Kanisa la Mateso
Mbili: Kanisa la Mateso (100—313 BK)
Kuanzia kukamilishwa Agano Jipya hadi kutolewa Hati ya Konstantino.
Hii inazindua kipindi ambacho kanisa liligandamizwa chini ya utawala wa kipagani wa Roma. Kinyume na mategemeo hayakutokeza marashi matamu kwa Mungu kwa kuwa katika karne hizo mbili kulikuwa na mashahidi kuuliwa mfululizo. Kutolewa kwa Hati ya Kostantino kutajadiliwa zaidi katika kipindi cha Kanisa la Kifalme.
Tuna kumbukumbu za matukio ya kipindi cha kanisa la kwanza kutoka kwa Biblia, ambayo tunaamini yametutia moyo. Hatuna kumbukumbu za kibiblia za wakati wowote wa kanisa. Hii ina maana kwamba si kila tunachokisoma ni kweli. Watu wawili wanaweza kushuhudia tukio moja na bado wakatoa taarifa tofauti kabisa kuhusu jambo hilo. Historia ni ngumu kwa sababu vyanzo vinaweza kuwa kweli au visiwe kweli. Kuna msemo unasema, "historia imeandikwa na washindi." Hii ni kwa sababu wale walioshindwa vita walishakufa, na hawakuweza kuandika ukweli wao wenyewe wa kile kilichotokea.
Mateso
Huu ulikuwa ni wakati wa mateso makali kwa kanisa. Watu ambao hawakuawa walilazimika kwenda mafichoni na huko walivumilia umaskini na maisha ya taabu.
Yesu aliwaeleza mapema kuhusu kipindi hicho cha mateso. Yesu aliwatia moyo wafuasi wake ili wasikiogope. Huo ulikuwa ni utabiri wa mateso ambayo kanisa lingeyapata kwa kipindi fulani.
Wengi walifungwa kwa sababu za kuhubiri injili katika kipindi hiki. Kuwa Mkristo ilifanywa kuwa ni kosa chini ya sheria ya Kirumi.
Katika mwaka wa 303 BK Mfalme Diocletiani alianzisha kipindi cha mateso makali sana kwa wakristo yaliyojulikana kama "Mateso Makuu." Hili lilikuwa ni jaribio la kuuondoa Ukristo katika uso wa dunia hii. Inasemekana Diocletiani alijenga mnara ulioandikwa: Kwa kumbukumbu ya kufukuzwa ushirikiano unaoitwa Ukristo. Wakristo wengi walichomwa moto wakiwa hai kwa sababu ya ushuhuda wao. Wakristo walitupiwa wanyama wakali ambao waliwararua na kuwala katika viwanja vya michezo.
Sababu zilizofanya kuwepo na mateso chini ya utawala wa kifalme
Ibada za kipagani zilikuwepo kutokana na uwepo miungu wapya wakati ambapo Ukristo ulitambua kuabudiwa kwa Mungu mmoja tu wa kweli tu
Miungu wapya walikubalika chini ya utawala uliotukuza utamaduni wa kuabudu miungu wengi wa Roma. Wakristo walishindwa kuvumilia kuabudiwa kwa miungu wa uongo na walizikataa njia za kipagani.
Ibada za kuabudu sanamu ziliingizwa katika maisha ya jamii
Sanamu zilijengwa katika nyumba nyingi na kutukuzwa. Mapicha yaliabudiwa kama miungu katika sherehe rasmi na shughuli nyingine za jamii. Wakristo ambao hawakukubali kushirikishwa katika ibada hizo za kipagani hawakuishi kwa amani na jamii hiyo ya watu wasioamini Mungu. Kwa sababu Wakristo hawakushiriki katika sherehe ya ibada ya kipagani, watu wengi hawakufikiri kwamba waliabudu wakati wote na kwamba hawakuamini Mungu.
Kuabudu Mfalme
Wakristo hawakubali wazo la kuabudu mfalme. Wakristo walimzungumzia Mfalme mwingine. Wakristo walitazamwa kama waliokosa utii kwa mfalme na wanapanga mapinduzi ya kumwondoa mfalme.
Katika karne ya kwanza dini ya Yuda ilikuwa dhehebu rasmi iliyokuwa imeruhusiwa kuwepo katika himaya ya Kirumi
Ukristo ulihesabiwa kama sehemu ya dini hiyo ya Yuda ambayo ilikuwa imeruhusiwa. Baada ya Yerusalemu kuharibiwa mwaka wa 70 BK, Ukristo ulisimama peke yake bila kulindwa na sheria.
Mikutano ya siri
Wakristo walianza kufanya mikutano yao kwa siri ili kujilinda wasikamatwe. Mikutano hiyo ya siri iliwatia wasiwasi sana watawala. Wakristo walishutumiwa kwamba mikutano yao ya siri ilikuwa ni ya kupanga kuuangusha Ufalme wa Kirumi uliokuwa madarakani. Kwa sababu ya Mlo wa Bwana na kuzungumza juu ya kula mwili wa Kristo, watu wengine walidhani kuwa walikuwa wachanga.
Usawa katika kanisa
Wakristo waliwaona watu wote kuwa sawa, kwa hiyo waliharibu utaratibu wa jamii wa kutukuza sanamu za miungu. Jambo hili lilikuwa ni kinyume na mila za jamii ya Kirumi.
Faida za kibiashara
Kustawi kwa Ukristo kulisababisha biashara iliyokuwa na faida kubwa ya kutengeneza na kuuza sanamu na picha za ibada za kipagani kufa.Watengenezaji wakubwa wa vitu hivyo waliunga mkono kuteswa kwa wakristo (Mdo. 19:23—28).
Mashahidi muhimu na viongozi wa makanisa ya liyoteseka
Inyasi
Inyasi alikuwa asikofu wa Antiokia huko Syria. Huyu alikuwa ni mwanafunzi wa mtume Yohana.
Inyasi alitupiwa wanyama wakali wamrarue katika kiwanja cha Coliseum. Akisimama katika uwanja huo wakati wanyama wakali wanamsogelea, Inyasi alisali ifuatavyo, "Nakushukuru ee Bwana kwa kuwa wewe umenitoa mimi ilinitukuke. Mimi ni punje ya Mungu ambaye nitasagiwa katikati ya meno ya wanyama wakali ili niwe mkate mtakatifu wa Bwana."
Shahidi Yustini
Shahidi Yustini alikuwa mwana falsafa aliyekuwa Mkristo baada ya kukutana na mtu mzee ambaye alielezea jinsi Yesu alivyotimiza unabii wa Agano la Kale. Alikuwa mmoja wa watetezi wa kwanza, ambaye ni mtu aliyetumia sababu na mantiki ili kulinda imani yake. Aliandika vitabu vingi ambavyo vipo hadi leo na vinatupatia taarifa nyingi za kipindi hicho. Mojawapo ya kazi zake muhimu ni Mazungumzo na Trypho maandishi ambayo hufundisha dhidi ya Waebionaiti (Ufunuo 2:9).
Aliandika mara moja, "Unaweza kutuua, lakini huwezi kutudhuru." Yustini shahidi alikatwa kichwa huko Roma mwaka 165 BK. Maneno yake ya mwisho yalikuwa, "Mimi ni Mkristo, nimewekwa huru na Kristo na kwa wema wake Kristo nina pokea pigo hili kwa tumaini moja."
Polikarpi
Polikarpi alikuwa asikofu wa Smirna katika Asia ndogo. Alifundishwa akiwa kijana na Mtume Yohana. Alikuwa mhudumu shupavu katika kizazi chake. Wakati polisi walipokuja kumkamata, aliwapokea kama wageni. Aliwapa chakula na kuomba muda wa lisaa wa kuomba, lakini alitumia masaa mawili.
Walimleta Polycarp kwa mtawala, ambaye alitishia kumchoma akiwa hai kwa moto kama hatamkana Kristo. Polikarpi akajibu, "Miaka themanini na sita nimemtumikia Kristo na hajanitendea kosa lolote; ni kwa nini basi nimkufuru mfalme wangu na ambaye ameniokoa? Unanitishia kwa moto unaowaka kwa saa moja na kuacha; lakini hujui moto wa hukumu ujao, na pia hufahamu moto wa adhabu ya milele. Leta chochote kama utakavyo."
Mtawala huyo alimsihi akisema, "Akae mbali na wasioamini Mungu!" (akimaanisha Wakristo), ili waweze kumruhusu awe huru. Polycarp aliugeukia umati uliokuwa unatazama huku akisema, "Akae mbali na wasioamini Mungu!" Kwa sababu hakuweza kupingana na imani yake ya Kikristo, aliteketezwa akiwa hai huko Smyrna mwaka wa 155 BK. Polycarpi alikuwa kiungo cha mwisho kwa Kanisa la Mitume.
Ireneusi
Ireneusi alikuwa mwanafunzi wa Polikarpi. Baadaye alikuwa askofu wa Lionsi (huko Gaul) mwaka 177 BK. Alisisitiza kanuni za msingi za Ukristo ambazo zilipingwa na Waagnosti. Wagnostiki waliamini "maarifa ya siri" ambayo waamini wachache tu wangepokea, lakini Ireneusi aliwakumbusha kwamba Mitume walifundishwa waziwazi na si kwa siri. Baadhi ya maandiko yake bado yanakuja leo.
Origen (185—254 BK)
Origen alikuwa mwanadolijia, ambayo ina maana kwamba alisoma kutoka kwenye vyanzo vya kidunia, kama vile falsafa ya Kigiriki, na kutumia mawazo yao kwa kufikiria kidini.
Aliamini kwamba kulikuwa na viwango vitatu vya maana ya Kibiblia: halisi, maadili, na ishara.
Tertullian (150—229 BK)
Tertullian alisema "Je, Athene inafanya nini na Yerusalemu?" Alikuwa akisema kuwa mawazo ya falsafa (Athene) hawakuweza kuongeza chochote kwenye mafundisho ya Ukristo (Yerusalemu). Hii ilikuwa shambulio dhidi ya mwanadolijia.
Aliamini kwamba mateso yalitoka kwa Mungu. Alidhani ilikuwa chombo kilichotenganisha waumini wa kweli kutoka kwa waongo.
Simeoni
Simeoni alikuwa kiongozi wa kanisa la Yerusalemu baada ya Yakobo. Alisulubiwa msalabani kwa amri ya Gavana wa Kirumi wa Palestina mwaka 107 BK wakati wa utawala wa Trajani.
Blandina
Blandina alikuwa msichana Mkristo aliyekuwa mtumwa ambaye aliteswa tangu asubuhi hadi usiku kisha akatamka, "mimi ni Mkristo na kat iyetu hakuna uovu unaotendwa."
Perpetua na Felista
Alikuwa ni mwanamke mwadilifu wa Kartago, Perpetua na mtumwa wake Felisita waliuawa na wanyama wakali mwaka 203 BK.
Uundaji wa kanuni za Agano Jipya
Neno kanuni lina maana "ya fimbo, sheria, au kifaa cha kupimia."
Inahusu vitabu vya Biblia ambavyo vinatambuliwa kama vifaa vya utukufu wa Mungu kwa asili yake (vilivyopumuliw ana Mungu) na vikajumlishwa katika Biblia kama sehemu yake.
Hakuna tarehe maalumu ambazo zinatambuliwa kama rasmi ambazo rasimu ya Agano Jipya ilipatikana lakini haiwezi ikawekwa mapema zaidi ya mwaka wa 300 BK.
Mafundisho ya uwongo yalizuka kipindi hiki
Wagnosti
Wagnosti walifundisha kwamba watu wanaweza kuokolewa kwa ujuzi wa siri. Wanapata jina lao kutoka Gnosis, ambayo ni neno la Kigriki limaanishalo "ujuzi." Waliamini kwamba wokovu haukuwa uhuru kutoka dhambini, lakini ilikuwa uhuru kutoka kwa ujinga.
Waliamini kwamba Yehova alikuwa mungu mwovu aliyeumba ulimwengu huu kama gereza kwa roho za wanadamu. Kwao, ulimwengu wa asili ulikuwa uovu, na hivyo roho za wanadamu zinapaswa kuepuka hilo kwa ujuzi huu wa siri. Ujuzi huu hauwezi kuja kutoka ulimwenguni, lakini njia yao ya kupokea ni kwa njia ya kukataa mwenyewe. Hawatashiriki ujuzi huu na watu nje ya kikundi chao.
Waebionaiti
Waebionaiti waliendeleza mila na sheria za Musa na walijaribu kushawishi wengine wafanye vile vile pia. Walikuwa Wayahudi ambao walidhani kwamba Mataifa wanapaswa kubadilika kwa Uyahudi. Wakamkataa Paulo kama mtume. Hawakuamini kwamba Yesu ni uungu. Maandiko pekee ambayo walitumia kutoka Agano Jipya ni sura ya 3-28 ya Injili ya Mathayo. Hawakutumia sura mbili za kwanza za Injili, kwa sababu zinaonyesha Yesu kama Mwana wa Mungu.
Wamarcioni
Walikuwa wafuasi wa Marcioni. Kikundi hiki kilikuwa kinyume cha Waebionaiti. Wao walitaka Wakristo kujitenga kabisa na chochote kinachohusiana na Wayahudi. Marcioni aliunda kanuni ya Biblia ambayo ilikuwa na injili tu ya Luka (ambaye alikuwa mtu wa Mataifa) na nyaraka kumi za Paulo (zilizobadilishwa ili kuondoa kumbukumbu za Uyahudi). Hakupenda Mungu wa Agano la Kale.
Wamontani
Walikuwa wafuasi wa Montanusi (150-170 BK). Hii ilikuwa kundi la kinabii ambalo liliamini kwamba Roho Mtakatifu alizungumza mambo mapya kwa kanisa. Waliamini kwamba wanachama wa Utatu walifanya kazi kwa nyakati tofauti:
- Baba alifanya kazi katika nyakati za Agano la Kale
- Mwana alifanya kazi katika nyakati za Agano Jipya
- Roho Mtakatifu anafanya kazi leo
Wasabelliani (pia inajulikana kama Wamodali)
Kundi hili liliamini kwamba kulikuwa na Mungu mmoja ambaye alikuwa na nafasi tatu (au muundo): Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.
No Comments