Skip to main content

Sura ya 1: Maelezo ya Kawaida ya Biblia

Maelezo ya Msingi ya Biblia

BIBLIA  NI   NINI?

  • Biblia ni Ufunuo wa Mapenzi ya Mungu kwa wanadamu.
  •  

    Mungu hakuandika kitabu kingine zaidi ya Biblia. Hakuna ushahidi mwingine wowote wenye maelezo ya kina ya mapenzi ya Mungu na uwezo  wake zaidi ya Biblia. Ni kwa kusoma Biblia peke yake ndio tunaweza kuwa na majibu kuhusu maswali mengi yanayomhusu Mungu.

     

    • Mungu ni nani?
    • Mungu anapenda nini?
    •  Mungu anataka nini?
    • Mpango wa Mungu ni nini?
    • Kwa nini Mungu anatenda kile anachotenda ?
    • Na, kadhalika.

     

    Katika Biblia Mungu ameandaa maelezo ya habari za mapenzi yake na kuonyesha upendo wake kwa binadamu. Ufunuo mwingine wowote unapaswa kuoana na kitabu hiki cha ajabu. Ni kiwango cha uhai wote—wa muda mfupi na wa milele!

     

    • Dhamira kuu ya Biblia ni wokovu kupitia  Yesu Kristo

    (‘ya katikati’ kuu , kiongozi, dhamira ya msingi – mada, kama ya hotuba.)

     

     

    • MAMBO YANAYOIHUSU BIBLIA
    •  

    Mwanzoni Agano la Kale liliandikwa kwa Kiebrania (na asilimia ndogo kwa Kiarabu.) Agano Jipya liliandikwa kwa lugha ya Kigiriki. Toleo la Kingereza la Mfalme Yakobo ni tafsiri inayotokana na lugha hizi asilia. ‘Kutafsiri’ maana yake ni kubadilisha kutoka lugha moja kwenda katika lugha nyingine.

     

    Biblia ni kitabu kimoja, historia moja, na simulizi moja  HISTORIA YAKE [Historia ya Mungu]! Tunaiita Biblia TAKATIFU kwa sababu ni Neno la Mungu na siyo hadithi tu ya wanadamu. Neno TAKATIFU maana yake tukufu, safi, isiyo na lawama, au ya kidini, iliyotengwa. Biblia ni kitabu cha Kimungu ingawaje Mungu aliwatumia watu kuueleza ukweli wake Mtakatifu. Watu watakatifu (asili yake binadamu) waliandika kama walivyo himizwa na Roho Mtakatifu (Utukufu wa asili ya Mungu). Kwa kuwa ni Neno la Mungu hatuwezi tukatimiza wazo kwa kitabu au taarifa moja ya Biblia.

     

    Biblia inavyo vitabu 66, 39 katika Agano la Kale na 27 katika Agano Jipya. Utukufu wa Kimungu umefunuliwa katika Biblia kwa utaratibu kuanzia kitabu cha Mwanzo hadi mwisho wake katika Kitabu cha Ufunuo. Mwanzo ni kitabu kinachoonyesha asili; Ufunuo ni kitahu kinachohusu mwishoni. Vitabu vya Biblia vya katikati ni maneno ya Mungu ya uamsho kutoka katika ulimwengu ulioharibika. Kila kitabu cha Biblia kinao ujumbe wake, hata hivyo kitabu kizima kinakuwa na ujumbe wa wokovu wa mwanadamu ambao unaonekana. Inaweza kusemwa pia kwamba Agano la Kale ni taarifa ya taifa ( Israeli ) na agano jipya ni taarifa za mwanadamu (Yesu)

     

    • MAJINA YA BIBLIA TAKATIFU

     

     

    • Biblia Takatifu

     

     

    • Neno hili Biblia haliko mahali popote katika maandishi ya Biblia. Neno biblia tunalipata katika neno la Kigiriki  biblios ambalo maana yake ni “vitabu.”  Neno biblios kwa asili yake lilitumiwa kuhusiana na maandishi ya yaliyotumia mafunjo{magombo} katika utengenezaji wa karatasi za kale. Neno la Kingereza biblia maana yake “vitabu.” Biblia Takatifu ni kuhusiana na mkusanyiko wa vitabu Vitakatifu.

     

     

    • Majina ya Biblia kwa yenyewe  

    • Kile Kitabu

     

    Mwanzo 5:1- Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu.

     

    Zaburi 40:7- Ndipo niliposema, Tazama nimekuja, (katika gombo la chuo nimeandikwa, (Ebr. 10:7)

     

    Mathayo 1:1- Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo mwana wa Daudi, Mwana wa Ibrahimu.

     

    Luka 4:17- Akapewa chuo cha Nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa.

     

    • Agano

     

    • Neno Agano maana yake mkataba au mapatano.  Vitabu vya Biblia kwa mapatano ya zamani vinaitwa Agano la Kale na vitabu vya Biblia katika mapatamo mapya vinaitwa Agano Jipya.

     

    II Wakorinto 3:14 – Ila fikra zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi, wakati lisomwapo Agano la Kale, utaji uo huo wakaa; yaani, haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo.

     

    II Wakorinto 3:6 – Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa Roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.

     

     

    • Andiko

     

    • Neno andiko maana yake “maandishi.”  Neno hili hutumiwa kuhusiana na maandishi matakatifu, na mara nyingi hutumiwa kwa uhusiano na Biblia. Yesu alizungumzia maandishi ya Nabii Isaya kama maandiko  (Lk. 4:21). Yesu aliwauliza wakuu wa makuhani na wazee: “Hamkupata kusoma katika maandiko .…” (Mt. 21:42) Kwa mara nyingine tena Yesu alitumia Neno hili alipokuwa akiongea na masadukayo: “mwapotea kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.” (Mt. 22:29) Sehemu nyingine kuhusu maandiko: Lk. 24:27, Rum. 1:2, Rum. 15:4, II Tim. 3:15-16; I Petro 1:20

     

    • Neno la Mungu

     

    •  Hili ndio muhimu, lenye nguvu na jina kamili la Biblia Takatifu.  Biblia ni Neno la Mungu lililoandikwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya mwanadamu. Biblia siyo Neno la mwanadamu. Biblia ni Neno la Mungu. Taarifa muhimu: Mk. 7:13, Rum. 10:17, II Kor. 2:17.
    • Waebrania 4:12 – Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na Roho na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

     

    • ULINGANISHO: AGANO LA KALE & AGANO JIPYA

     

    • Yote mawili huanza na Uungu.
    •  
    • Agano la Kale huanza na Mungu. –  Mwanzo 1:1
    •  
    • Agano Jipya huanza na Kristo.–  Mathayo 1:1

     

    • Yote mawili hushirikiana dhamira moja.

     

    • Wokovu kwa njia ya Yesu Kristo ni dhamira  kwa Maagano yote mawili.
    •  
    • Agano la Kale huangalia mbele kwa imani katika msalaba. Ukombozi kwa damu ya Yesu ulikuwa mpango wa Mungu kwa Agano la Kale na ndio mpango wa Mungu kwa Agano jipya.

     

     

    Ufunuo 13:8 – Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana -  Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.

     

    Mpango wa Mungu toka mwanzo wa nyakati ni wa Yesu ambaye ni Kondoo wa Mungu kumwaga Damu Yake Takatifu kwa malipo ya ukombozi wetu.

     

    • Agano Jipya huangalia nyuma katika kazi iliyokamilishwa katika msalaba.

     

    • Kristo yupo katikati ya yote mawili.

     

    • Agano la kale limejaa utabiri wa Kristo. Utabiri huu huitwa Utabiri wa Mesia. Agano la kale linavivuli vingi na viashiria vinavyoonesha ujio wa Kristo. Sheria ni mwalimu wa kutupeleka kwa Kristo. – Gal. 3:24  Kristo ni utimilifu wa sheria.  

     

    Mathayo 5:17 – Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; laa, sikuja kutangua bali kutimiliza.

     

    Kristo ndie mtu wa katikati katika Agano Jipya. Kristo ndiye mpatanishi wa Agano Jipya – Ebr. 12:24     

    •  
    • AGANO LA KALE NA AGANO JIPYA: LILIVYO TENGANISHWA

     

    • Historia
    • Yoshua
    • Waamuzi
    • Ruthu
    • 1 Samweli
    • 2 Samweli
    • 1 Wafalme
    • 2 Wafalme
    • 1 Mambo ya Nyalati
    • 2 Mambo ya Nyalati
    • Ezra
    • Nehemia
    • Esta
    • Ushairi
    • Ayubu
    • Zaburi
    • Mithali
    • Mhubiri
    • Wimbo ulio bora
    • Manabii Wakuus
    • Isaya
    • Yeremia
    • Maombolezo
    • Ezekieli
    • Danieli
    • Manabii Wadogo
    • Hosea
    • Yoeli
    • Amosi
    • Obadia
    • Jona
    • Mika
    • Nahumu
    • Habakuki
    • Sefania
    • Hagai
    • Zekaria
    • Malaki

     

    • Agano Jipya
    • Injili
    • Mathay
    • Marko
    • Luka
    • Yohana
    • Historia
    • Matendo
    • Nyaraka za Paulo
    • Warumi
    • 1 Wakorinto
    • 2 Wakorinto
    • Wagalatia
    • Waefeso
    • Wafilipi
    • Wakolosai
    • 1 Wathesalonike
    • 2 Wathesalonike
    • 1 Timotheo
    • 2 Timotheo
    • Tito
    • Filemoni
    • Mkuu wa nyaraka
    • Waebrania
    • Yakobo
    • 1 Petro
    • 2 Perto
    • 1 Yohana
    • 2 Yohana
    • 3 Yohana
    • Yuda
    • Unabii
    • Ufunuo

     

    • KUSUDI LA BIBLIA

     

    • Biblia iliandikwa ili wanadamu wa weze kuamini, kuelewa, kufahamu, kupenda, na kumfuata Kristo.

     

    • Kwamba wanadamu wataweza kuamini kuwa Yesu ndiye Kristo. Dhamira kuu ya Biblia ni ukombozi kwa njia ya Yesu Kristo. Neno Kristo maana yake “aliyepakwa mafuta”, na ni kumhusu Masia. Wanadamu wanapaswa kuamini kwamba Yesu ndiye Mwokozi. (Warumi. 1:16)  

    Yohana 20:31— Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, mwana wa Mungu; na kwa kuamini muwe na uzima kwa jina lake.

     

     

    • Kwamba wanadamu wataweza kuelewa Kristo ni nani. Yesu anajifunua Mwenyewe katika Neno Lake.  Biblia inatuambia kwamba Maandiko yanamthibitisha Yesu. Wanadamu wanapaswa kuelewa kwa tafakari ya Neno kwamba Yesu ndiye Masia; Yeye ndiye Mwokozi na njia pekee ya kupata Wokovu.

     Yohana 5:39—Mwayachunguza Maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia.

     

     

    • Ili wanadamu waweze kumfahamu Kristo. Biblia huwasaidia wanadamu kumfahamu Kristo. Mwandishi wa wimbo alitamka, “Ninayo furaha kwa kuwa ninamjua Yesu!”  Paulo alitamani kumfahamu Kristo kwa undani zaidi. Wakristo wanaweza kufahamu Yesu ni nani na wanaweza pia kumjua binafsi kwa kushirikiana naye katika masomo

    Yohana 17:3—Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

     

    • Ili wanadamu wampende Kristo. Kufuatana na Maandiko, ili mwanadamu ampende Kristo anapaswa kuyashika maneno yake Kristo ambayo yamo katika Biblia.  Inatupasa kujifunza Biblia ili tuweze kulitii Neno la Mungu na kumpenda Yesu.    

    Yohana 14:23—… mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda …

    I Yohana 2:5—Lakini yeye alishikaye Neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika …

    • Ili wanadamu weweze kumfuata Kristo. Neno Mkiristo maana yake “Mtu anayemfuata Kristo.” Biblia imeandikwa ili wanadamu waweze kumfuata Kristo.

    Yohana 10:27—Kondo wangu waisikie sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata.

    Yohana 12:26—Mtu akinitumikia, na anifuate

     

    • Biblia inaonesha kusudi na mpango wa Mungu.

     

    • Mambo yanayohusu Wokovu. Biblia inaeleza kwamba wokovu unapokelewa kwa njia ya kumwamini Yesu na inaonyesha jinsi mwanadamu anavyohitaji wokovu.
    • Yohana 3:16—Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

     

    • Kulihusu Kanisa. Katika mpango wa Mungu kulihusu kanisa lake ni kwamba ndilo linalopaswa kuwa tukufu, takatifu lisilo na mawaa.  Yapo maagizo mengi kwa kanisa katika Biblia.

     Waefeso 5:27—Ili apate kujiletea kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.

    • Kuhusu siku za mwisho. Biblia inaonyesha mpango wa Mungu kwa siku za mwisho.  Tunaelewa kwamba Biblia inasema tunaishi katika siku za mwisho naye Mungu alituonya kuhusu matukio yatakayokuja kupita katika siku hizi za mwisho.

    II Timotheo 3:1—Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.

     

    • Biblia ni andiko la Neno la Mungu kwa mwanadamu.

     

    • Ni neno la hakika lililotabiriwa na manabii. Bibilia ni Neno la Mungu lisilokuwa na kosa.  Siyo kwamba lina neno la Mungu ndani yake bali ni Neno la Mungu.  Biblia ni Neno makini katika saa ya giza.

    II Petro 1:19-21—Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi,  ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu. 20. Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. 21. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

     

     

    • Ni msingi imara. (I Kor. 3:11) neno la Mungu ni msingi imara wa imani yetu.  Yesu ni mwamba wa wokovu wetu. Yesu ni Neno lililogeuka nyama. Wakati kila kitu kingine kikiwa kinazama; Neno la Mungu halitashindwa.

     

    I Wakorinto 3:11—Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani,  Yesu Kristo.

     

    • Ni Neno lenye nguvu lisilokuwa na kosa. Neno nguvu maana yake “Lenye pumzi ya Mungu.”  Kuna uhai katika Neno ambao ni pumzi halisi ya Mungu.  Neno la Mungu ni bila makosa au kupingana.  

    II Tim. 3:16—Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kuwaonya watu makosa yao, na kuwaongoza, na kuwaadibisha katika haki:

     

    • Biblia ni mamlaka ya mwisho.

     

     

    • Kuhubiri na kufundisha ni lazima msingi wake uwe ni Neno la Mungu.
    • (II Tim. 4:2) Paulo alimwambia Timotheo alihubiri Neno. Neno ni msingi wa imani yetu  (Rum. 10:17)  Tunachoamini na kukihubiri kinapaswa kuwa na uelewano mzuri na Biblia.

     

    • Kila swali linapaswa kutulizwa kwa Neno la Mungu. Ni sharti Biblia iwe mamlaka kuu katika kila eneo la swali katika maisha ya wanadamu. Mamlaka ya Neno la Mungu haipaswi kuwekewa maswali na mtakatifu wa Mungu.  Hii ndio sababu inayotufanya tulazimike kufahamu bila mashaka yoyote kwamba tunalo neno la Mungu leo.
    •  
    • Sehemu muhimu katika Biblia

    Ifuatayo ni orodha ya sehemu muhimu za Biblia na maelezo mafupi kuhusu kilichotokea katika kila sehemu mojawapo. Kujifunza kwa moyo sehemu hizi na kujua kilichotokea katika kila sehemu mojawapo kutakupatia picha nzuri ya Biblia yote.

     

     

    • SEHEMU MUHIMU KATIKA AGANO LA KALE

     

    MAHALI

    MAELEZO

    ANDIKO

    Edeni

    Mungu alimuumba mwanadamu na kumweka katika Bustani ya Edeni. Eneo la anguko la mwanadamu

    Mwanzo. 2:8

    Mlima Ararat

    Mahali safina ya Nuhu ilipokuja kusimama baada ya ile gharika.

    Mwanzo. 8:1-5

    Babeli

    Mnara uliojengwa kuifikia mbingu na Mungu akawafanya wanadamu waongee katika lugha tofauti.  Babeli maana yake mkanganyiko

    Mwanzo. 10:10; 11:4

    Uri wa Wakaldayo

    Mahali abrahamu alipoambiwa mwanzoni aende Kanaani. Nchi ambayo baadaye ilikuja kuitwa Babeli.

    Nehemia. 9:7

    Kanani

    Nchi ya ahadi ambayo walimoishi Abrahamu, Isaka na Yakobo. Yoshua aliiteka na kugawia kila kabila sehemu.

    Mwanzo. 12:5

    Misri

    Nchi Yusufu alikouzwa kuwa mtumwa.  Israeli ikadumu utumwani miaka 400. Musa aliitoa Israeli kutoka Misri.

    Mwanzo. 12:10

    Mlima Sinai

    Mahali Musa alipoona kichaka kinachowaka moto na baadaye akapokea sheria na agano.

    Kutoka. 19:11

    Nyikani

    Watoto wa Israeli walihangaika jangwani kwa miaka 40 kwa kutoamini kwao.

    Matendo 7:42

    Syria

    Mateka wa Israeli walipelekwa Syria.

    2 Fal. 18:11

    Babeli

    Mateka wa Yuda walipelekwa Babeli. Danieli alikuwa mmoja wao

    Danieli 1:1

     

    • AGANO JIPYA – MAENEO MUHIMU

     

    MAHALI

    MAELEZO

    ANDIKO

    Betlehemu

    Mahali pa asili—Kuzaliwa Kristo katika hori.

    Luka 2:7

    Galilaya

    Palistina iligawanywa katika mikoa mitatu, Yudea, Samaria, na Galilaya, ambayo ilijumuisha eneo lote la kaskazini la nchi (Mdo. 9:31), ambao ndio mkubwa zaidi.

    Luka 4:14

    Getsemane

    Mahali pa Kristo pa sala na aliposalitiwa na Yuda.

    Mat. 26:39

    Golgota

    Mahali Kristo aliposulubiwa. “Mahali pa fuvu la kichwa.”

    Marko 15:22-28

    Yerusalemu

    Huitwa pia: Salemu, Arieli, Yebusi, "Mji wa Mungu,"  "mji mtakatifu;" wakati fulani "Mji wa Yuda" Mahali lilipozaliwa kanisa la Agano Jipya.

    Mdo 1:8 (2:25,28)

    Samaria

    Samaria mkoa ulioko katikati ya Palestina lakini hauchukuliwi kama nchi takatifu. Umbali kati ya Samaria na Israeli ambayo ni mji mikuu ya falme mbili ni maili 35 tu katika mstari ulionyooka.

    Yoh. 4:1-5

    • IX Watendaji muhimu katika Agano la Kale

     

    Mungu— Biblia inatueleza kwamba Mungu ni roho (Yohana 4:24).  Mungu ni Roho nao wamuabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli (Strong) Mungu ni zaidi ya mtendaji katika Biblia; Mungu ni chimbuko la kila kiumbe.  Biblia inamfunua Mungu kwa mwanadamu.

    Shetani—Neno shetani maana yake anayeshtaki. Yeye ndiye anayeshtaki kati ya wanaoamini. –  Ufunuo 12:10. Shetani huitwa pia muovu.  Mungu hakumuumba muovu.  Mungu alimuumba malaika Lusiferi ambaye alianguka kwa sababu ya dhambi akawa muovu. – Isaya. 14:12, Lk.10:18.

     Adamu— Mungu alimuumba Adamu, mwanadamu wa kwanza, akamuweka katika Bustani ya Edeni.  Ni yeye ndiye aliyeingiza dhambi katika jamii ya wanadamu. – Rum. 5:12

    Eva—Mungu alimuumba Eva, mwanamke wa kwanza, kutokana na ubavu mmoja wa Adamu. – Mwanzo 2:21-22

    Kaini— Mwanaye Adamu wa kwanza. Alikuwa mkulimaAlimuua nduguye Abeli na kuwa muuaji wa kwanza. – Mwa. 4;1

    Abeli—mwanaye Adamu wa pili aliyeuawa na Kaini. Alikuwa mchungaji. Mwa. 4:2

    Seti—Mwanae Adamu wa tatu. -  Mwa. 5:3

    Nuhu—Alijenga safina kulinda uhai katika dunia. Mwa. 6:13-22

    Abram—Mungu alimwita Abram aondoke nyumbani na kwenda katika nchi isiyojulikana ambako Mungu atamfanya baba wa taifa kubwa, ndio historia ya Wayahudi ikaanza. Mwa. 12:1-3 Mungu alibadili jina lake kutoka Abram Baba Mkubwa kuwa Abrahamu  Baba wa Umati. Mwa. 17:5

    Isaka—Mwanaye Abrahamu wa agano aliyempata kwa ahadi uzeeni. Mwa. 17:19

    Yakobo—Jina lake lilibadilishwa na Mungu likawa Israeli. Wanae 12 ndio waliounda makabila ya taifa la Israeli. Mwa. 32:28

    Yusufu— Mwanaye Yakobo ambaye aliuzwa utumwani Misri.  Mungu alimpandisha cheo hadi nafasi ya pili katika ufalume na akamtumia kuilinda Misri na Israeli.  Yakobo na familia yake walihamia Gosheni wilaya iliyoko Misri. Mwa. 37:36,42:1-3.

    Farao—Cheo cha mtawala wa Misri. Watoto wa Israeli walikuwa utumwani Misri kwa miaka 400. Mungu aliufanya moyo wa Farao aliyetawala wakati wa Kutoka kuwa mgumu na akawaondoa Waisraeli kutoka Misri kwa mkono wenye nguvu. Kut. 1:11-14, 6:1

    Musa— Mungu alimwinua Musa kwenda kuwatoa utumwani Misri wana wa Israeli.  Alipokea amri zake na agano katika mlima Sinai.  Aliwaongoza Waisraeli kwa miaka 40.  Kut. 3:10-12

    Aroni—Ndugu yake Musa na Kuhani Mkuu kwa utaratibu wa Makuhani. Kut. 28:1-3

    Kalebi—Mmojawapo wa wapelelezi aliowatuma Musa wakamletea taarifa nzuri. Nu. 13:30

    Yoshua—Aliteuliwa na Mungu kuwa mrithi wa Musa.  Yoshua aliwaongoza Waisraeli wakaishinda Kanani. – Nu. 27:18-23

    Waamuzi—Walikuwepo Waamuzi 15 waliotawala Israeli baada ya kifo cha Yoshua.  Hili ni jina la kitabu kimojawapo katika Agano la Kale

    Ruthu—Wamoabi ambao walirudi Betlehemu pamoja na Naomi mume wake alifia Moabu kabla Naomi hajarudi Betlehemu.  Ruthu aliolewa na Boazi akawa mmoja katika uzao wa mstari wa Kristo.  

    Samweli—Aliitwa akiwa kijana na akawa mmoja wa manabii wakuu wa Israeli. I Sam. 3:20

    Saulo—Mfalume wa kwanza wa Israeli. I Sam. 15:1

    Daudi—Kijana mchungaji aliyemuua Goliati. Mungu alimteua kuwa mfalume wa Israeli badala ya Saulo. II Sam. 5:3-12

    Solomoni—Mwanae daudi na mrithi wa ufalme wake. Mungu alimruhusu achague chochote apendacho. Yeya aliomba moyo mnyoofu na Mungu alimfanya awe na busara kuliko binadamu yeyote.  Alijenga hekalu lililojulikana kama Hekalu la Solomoni. I Fal. 3:5-12

    Eliya—Nabii shupavu wa Mungu. Aliilaani Israeli ikapigwa na ukame kwa sababu ya dhambi. Aliomba moto ushuke kutoka mbinguni katika mapambano yake na manabii wa baali katika mlima Karmeli. Alishinda kifo na alipanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli.

    II Fal. 2:11

    Elisha— Mtumishi wa Eliya.  Aliyechaguliwa na Mungu achukue nafasi yake kama nabii wa Israeli. I Fal. 19:16

    Isaya—Alimuona Bwana ameketi katika kiti cha Enzi kilicho juu sana na kuinuliwa sana na pindo za vazi lake zikalijaza Hekalu. Nabii aliyeonya Taifa la Israeli kutubu vinginevyo hukumu ya Mungu italiangukia. – Isaya. 6:1

    Yeremia—Aliitwa kuwa nabii wa Mungu akiwa tumboni kwa mama yake.  Alielezewa kama Nabii aliaye aliyeshinda dhambi za Israeli. – Yer.. 1:5

    Ezekieli—Alitabiri kutekwa kwa Yerusalemu kwa sababu ya dhambi zao. –Eze. 3:4

    Danieli—Alichukuliwa na Nebukadneza kama mmojawapo wa mateka ya Yerusalemu. Alitafsiri ndoto ya Nebukadneza na kuelezea kuzuka kwa Himaya nyingi. Alipokea maono ya siku za mwisho na alikuwa mashuhuri katika himaya za Babeli na Persia – Dan. 1:6

    Ezra—Kuhani na Mwandishi aliyerudi Yerusalemu kulijenga tena Hekalu. – Ezra 7:6

    Nehemia—Alikuwa mbeba kikombe aliyerudi Yerusalemu na kuwa kiongozi katika ujenzi mpya wa Hekalu. – Imeelezwa katika kitabu cha Nehemia.

    Esta—Malikia wa Ahesueru ambaye alikuwa mfalme katika mkoa wa Persia.  Alitimiwa na Mungu kusimamisha njama za kuwaangamiza watu wake ambao ni Wayahudi. Imeelezwa katika kitabu cha Ester

     

    • X Wahusika Wakuu katika Agano Jipya

     

    Yohana Mbatizaji—Aliyemtangulia Kristo.  Alibatiza wale waliotubu dhambi zao katika mto Yordani. Mt. 3:5-6

     Yesu Kristo—Mwana pekee wa Mungu. Mhusika Mkuu katika Agano Jipya. Agano jipya lote kwa kipekee linaweka katikati kazi za Kristo duniani, lakini Biblia kwa ujumla wake inaonyesha kwamba inamhusu kwa njia moja au nyingine.

    Wafuasi 12 – Waliitwa na kufundishwa na Yesu; Kwamba watakuwa viongozi wa kanisa katika Agano Jipya. 1) Petro, 2)Andrea ndugu yake Petro 3)Yakobo mwanaye Zebedayo 4)Yohana ndugu yake Yakobo 5)Filipo, 6)Bartolomeo 7)Tomaso 8)Matayo  aliyekuwa mtumishi 9)Yakobo mwanaye Alfayo 10)Tadei 11)Simoni wa Kanani, na 12)Yuda Iskarioti.

    Stefano—Mmoja wapo wa wale Mashemasi saba wa Kanisa waliochaguliwa kwanza katika Yerusalemu na kutofautishwa kati yao kama "mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu."  Alipigwa mawe hadi kufa chini ya utawala wa Sanhedrin ambao Saulo wa Tarso alikuwa mwanachama wake. Kifo cha Stefano ilikuwa ni mwanzo wa mateso makali kwa juhudi zilizoongozwa na Saulo, ambazo zilisababisha kuenea zaidi kwa Neno la Mungu.

    (Mdo. 8:1,4; 11:19-21)

    Philipo—Shemasi na Mwinjilisti (Mdo. 6:5; 21:8; Efe. 4:11). Alikuwa na watoto wa kike wanne waliojaliwa kipaji cha unabii (Mdo. 2:17; 21:8-9).  Baada ya kifo cha Stefano alihubiri injili toka Samaria na kwa towashi Mhabeshi kwa mafaniko makubwa na kukawepo na miujiza mingi.

    Paulo—Aliinuliwa kuwa Mtume wa Mataifa. Alikuwa chombo cha kibinadamu kilichofikisha sehemu kubwa ya Agano Jipya kwa mataifa.  Mdo. 9:15

     

    • XI Matukio Makuu ya Biblia
    •  
    • Uumbaji. Taarifa ya Uumbaji wa dunia. – Mwanzo. 1,2
    • Anguko la mwanadamu. Eva alishauriwa na nyoka kula tunda lililokatazwa. Adamu pia alikula tunda alipopewa na Eva. Biblia inatueleza kwamba Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi: Rum. 5:12 taarifa hii ya dhambi ya kwanza huelezwa kama anguko la mwanadamu.
    • Gharika kuu. Mungu alimwambia Nuhu kwamba ataharibu kila kiumbe kwa sababu ya dhambi ya mwanadamu. Mungu alimwagiza Nuhu ajenge safina ili imuokoe Yeye na familia yake. Mungu alimwagiza Nuhu kuwaleta wawili katika kila aina ya mnyama asiyekuwa msafi na wanyama saba kati ya walio safi katika safina. Mwa. 6
    • Kuitwa Abram. Bwana alimwita Abram kutoka Uri ya Kaldayo. Mungu akamwambia kwamba atamwonyesha njia ya kwenda nchi nyingine.  Abram akaipokea ahadi kwamba atakuwa taifa kubwa.  Nchi ya Kanani ndio iliyokuwa nchi ambayo Mungu alimwelekeza. Abram aliipokea ahadi kwamba familia zote zitabarikiwa katika Abram.  Hii ni ahadi kwamba Masiha.  Mwa. 12:1-3
    • Utumwani Misri. Yakobo aliwatuma wanae Misri kununua mkate kwa sababu nchi ilikuwa na njaa. Mungu akamuweka Yusufu nafasi ya pili katika uongozi wa Misri.  Yakobo na wanaye walikuja kuishi Gosheni jimbo mojawapo la misiri ili kuwaweka watoto wa Israeli hai wakati wa njaa. Baadaye aliinuka Farao, Mfalme aliyewaingiza utumwani Wayahudi.
    • Kutoka. Mungu akamwinua Musa akawatoe utumwani Israeli kutoka Misri. Mungu aliongoza Israeli kutoka Misri kwa mkono wenye nguvu. Kuondoka huku kutoka Misri huitwa Kutoka.
    • Kupokea Amri. Musa alipokea Sheria ya Mungu katika mlima Sinai. Mungu alimkabidhi zile Amri Kumi katika vigae viwili vya mawe.  
    • Kutangatanga Nyikani. Watoto wa Israeli walitangatanga katika nyika kwa miaka 40 kwa sababu ya dhambi.  Mungu hakuwaruhusu waingie katika Nchi ya Ahadi kwa sababu ya kutokuamini kwao.  Ebr. 3:19
    • Kuishinda Kanani. Mungu alimwinua Yoshua  kuwaongoza Waisraeli hadi katika nchi ya Ahadi. Taarifa ya Israeli kujipatia Nchi ya Ahadi huitwa kuishinda Kanani.
    • Ujenzi wa Hekalu. Mungu alimtumia Solomoni kumjengea nyumba ya kudumu kwa ajili ya kuabudia.  Israeli walitumia chombo kinachohamishika kinachoitwa Tabernakulo kuabudia walipokuwa njiani kuelekea Kanani.  Mungu alimwagiza Sulemani kumjengea nyumba ya kudumu ya kuabudia walipo stawi katika ile nchi.
    • Mateka Babeli. Mungu aliruhusu Israeli ishindwe na Babeli kwa sababu ya dhambi yao. Hekalu lilibomolewa na vyombo vya dhahabu vikaporwa.  Kuna vipindi vitatu ambapo Israeli waliwekwa mateka na kupelekwa Babeli.
    • Hekalu kujengwa tena. Mungu alimwinua Ezra na Nehemia kulijenga tena Hekalu.
    • Kuzaliwa Kristo. Kristo alizaliwa Betlehemu kama ilivyo katika maandiko. Kuzaliwa kwa Kristo ni jambo kuu katika historia yote.  Tarehe huandikwa KK  Kabla ya Kristo na KB   katika mwaka wa Bwana.
    • Kristo kusulubiwa. Yesu alikuja kuununua wokovu wa mwanadamu. Kristo alisulubiwa kama sadaka kuu kwa ajili ya dhambi za wanadamu.
    • Ufufuko wa Kristo. Yesu alifufuka katika wafu.  Kwa kifo Kristo alivunja nguvu za yule aliyekuwa na uwezo juu ya kifo; ambaye ni yule muovu.  Ebr. 2:14
    • Siku ya Pentekoste. Kanisa lilizaliwa katika Siku ya Pentekoste.  Hii ni ile siku ambayo Mungu alitoa zawadi ya ubatizo kwa Roho Mtakatifu.

     

    • XII Muhtasari wa Biblia
    •  
    • Muhtasari wa Agano la Kale
    •  
    • TORATI
    • Mwanzo ni kitabu cha mambo yaliyoanza.  Kitabu hiki kina taarifa ya uumbaji wa ulimwengu wote. Kinazo habari za historia ya mwanzo ya Abrahamu na Israeli.
    • Kutoka inazo habari za kipindi cha Israeli kuwa ugenini na kukombolewa kwao kutoka utumwani Misri. Zile Amri kumi na safari za Israeli kwanda kanani zinajumuishwa.
    • Mambo ya Walawi. Kitabu chenye Sheria za Mungu.
    • Hesabu. Kitabu cha miaka 40 ya Israeli kutangatanga nyikani.
    • Torati. Kitabu hiki kina marudio ya Sheria za Mungu.

     

    • HISTORIA
    • Yoshua. Taarifa ya kuinyakuwa Kaanani chini ya uongozi wa Yoshua na ugawaji wan chi kwa makabila 12.
    • Waamuzi. Historia ya utoaji wa nchi kwa uongozi wa waamuzi.
    • Ruthu. Hadithi ya mwanamke asiyekuwa Muisraeli aliyeolewa na Boazi na kuwa sehemu ya mstari wa kuzaliwa Kristo
    • I& II Samweli. Historia ya Samweli na miaka ya mwanzo ya wafalme Saulo na Daudi.
    • I&II Wafalme – Historia ya mwanzoni ya ufalme wa Israeli na ufalme uliogawanyika. Manabii Eliya na Elisha wanaonekana katika vitabu hivi.
    • I&II Mambo ya Nyakati – Taarifa ya utawala wa Daudi na Sulemani na ufalume wa Yuda mpaka wakati wa kuchukuliwa mateka.
    • Ezra. Taarifa ya kurudi kwa Wayahudi kutoka kuwa mateka na kujengwa upya Hekalu.
    • Nehemia – Inaelezea ujenzi mpya wa kuta za Yerusalemu na kurudishwa tena Sheria.
    • Esta. Hadithi ya Israeli na ya Esta kuhusu ukombozi kutoka katika njama ovu za Hamani.

     

    • USHAIRI
    • Ayubu –Masimulizi ya mateso ya Yobu na ushindi wa wake. Huenda hiki ndio kitabu cha zamani zaidi katika Biblia.
    • Zaburi. Mkusanyiko wa mashairi, sala na nyimbo za rohoni.
    • Methali. Mkusanyiko wa mambo ya maadili na, kidini pamoja na maagizo kwa hekima.
    • Mhubiri. Mawazo kuhusu umuhimu wa maisha na wajibu wa mwanadamu kwa Mungu.
    • Wimbo ulio Bora. Shairi linaloonesha upenda kati ya Kristo na Bibi harusi wake.

     

    • MANABII WAKUU
    • Isaya. Manabii Mkuu wa ukombozi.  Isaya anaionya Israeli kutotenda dhambi.
    • Yeremia. Nabii aliaye aliyeomboleza dhambi za watu wake. Aliwaonya watubu au wategemee kupata hukumu ya Mungu.
    • Maombolezo. Taarifa ya maombolezo ya Nabii Yeremia.
    • Ezekieli. Ezekieli anaonesha hali ya kurudi rudi nyuma ya watu wa Mungu.
    • Danieli. Taarifa ya baadhi ya matukio wakati wakiwa mateka.  Danieli alikuwa ni mmoja wapo wa mateka aliyepelekwa Babeli.  Ipo taarifa ya kuhamishwa mamlaka kutoka Babeli kwenda uajemi.  Kitabu hiki kina maono nyakati za mwisho.

     

    • MANABII WADOGO
    • Hosea. Nabii huyu ni wa wakati mmoja na Isaya na Mika. Uasi wa Israeli ni wazo kuu la kitabu hiki.
    • Yoeli. Nabii wa nchi ya Yuda anaye litaka taifa litubu kitabu hiki kina taarifa za mwisho za utabiri na ahadi za ujio wa Roho  Mtakatifu.  .    
    • Amosi. Nabii mchungaji.  Analaani utendaji dhambi wa watu.
    • Obadia. Anatabiri kuangamia kwa Edomu na mwisho ukombozi wa Israeli.
    • Yona. Nabii aliyesita alipoagizwa na Mungu aende Ninawi. Alimezwa na samaki na kutapikwa alipofikishwa Ninawi kama Mungu alivyotaka.
    • Mika. Kitabu hiki kinaonesha hali mbaya ya maadili ya Israeli na Yuda.  
    • Nahumu. Kinao utabiri wa kuharibiwa kwa Ninawi. Yuda kuahidiwa ukombozi kutoka Siria.
    • Habakuki. Kiliandikwa kipindi cha Kaldayo.  Kitabu hiki kinazungumzia uwezekano wa Mungu kuruhusu hukumu kuifikia Israeli.
    • Sefania. Kinazo taarifa za utukufu ujao wa Israeli.
    • Hagai. Nabii wa wakati mmoja na Zekaria.  Anawakemea watu kwa uvivu wao katika kujenga hekalu la pili. Ipo ahadi ya ukuu wa kurudi tena kwa utukufu wa Mungu katika hekalu.
    • Zekaria. Alisaidia kuhamasisha Wayahudi kulijenga upya Hekalu.  
    • Malaki. Anaonesha kipindi cha mwisho cha historia ya Agano la Kale. Anazungumzia haja ya kufanya mabadiliko kabla ya ujio wa Masiha.   

     

    • Muhtasari wa Agano Jipya

     

    •  
    • Injili
    • Neno Injili maana yake: habari njema.  Injili zinasimulia Habari Njema za Yesu Kristo.  Siyo historia za watu na hazielezi kila tukio katika maisha ya Kristo.  
    • Mathayo. Mathayo anaandika kama "Muisraeli hasa," Myahudi aliyegeuzwa akiagiza jamii yake.  Ananukuu mara nyingi kutoka Agano la Kale na kusisitiza Umasiha wa Kristo.
    • Marko. Marko kimsingi aliwaandikia Warumi (ndio kusema anaelezea mara kwa mara mila za Kiyahudi). Marko anakariri ukweli kwa matendo na mwelekeo na anasisitiza tabia ya Utumishi wa Kristo.
    • Luka. Luka anawakilisha Kristo kama rafiki mnyenyekevu wa watenda dhambi, Mkombozi wa ulimwengu.  Hii ni injili ya wema wa Mungu kwa ulimwengu. Imelelekezwa kwa mataifa na imesisitiza Utu wa kristo kwa kurudia kumuita “Mwana wa adamu.”
    • Yohana. Yohana anamtambulisha Kristo kama mwana wa Mungu katika mwili. Ni injili ya kiroho zaidi kuliko ya kihistoria, ambayo imeondoa mambo kadhaa ya wainjilisti wengine na inayo mambo mengi zaidi kuliko wanayofanya kwa mawazo ya kiroho.  Yohana anasisitiza Uungu wa Kristo na inayo aya muhimu ya Biblia: Yohana 3:16.

     

    • Historia
    • Matendo ni taarifa ya kuzaliwa kwa kanisa siku ya Pentekoste. Hii ni historia ya maendeleo ya kanisa la mwanzo.

     

     

     

    • Nyaraka za Mtume Paulo

    Waraka ni barua. Hizi ni barua zenye pumzi ya Roho Mtakatifu kwa ajili ya Kanisa.

    • Warumi. Dhamira kuu ni kuhesabiwa haki kwa imani. Paulo anawaandikia Wakristo wajibu wao katika nusu ya pili ya kitabu hiki.
    • I&II Wakorinto. Walioandikiwa ni waumini wa Kanisa la Korinto. Kitabu hiki kinasafisha makosa katika kanisa. Paulo anatoa maagizo kwa Kanisa.  Neno hili bado linafaa katika kanisa hadi leo.
    • Wagalatia. Walioandikiwa ni waumini wa kanisa la Galatia.  Paulo anafafanua kuhesabiwa haki kwa imani na analionya kanisa kuhusu kurudia ibada za Yuda.
    • Waefeso. Walioandikiwa ni waumini wa kanisa la Efeso. dhamira kuu ni umoja wa watakatifu.  Paulo anahamasisha umoja kati ya Wayahudi waliogeuka na Mataifa watakatifu.
    • Wafilipi. Walioandikiwa ni waumini wa kanisa la Wafilipi. Yesu Kristo ndiye ujumbe mahususi.
    • Wakolosai. Walioandikiwa ni waumini wa kanisa la Kolosai. Kristo amesisitizwa kwamba Yeye ni kichwa cha kanisa.  Paulo anahamasisha kanisa na kuwaonya dhidi ya mafundisho ya uongo.
    • I&II Wathesalonike. Walioandikiwa ni waumini wa kanisa la Thesalonike. Paulo analitia moyo kanisa. Barua hizi zinahusu ujio wa pili wa Kristo.
    • I&II Timotheo. Paulo anamshauri kijana Timotheo kuhusu utumishi. Paulo anamhimiza Timotheo kulihubiri Neno.  Ushauri huu na hamasa unamhusu kila mhudumu.

     

    • Tito. Paulo anaangalia kazi za kichungaji.  Kazi nzuri zinahimizwa katika waraka huu.
    • Filemoni. Hii ni barua aliyoandika Paulo kwa Filemoni kuhusu mtumwa Onesmo aliyekimbia.  Paulo anamuomba Filemoni amsamehe Onesmo ambaye alishageuka na kumrudisha kazini.  Paulo anaongoza kwa mfano kwa kumsamehe Onesmo na kujali mahitaji yake binafsi.
    • Waebrania. Barua hii imeelekezwa kwa Waebrania waliogeuka. Mwandishi hakutajwa katika kitabu hiki.  Inawezekana ni waraka mwingine wa Paulo. Waraka huu unamuonesha Kristo kuwa ni masia mwenye utimilifu kama Nabii, Mchungaji na Mfalme.

     

    • Nyaraka kuu
    • Yakobo. Waraka huu huenda uliandikwa na Yakobo aliyekuwa ndugu yake Bwana. Waraka huu unaonesha kwamba imani bila matendo imekufa. Jambo hili linahusu matendo ya kidini na tabia ya Mkristo wa kweli.
    • I&II Petro Waraka huu uliandikwa na Mtume Petro kuhamasisha na kuliimarisha kanisa. Ahadi ya urithi uliohifadhiwa umeoneshwa katika waraka huu. Petro anawatia moyo waumini kupokea ahadi ya Mungu yenye thamani kubwa. Waraka huu unasisitiza msukumo wa maandiko Matakatifu. Waraka huu unaloonyo dhidi ya manabii wa uongo.
    • I,II &III Yohana. Uliandikwa na Mtume Yohana.  Mungu ni uzima, nuru na upendo wa haki. Ni onyo dhidi ya makosa na walimu waongo. Kuaswa kutembea ndani ya ukweli.
    • Yuda. Wito wa kuzingatia imani ambayo iliosilishwa kwa Watakatifu. Angalizo la kujichunga dhidi ya walimu waongo.

     

    • Utabiri
    • Ufunuo. Ulipokelewa na Yohana katika kisiwa cha Patmo mwaka 100 wakati wa Kristo. Unao utabiri na maono kuhusu siku za mwisho na mwisho wa nyakati.