Boazi akawa mmoja katika uzao wa mstari wa Kristo.
  • Samweli—Aliitwa akiwa kijana na akawa mmoja wa manabii wakuu wa Israeli (I Sam. 3:20).
  • Saulo—Mfalume wa kwanza wa Israeli (I Sam. 15:1).
  • Daudi—Kijana mchungaji aliyemuua Goliati. Mungu alimteua kuwa mfalume wa Israeli badala ya Saulo (II Sam. 5:3-12).
  • Solomoni—Mwanae daudi na mrithi wa ufalme wake. Mungu alimruhusu achague chochote apendacho. Yeya aliomba moyo mnyoofu na Mungu alimfanya awe na busara kuliko binadamu yeyote. Alijenga hekalu lililojulikana kama Hekalu la Solomoni (I Fal. 3:5-12).
  • Eliya—Nabii shupavu wa Mungu. Aliilaani Israeli ikapigwa na ukame kwa sababu ya dhambi. Aliomba moto ushuke kutoka mbinguni katika mapambano yake na manabii wa baali katika mlima Karmeli. Alishinda kifo na alipanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli (II Fal. 2:11).
  • Elisha—Mtumishi wa Eliya. Aliyechaguliwa na Mungu achukue nafasi yake kama nabii wa Israeli (I Fal. 19:16).
  • Isaya—Alimuona Bwana ameketi katika kiti cha Enzi kilicho juu sana na kuinuliwa sana na pindo za vazi lake zikalijaza Hekalu. Nabii aliyeonya Taifa la Israeli kutubu vinginevyo hukumu ya Mungu italiangukia (Isaya. 6:1).
  • Yeremia—Aliitwa kuwa nabii wa Mungu akiwa tumboni kwa mama yake. Alielezewa kama Nabii aliaye aliyeshinda dhambi za Israeli (Yer. 1:5).
  • Ezekieli—Alitabiri kutekwa kwa Yerusalemu kwa sababu ya dhambi zao (Eze. 3:4).
  • Danieli—Alichukuliwa na Nebukadneza kama mmojawapo wa mateka ya Yerusalemu. Alitafsiri ndoto ya Nebukadneza na kuelezea kuzuka kwa Himaya nyingi. Alipokea maono ya siku za mwisho na alikuwa mashuhuri katika himaya za Babeli na Persia (Dan. 1:6).
  • Ezra—Kuhani na Mwandishi aliyerudi Yerusalemu kulijenga tena Hekalu (Ezra 7:6).
  • Nehemia—Alikuwa mbeba kikombe aliyerudi Yerusalemu na kuwa kiongozi katika ujenzi mpya wa Hekalu. Imeelezwa katika kitabu cha Nehemia.
  • Esta—Malikia wa Ahesueru ambaye alikuwa mfalme katika mkoa wa Persia. Alitimiwa na Mungu kusimamisha njama za kuwaangamiza watu wake ambao ni Wayahudi. Imeelezwa katika kitabu cha Ester

Wahusika Wakuu katika Agano Jipya

  • Yohana Mbatizaji—Aliyemtangulia Kristo. Alibatiza wale waliotubu dhambi zao katika mto Yordani (Mt. 3:5-6).
  • Yesu Kristo—Mwana pekee wa Mungu. Mhusika Mkuu katika Agano Jipya. Agano jipya lote kwa kipekee linaweka katikati kazi za Kristo duniani, lakini Biblia kwa ujumla wake inaonyesha kwamba inamhusu kwa njia moja au nyingine.
  • Wafuasi 12–Waliitwa na kufundishwa na Yesu; Kwamba watakuwa viongozi wa kanisa katika Agano Jipya. 1) Petro, 2)Andrea ndugu yake Petro 3)Yakobo mwanaye Zebedayo 4) Yohana ndugu yake Yakobo 5) Filipo 6) Bartolomeo 7) Tomaso 8) Matayo aliyekuwa mtumishi 9) Yakobo mwanaye Alfayo 10) Tadei 11) Simoni wa Kanani, na 12) Yuda Iskarioti.
  • Stefano—Mmoja wapo wa wale Mashemasi saba wa Kanisa waliochaguliwa kwanza katika Yerusalemu na kutofautishwa kati yao kama "mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu." Alipigwa mawe hadi kufa chini ya utawala wa Sanhedrin ambao Saulo wa Tarso alikuwa mwanachama wake. Kifo cha Stefano ilikuwa ni mwanzo wa mateso makali kwa juhudi zilizoongozwa na Saulo, ambazo zilisababisha kuenea zaidi kwa Neno la Mungu (Mdo. 8:1, 4; 11:19-21).
  • Philipo—Shemasi na Mwinjilisti (Mdo. 6:5; 21:8; Efe. 4:11). Alikuwa na watoto wa kike wanne waliojaliwa kipaji cha unabii (Mdo. 2:17; 21:8-9). Baada ya kifo cha Stefano alihubiri injili toka Samaria na kwa towashi Mhabeshi kwa mafaniko makubwa na kukawepo na miujiza mingi.
  • Paulo—Aliinuliwa kuwa Mtume wa Mataifa. Alikuwa chombo cha kibinadamu kilichofikisha sehemu kubwa ya Agano Jipya kwa mataifa (Mdo. 9:15).

Matukio Makuu ya Biblia

Uumbaji

Taarifa ya Uumbaji wa dunia (Mwanzo 1, 2).

Anguko la mwanadamu

Eva alishauriwa na nyoka kula tunda lililokatazwa. Adamu pia alikula tunda alipopewa na Eva. Biblia inatueleza kwamba Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi: Rum. 5:12 taarifa hii ya dhambi ya kwanza huelezwa kama anguko la mwanadamu.

Gharika kuu

Mungu alimwambia Nuhu kwamba ataharibu kila kiumbe kwa sababu ya dhambi ya mwanadamu. Mungu alimwagiza Nuhu ajenge safina ili imuokoe Yeye na familia yake. Mungu alimwagiza Nuhu kuwaleta wawili katika kila aina ya mnyama asiyekuwa msafi na wanyama saba kati ya walio safi katika safina (Mwa. 6).

Kuitwa Abram

Bwana alimwita Abram kutoka Uri ya Kaldayo. Mungu akamwambia kwamba atamwonyesha njia ya kwenda nchi nyingine. Abram akaipokea ahadi kwamba atakuwa taifa kubwa. Nchi ya Kanani ndio iliyokuwa nchi ambayo Mungu alimwelekeza. Abram aliipokea ahadi kwamba familia zote zitabarikiwa katika Abram. Hii ni ahadi kwamba Masiha (Mwa. 12:1-3).

Utumwani Misri

Yakobo aliwatuma wanae Misri kununua mkate kwa sababu nchi ilikuwa na njaa. Mungu akamuweka Yusufu nafasi ya pili katika uongozi wa Misri. Yakobo na wanaye walikuja kuishi Gosheni jimbo mojawapo la misiri ili kuwaweka watoto wa Israeli hai wakati wa njaa. Baadaye aliinuka Farao, Mfalme aliyewaingiza utumwani Wayahudi.

Kutoka

Mungu akamwinua Musa akawatoe utumwani Israeli kutoka Misri. Mungu aliongoza Israeli kutoka Misri kwa mkono wenye nguvu. Kuondoka huku kutoka Misri huitwa Kutoka.

Kupokea Amri

Musa alipokea Sheria ya Mungu katika mlima Sinai. Mungu alimkabidhi zile Amri Kumi katika vigae viwili vya mawe. Kutangatanga Nyikani. Watoto wa Israeli walitangatanga katika nyika kwa miaka 40 kwa sababu ya dhambi. Mungu hakuwaruhusu waingie katika Nchi ya Ahadi kwa sababu ya kutokuamini kwao (Ebr. 3:19).

Kuishinda Kanani

Mungu alimwinua Yoshua kuwaongoza Waisraeli hadi katika nchi ya Ahadi. Taarifa ya Israeli kujipatia Nchi ya Ahadi huitwa kuishinda Kanani.

Ujenzi wa Hekalu

Mungu alimtumia Solomoni kumjengea nyumba ya kudumu kwa ajili ya kuabudia. Israeli walitumia chombo kinachohamishika kinachoitwa Tabernakulo kuabudia walipokuwa njiani kuelekea Kanani. Mungu alimwagiza Sulemani kumjengea nyumba ya kudumu ya kuabudia walipo stawi katika ile nchi. Mateka Babeli. Mungu aliruhusu Israeli ishindwe na Babeli kwa sababu ya dhambi yao. Hekalu lilibomolewa na vyombo vya dhahabu vikaporwa. Kuna vipindi vitatu ambapo Israeli waliwekwa mateka na kupelekwa Babeli.

Hekalu kujengwa tena

Mungu alimwinua Ezra na Nehemia kulijenga tena Hekalu.

Kuzaliwa Kristo

Kristo alizaliwa Betlehemu kama ilivyo katika maandiko. Kuzaliwa kwa Kristo ni jambo kuu katika historia yote. Tarehe huandikwa KK Kabla ya Kristo na KB katika mwaka wa Bwana.

Kristo kusulubiwa

Yesu alikuja kuununua wokovu wa mwanadamu. Kristo alisulubiwa kama sadaka kuu kwa ajili ya dhambi za wanadamu.

Ufufuko wa Kristo

Yesu alifufuka katika wafu. Kwa kifo Kristo alivunja nguvu za yule aliyekuwa na uwezo juu ya kifo; ambaye ni yule muovu (Ebr. 2:14).

Siku ya Pentekoste

Kanisa lilizaliwa katika Siku ya Pentekoste. Hii ni ile siku ambayo Mungu alitoa zawadi ya ubatizo kwa Roho Mtakatifu.

Muhtasari wa Biblia

Muhtasari wa Agano la Kale

TORATI

  • Mwanzo ni kitabu cha mambo yaliyoanza. Kitabu hiki kina taarifa ya uumbaji wa ulimwengu wote. Kinazo habari za historia ya mwanzo ya Abrahamu na Israeli.
  • Kutoka inazo habari za kipindi cha Israeli kuwa ugenini na kukombolewa kwao kutoka utumwani Misri. Zile Amri kumi na safari za Israeli kwanda kanani zinajumuishwa.
  • Mambo ya Walawi. Kitabu chenye Sheria za Mungu.
  • Hesabu. Kitabu cha miaka 40 ya Israeli kutangatanga nyikani.
  • Torati. Kitabu hiki kina marudio ya Sheria za Mungu.

HISTORIA

  • Yoshua. Taarifa ya kuinyakuwa Kaanani chini ya uongozi wa Yoshua na ugawaji wan chi kwa makabila 12.
  • Waamuzi. Historia ya utoaji wa nchi kwa uongozi wa waamuzi.
  • Ruthu. Hadithi ya mwanamke asiyekuwa Muisraeli aliyeolewa na Boazi na kuwa sehemu ya mstari wa kuzaliwa Kristo
  • I & II Samweli. Historia ya Samweli na miaka ya mwanzo ya wafalme Saulo na Daudi.
  • I & II Wafalme. Historia ya mwanzoni ya ufalme wa Israeli na ufalme uliogawanyika. Manabii Eliya na Elisha wanaonekana katika vitabu hivi.
  • I & II Mambo ya Nyakati. Taarifa ya utawala wa Daudi na Sulemani na ufalume wa Yuda mpaka wakati wa kuchukuliwa mateka.
  • Ezra. Taarifa ya kurudi kwa Wayahudi kutoka kuwa mateka na kujengwa upya Hekalu.
  • Nehemia. Inaelezea ujenzi mpya wa kuta za Yerusalemu na kurudishwa tena Sheria.
  • Esta. Hadithi ya Israeli na ya Esta kuhusu ukombozi kutoka katika njama ovu za Hamani.

USHAIRI

  • Ayubu. Masimulizi ya mateso ya Yobu na ushindi wa wake. Huenda hiki ndio kitabu cha zamani zaidi katika Biblia.
  • Zaburi. Mkusanyiko wa mashairi, sala na nyimbo za rohoni.
  • Methali. Mkusanyiko wa mambo ya maadili na, kidini pamoja na maagizo kwa hekima.
  • Mhubiri. Mawazo kuhusu umuhimu wa maisha na wajibu wa mwanadamu kwa Mungu.
  • Wimbo ulio Bora. Shairi linaloonesha upenda kati ya Kristo na Bibi harusi wake.

MANABII WAKUU

  • Isaya. Manabii Mkuu wa ukombozi. Isaya anaionya Israeli kutotenda dhambi.
  • Yeremia. Nabii aliaye aliyeomboleza dhambi za watu wake. Aliwaonya watubu au wategemee kupata hukumu ya Mungu.
  • Maombolezo. Taarifa ya maombolezo ya Nabii Yeremia.
  • Ezekieli. Ezekieli anaonesha hali ya kurudi rudi nyuma ya watu wa Mungu.
  • Danieli. Taarifa ya baadhi ya matukio wakati wakiwa mateka. Danieli alikuwa ni mmoja wapo wa mateka aliyepelekwa Babeli. Ipo taarifa ya kuhamishwa mamlaka kutoka Babeli kwenda uajemi. Kitabu hiki kina maono nyakati za mwisho.

MANABII WADOGO

  • Hosea. Nabii huyu ni wa wakati mmoja na Isaya na Mika. Uasi wa Israeli ni wazo kuu la kitabu hiki.
  • Yoeli. Nabii wa nchi ya Yuda anaye litaka taifa litubu kitabu hiki kina taarifa za mwisho za utabiri na ahadi za ujio wa Roho Mtakatifu. .
  • Amosi. Nabii mchungaji. Analaani utendaji dhambi wa watu.
  • Obadia. Anatabiri kuangamia kwa Edomu na mwisho ukombozi wa Israeli.
  • Yona. Nabii aliyesita alipoagizwa na Mungu aende Ninawi. Alimezwa na samaki na kutapikwa alipofikishwa Ninawi kama Mungu alivyotaka.
  • Mika. Kitabu hiki kinaonesha hali mbaya ya maadili ya Israeli na Yuda.
  • Nahumu. Kinao utabiri wa kuharibiwa kwa Ninawi. Yuda kuahidiwa ukombozi kutoka Siria.
  • Habakuki. Kiliandikwa kipindi cha Kaldayo. Kitabu hiki kinazungumzia uwezekano wa Mungu kuruhusu hukumu kuifikia Israeli.
  • Sefania. Kinazo taarifa za utukufu ujao wa Israeli.
  • Hagai. Nabii wa wakati mmoja na Zekaria. Anawakemea watu kwa uvivu wao katika kujenga hekalu la pili. Ipo ahadi ya ukuu wa kurudi tena kwa utukufu wa Mungu katika hekalu.
  • Zekaria. Alisaidia kuhamasisha Wayahudi kulijenga upya Hekalu.
  • Malaki. Anaonesha kipindi cha mwisho cha historia ya Agano la Kale. Anazungumzia haja ya kufanya mabadiliko kabla ya ujio wa Masiha.

Muhtasari wa Agano Jipya

Injili

Neno Injili maana yake: habari njema. Injili zinasimulia Habari Njema za Yesu Kristo. Siyo historia za watu na hazielezi kila tukio katika maisha ya Kristo.

  • Mathayo. Mathayo anaandika kama "Muisraeli hasa," Myahudi aliyegeuzwa akiagiza jamii yake. Ananukuu mara nyingi kutoka Agano la Kale na kusisitiza Umasiha wa Kristo.
  • Marko. Marko kimsingi aliwaandikia Warumi (ndio kusema anaelezea mara kwa mara mila za Kiyahudi). Marko anakariri ukweli kwa matendo na mwelekeo na anasisitiza tabia ya Utumishi wa Kristo.
  • Luka. Luka anawakilisha Kristo kama rafiki mnyenyekevu wa watenda dhambi, Mkombozi wa ulimwengu. Hii ni injili ya wema wa Mungu kwa ulimwengu. Imelelekezwa kwa mataifa na imesisitiza Utu wa kristo kwa kurudia kumuita “Mwana wa adamu.”
  • Yohana. Yohana anamtambulisha Kristo kama mwana wa Mungu katika mwili. Ni injili ya kiroho zaidi kuliko ya kihistoria, ambayo imeondoa mambo kadhaa ya wainjilisti wengine na inayo mambo mengi zaidi kuliko wanayofanya kwa mawazo ya kiroho. Yohana anasisitiza Uungu wa Kristo na inayo aya muhimu ya Biblia: Yohana 3:16.

Historia

  • Matendo ni taarifa ya kuzaliwa kwa kanisa siku ya Pentekoste. Hii ni historia ya maendeleo ya kanisa la mwanzo.

Nyaraka za Mtume Paulo

  • Waraka ni barua. Hizi ni barua zenye pumzi ya Roho Mtakatifu kwa ajili ya Kanisa.
  • Warumi. Dhamira kuu ni kuhesabiwa haki kwa imani. Paulo anawaandikia Wakristo wajibu wao katika nusu ya pili ya kitabu hiki.
  • I & II Wakorinto. Walioandikiwa ni waumini wa Kanisa la Korinto. Kitabu hiki kinasafisha makosa katika kanisa. Paulo anatoa maagizo kwa Kanisa. Neno hili bado linafaa katika kanisa hadi leo.
  • Wagalatia. Walioandikiwa ni waumini wa kanisa la Galatia. Paulo anafafanua kuhesabiwa haki kwa imani na analionya kanisa kuhusu kurudia ibada za Yuda.
  • Waefeso. Walioandikiwa ni waumini wa kanisa la Efeso. dhamira kuu ni umoja wa watakatifu. Paulo anahamasisha umoja kati ya Wayahudi waliogeuka na Mataifa watakatifu.
  • Wafilipi. Walioandikiwa ni waumini wa kanisa la Wafilipi. Yesu Kristo ndiye ujumbe mahususi.
  • Wakolosai. Walioandikiwa ni waumini wa kanisa la Kolosai. Kristo amesisitizwa kwamba Yeye ni kichwa cha kanisa. Paulo anahamasisha kanisa na kuwaonya dhidi ya mafundisho ya uongo.
  • I & II Wathesalonike. Walioandikiwa ni waumini wa kanisa la Thesalonike. Paulo analitia moyo kanisa. Barua hizi zinahusu ujio wa pili wa Kristo.
  • I & II Timotheo. Paulo anamshauri kijana Timotheo kuhusu utumishi. Paulo anamhimiza Timotheo kulihubiri Neno. Ushauri huu na hamasa unamhusu kila mhudumu.
  • Tito. Paulo anaangalia kazi za kichungaji. Kazi nzuri zinahimizwa katika waraka huu.
  • Filemoni. Hii ni barua aliyoandika Paulo kwa Filemoni kuhusu mtumwa Onesmo aliyekimbia. Paulo anamuomba Filemoni amsamehe Onesmo ambaye alishageuka na kumrudisha kazini. Paulo anaongoza kwa mfano kwa kumsamehe Onesmo na kujali mahitaji yake binafsi.

Nyaraka kuu

  • Waebrania. Barua hii imeelekezwa kwa Waebrania waliogeuka. Mwandishi hakutajwa katika kitabu hiki. Inawezekana ni waraka mwingine wa Paulo. Waraka huu unamuonesha Kristo kuwa ni masia mwenye utimilifu kama Nabii, Mchungaji na Mfalme.
  • Yakobo. Waraka huu huenda uliandikwa na Yakobo aliyekuwa ndugu yake Bwana. Waraka huu unaonesha kwamba imani bila matendo imekufa. Jambo hili linahusu matendo ya kidini na tabia ya Mkristo wa kweli.
  • I & II Petro. Waraka huu uliandikwa na Mtume Petro kuhamasisha na kuliimarisha kanisa. Ahadi ya urithi uliohifadhiwa umeoneshwa katika waraka huu. Petro anawatia moyo waumini kupokea ahadi ya Mungu yenye thamani kubwa. Waraka huu unasisitiza msukumo wa maandiko Matakatifu. Waraka huu unaloonyo dhidi ya manabii wa uongo.
  • I, II, & III Yohana. Uliandikwa na Mtume Yohana. Mungu ni uzima, nuru na upendo wa haki. Ni onyo dhidi ya makosa na walimu waongo. Kuaswa kutembea ndani ya ukweli.
  • Yuda. Wito wa kuzingatia imani ambayo iliosilishwa kwa Watakatifu. Angalizo la kujichunga dhidi ya walimu waongo.

Utabiri

  • Ufunuo. Ulipokelewa na Yohana katika kisiwa cha Patmo mwaka 100 wakati wa Kristo. Unao utabiri na maono kuhusu siku za mwisho na mwisho wa nyakati.

Umoja Kamili wa Biblia

Ukombozi ni Dhamira moja Kuu ya Biblia

Ukombozi ni tendo la kununua au kulipia kwa ukamilifu

Mwanadamu amekombolewa kwa damu ya Yesu Kristo. Yesu ameshalipa kikamilifu kwa damu yake iliyomwagwa msalabani bei ya ukombozi wa mwanadamu. Wokovu kwa Damu ya Yesu ndio dhamira kuu ya Biblia. Dhamira hii inapatikana tangu kitabu cha Mwanzo mpaka Ufunuo. Ahadi ya kwanza ya ukombozi imetolewa katika Mwa. 3:15. Nami nitaweka uadui kati yao na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huu utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.

Huu ni utabiri kwamba Yule Masiha ambaye atakuja kutokana na uzao wa mwanamke siku moja atakiponda kichwa cha nyoka. Mada hii inaendelea mpaka kitabu cha Ufunuo.

Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukatukomboa kwenda kwa Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa (Ufunuo 5:9). Andiko hili linahusu kufufuka kwa Kristo aliyetukomboa kwa Damu Yake.

Mkombozi wetu Kristo ndiye Mtu muhimu katika Biblia

Sadaka za kumwaga damu katika Agano la Kale zilikuwa ni aina inayofanana na Yesu ambaye ni Mwanakondoo aliyechinjwa kabla ya misingi ya ulimwengu. Wakisema kwa sauti kuu, Anastahili Mwana – Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka (Ufu. 5:12). Agano la Kale huangalia mbele kwa imani katika msalaba wa Kristo. Injili hii inamuonesha Kristo na Kifo chake juu ya msalaba. Agano Jipya huangalia nyuma katika kazi iliyomaliziwa katika msalaba.

Kristo hujidhihirisha mwenyewe katika Agano la Kale kwa nyakati tofauti na kwa njia mbalimbali. Kristo ameelezwa kwa namna ya kinabii kuwa ni Masiha ajaye.

Tangu Adamu hadi Abrahamu tunaona -> mwanzo wa jamii ya mwanadamu (Mwanzo 1:26, 27, 4:1, 5:1-5, 32; 6:9, 10 ; 7:17-23; 9:1; 11:10, 27).

Kizazi - taarifa ya historia ya ukoo wa mtu somo la mtiririko wa familia

Tangu Abraham mpaka Kristo tunaona -> mwanzo wa kabila teule. Taifa la waebrania (Mwanzo 12:1, 2; 22:15-18; 32:9-12; Yoshua 1:1-3; Mathayo 1:1, 2, 16). (Taifa hili lilianzishwa na kulelewa na mungu ili kumleta mwanadamu ulimwenguni.)

Tangu Kristo na kuendelea tunaona -> Mwanzo wa kanisa (Mathayo 16:18; Matendo 2:47; 11:26).

Tunapata mwonekano wake katika kila ukurasa, katika maandishi matakatifu yaliyochirwa kwa Nuru, Mkombozi, Nabii, Kuhani.

Biblia Haipingani

Hakuna kosa katika Biblia

Biblia ni Neno la Mungu la hakika. Neno la Mungu halina makosa au mgongano. Biblia ni sahihi na kamili. Biblia ni sahihi kihistoria na kisayansi. Hakuna mgongano kati ya sayansi ya kweli na Biblia. Taarifa ya kweli ya historia na taarifa za ugunduzi zinakubaliana kikamilifu na Biblia.

Kuna utulivu kamili katika Biblia yenyewe

Kilichoandikwa katika sehemu moja ya Biblia kinaoana na kilichoandikwa katika sehemu nyingine ya Biblia. Upo umoja kamilifu ndani ya Biblia yenyewe.

Biblia ina umoja

Biblia ina umoja katika unabii

Agano la Kale linao unabii mwingi. Unabii ni tangazo la tukio ambalo litakuja kutokea. Ni historia ambayo imeandikwa mapema. Utabiri wote huo unakubaliana na kila mmoja wapo. Baadhi ya unabii katika Agano la Kale umeshakamilika katika tarehe za baadaye katika Agano la Kale. Unabii mwingi katika Agano la Kale ulielezea ujio wa Masiha.

Agano Jipya limekamilisha mambo mengi yaliyotabiriwa katika Agano la Kale. Unabii huo ulikamilishwa vya kutosha bila upungufu. Msisitizo wa Nabii katika kila kitabu unaoana na kila unabii mwingine.

Biblia ni umoja katika mafundisho

Mafundisho ni ukweli wa msingi wa Biblia uliopangwa kwa mfumo sahihi. Ukweli wa Biblia umeendelea kuwa ule ule katika Neno la Mungu lote. Kuna uelewano mmoja ulio sahihi kwa Kanuni ya Biblia. Umoja huu umeendelezwa kutoka Agano la Kale hadi katika Agano Jipya. Biblia ni taarifa sahihi iliyofunuliwa kwa mwanadamu ikiwa na uelewano wa kutosha kwa kila mafundisho na ukweli.

Biblia ni umoja kamili wa ukweli. Ukweli haubadiliki. Kamusi ya Webster inafafanua ukweli kama: Kukubaliana na hali halisi kwa ukamilifu kwa kuzingatia kitu kilichopo, au kilichokuwepo au kitakachokuwepo. Ukweli wa Biblia unabakiwa kuwa sawasawa kuanzia kitabu cha Mwanzo mpaka kitabu cha Ufunuo. Uwatakase kwa ile kweli; Neno lako ndiyo kweli (Yohana 17:17).

Biblia ni Umoja kwa Kusudi

Kusudi la Biblia ni kuonesha mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu. Biblia inaonesha mpango wa Mungu katika nyakati zote. Neno la Mungu hutoa maagizo na mwongozo kwa roho za wanadamu. Mpango wa ukombozi unaoneshwa kwa mwanadamu katika Biblia.

Kila kitabu cha Biblia hutanguliza lengo moja la Biblia. Mungu ameonyesha mapenzi yake kwa watu mbalimbali katika vipindi tofauti katika Biblia yote. Biblia nzima huongoza wanadamu kwa Kristo na mpango wa ukombozi ambao ni dhamira kuu ya Biblia.

Biblia ni Moja kwa Umbile

Kila agano limeundwa kwa sehemu tatu kuu: historia, maagizo, na unabii.

Ipo Biblia moja yenye Agano Jipya na Agano la Kale.

  • Jipya liko katika la Kale ndani yake; la Kale limeelezewa katika Jipya;
  • Jipya liko katika la Kale linefichwa; la Kale ni katika Jipya limeoneshwa;
  • Jipya liko katika la Kale limetangulia kuoneshwa; la Kale liko katika Jipya limekomaa.

“Huu mtungamano wote wa Biblia katika maelezo na mchoro, kwa uelewano wake utulivu na uthibitisho unaoelewana ungekuwa kunaonekana wazi kama ingekuwa umekamilishwa na kikundi cha wasomi waliofanya kazi pamoja wakiwa na mawasiliano ya kudumu ya habari na mawazo. Hata katika hali ya namna hioyo ambapo kila mwandishi angegawiwa sehemu iliyohaririwa na bingwa wa mawazo na ikapitishwa na kikundi kipana umoja uliounganishwa wa maandiko hayo ungekuwa ni mafanikio ya ajabu. LAKINI, Biblia haikuandikwa kwa njia hiyo! Iliandaliwa na waandishi 40 au zaidi ambao waliishi katika kipindi kinachozidi miaka 1600 katika nchi 13 tofauti ndani ya mabara 3 ambao waliandika kutoka katika maeneo na ujuzi usiofanana kabisa. Walikuwa wachunga kondoo, wafalme, wanajeshi, wana wa wafalme, makuhani, wavuvi, wasomi, wanahistoria, watalaam na vibarua wa kawaida. Kazi yao ilifanyikia maporini, majangwani, mapangoni, makasri, magerezani, kwenye meli na nyumbani. Waliandika kuhusu mada nyingi kwa mbinu tofauti katika angalao lugha tatu. Hata hivyo pamoja na tofauti za namna hiyo na matatizo yaliyotokana na kazi zao mbalimbali walichofanya kinaoana kwa hakika na ni sare, inayoonekana kuandaliwa moja kwa ajili ya nyingine.”

Kristo katika Vitabu 66 vya Biblia

  • Katika Mwanzo, Yeye ni uzao wa mwanamke (3:15)
  • Katika Kutoka, Yeye ni Mwanakondoo wa Pasaka (12:1-28)
  • KatikaMambo ya Walawi, Yeye ni Sadaka ya upatanisho (1:14)
  • Katika Hesabu, Yeye ni Mwamba, na yule Nyoka wa Shaba (20:8-11; 21:8, 9)
  • Katika Kumbukumbu, Yeye ni Nabii ambaye Atakuja (18:15, 18, 19)
  • Katika Yoshua, Yeye ni Amiri wa jeshi la Bwana (5:13-15)
  • Katika Waamuzi, Yeye ndiye aliyewakomboa watu wa Mungu (2:16, 18)
  • Katika Ruthu, Yeye ni Mkombozi wa jamii (4:1-10)
  • Katika I Samweli, Yeye ni Mpakwa mafuta (16:10-17)
  • Katika II Samweli, Yeye ni Mfalme Aliyetawazwa (5:3-5)
  • Katika I Wafalme, Yeye ni utukufu unaolijaza hekalu (8:10, 11)
  • Katika II Wafalme, Yeye ni uzao wa kifalme aliyeokolewa kutoka kwa mchinjaji (11:1-3)
  • Katika I Mambo ya Nyakati, Yeye ni Mfalme Mtukufu (11:2, 3; 14:17)
  • Katika II Mambo ya Nyakati, Yeye ni Bwana aliyemtokea Sulemani (7:12)
  • Katika Ezra, Yeye ni Mtawanyaji Mkuu wa wanadamu (sura ya 10)
  • Katika Nehemia, Yeye ni Mrejezi mpya wa Taifa la Israeli (2:5)
  • Katika Esta, Yeye ni Wakili wa watu wake (7:2-4)
  • Katika Ayubu, Yeye ni Mtetezi aliye hai na sauti katika upepo wa kisulisuli (19:25; 38:1)
  • Katika Zaburi, Yeye ni Mchungaji, ni Mwana, ni Mfalme wa Amani, ni Mungu wa Majeshi, ni Mwenyezi Mungu (23:1; 2:12; 24)
  • Katika Mithali, Yeye ni Hekima na ni rafiki akaaye karibu kuliko ndugu (Mt. 8, 9; 18:24)
  • Katika Mhubiri, Yeye ni Msingi wa Uhai (Sura ya 12)
  • Katika Wimbo ulio Bora, Yeye ni Bwana Harusi Mtukufu
  • Katika Isaya, Yeye ni Imanueli, Mshauri wa Ajabu, Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani, na Bwana wa Mateso alichubuliwa kwa maovu yetu (9:6; 53:3-6)
  • Katika Yeremia, Yeye ni mfinyanzi wa Kimungu, Chipukizi la Haki, na BWANA ambaye ni haki yetu (18:1-6; 23:5; 23:6)
  • Katika Maombolezo, Yeye ni Yehova anayesikitika ambaye huwalea watu wake (1:1-6)
  • Katika Ezekieli, Yeye ni Utukufu wa Bwana na ni yule Mfalme atakaye kuja (10:4, 18;11:23; 44:4 21:26, 27; 37:24)
  • Katika Danieli, Yeye ni Jiwe Lililokatwa bila kazi ya mikono, ndiye Mtu wa nne katika lile tanuru la moto, katika siku za zamani (2:34; 3:25; 7:22)
  • Katika Hosea, Yeye ni mtoto aliyeitwa toka Misri (11:1)
  • Katika Yoeli, Yeye ni Simba aungurumaye kutoka Sayuni (3:16)
  • Katika Amosi, Yeye ni Hakimu wa Mataifa (9:8)
  • Katika Obadia, Yeye ni Mfalme wa Ufalme utakaokuja (1:21)
  • Katika Yona, Yeye ni mjumbe wa Bwana kwa Mataifa (1:1, 2; 3:3-5)
  • Katika Mika, Yeye ni Mtoto wa Betlehemu mtawala wa Israeli (5:2)
  • Katika Nahumu, Yeye ni Ngome katika siku za tabu (1:7)
  • Katika Habakuki, Yeye ni Bwana wa hekalu Lake takatifu (2:20)
  • Katika Sefania, Yeye ni Mfalme wa Israeli (3:15-17)
  • Katika Hagai, Yeye ni Bwana wa majeshi, ni Tamanio la mataifa (2:7)
  • Katika Zekaria, Yeye ni Mfalme aliyepanda mwana punda na ni Mchungaji Aliyepigwa (9:9; 13:7)
  • Katika Malaki, Yeye ni Mjumbe wa Mungu, na Jua la Uchamungu linalochomoza kwa uponyaji katika mbawa Zake (3:1; 4:2)
  • katika zile Injili Nne, Yeye ni Mungu – Mtu akifundisha, akiponya, akihubiri, akifa, na akifufuka tena (Yoh. 1:14; Mt. 9:35; Lk. 23:44-46; Mk. 16:5, 6)
  • Katika Matendo, Yeye ni Bwana Aliyeshuka akiwa kazini ulimwenguni kwa Roho (Yake 1:8, 9)
  • Katika Nyaraka, Yeye ni Kristo katika mkono wa kuume wa Baba Mpatanishi wetu (Kol. 3:1; I Tim. 2:5; Ebr. 7:25; I Yh. 2:1)
  • Katika Ufunuo, Yeye ni Mshindi wa dhambi na kifo anayerudi katika utukufu (19:11-16)

Uvuvio wa Biblia

Ufafanuzi kuhusu uvuvio wa Biblia

Uvuvio maana yake ni nini?

Kamusi ya Webster inafafanua uvuvio kama: kitendo chochote cha kupumlia.

Neno Uvuvio linatokana na Neno la kiingereza inspiration ambalo kwa kilatini ni in spiro maana yake ‘pumulia ndani.’

Neno hilo kwa maana yake halisi enye pumzi ya Mungu.

2 Tim. 3:16—Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, la faa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadabisha katika haki.

Maneno katika taarifa ya kuwa na pumzi ya Mungu ni tafsiri kutoka katika neno moja la Kiyunani: theopneustos, ambalo limetolewa katika neno Theos - Mungu na pneuma – Roho Mtakatifu. Pneuma limetolewa kutoka neno lenye maana ya pumzi. Tafsiri halisi ya maneno haya (iliyotolewa kwa pumzi ya Mungu) ni: ILIYO PUMULIWA NA MUNGU.

Neno hili limetumiwa kuhusiana na asili ya Kimungu ya Maandiko.

Biblia haikuandikwa na Mwanadamu Roho Mtakatifu alilipumulia Neno kwa watu ambao walikuwa ni vyombo vya kibinadamu vya Mwandishi ambaye ni Mungu.

II Petro 1:21—Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Unabii katika maandiko haya yanahusiana na aya ya 20 inayosema: Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Aya hizi zinahusu unabii ulioko katika Maandiko. Maandiko hayakuletwa kwetu na mwanadamu. Wale wanadamu walisukumwa na Roho Mtakatifu. Kitendo hiki Kitukufu cha Mungu.

Je tumeshapata Neno lenye pumzi ya Mungu? Ndiyo, tumeshapata! Haitoshi kujibu ndiyo peke yake swali kama hili, kila muamini anapaswa kufahamu bila shaka yeyote kwamba Biblia siyo kitu kingine zaidi ya pumzi ya Mwenyezi Mungu.

Mawazo Potofu kuhusu Uvuvio wa Biblia

Biblia ilipatikana kwa uvuvio wa asili

Wazo hili la uwongo hushikilia kwamba Biblia ni tunda la mtu mmoja mwerevu wa hali ya juu, ila siyo mwenye nguvu za ajabu au za Utukufu. Hii ni aina ya msukumo ambao umeoneshwa katika maandishi ya Milton, Shakespeare au Confusius. Hakuna binadamu mwenye kipaji hata kiwe cha namna gani, ambaye akisoma alichoandika Shakespeare kisha akaisoma Biblia atashindwa kuona tofauti kati ya mambo haya mawili kuwa ni kubwa sana. Kitabu kinaweza kuwa na uvuvio bila kuwa na pumzi. Biblia inavipita kwa mbali vitabu vya wanadamu.

Mungu alitumia ngazi mbalimbali za uvuvio kutupatia Biblia

Wazo hili la uongo hudai kwamba Mungu alitumia ngazi mbalimbali za udhibiti kwa vipindi tofauti katika mchakato wa msukumo. Wazo hili linatetewa zaidi kwamba Mungu alitumia utukufu wake na wakati mwingine, alitoa tu mapendekezo au alianzisha jambo kwa maagizo. Hii ni kinyume kabisa na msukumo wa kweli wa Biblia.

Mungu alitoa pendekezo au maoni kwa wanadamu ambao waliiandika Biblia

Wale wanaoshabikia wazo hili la uongo wanasema kwamba mapendekezo au mawazo hayo yalipewa uvuvio. Msimamo huu unawapa wanadamu nafasi ya kutumia maneno yao katika taarifa hizo kutoka akili mwao. Hii ni kinyume na maana halisi ya uvuvio wa kweli wa Biblia.

Sehemu chache tu za Biblia zimepumuliwa

Haya ni mafundisho ya uongo ambayo ni hatari kuzungumzia sehemu tu kuwa na pumzi. Msimamo huu unatamka kwamba Biblia inalo Neno la Mungu lakini siyo maandiko yote yamepumuliwa. Ni nani basi wa kuamua nini ndiyo na kipi hakijapumuliwa? Nadharia ya namna hiyo inamuacha mwanadamu katika hali tata na hatari ya kutokuwa na uhakika.

Ni nini uelewa sahihi wa uvuvio wa Biblia?

“Uvuvio wa mdomo na wa mamlaka” ndio sahihi. (jambo hili litaelezwa kwa kina baadaye)

Matangazo ya Uvuvio wa kiBiblia

Biblia nzima inayo pumzi ya Mungu

II Tim. 3:16—Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu…

Wazo kwamba Biblia katika ukamilifu wake inayo pumzi ya Mungu huitwa uvuvio kwa mamlaka. Mamlaka maana yake kamili au timia. Biblia kamili huanzia mwanzo mpaka ufunuo ni Neno la Mungu lenye uvuvio. Maandiko yote yamepumliwa sawasawa.

Kwa kuwa imepumuliwa na Mungu Biblia haiwezi kuwa na kosa. Haiwezi kuwa na kosa maana yake imetenganishwa kabisa na uwezekano wa kukosewa. Maneno hayo huhusishwa na Mungu ambaye hawezi kufanya kosa au kughafilika. Katika matumizi yake kuihusu Biblia kutokuwa na kosa kunahusu Utukufu wa Mwandishi wa Maandiko. Muandishi huyu Mtukufu hafanyi makosa na kwa hiyo Neno lake haliwezi kuwa na kosa.

Agano la Kale limevuviwa na Mungu

Mara kwa mara tena tunaweza kupata maelezo yafuatayo katika Agano la Kale:

  • “Neno la Bwana”
  • “Mungu akaamuru”
  • “Mungu akasema/akaonge
  • “Bwana akasema”
  • “Mungu akatokea”
  • “Asema Bwana”

Maelezo kama haya yanadhibitisha uvuvio wa Agano la Kale. Uthibitisho wa madai haya uko wazi kutokana na umakini wa kila neno la taarifa na majina, nyakati na mahali ambako watendaji walikamilisha ujumbe wao na, ukamilifu wa kutimia kwa unabii wao.

Matendo 28:25—Na walipokuwa hawapatani wao kwa wao, wakaenda zao, Paulo alipokwisha kusema neno hili moja, ya kwamba, Roho Mtakatifu alinena vyema na baba zetu, kwa kinywa cha nabii Isaya,

2 Petro 1:21—Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Waebrania 1:1—Mungu ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi.

Kumb. 18:18-22—Atakaponena nabii kwa jina la Bwana, lisifuate jambo lile wala kutimia hilo ndilo neno asilonena Bwana; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimuogope.

Agano Jipya limevuviwa na Mungu

Waandishi wa Agano Jipya wanadai kuwa uvuvio kwa waandishi wa Agano la Kale unawahusu wao pia:

Matendo 1:16—…ilipasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daudi kwa habari za Yuda aliyewaongoza wao waliomkamata Yesu....,

Wale watu walivuviwa

Maandiko yanatamka kwamba watu watakatifu wa Mungu waliongea kama walivyosukumwa na Roho Mtakatifu (2 Petro 1:21). Mungu aliwavuvia Neno lake watu ambao walikuwa ni vyombo vya kibinadamu kuandika Biblia. Kauli za Manabii kutoka kwa Mungu zilitumiwa na Mungu kuwasiliana na watu Wake. Bwana aliwaagiza wengi wa watu hao kuandika Maneno Yake. Watu hao walivuviwa na kuagizwa na Mungu kuwapatia watu wake Neno lake.

Yale Maneno Yalivuviwa

Siyo wale watu waliovuviwa na Mungu peke yao, bali uchaguzi wa maneno ulikuja moja kwa moja kutoka katika kiti cha enzi cha Mungu. Mungu alivuvia uchaguzi wa maneno ya Maandiko. Jambo hili hujulikana kama uvuvio wa maneno. Wale waandishi hawakuachwa peke yao katika uchaguzi wa maneno ambayo yatatumika. Mungu aliongoza katika uchaguzi wa maneno katika Biblia.

Yuda 17—Bali ninyi, wapenzi, yakumbukeni maneno yaliyonenwa zamani na mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo;

2 Petro 3:2—Mpate kuyakumbuka yale maneno yaliyonenwa zamani na manabii watakatifu, na ile amri ya Bwana na Mokozi iliyoletwa na mitume wenu.

Yohana 12:48—Yeye anikataaye mimi, asiye yakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.

Zile Herufi zilikuwa na uvuvio

Zile herufi za maneno ya Biblia zimevuviwa kwa Utukufu wa Mungu. Kwa mfano, hebu tuangalie mafundisho ya “punje moja na siyo nyingi” kwa njia ya Kristo ambao ilidhibitishwa kwa matumizi ya herufi: ‘u.’

Wagalatia 3:16—Basi ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu kwa mzao wake. Hasemi, kwa wazao kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani, Kristo. (linganisha na Mwanzo. 22:16-18)

Herufi ‘u’ katika aya hii inaweka tofauti KUBWA. Herufi ‘u’ inaweka tofauti kati ya umoja na wingi na muhimu zaidi tofauti ya kutamka kwamba kuna msuluhishi mmoja au kutamka kwamba wapo wasuluhishi wengi. Iwapo Mungu angesema ‘wazao’ badala ya ‘uzao’ ahadi hizo zingeweza kutolewa kupitia Confucius, Buddha, Mohammed, Papa au mwingine yeyote ambaye amechagua kujitwalia umaarufu huu. Kwa kutumia umoja, Mungu ameufunga mlango kwa manabii wa uongo na kumnyanyua Kristo kama njia PEKEE ya kwenda kwa Mungu. Punje ya Ahadi inaweza kuwa Kristo tu, na siyo Kristo na Buddha au Kristo na Muhammed. Yesu Kristo peke yake alikuwa ndiye punje ya ahadi.

Kila chembe Ilivuviwa

Mathayo 5:18—Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka Mbingu na Nchi zitakapoondoka yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.

Yodi inaweza kulinganishwa na apostrofi (‘) na nukta kulinganishwa na kistari ungio (-).

“Biblia siyo kitu kingine isipokuwa ni sauti Yake yule akaaye katika kiti cha enzi. Kila kitabu chake, kila mlango, kila aya, kila neno, kila silabi, kila herufi, ni tamshi lake Yule Aliye Juu ya Yote.”
—Dan Burgon

Ufafanuzi wa Uvuvio wa kiBiblia

Huzalisha watu “waliozaliwa mara ya pili”

II Kor. 5:17—Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.

Jedwali lifuatalo ni orodha ya watu wa Mungu ambao waligeuka kupitia sehemu mbalimbali za maandiko. Maandiko haya yalikuwa na matokeo katika maisha ya watu hawa wa Mungu.

| John Calvin | Isaya 53:5 | C. H. Spurgeon | Isaya 45:22 | | Henry Moorhouse | Mathayo 1:21 | John Williams | Marko 8:36 | | Sir James Simpson | Yohana 3:14, 15 | W. P. Lockhart | Yohana 19:30 | | David Livingston | Matendo 16:31 | William Cowper | Warumi 3:25 | | Sir George Williams | I Wakorinto 15:1-4 | Martin Luther | Wagalatia 3:11 | | Lord Shaftesbury | I Petro 3:18 | Hedley Vicars | I Yohana 1:7 | | James Chalmers | Ufunuo 22:17 | Robert Moffat | Yohana 3:16 | | Duncan Mathieson | Yohana 3:16 | Richard Weaver | Yohana 3:16 |

Hakuna yeyote aliyewahi kusikia mtu aliyefanywa “kiumbe kipya” kupitia Homer, Shakespeare, Scott, Dickens, Macauley, Huxley, Carlyle, Eliot, Kipling, Wells, au mtu mwingine yeyote? Mamilioni ya watu wamefanywa wapya kwa kusoma na kuiamini Biblia ambayo ni Neno la Mungu.

Huzalisha ukuaji wa Kiroho

Biblia huzalisha ukuaji wa Kiroho katika maisha ya Watakatifu wa Mungu. Biblia ni chakula cha roho ya Mkristo na inapaswa kusomwa kila siku ili kupata nguvu na kukua Kikristo.

Yeremia 15:16—Maneno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ya furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu maana nimeitwa kwa jina lako, Ee BWANA, Mungu wa Majeshi.

1 Petro 2:2—Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu: Husafisha Maisha.

Biblia inaweza kuyasafisha maisha ya wanaume na wanawake. Roho Mtakatifu atawahukumu wanadamu kwa Neno. Biblia itaonesha wanadamu kitu kinachopaswa kubadilishwa katika maisha yao. Maji yaliyopo katika Hema ya kukutania ni alama ya Neno la Mungu. Makuhani walipaswa kunawa katika maji hayo kila wakati waendapo kufanya ibada ya Bwana.

Yohana 15:3—Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu lile neno nililowaambia. (Eph. 5:26)

Zaburi 119:9—Jinsi kijana aisafisha njia yake? Kwa kutii akilifuata Neno lako.

Humjenga Aaminiye

Kunakuwepo na nguvu na kuwa na moyo katika neno la Mungu. Neno la Mungu litakujenga na kukuweka imara katika wakati mgumu. Wakristo wanaweza kusimama katika mwamba huu imara.

Warumi 16:25—Sasa na atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara sawasawa na Injili yangu…

Waefeso 2:20-22—Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe Hekalu Takatifu katika Bwana. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.

Hukamilishwa katika utimilifu (Soma Waefeso 4:11-15)

Udhibitisho wa hakika wa uvuvio wa Biblia

Upo ushahidi ulio wazi wa kudhibitisha uvuvio wa Biblia. Zaidi ya matamko yaliyomo katika maandishi yenyewe, taarifa nyingi za ukweli wa Biblia zinaonyesha kwamba maandiko yalivuviwa kwa utukufu.

Haijavunjwa na iko katika utimilifu ulio pamoja

Biblia inavyo vitabu 66 vilivyoandikwa kwa lugha 4 na watu 40 ambao walikuwa wakiishi umbali wa zaidi ya maili 1500 katika kipindi cha miaka 1600. Watu waliotumiwa walitoka katika ngazi mbalimbali za maisha; Baadhi yao walikuwa wafalme, madaktari, manabii, wachungaji, wafanya kazi, wavuvi, na mmoja alikuwa mtoza ushuru. Pamoja na ukweli huo mtiririko wake haukuvunjika na inao utimilifu ulio na umoja katika Biblia nzima. Hii inaweza kuwa kazi ya Mungu peke yake.

Haiogopi kutoa Unabii

Biblia husema mapema kuhusu matukio ya miaka au karne nyingi zijazo kabla hayajatokea. Wakati wa kuandikwa kwa unabii ulioko katika Agano la Kale unaweza kuelezwa kwa historia kwa sababu taarifa sahihi za historia kati ya maagano yote mawili imeendelea kuwepo. Taarifa hii ya kihistoria inathibitisha tarehe ya kuisha kwa Agano la Kale kwa kuweka kipindi cha miaka 400 ambacho Biblia imekuwa kimya kati ya utabiri wa mwisho wa Agano la Kale na ukamilishaji wake kuanza katika Agano Jipya.

Tarehe ambazo vitabu vya Biblia zimeandikwa zinaweza kupatikana katika historia. Uwepo wa Septuaginti, yaani ile tafsiri ya Kiyunani ya Agano la Kale unaweza kuwekwa kwa usahihi katika miaka 250 kabla ya Kristo. Kwa kuwa Septuaginti ilitafsiriwa kutoka katika maandishi ya Kiebrania ni lazima kulikuwepo na Agano la Kale la Kiebrania angalau miaka 250 kabla ya kuwepo kwa Agano Jipya. Uthibitisho huu ni wa kihistoria kwamba unabii huo uliandikwa miaka 100 kadhaa kabla ya kutokea utimilifu wake katika Agano Jipya. Hakuna uwezekano wa mwanadamu kuweza kutabiri kwa uhakika wa namna hiyo. Huu ni uthibitisho usiokuwa na ubishi ya kwamba Maandiko ya Injili yamevuviwa.

MIFANO YA UNABII ULIOKAMILISHWA KWA UHAKIKA:

Unabii wa Kristo

  • Atakuwa ni wa uzao wa Abraham (Mwanzo 22:18; Mathayo 1:1)
  • Atakuwa wa ukoo wa Daudi (Yeremia 23:5; Mathayo 1:1)
  • Atatoka katika kabila la Yuda (Mika 5:2; Mathayo 1:2; Waebrania 7:14)
  • Atazaliwa katika mji wa Betlehemu (Mika 5:2; Mathayo 2:1)
  • Kulikuwepo na unabii mara 29 uliotimia katika siku moja katika yale matukio ya kusulubiwa kwa Yesu ambayo utabiri wake ulikuwa na taarifa za kina tangu karne kadhaa kabla ya kifo chake.
  • Kulikuwepo na unabii zaidi ya mia tatu kuhusu Masiha iliyotimia kwa Kristo.

Mdo. 3:18—Lakini mambo yale aliyohubiri Mungu tangu zamani kwa kinywa cha manabii wake wote, ya kwamba Kristo wake atateswa, ameyatimiza hivyo.

Kristo alitimiza unabii wote katika Agano la Kale kumhusu yeye pamoja na mashaka yote. Hakuna mwanadamu mwenye uwezo wa kuchagua ukoo wake kabla ya kuzaliwa ingawa Yesu alizaliwa katika ukoo kama ilivyokuwa imetabiriwa na manabii. Walikuwepo watu wengine waliohusika katika ukamilisho wa unabii huo kama askari wa Kirumi ambao waligawana mavazi ya Yesu kati yao na kuipigia kanzu yake kura. Hata lile giza lililotokea Kristo alipofariki linaweza kuthibitishwa kwa taarifa za historia na nyingine zilizoandikwa. Nabii Amosi alitabiri giza lile miaka mia 700 hivi iliyopita kabla ya kutokea kwake. Hakuna mwanadamu anayeweza kuelezea kwa usahihi kutimia kwa utabiri huu wa Kimasiha. Huu ni uthibitisho ulio wazi wa uvuvio wa Biblia!

Unabii wa Israel

  • Musa alitabiri maisha ya baadaye ya Israel (Kumb. 4:23-38)
  • Watawekwa mateka kwa sababu ya dhambi yao (Isaya 22:17; Yeremia 20:6)
  • Watatawanyishwa katika nchi zote (Kumb. 30:1-3)
  • Watapata mateso (Lk. 19:41-44)
  • Kabla wa wakati wa kurudi Kristo, Israel itakusanywa tena katika ardhi yake. (Luka 21:29-32; Eze. 36-37) hili lilitimia 14, Mei 1948 (Ezekieli 36:24)
  • Mungu alitamka kwamba atawalinda watu wake wa Israeli kama mchungaji (Yeremia 31:10). Chini ya saa 24 baada ya Israeli kutangaza uhuru wake mwaka 1948, nchi zinazoizunguka (Misri, Yordani, Iraq, Syria, na Lebanoni) ziliivamia Israeli kwa mategemeo kwamba wataliondoa Taifa la Kiyahudi na kuweka Taifa la Kiarabu. Nchi hizi ni kubwa kuliko Israeli, lakini Israeli kwa udogo wake iliendelea kuwepo hata baada ya kuwepo vita nyingine mbili kubwa (Vita ya siku 6, 1967 na Vita ya Yom Kippur, 1973).

Utabiri wa Mataifa

  • Babeli ilipinduliwa na kuangushwa kama Sodoma kama ilivyotabiriwa (Isaya. 13:19; Yer. 51:37). Katika Danieli 5 kuna maelezo kuhusu kuhamishwa kwa madaraka kutoka Wamede na Waajemi.
  • Himaya ya Gresi ndio utawala wa tatu wa Shaba ndio utawala wa tatu ulioelezwa katika ndoto ya nabii kwenye kitabu cha Danieli 2:39 Babeli ukiwa ni Ufalme wa kwanza. Aleksanda Mkuu aliushinda ulimwengu kama ilivyo tabiriwa katika unabii huu. (ndoto hii ya Nabii inasomwa kwa kina katika mwaka wa tatu kwenye somo la Utabiri wa Manabii.)
  • Kugawanyika kwa Himaya ya Kirumi kumetabiriwa katika mgawanyiko wa miguu aliouona katika ndoto ni Nebukadneza katika Danieli 2.
  • Ninawi iliharibiwa kwa ya mataifa wahamiaji. Nahumu (1-3, 3:7) ilitabiriwa kwamba malango yatawekwa wazi kabisa kwa manufaa yaadui zako (3:13). Mto Tigrisi ulifurika wakati wa mashambulio na kubeba zile kuta pamoja na malango ya mji.
  • Yesu alitangulia kuuzungumzia kuharibiwa kwa Hekalu la Yerusalemu (Mt. 24:1-2; Mk. 13:1-3). Mji wa Yerusalemu uliharibiwa mwaka wa 70 Baada ya Kristo chini ya Jemadari Tito wa Kirumi. Lile Hekalu lilichomwa moto na ile dhahabu iliyokuwemo iliyeyukia katikati ya mawe yake. Wale askari walilivunja lile Hekalu Jiwe kwa Jiwe ili kuitoa dhahabu. Kwa mara nyingine utabiri wa nabii umekamilika kwa kina kama Yesu alivyosema itakuwa.
  • Mji wa Tiro ulikuwa uharibiwe kama ilivyo katika kitabu cha Ezekieli 26:3-14. Huu ni utabiri mahsusi uliotolewa 588 kabla ya Kristo. Maandiko yanatamka kwamba mataifa mengi yataupinga mji wa Tiro. Sura ya 3.

Mungu alisema atamleta Mfalme wa Babeli kuwapinga. Aya ya 7. Utabiri huu unasema kwamba yale mawe, mbao na udongo vitatupwa katika maji. Aya ya 12. Nebukadneza, Mfalme wa Babeli, aliuzingira mji wa Tiro kwa miaka 13. Aleksanda Mkuu aliuteka mji wa Tiro katika kile kisiwa mwaka 332 Kabla ya Kristo kwa kujenga daraja toka nchi kavu hadi kisiwani. Walitumia mawe, mbao kutoka kwenye majengo yaliyoharibiwa na udongo wakaujaza kutengeneza kinachoitwa bomazuizi (daraja la udongo) katika maji. Wale Askari waliweka mawe, mbao, na udongo majini kama ilivyotabiriwa na manabii. Jambo hili la hakika lililotabiriwa na likatokea siyo kubahatisha kwa binadamu peke yake. Biblia ni Neno lililovuviwa la Mwenyezi Mungu. Lile Bomazuizi la Aleksanda Mkuu bado liko mahali pale hadi leo.

Unabii wa Siku za mwisho

2 Timotheo 3:1-9

Yako maelezo mengi ambayo ni sahihi kuhusu siku za mwisho yanayopatikana katika Maandiko. Haya ni baadhi tu ya mambo yaliyotabiriwa ambayo yanaeleza hali ya siku zetu:

  • Kuongezeka kwa maarifa (Danieli 12:4)
  • Fikiria kuhusu vitu vyote vipya vilivyogunduliwa katika kipindi cha miaka 100. Wale ndugu wawili wajulikanao kama Wright waliruka kwa ndege kwa mara ya kwanza 1903 na leo usafiri wa anga ni njia ya kawaida ya usafirishaji. Kumekuwa na maendeleo makubwa ya Teknologia katika muda mfupi sana.
  • Manabii wengi wa uongo (Mathayo 24:5, 11)
  • Vita nyingi na tetesi za vita (Mathayo 24:6)
  • Njaa, majanga na matetemeko ya ardhi (Mathayo 24:7)
  • Kutokuwepo usawa kumeenea (Mathayo 24:12)
  • Injili kuhubiriwa ulimwenguni kote (Mathayo 24:14)
  • Kula, kunywa na kuoana (Mathayo 24:38)
  • Ni kama ilivyokuwa wakati wa Lutu (Luka 17:28-29) (walikunywa, wakauza, wakanunua, wakapanda na wakajenga. Hali hii inasikika sana kama ilivyo kwa watu wa leo. Kuna ongezeko pia la dhambi ya ushoga leo kuliko ilivyokuwa siku za Lutu.)
  • Kuiacha ile Imani (I Timotheo 4:1)

Usahihi wake Kihistoria

Akiolojia ni kuhusu mafunzo mambo ya kale kwa kutafuta vitu vilivyotumiwa na watu wa zamani. Vitu hivi vya zamani vinatupatia habari kuwahusu watu ambao walivitumia. Kumesha gunduliwa vitu vingi kudhihirisha usahihi wa kihistoria wa Biblia. Kwa kweli, hakuna chochote cha akiolojia kilichopatikana kinachopinga Biblia. Wakosoaji wamebisha kwamba Biblia si sahihi kwa historia lakini akiolojia inaendelea kudhihirisha kwamba Biblia ni ya kweli.

Makitaba ya Wahiti iligunduliwa huko Uturuki 1906 ikidhibitisha usahihi wa Taarifa ya Biblia kuhusu jamii ya Wahiti.

Kumekuwep na vionzi vya mfupa vilivyopatikana vya majitu makubwa kudhibitisha maelezo ya majitu iliyoko katika Biblia.

Masalia ya mtu aliye uawa kwa kusulubiwa yalipatikana Yerusalemu mwaka 1968. Masalia hayo yalikuwa na tundu la msumari katika miguu yake lililopita katika nyayo zote mbili na tundu moja la msumari katika viganja vya mikono. Mtu huyo aliaminika kwamba aliuawa na Warumi wakati wa uasi wa Wayahudi mwaka wa 70 baada ya Kristo. Hii inathibitisha kwamba kusulubu msalabani ilikuwa ni njia ya kutekeleza hukumu ya kifo iliyotumiwa na Warumi kama ilivyoelezwa katika taarifa za Biblia kuhusu kusulubiwa kwa Yesu.

Kitabu cha Matendo kimethibitishwa kihistoria kuwa sahihi.

Michoro imegunduliwa yenye majina ya watu walioelezwa katika Biblia katika maeneo ambamo Biblia imewaweka.

Zimekuwepo taarifa za kupatikana kwa vifaa vya akiolojia vinavyoendelea kudhibitisha usahihi kihistoria wa Biblia. Huu ni ushahidi zaidi ambao unathibitisha uvuvio wa Neno la Mungu.

Usahihi wa Kisayansi

Biblia iko sahihi kisayansi. Yapo mambo kadhaa katika Biblia ambayo wanadamu walioyaandika hawakuwa na uelewa wa kuweza kuyajua. Mungu ndiye mwandishi wa Maandiko Matakatifu na anafahamu mambo yote. Maelezo yaliyoka katika Biblia ni ya kweli na yako sahihi kisayansi.

Vipimo vya safina ya Nuhu alivyopewa na Mungu vinalingana na meli inayofaa kabisa kwa usafirishaji baharini. Meli za kisasa zimeundwa kwa uelewa mkubwa wa fizikia na matumizi ya teknologia ya kompyuta na zinatumia vipimo kama alivyotumia Nuhu. Isingewezekana Nuhu apate elimu hiyo kwa wakati wake. Ni jambo la busara katika hali kama hiyo kuamini kwamba taarifa kuhusu vipimo vya safina katika Biblia ambavyo Mungu alimpatia Nuhu ni sahihi.

Katika kitabu cha Ayubu kuna taarifa kuhusu kugawanywa kwa mwanga (Ayubu 38:24). Mwanga unaweza kugawanywa katika vipande kwa kutumia mche wa kioo. Hakuna uwezekano wa Ayubu katika kitabu chake ambacho ni cha zamani zaidi kuliko vyote katika Biblia aweze kufahamu kwamba mwanga unaweza kugawanywa. Kitabu cha Mhubiri kinazungumzia mizunguko ya upepo. Kuna mizunguko ya upepo na maumbo yake ambayo imegundulika katika sayansi hivi karibuni kwa matumizi ya setelaiti na kompyuta. Watu katika zama za Agano la Kale wasingeweza kuwa na habari kama hizo japo kwa mara nyingine Biblia inayo taarifa sahihi kuhusu mizunguko ya upepo. Mwandishi wa kitabu cha maombolezo angewezaje kujua kwamba mito ilimwagikia baharini (Mhubiri. 1:7). Nabii Isaya alizungumza kuhusu Mungu akiwa ameketi katika duara ya dunia (Isaya 40:22). Dunia haikuthibitishwa kuwa duara mpaka Magellani alipoizunguka kwa merikebu miaka ya 1500. Isaya hakuwa na uwezo wa kupata habari hizo. Ili kwa mara nyingine tena ni jambo linalothibitisha uvuvio wa Maandiko.

Ni Nguvu Isiyotegemea Rika

Warumi 1:16—Kwa maana siionei haua Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao Wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia.

Biblia ni zaidi ya kitabu. Biblia ni neno la Mungu. Wale ambao wanaisoma Biblia kwa umakini katika imani wanaweza kubadilishwa kwa nguvu ya Mungu. Mungu anaweza kuitumia Biblia kubadilisha maisha ya wanadamu. Maisha ya watu wengi yameshabadilika kwa nguvu za Mungu kwa kuisoma tu Biblia na kuiamini.

Biblia inanguvu za kuwaokoa watu katika hali zote za maisha: walevi, wabuya unga, malaya, wezi, wauaji, watenda dhambi wote. Wote wanaweza kuokolewa kwa njia ya Yesu Kristo. Tunaweza kupata muongozo katika Neno la Mungu kwa kila tukio la maisha yetu, kwa ushauri usiokuwa na ubaguzi wowote. Biblia inasimama imara juu ya kitabu chochote kile kilichoandikwa bila ushindani wala kupingana. Kwa usahihi Biblia ndio kitabu pekee alichoandika Mungu.

Kuorodheshwa kwa vitabu vya Biblia

Mchakato wa ukusanyaji wa vitabu vya Biblia katika mfumo wake wa sasa ndio kunakoitwa: kuorodheshwa kwa vitabu vya Biblia. Jambo hii halikufanyika kwa siku moja. Ikumbukwe kwamba kila kitabu kimoja ilibidi kiandikwe kwa mkono na kwa umakini mkubwa. Vitabu hivyo vilitumiwa na kusambazwa na viongozi wa dini wa siku hizo. Kulikuwepo pia vitabu vingine vilivyodai kuwa na uvuvio ambavyo havikuingizwa katika Biblia. Kulikuwepo na vitabu vya dini na historia ambavyo vilikuwa vinasambazwa wakati wa kuamua ni vitabu gani viingizwe katika Orodha hiyo. Mchakato huu wa kutambua vitabu vyenye uvuvio na vipi havina ndio jambo tutakaloangalia katika somo la sehemu hii. Tutajaribu pia kulijibu swali: Biblia iliwezaje kufikia katika hali iliyo nayo sasa?

Ufafanuzi Kuhusu Kanoni

Neno Kanoni linatokana na mzizi wa neno mtete

Jani la mtete lilitumiwa kama kifaa cha kupimia. Neno lake la Kingereza ni fimbo (cane) na Kiyunani ni kanuni. Neno kanuni maana yake ufito, rula au kifaa cha kupimia urefu. Kiongozi wa kanisa la karne ya 3 aitwaye Origeni alitumia neno kanuni akimaanisha kipimo cha imani.

Neno kanuni lilitumiwa kuvihusu vitabu vilivyoamuliwa kuwa na asili ya Mungu

Kanuni ya Biblia ni vitabu vyenye uvuvio ambavyo vilikusanywa pamoja katika Biblia Takatifu. Kumbuka kwamba neno Biblia maana yake vitabu na Biblia Takatifu ni mkusanyiko wa vitabu Vitakatifu. Neno kanuni ni neno la kawaida ambalo hutumiwa kuuhusu mkusanyo huu wa vitabu vitakatifu ambavyo tunaviita Biblia ambayo ndilo Neno la Mungu lenye uvuvio.

Kanoni ya Agano la Kale inahusu vitabu vya Agano la Kale ambavyo viliamuliwa kuwa na uvuvio wa Mungu na kuingizwa katika Biblia kama sehemu yake tunayoiita Agano la Kale.

Kanoni ya Agano Jipya inahusu vitabu vya Agano Jipya ambavyo viliamuliwa kuwa na uvuvio wa Mungu na kuingizwa katika Biblia kama sehemu yake tunayoiita Agano Jipya.

Mchakato wa kuorodhesha maandiko kwa kanoni ya Biblia

Mwandishi Mtukufu aliwapa watu Watakatifu wa Mungu Maandiko

Maandishi ya mkono yalinakiliwa kwa umakini mkubwa

Vitabu vile havikukusanywa pamoja katika mfumo wake wa sasa kwa haraka.

Waandishi wa Kiyahudi na viongozi wa dini walivikusanya vile vitabu ambavyo asili yake ilidhihirika kuwa ni Mungu pamoja katika Kanoni ya Agano la Kale

Viongozi wa kale wa kanisa walivikusanya vitabu vile pamoja ambavyo vilithihirika kuwa na asili ya Mungu na kuviweka katika Kanoni ya Agano Jipya

Uwepo wa Kanoni humaanisha ukweli kwamba kitabu kinachohusika kimeshadhihirika kuwa na asili ya Mungu na kuingizwa katika Kanoni

Mfano: uwepo wa Kanoni katika Kitabu cha Isaya ulitambuliwa kwa sababu iliaminika kuwepo na uvuvio wa Mungu.

Uwepo wa Kanoni katika hali kama hii haupaswi kuchanganywa na ule unaotumiwa na Kanisa katoliki ambao huusu utaratibu wa kuwafanya watu waliokufa watakatifu.

Namna ya kuamua uwepo wa Kanuni

Ni Kigezo gani kilitumika kuamua vitabu gani viingizwe katika Biblia na vitabu vipi visiingizwe katika orodha ya Maandiko Matakatifu? Hili ni swali muhimu ambalo inabidi lipatiwe majibu na mwanafunzi makini wa Biblia. Uanapaswa kufahamu bila shaka yeyote kwamba Biblia katika mfumo wake wa sasa ndio NENO LA MUNGU LENYE UVUVIO.

Fikra potofu kuhusu Uamuzi wa vitabu vya Kuorodhesha katika Biblia

Viongozi wa kidini ndio walioamua orodha ya vitabu vya Biblia

Mabaraza ya dini hayakuamua vitabu vya kuorodheshwa katika Biblia. Mabaraza ya wanadamu hayawezi kufanya kitabu kuwa Andiko Takatifu ambacho katika asili yake siyo maandiko matakatifu.

Wakosoaji watasisitiza kwamba ilibidi mwanadamu aamue vitabu vya kuingiza katika orodha ya Biblia hali inayotia shaka kuaminika kwa Biblia

Kumekuwepo na madai kwamba wanadamu walichagua vile vitabu ambavyo vinawiana na mtizamo wa dini zao ambao waliuorodhesha katika Kanoni

Hali hii ndio inayosemekana kwamba ni sababu pekee ya umoja na uelewano wa Maandiko Matakatifu. Ubishi ni kwamba wanadamu waliondoa vitabu ambavyo havikukubaliana na maoni yao na kuingiza vile ambavyo vilikubaliana na maoni yao. Maoni haya ya yongo humuweka mwanadamu katika nafasi ya uamuzi wa orodha ya kanoni.

Mawazo sahihi kuhusu uamuzi wa orodha ya vitabu vya Biblia

Mungu aliamua kanoni ya uorodheshaji wa vitabu vya Biblia

Mungu alimpatia mwanadamu vitabu ambavyo alitaka viingizwe katika Biblia. Mungu alilinda na kuhifadhi vile vitabu alivyovivuvia na kuvitunza hadi wakati wa kuviweka katika orodha ya Biblia.

Uvuvio wa Kiungu wa kitabu kilicho amliwa kikanoni

Kitabu kiliweza kuingizwa katika Kanoni kwa sababu ya kutambuliwa kwake kuwa na Uvuvio wa Wakiungu wa Neno la Mungu. Kitabu ambacho kilionekana kutokuwa na Mamlaka ya Kiungu hakikuingizwa katika Biblia kama sehemu ya kanoni ya Maandiko Matakatifu.

Maelezo ya Kanuni ya Agano la Kale

Kanuni ya Agano la Kale iligawanywa katika sehemu tatu.

Sheria – Maandishi ya Musa.

Manabii – Maandishi ya watu waliokuwa na cheo cha manabii.

Maandishi – Ukiondoa Ruthu na Maombolezo maandishi ya watu ambao hawakuwa na cheo cha nabii. Shehemu hii huitwa pia Hagiografa katika taarifa nyingi za Kiyahudi.

Taarifa za Kimasoreti

Neno masoreti maana yake a desturi. Maandishi ya Kimasoreti yanahusu Maandiko yanayokubalika ya Kiebrania. Maandiko ya Kimasoreti mwanzoni yalithibitiwa na kikundi cha Wayahudi wanaojulikana kama Masoreti.

Maandishi ya Kimasoreti ni taarifa katika vitabu 24 zenye mamlaka vya kanoni ya Kiyahudi (Tanakh au Biblia ya Kiebrania) ambayo ni kamili ikiwa na maelezo, sarufi, matamshi, na herufi zinavyotamkwa na maelezo ya kina kuhusu maandishi. (kwa mfano idadi ya herufi katika ukurasa fulani inaweza kuwekwa pembeni mwa Taarifa ya Masoreti.)

Lengo la Masoreti lilikuwa ni kuhifadhi mfumo halisi, maneno na maana ya Maandiko. Upungufu au badiliko lolote halikukubaliwa.

Maandiko ya Kiebrania yalihifadhiwa na makuhani

Ulikuwa ni wajibu wa Makuhani kuifadhi ufunuo uliokuwa katika Maandishi wa Maandiko. Makuhani walikuwa ndio wateule wa Mungu wa kutunza Sheria yake na kuifundisha.

Kumbukumbu 31:24-26—Basi ikawa hapo Musa alipomaliza kuandika maneno ya Torati hii katika Chuo, hata yakaisha, 25 ndipo Musa akawaamuru Walawi waliokuwa wakilichukua sanduku la Agano la BWANA akawaambia, 26 Twaeni chuo hiki cha Torati, mkiweke kando la agano la BWANA, Mungu wenu, ili kiwepo kama shahidi juu yako.

Sheria iliwekwa kama muongozo kwa Makuhani ili kuitunza pamoja na lile Agano. Makuhani hao waliagizwa kuisoma Sheria kila miaka saba.

Makuhani walisimania matengenezo ya Nakala sahihi za sheria kwa ajili ya matumizi ya wafalme na watawala.

Uangalifu Mkubwa ulitumika katika kulinda na kuhifadhi maandishi yaliyovuviwa

Kristo alikuwa mwaminifu kwa ahadi yake kwamba Maandiko ya Agano la Kale hayatapotea.

Mathayo 5:18—Kwa maana Amini, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya Torati haitaondoka, hata yote yatimie.

Waandishi walitumia mbinu mbalimbali kuhakikisha usahihi wa nakala za maandishi zilizotolewa za taarifa za Kiebrania. Walitumia majaribio kama ya kuhesabu maumbo ya irabu na kukagua uwekaji wa maneno fulani katika taarifa wakati wa kuthibitisha usahihi wa nakala iliyokamilishwa upya. Nakala yote nzima ilitupwa kama ikikutwa na kosa lolote.

Tangu mwanzo wa karne ya kwanza mpaka Mageuzo ya kanisa la Protestanti, Agano la Kale la Waebrania lilihifadhiwa na Wayahudi. Waandishi wa Kiyahudi walinakili kwa uangalifu mkubwa na kuhifadhi maandishi ya Agano la Kale. Augustino alisema, waandishi wa Kiyahudi walikuwa ni Wakutubi wa kanisa la Kikristo. Waandishi wa mwanzo kabisa kati ya hawa waliitwa Tannaim (walimu) walinakili maandishi ya Agano la Kale kwa usahihi mkubwa. Watannaim walifuatwa kwa hadhi na kikundi cha waandishi walioitwa Amoraim (wafichuaji). Hawa walikuwa ni wasomi waliofanya kazi siyo kama wa kunakili tu, bali walizalisha pia ile Talmud ambayo ni kitabu kinachoweka hadharani sheria na mila za Wayahudi.

Zile desturi (Taarifa za Masoreti) zilizoandikwa na kuchapishwa mwishoni mwa enzi za kale. Zaburi zilichapishwa 1477. Katika mwaka 1488 Biblia nzima ya Waebrania ilichapishwa kwa mara ya kwanza.

Kuzikwa kwa Maandiko ya Waebrania. Walimu (Rabi) wa Kiyahudi waliziweka nakala za Maandiko Matakatifu katika heshima ya hadhi ya juu. Wakati andiko lolote lilipo zeeka au kuchujika na kuonekana halifai kwa matumizi lilipumzishwa kwa heshima kuu. Iliaminika kwamba ni bora zaidi kuzizika kwa heshima kuliko kuthubutu kuziacha ziangukue mikono isiyofaa au kudharauriwa. Hii ndio sababu ya kuwepo nakala nyingi za Agano la Kale zilizoandikwa.

Ugawaji wa Maandiko ya Waebrania katika sura na aya mbalimbali. Kugawanywa kwa Maandiko katika Aya ni jambo lililofanyika mapema kabisa na familia ya Masoreti ya ben Asheri miaka ya 900 baada ya Kristo. Mfumo huu unagawanya vitabu 39 vya Agano la Kale (kama tunavyoona katika Biblia) katika aya 23,100. Maandiko ya Waebrania yamegawanywa katika ubeti. Mgawanyiko katika sura ulifanywa kwa mara ya kwanza na Kadinali Hugh wa Mtakatifu Cher mwaka 1244 BK.

Ugunduzi wa Kanuni ya Agano la Kale

Uhusiano wa ndani katika taarifa

Hakuna taarifa ya Historia iliyo kamili ya kukubalika kwa kila kitabu cha Agano la Kale, kwa hiyo, maelezo ya Biblia yenyewe ndio taarifa za kihistoria zilizopo ambazo ni bora zaidi.

  • Vitabu vya sheria vilikubaliwa mara moja na Israeli (Kut. 24:3-4).
  • Yoshua aliandika katika kitabu cha Sheria ya Mungu (Yoshua 24:26).
  • Kitabu cha Samweli kiliwekwa mbele ya Bwana (I Samweli 10:25).
  • Kitabu cha Sheria kilianzishwa upya kipindi cha Yosia (II Fal 22:8-11, 23:1-2).
  • Ezra na Nehemia waliwaonya watu kuwa wataiendea torati ya Mungu (Nehemiah sura ya 8 na 10:28-29)
  • Waandishi wa baadaye walitambua maandiko ya mwanzo kama neno la Mungu lenye mamlaka.
    • Danieli alitambua kitabu cha Yeremia kuwa chatoka kwa Bwana (Danieli. 9:2).
    • Vitabu vya Sheria ya Musa vimetajwa katika vitabu vingine vya Agano la Kale (Yos. 1:8, 8:31, I Fal 2:3, II Fal 14:6, 21:8, 23:25, Dan. 9:11-13, Mal 4:4).
    • Maandiko ya Sulemani yanatajwa katika I Wafalme 4:32
    • Yeremia aliutaja unabii wa Mika kuanzia karne moja nyuma (Yer. 26:17-29).

Kuijaribu kanoni ya Agano la Kale

Yapo majaribio yaliyotumiwa na viongozi wa Wayahudi ili kuamua kanoni ya kitabu misingi hii ilizingatia walichotaka waandishi wa historia ya Biblia na kanisa. Ulikuwepo mfumo maalumu wa kuangalia utambuzi wa kanoni ya kitabu. Sehemu hii inataja waandishi wa kanoni za vitabu vya Biblia. Maelekezo haya ni kuhusu ukweli kwamba walikuwa ni vyombo vya kibinadamu vya mwandishi wa kiungu.

Iliandikwa na Musa?

Uandishi wa Musa wa kitabu ulichukuliwa kama jaribio halali la uvuvio na Wayahudi tangu zamani. Musa anatajwa kama nabii mkuu wa Wayahudi. Vitabu ambavyo viliandikwa na Musa vinachukuliwa kama vyenye asili ya Mungu kutoka mwanzoni kabisa mwa taarifa za historia ya Wayahudi. Ushahidi wa akiolojia wa Palestina unaimarisha sana mtazamo huu wa kitamaduni. Yesu alithibitisha kwamba Musa ndiye chombo cha kibinadamu kilichopokea ile Sheria. Musa hakuwapa torati? (Yoh. 7:19). Kama tunavyofahamu taarifa iliyoandikwa katika Biblia inaonesha kukubalika mara moja kwa vitabu vya sheria kama vilivyotolewa na Mungu.

Iliandikwa na nabii wa Mungu anayejulikana?

Iwapo kitabu hicho kiliandikwa na nabii wa Mungu anayejulikana ambaye alifikiriwa kama mwaguzi wa Mungu; kitabu hicho kiliaminiwa kuwa ni Neno la Mungu.

Mwandishi wake alithibitishwa kwa matendo ya Mungu?

Mwandishi alichukuliwa kuwa mtu wa Mungu iwapo alionesha ushahidi wa nguvu za Mungu katika maisha yake. Kama mwandishi alichukuliwa kama mtu wa Mungu na maandishi yake pia yaliaminika kwamba yametoka kwa Mungu. Watoto wa manabii walitambua mamlaka ya Elisha walipomuona amechukua nafasi ya Eliya na kuutenganisha mtu Yordani (II Fal 2:15).

Inao uelewano na kanuni nyingine za Maandiko?

Ni lazima kuwepo umoja kamili wa Maandiko. Kanuni katika sehemu moja ya Maandiko ni lazima ielewane na ukweli ulioko katika sehemu nyingine za Maandiko. Kama ilivyokwisha tamkwa wengine watabisha kwamba vitabu vilivyochaguliwa ni vile vinavyopatana na maoni ya viongozi ambao walivichagua. Hata hivyo kitabu kisingeweza kuhesabika kama cha Kanoni iwapo isingekuwa kinakubaliana na Maandiko mengine yaliyopokelewa. Kitabu kilitambuliwa kuwa cha Kanoni kwa sababu ya kuwa na uvuvio. Jambo hili kama tunavyoweza kuona siyo jaribio pekee la kuthibitisha kanoni ya kitabu. Ni wazi kwamba Kitabu chenye asili ya Mungu hakitapingana na kitabu kingine chenye asili ya Mungu.

Kinasema ukweli kumhusu Mungu?

Ni lazima kitabu kiwe sahihi katika maelezo yake kumhusu Mungu na kuhusu vitu vya Mungu. Kitabu hicho kitakaliwa kwa kutokuwa na uvuvio iwapo kutakuwa na makosa kuhusu teolojia.

Kilikubaliwa na viongozi wa Kiyahudi kama chenye mamlaka ya Maandiko?

Baadhi ya vitabu vilikubaliwa na viongozi wa Wayahudi kama vya kanoni na vingine vilikataliwa. Huu ni ushahidi kwamba viongozi wa Kiyahudi walitambua vitabu hivyo ambavyo viliingizwa katika Kanoni kama Maandiko yenye mamlaka.

Ushuhuda wa Agano Jipya unaohusu Kanuni ya Agano la Kale

Yesu alithibitisha mamlaka ya Kanoni ya Agano la Kale.

Yesu alizungumzia sehemu tatu za Kanoni ya Agano la Kale: Sheria, Manabii, na Maandiko.

Luka 24:44—…ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi.

Ni jambo la kawaida wakati wa Kristo kwa Agano la Kale kuwa katika mgawanyiko wenye sehemu hizo tatu. Kwa kuzitaja sehemu hizo, Yesu alithibitisha mamlaka ya Kanoni ya Agano la Kale kama ilivyogawanywa. Wayahudi wa siku za Yesu wangeweza kuelewa kwamba alikuwa anazungumzia ile Kanuni kamili (ya Agano la Kale) katika tamko hili:

  • Yesu aliwauliza Wayahudi: Musa hakuwapa ile Sheria? (Yoh. 7:19)
  • Yesu anatamka ile sheria na wale Manabii (Mt. 5:17; 22:40)
  • Zaburi kwa kwa ujumla inagusia sehemu ambayo kwa kawaida huitwa Maandiko

Yesu alisoma kutoka kitabu cha Isaya. Lk. 4:17-21. Yesu alizitaja taarifa hizi kama Habari Njema kwa hiyo alithibitisha mamlaka na uvuvio wake. Yesu asingetumia taarifa kutoka vitabu vya Agano la Kale kama visingekuwa na uvuvio.

Agano jipya linathibitisha mamlaka ya Agano la Kale.

Agano la Kale limetajwa mara 263 katika Agano Jipya. Matumizi ya maandiko haya katika Agano Jipya ni uthibitisho kwamba yalichukuliwa kama yenye Mamlaka katika Neno la Mungu. Paulo ametaja za taarifa za Agano Jipya kama Maandiko (Rum. 10:11; 11:2; Gal. 3:8).

Maelezo ya Kanuni ya Agano Jipya

Kanoni ya Agano Jipya imegawanywa katika sehemu tano:

  1. Injili – Mathayo, Marko, Luka, Yohana
  2. Historia – Matendo
  3. Nyaraka za Paulo – Warumi, 1&2 Wakorinto, Wagalatia, Waefeso, Wafilipi, Wakolosai, 1&2 Wathesalonike, 1&2 Timotheo, Tito, Filemoni
  4. Nyaraka za Kawaida – Waebrania, Yakobo, I&2 Petro, 1, 2, na 3 Yohana, Yuda
  5. Unabii – Ufunuo

Maandishi yaliyopokelewa (Textus Receptus)

Neno la Kilatini Textus Receptus maana yake maandishi yaliyopokelewa na yanahusu Agano Jipya la Kiyunani kama lilivyo katika maandishi ambayo yalikubaliwa na Kanisa la mwanzo. Kuna historia inayopatikana ambayo inayo taarifa yenye uvuvio ambayo ilikubaliwa na kanisa la mwanzo. Mungu alihifadhi neno lake katika vizazi vyote.

Maandishi yaliyopokelewa ndio maandishi yaliyotumiwa na wale Wanamageuzi. Kanisa la Kikristo linatambua vitabu 27 vya maandishi haya kuwa ni kanuni ya Agano Jipya na maandishi mengine yanayobakia yanapingana na yamechanganyika kiasi ambacho ni vigumu kuyafikiria kama yanaweza kuaminika.

Uchapishaji wa kwanza wa Agano Jipya la Kiyunani

Erasmo alichapisha Agano Jipya la Kiyunani mwaka 1516. Erasmo alitumia maandishi yote yaliyokuwepo katika kuchapisha hili Agano Jipya la Kigiriki. Alitaja pia mkusanyiko wa Kilatini (Latin Vulgate) ambao aliamini kuwa inazo dosari nyingi na kukosa maadili ili kuhakikisha kwamba ameangalia kila kianzio kilichokuwepo. Alitegemea kupata taarifa sahihi ambayo ni halisi na inao uvuvio wa Roho Mtakatifu. Agano Jipya la Kiyunani la Erasmo lilikuwa ni matokeo yenye uelewano na uaminifu wa taarifa za Kiyunani zilizoandikwa kwa mikono ambazo zilitumiwa kabla ya kuwepo mashine za uchapishaji. Alitumia kila daftari iliyokuwa imeandikwa na akazilinganisha kwa uangalifu mkubwa ili kuhakikisha anapata Agano Jipya la Kiyunani lililo sahihi ambalo litachapishwa na kusambazwa kwa mara ya kwanza.

Erasmo hakuanzisha maandishi yaliyopokelewa; alikusanya na kuchapisha. Alikusanya nakala nyingi zilizoandikwa kwa mkono za Maandiko zilizokuwa katika mzunguko na kwa kulinganisha moja na nyingine alipata msimamo kati yake ambao aliuchapisha kama Agano Jipya.

Hatupaswi kulionyesha kama ni chimbuko la Erasmo la ‘maandishi yaliyopokelewa’ bali kama muendelezo wa kutoka kwenye maandishi ya mkono iliyozooeleka jinsi ilivyopokelewa kwenda kwenye mfumo wa kuchapisha, ambao uliendelea kuwepo kwa karne tatu.
–Kenneth W. Clark, msomi wa Maandishi ya Kiyunani (msisitizo umeongezwa)

Roho Mtakatifu alizilinda na kuzihifadhi taarifa za kweli za Agano Jipya

Neno la Mungu halitapita

Mathayo 24:35—Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

I Petro 1:23—Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili si kwa mbegu iharibikayo bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima lidumulo hata milele.

Roho Mtakatifu aliwafundisha Wakristo ni vitabu vipi vyenye uvuvio

Yohana 14:25-26—Hayo ndiyo niliyowaambia wakati nilipokuwa nikikaa kwenu. Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

Roho Mtakatifu aliwaongoza pia Wakristo kutambua ni vitabu gani vilivyokosa uvuvio

Baadhi ya vitabu vilichukuliwa kwa makosa kama vyenye kanoni na baadhi ya Wakristo wa mwanzo. Kwa mfano Ireneo alichukulia kitabu cha “mchungaji wa Hermesi” kuwa ni kimojawapo chenye uvuvio. Roho Mtakatifu aliweka kanoni katika hali yake ya sasa kwa vitabu 27 vya agano Jipya.

Taarifa zilizopokelewa za Agano Jipya zilihifadhiwa na viongozi wa kanisa

Mwanzoni kabisa mwa kanisa Mitume waliagiza kanisa ni vitabu vipi vyenye uvuvio na vipi havina. Mkumbuke Yohana, yule mtume wa mwisho kati ya Wafuasi waanzilishi, alikuwa na umuhimu katika kuliagiza kanisa na kulifikishia maandiko ya kweli yenye uvuvio ya Agano Jipya hadi mwaka wa 100 Baada ya Kristo.

Viongozi wa kwanza wa kanisa walizifikisha taarifa hizo za Agano Jipya kwa waliowapokea. Inyasi na Polikarpi ambao walikuwa ni viongozi wa kanisa la mwanzo walifundishwa na Mtume Yohane kwa kuwapa maagizo ya kitume moja kwa moja kuhusu elimu ya maandishi yenye uvuvio. Polikarpi alimfundisha Ireneo ambaye baadaye alikuja kuwa kiongozi wa kanisa. Wale viongozi waliwafundisha warithi wao ukweli wa Neno la Mungu.

Ugunduzi wa Kanoni ya Agano Jipya

Zipo taarifa za Kihistoria kuhusu kukubalika kwa Kanoni ya Agano Jipya

Vitabu vya mwanzo vya Agano Jipya vilivyokusanywa pamoja ni nyaraka za Paulo. Mkusanyo wa nyaraka za Paulo ulikuwepo katika mzunguko mwanzoni mwa karne ya pili. Inyasi ambaye ni kiongozi wa Karne ya Pili alitaja nyaraka za Paulo kama Injili. Mkusanyiko wa barua za Paulo ulikuwepo wakati Polikarpi alipowaandikia Wafilipo na wakati Inyasi alipoandika barua zake saba kwa makanisa ya Asia ndogo mwaka 115 Baada ya Kristo.

Zile Injili nne zilikusanywa pamoja na kuwekwa katika mfumo muda fulani katika karne ya pili. Tarehe kamili ambapo Injili hizo nne ziliwekwa pamoja haijulikani. Inakubaliwa kwa ujumla kwamba ziliwekwa pamoja na kukubaliwa kabla ya mwaka 170 Baada ya Kristo, kwa sababu injili hizo nne za Kanoni zilitumiwa na Tatiano ambaye alikuwa ni kiongozi wa Kanisa katika kongamano lake la Injili lililoandikwa mwaka wa 170 Baada ya Kristo. Ireneo, katika kitabu chake "kinyume cha upotofu" (mwaka 182-88 Baada ya Kristo), anazitaja injili hizo nne za Agano Jipya akizisema ni Maandiko.

Injili nne zinazotajwa kama Injili na nyaraka za Paulo anayetajwa kama Mtume zilikuwemo katika mzunguko kama mkusanyo tofauti miaka ya mwanzo ya karne ya pili. Sehemu hizi mbili ziliunganishwa baadaye kwa kitabu cha Matendo ambacho kilizileta pamoja katika mkusanyo mmoja wa vitabu. Hii ilikuwa ni hatua ya mwanzo ya kuvikusanya vitabu vya Agano Jipya katika kanoni moja iliyo kamilika.

Kabla ya mwaka 200 Baada ya Kristo nyaraka za Paulo, Injili, Matendo, I Petro na I Yohana zilitambuliwa kama Maandiko na kanisa la Kikristo. Maandishi ya Ireneo, Klementi wa Aleksandria na Tertuliano yanaonyesha kukubaliwa kwa vitabu hivi kama vyenye uvuvio na vilivyo hesabika kuwa na mamlaka sawa na yale yaliyoandikwa katika Agano la Kale. Vitabu saba vilivyobaki, Yohana 2 na 3, Petro 2, Waebrania, Yakobo, Yuda na Ufunuo, vilikubaliwa kama Injili mwaka 300 Baada ya Kristo.

Ushuhuda uliomo katika Agano Jipya lenyewe

Mtume Petro muda mfupi kabla ya kufa kwake, alitaja nyaraka za Paulo kama Maandiko na Injili nyingine zilizobaki kuonyesha kwamba anaziheshimu kazi nyingine katika vitabu vyenye uvuvio vya Injili (II Petro 3:15-16). Kitabu cha Ufunuo kinayo taarifa kwamba ni cha unabii (Ufu. 1:3, 22:18, 19).

Upo ushahidi wa kihistoria wa matumizi ya vitabu vya Agano Jipya uliofanywa na viongozi wa zamani wa kanisa

Klementi wa Roma (97-140 BK) aliandika mengi kutokana na kuhusu Agano Jipya

Klementi wa Roma mwaka 95 Baada ya Kristo aliandika barua kwa jina la Wakristo wa Roma kwa wale walioko Korinto. Katika barua hiyo anatumia taarifa zinazopatikana katika Mathayo na Luka.

Inyasi (35-116 BK) inataja maeneo makubwa ya Agano Jipya

Barua za Inyasi (115 BK) zimetumia lugha inayopatikana katika nyaraka zote za mtume Paulo. Waraka kwa Polikarpi unataja sehemu za kitabu cha Wafilipi na kugusia barua tisa kati ya barua za Paulo. Inyasi ananukuu kutoka Mathayo na I Petro na I Yohana pia.

Polikarpi (69- 155 BK) amerejea mara nyingi katika maandiko ya Agano Jipya

Kunao ushuhuda wa kihistoria wa kukubalika kwa kanuni kwa viongozi wa Kanisa

Theofilo (115-188 BK), Askofu wa Antiokia mwaka 168 BK, aliwataja wainjilisti na Maandiko Matakatifu ya Agano Jipya

Klementi wa Aleksandria (115-188 BK) katika kipindi cha pili cha karne ya pili panatajwa ukusanyaji wa Injili nne ambazo zilitambuliwa kama Maandiko

Ireneo (130-200 BK) analitaja Agano Jipya kama Maandiko Maandiko Matakatifu

Ananukuu kutoka kila kitabu cha Agano Jipya isipokuwa Filemoni na III Yohana. Kanoni ya Agano Jipya inayo tambuliwa na Ireneo inafanana sana na tuliyonayo leo.

Tertuliano (160-221 BK) alitumia kwa mara ya kwanza maneno Agano Jipya na anaiita Biblia kamili kama chombo kizima cha Maagano yote mawili

Eusebio (260-340 BK) kwenye mwaka wa 330 BK aligawa vitabu vyote 27 vya Agano Jipya katika mafungu ya vinavyobishaniwa na visivyokuwa na ubishani

Atanasi (298-373 BK), Askofu wa Aleksandria, katika barua yake ya pasaka ya mwaka 367 BK aliorodhesha vile vitabu 27 vya Agano Jipya na akatumia maneno kuwekwa kanoni kuvihusu.

Majaribio ya uwepo Kanoni katika Agano Jipya

Yalikuwepo majaribio ambayo yalitumiwa na kanisa la mwanzo kuamua kuwepo kwa kanoni katika kitabu. Walikuwepo viongozi wa kanisa waliohusika kwa wakati mbalimbali ambao waliamua ni vitabu gani vyenye uvuvio na visivyokuwa nao. Ifuatayo ni miongozo mnne iliyotumiwa na viongozi hawa katika ugunduzi wao wa kanoni ya Agano Jipya.

Kitabu hiki kiliandikwa na Mtume?

Tunaelewa kwamba Mungu ndiye mwandishi wa Agano Jipya. wale Mitume walikuwa ni baadhi ya watu watakatifu wa Mungu ambao kwa Utukufu wake Mwandishi aliongea kuwapitia wao. Kama kitabu kiliweza kuthibitishwa kuandikwa na mmoja wa wale mitume wa mwanzo wa Yesu kilichukuliwa kama chenye asili ya Mungu. Uzito mkubwa uliwekwa katika ufundishaji na maagizo ya mitume wale wa mwanzo. Maandiko yaliyowahusu wao yalisambazwa kati ya jamii za Kikristo za kwanza kabisa.

Kitabu hiki kiliidhinishwa na Mtume?

Iliaminika kwamba wale mitume wa kwanza walifahamu zaidi ni vitabu vipi vyenye uvuvio na ni vipi visivyokuwa nao. Kitabu ambacho hakikuandikwa na mtume ambacho kilikuwa na idhini ya Kitume kilichukuliwa kuwa na asili ya Mungu.

Kitabu hiki kilipokelewa kimataifa na kanisa la mwanzo mwishoni mwa karne ya nne?

Vipo vitabu fulani ambavyo vilikubaliwa haraka na kanisa la mwanzo kuwa Maandiko yenye Utukufu wa Mungu. Vitabu hivi viliingizwa mara moja katika Kanuni. Kulikuwepo na vitabu vingine ambavyo vilichukua muda kukubaliwa na kanisa kuwekwa katika orodha ya kanoni.

Kitabu hiki kilisomwa hadharani wakati kanisa la mwanzo lilipokusanyika kwa Karamu ya Bwana?

Tunayo taarifa ya kihistoria kutoka kwa viongozi wa mwanzo wa kanisa zinazoonesha kwamba ni vitabu gani vilisomwa katika makusanyiko ya kanisa. Vitabu hivi vilitumiwa na kanisa kwa sababu vilichukuliwa kama vyenye uvuvio.

Kitabu hiki kinao uwiyano na vitabu vingine vilivyokubalika vya Maandiko?

Kama ilivyokwisha tamkwa kuhusu kukubaliwa kwa Maandiko ya Agano la Kale kwamba ni lazima kitabu kioane vizuri na vitabu vingine vyenye kanoni iliyokwisha kubalika. Pamoja na hayo, vitabu vya Agano Jipya ambavyo vilipokelewa vinapaswa kuwa na uwiano na kanoni ya Agano la Kale na kanoni ya Agani Jipya ya Maandiko Matakatifu.

Vitabu vinavyoitwa Homologoumena na Antilegomena

Homologoumena maana yake iliyokubalika na inahusu vitabu vya Agano Jipya ambavyo vilikubalika mara moja. Vitabu 20 kati ya 27 vya Agano Jipya vilikubalika mara moja na vikapokelewa ulimwenguni pote kuwa asilia na kuitwa Homologoumena. Vitabu hivi 20 ni zile Injili nne, Matendo, Nyaraka za Paulo (isipokuwa Waebrania), na nyaraka za kwanza za Yohana na Petro.

Antilegomena maana yake kupinga na inahusu vitabu ambavyo viongozi wa kanisa hawakuvikubali haraka na walichukua muda zaidi kuvikubali katika kanoni ya Maandiko. Vitabu vile saba vya Waebrania, II Yohana na III, II petro, Yuda, Yakobo, Ufunuo vilipingwa kwa kipindi fulani na kuitwa Antilegomena. Yalikuwepo maswali kadhaa kuhusu vitabu vilivyoitwa Antilegomena. Moja ya maswali hayo ni lile la kwamba viliandikwa kweli na wale watu wanaoitwa waandishi wake. Waebrania kilikuwa hakina jina la mwandishi wake na kilitofautiana na mwelekeo wa nyaraka za Paulo uliofahamika; II Petro ilikuwa na tofauti na I Petro; Yakobo na Yuda walijiita watumishi; na siyo mitume; mwandishi wa II Yohana na III Yohana alijiita mzee na siyo mtume. Uandishi wa kitume ulichukuliwa kama kigezo muhimu katika kutambua kanoni ya kitabu. Yalikuwepo maigizo mengi yaliyodai mamlaka ya kitume, kwa hiyo vitabu hivi vilichunguzwa kwa makini kabla ya kuingizwa katika kanoni.

Swali lingine ni kwamba Yuda aliandika taarifa ambazo hazijatajwa mahali pengine katika Maandiko na anamtaja Henoko jambo ambalo lilihusishwa na Apokrifa. Kitabu cha Ufunuo hakikueleweka kwa viongozi wengi wa kanisa kwa hiyo kikazua maulizo katika akili zao. Vitabu hivi havikukubalika mara moja na kuwekwa mahali pake katika kanoni. Baada ya kuchunguzwa kwa makusudi mwishoni vilipokelewa kama halisi, na ucheleweshaji wake ukathibitisha uchunguzi ambao ulitumika katika mchakato wa kuviweka kanoni. Mwanzoni mwa karne ya nne vilipokelewa katika makanisa mengi na mwishoni mwa karne hiyo vikapokelewa na makanisa yote.

Vitabu vya Apokrifa

Neno hili Apokraifa hutumiwa kwa vitabu vilivyoko kati ya Agano la Kale na Agano jipya na hujumlishwa kama rejea kwa baadhi ya kanoni. Vitabu hivi vimepata jina lake kutokana na neno la Kiyunani apokruphos, maana yake iliyofichika. Vilipewa jina hili kwa sababu vilifichika na mamlaka yake hayajulikani. Kanisa la Katoliki la Roma linakubali Apokraifa kama sehemu ya kanoni yao ya Maandiko. Wayahudi wanavitambua kama sehemu muhimu ya historia ya Taifa lao. Vitabu hivi havikufikia kiwango cha msingi wa majaribio ya kuwekwa kanoni. Havikutambuliwa kama vitabu vyenye uvuvio na Wayahudi. Vilipewa sehemu yake vyenyewe katika kitabu hicho kitakatifu vikiwa na maelezo ya kutosha kwamba havihesabiwi kama vyenye mamlaka yaliyosawa na vitabu vyenye kanoni. Baadhi ya viongozi wa kanisa walitumia neno hili kwa vitabu ambavyo havina kanoni.

Maandiko yenye maana ndogo

Maneno haya yalitumika kuvihusu vitabu vilivyoonekana kudai kutambuliwa kuwa na umuhimu au thamani ya kidini. Baadhi ya vitabu vilivyomo katika kundi hili vilionekana kulaghai kwa kudai kuwa na asili ya Kitume kama injili ya Tomaso. Vilikuwepo vitabu vingi vilivyoandikwa ambavyo havikuwa na uvuvio ijapokuwa vilidai aina fulani ya utukufu wa Mungu. Vitabu vilivyomo katika kundi hili huitwa maandiko yenye maana ndogo. Haya ni maneno ambayo yanatumika katika tahariri nyingi na machapisho ya utafiti. Mwanafunzi makini wa Biblia anapaswa angalau kuwa na uelewa wa msingi wa kinachofahamika kuhusu maneno haya.

Orodha ya Kanuni mbalimbali

Kanuni tofauti zimeorodheshwa na madhehebu mengi ya kidini na viongozi wa kanisa katika historia yote.

Kanuni ya Kiyahudi

Kanuni ya Kiyahudi inaundwa na vitabu 39 vya Agano la Kale.

Kanuni ya Kisamaria

Kanuni ya Kisamaria ndiyo Biblia iliyo ndogo kuliko zote duniani na ambayo hutambua vitabu vitano tu vya Pentateukia.

Kanuni ya Marsiyo

Marisiyo ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kutengeneza orodha ya baadhi ya vitabu vya Agano Jipya. Marisiyo alilikataa Agano la kale lote na akamuona Mungu wa Agano la Kale kuwa ni mdogo kwa Yesu. Kanoni ya Marsiyo iliundwa na vitabu 10 tu ambavyo ni nyaraka za Paulo (ukiondoa ambazo za kichungaji) na injili ya Luka. Vitabu hivi alivifanyia masahihisho ili vielewane na ufundishaji wake uliokengeuka. Ingawaje alikuwa muongo kuibuka kwa mafundisho ya uongo kulilifanya kanisa ligundue umuhinu wa kufafanua kanoni ya kweli ya Maandiko.

Kanuni ya Muratoriano iliyotawanyika

Mtawanyiko wa Kanuni Muratoriano unaorodhesha kanoni ya vitabu vya Agano Jipya. Mtawanyiko wa Muratoriano ambao ni maandishi ya kale sana katika miaka ya 200 Baada ya Kristo inayo orodha ya Kanoni kwa vitabu vya Agano Jipya. Haisomeki yote kwa hiyo inaelezewa kama iliyotawanyika. Inavitambua vitabu vyote isipokuwa Waebrania, Yakobo, II Petro, na III Yohana. Lipo pia suala la I Petro ilivyotajwa au hapana. Imejumuisha pia kitabu kimoja kiitwacho Apokalipse cha Petro ambacho kilikataliwa baadaye kwa kutokuwa na Kanuni.

Kanuni ya Terituliano

Tertuliano (160-221 Baada ya Kristo) anavyo vitabu 22 katika kanoni yake ya Agano Jipya inayohusu Injili nne, Matendo, nyaraka 13 za Paulo, I Petro, I Yohana, Yuda na Ufunuo. Hakukiona kitabu cha Waebrania kama chenye kanoni.

Kanoni ya Origeni

Origeni (185-254 Baada ya Kristo) alikiri Injili nne zenye kanuni, matendo, Nyaraka za Mtume Paulo na Waebrania, I Petro, I Yohana na Ufunuo kama vitabu visivyokuwa na upinzani. Origeni alikiri kwamba Waebrania, II Petro, II na III Yohana, Yakobo na Yuda ni vitabu visivyokuwa na upinzani.

Kanuni ya Eusebio

Eusebio (260-340 Baada ya Kristo) anachukuliwa kama mwanahistoria wa kanisa. Anatupatia taarifa kamili yenye maelezo ya nafasi ya kanisa kwa upana. Anaonesha tofauti muhimu kati ya homologoumena (vitabu vilivyokubaliwa) na antilegomena (vitabu vilivyopingwa). Vitabu vilivyo kubaliwa ni zile Injili, Matrndo, Nyaraka za Paulo pamoja na Waebrania, I Petro, I Yohana, na Ufunuo. Amevigawanya vitabu vilivyopingwa katika mafungu mawili madogo: (1) vile vinavyoelekea kufaa kuingizwa katika Kanoni - Yakobo, Yuda, II Petro, II na III Yohana (2) vile visivyoelekea kufaa kuingizwa katika kanoni — Matendo ya Paulo, Mchungaji wa Herimesi, Apokalipse ya Petro, Didisi, Barnaba. Alihoji kuingizwa kwa ufunuo kutokana na wasiwasi wa kuhusika Mtume katika Uandishi wake. Ukiacha kusita huku kwenye Ufunuo kwa Eusebio yeye katika Agano Jipya anafanana na la wakati wetu.

Kanuni ya Atanasio

Atanasio (298-373 Baada ya Kristo), Atanasio amaorodhesha vitabu 27 vya Agano Jipya la wakati wetu.

Kanuni ya Katoliki ya Roma

Kanisa Katoliki la Roma linaingiza ndani vitabu 66 vya Biblia yetu na kukubali pia vitabu vya Apokraifa kama sehemu ya kanoni yao ya Maandiko. Hii ni kanoni ile ile ya Yerome aliyetengeneza Vulgeti ya Kilatini ambayo ni msingi wa Biblia ya Katoliki ya Roma.

Kanuni ya kweli inayotambuliwa na kanisa la Kikriso

Kanoni ya kweli imeundwa kwa vitabu 39 vya Agano la Kale na vitabu 27 vya Agano Jipya la Biblia.

Kanuni ya Lutheri

Martini Lutheri aliorodhesha vitabu 27 vya Agano Jipya kama lilivyo isipokuwa vitabu vinne alivyoviona kama vyenye utata. Aliweka Waebrania, Yakobo, Yuda na Ufunuo kwa utenganisho mwishoni mwa Agano Jipya.

Vipindi Saba Maalum katika Maandiko Matakatifu

I II III IV V VI VII
MWANZONI VIONGOZI WAKUU WAFALME WATAWALA WAGENI UJIO WA KWANZA WA KRISTO KANISA UJIO WA PILI WA KRISTO
KUTOKA: Uumbaji KUTOKA: Musa KUTOKA: Saulo KUTOKA: Kutekwa KUTOKA: Uzalio wa Bikra KUTOKA: Pentekoste KUTOKA: Millenia
HADI: Musa HADI: Paulo HADI: Kutekwa HADI: Kristo HADI: Kupaa HADI: Mateso HADI: Mbingu mpya & Dunia Mpya
VITABU: Mwanzo, Kutoka VITABU: Kutoka, Walawi, Hesabu, Kumbukumbu, Yoshua, Waamuzi, Ruthu, I Samweli VITABU: I & II Samweli, I & II Wafalme, I & II Nyakati, Vitabu vya Manabii VITABU: Ezra, Nehemia, Esta, Danieli, Ezekieli VITABU: Mathayo, Marko, Luka, Yohana VITABU: Matendo Nyaraka VITABU: Ufunuo