Skip to main content

HISTORIA YA KANISA LA TANZANIA KUANZIA KIPINDI CHA UKOLONI MPAKA UHURU

HISTORIA YA KANISA LA TANZANIA KUANZIA KIPINDI CHA UKOLONI MPAKA UHURU

UTANGULIZI

David Livingstone-Msafiri wa Mungu.

Katikati ya karne ya 19 wavumbuzi wengi waliofika kutoka sehemu mbalimbali huko Ulaya katika bara la Afrika. Rebman alikuwa Mzungu wa kwanza kuuona Mlima Kilimanjaro, na Krapf aliuona Mlima Kenya. Mwaka 1856 wavumbuzi wawili toka Uingereza R. Burton na J.H. Sperk, waliendelea katika Ziwa Nyasa na Ziwa Tanganyika. Mvumbuzi mwingine alitoka Uingereza alifanya safari nyingi katika sehemu ya Bukoba, Uganda na Zaire miaka ya 1874-1877.

Lakini kuliko wote ni David Livingstone. Yeye alizaliwanchini Skotland mwaka 1813. Tangu mwaka 1840 alianza kufanya kazi katika chama cha "London Missionary Society" (LMS). Pia yeye ndiye aliyepinga biashara ya utumwa Afrika Mashariki.

KANISA CHINI YA WAJERUMANI

Wajerumani walianzisha shirika huko kwao liitwalo 'Die Gesellschaft fur Deutsche Kolonisation' (The society for German Colonisation). Mwanzilishi wa kanisa hilo alikuwa Karl Peters 1856-1918.

VYAMA VYA KILUTHERI

Greiner alifika Dar-es-salaam mwezi wa julai 1887 baada ya kufanya kazi Uhabeshi. Wakati ule Dar-es-salaam kulikuwa na wakazi 2000 tu, baadhi yao walikuwa watumwa 500 wahindi 200, na waarabu 150. Greiner alijenga nje kidogo ya mji kambi iitwayo "Immanuelskap" (maana yake Mungu yupo pamoja nasi). Pia alifungua kazi nyingine Mbuyukenda huko Tanga 1831-1910.

WAMORAVIAN

Februari 7, 1897 ilikuwa siku ya moto huko Rungwe, Mmishenari wa Kimorovian Traugott Buchmann alihubiri kutoka Mat. 13:24-34 juu ya magugu kati ya ngano. Baada ya mahubiri mwanamke mmoja Fyabalema, alisimama na kusogea kwenye mimbara, akanyamaza kwa daakika moja halafu akasema "Nataka kumfuata Yesu na kuwa wake peke yake". Usiku wake akabatizwa na kuitwa "Numwagile" Maana yake kwa Kinyakyusa "NIMEMPATA". Baada ya wiki moja mtoto wake Mwasanyila alibatizwa pia na kuitwa "Niganile" maana yake "NIKO RADHI".

Baada ya miaka michache kazi ilienea maeneo mbalimbali kama vile Mbeya, Tabora, Kilimanjaro, Arusha na n.k

WAKATOLIKI

Wakatoliki kama Holy Ghost Father (HGF) (Mapadre wa Roho Mtakatifu) walifaulu kubaki nchini baada ya vita 1870-1871 kwasababu sehemu ya kaskazini mashariki ya Ufaransa ilikuwa chini ya Koloni ya Wajerumani. Kwahiyo Mapadre hawa wa Kifaransa waliruhusiwa na Wajerumani kubaki hapa nchini Tanzania na kuendelea na shughuli zao za kidini.

Ingawa serikali ya Kijerumani ilikuwa na mashaka kuhusu hawa Wakatoliki ambao waliongea Kiaransa maana wanaweza kuwa wapinzani kwa siri.

Chama cha HGF Kilianzisha vituo vipya katoka sehemu yao ya Mapadreorogoro kama Matombo, mgeta, Hhantee, Mulu, Msakti, Kurio, Kidunda, Lugoba, Ilonga, Kondoa Irangi, Galapo na Bahi.

MISIONI ZA KWANZA KUTOKA MAREKANI

Karne ya 20 kweli ilikuwa karne ya Marekani katika historia ya Misioni. Vyama ving ikutoka Marekani vilieneza injili ulimwenguni hata pia Tanganyika.

SEVENTH DAY ADVENTIST (WASABATO)

Wasabato (au rasmi "Seventh Day Adventist").

Dhehebu hili lilikuwa kibatisti na lilikaza mwanzoni hasa kurudi kwake Yesu. Wasabato walipata hili jina kwasababu waliabudu jumamosi (Sabato ya Kiyahudi) na sio jumapili.

Wamisionari wa kwanza walikuwa wa Kijerumani, W. Ehlers na A. C. Enn, ambao walifika Suji karibu na Korogwe mwaka 1903, ambapo walipata mahali pa kuanzisha kazi huko Kihurio na Vunta. Mwaka 1908 ndio ulikuwa ubatizo wa kwanza kwao. Mwaka huo huo Wasabato walipata ruhusa kuanza kanza kazi sehemu ya Ziwa Victoria na kufungua vituo pale eneo la Mara-Mjita, Ikizu, Sikazi na Nyatrangi. Mwaka 1912 walianza kazi Bupandogila na baadaye kidogo Bariadi na Itusili (sehemu ya Shinyanga).

KANISA LA PENTEKOSTE TANZANIA 1961-1985

Baada ya vita ya pili ya dunia Wapentekoste walipata mafanikio makubwa sana. Mwaka 1923-2013 Mhubiri T.L. Osborn toka Marekani aliingiza kwa nguvu Upentekoste Afrika Mashariki. Alianzisha (PEFA) Pentecostal Evangelistic Felloship of Afrika. Hapa Tanzania PEFA ilianzia katika mkoa wa Mara.

  • Pentecostal Assemblies of God (PAG)-1963 chini ya Wakanada
  • Walipanua kazi yao mpaka Bukoba na baadaye Tanga (1970) Arusha (1973), Morogoro na Dar-es-salaam 1983.
  • Tanzania Assemblies of God (TAG)-Katika miaka ya 1980 Kanisa lilienea sehemu zote za Tanzania- Iringa, Dodoma, Dar-es-salaam, Moshi, Arusha na Mwanza. Walijikita zaidi maeneo ya Mbeya na Njombe na kuanzisha shule ya Biblia huko Tukuyu 1967.
  • Emmanuel Lazaro ndiye Mtanzania wa kwanza kuwa Askofu mkuu wa kanisa hili hadi 1992.
  • TAG- Iligawanyika mwaka 1982 na Mhubiri maarufu Mosses Kulola aliunda EAGT.
  • Baada ya 1961 kazi ya "Swidish Free Mission" [SFM] Pia ilipanuka karibu nchi nzima. Singida 1963, Marangu 1963, Bukoba 1963, Korogwe 1963, Same 1964, Iguguno 1964, Masasi 1965, Lushoto 1968, Kilosa 1968, Nzega 1969, Lindi 1970, Arusha 1979.
  • Mwaka 1977 (SFM) Walianzisha kituo cha Radio na vitabu huko Marangu. Mwaka 1984 walihamisha kituo hichi cha "Radio Habari Maalum" Ngaramtoni ya juu pale Arusha.
  • Pia kati ya 1961-1985, yalikuwepo madhehebu manne Nchini Tanzania.
  1. Kanisa la Katoliki
  2. Kanisa la Kilutheri
  3. Kanisa la Kianglikana
  4. Kanisa la Pentekoste

KANISA LA PENTEKOSTE KWA WAKATI WETU 1986-2015

Kanisa lilikuwa na maendeleo makubwa na kufanikiwa kufungua kazi nchini kote, Uamsho huu ulisaidia kuongezeka kwa idadi kubwa ya Wapentekoste Nchini. Pamoja kuwa na mafanikio ya kanisa kuongezeka, pia kanisa lilikuwa na changamoto ambazo zilizikumba kanisa. Zifuatazo ni baadhi ya changamoto ambazo kanisa lilipitia.

CHANGAMOTO YA KWANZA

Migawanyiko. Kwasababu Wachungaji na Wainjilisti waliongezeka sana, na walikuwa na hamu ya kuanza huduma binafsi katika makanisa, na kutopata nafasi ya kuhudumia, hivyo walijikuta wakianzisha makanisa yao binafsi. Wakati huo huo unaweza kukuta kanisa la familia moja na majirani wachache tu. Hii inaleta picha ya aibu kwa Ukristo.

Watumishi wengi walianzisha huduma hiyo sio kutokana na moyo wa utumishi, lakini ni ile hamu ya Mchungaji na Mwinjilisti kupata mapato.

CHANGAMOTO YA PILI

Ukristo wa Jina. Wakristo wengi hawaendi kanisani kwa kuwa wamebadilika mioyo yao, ila ni kwa mazoea na kwa desturi ya wazazi na marafiki tu.

CHANGAMOTO YA TATU

Mitandao. Makanisa yaliongezeka na kukua, hivyo kila mtu alitaka kuwa kiongozi wa juu kwa kujivunia kuwa na idadi ya watu, pale ndivyo mawasiliano yaliktaika na kubakia na makanisa ya kanda flani na kabila flani.

Hii historia ya kanisa imepatikana kwa kusoma vitabu baadhi ya historia mbalimbali ya makanisa tofauti. Japo imeandikwa kwa ufupi sana.