Skip to main content

Kanisa la Mitume

Moja: Kanisa la Mitume (30–100 BK)

Kutoka siku ya Penstekoste hadi kukamilishwa Agano Jipya

Maelezo ya kanisa la kwanza

Nguvu za kanisa

Walipokea nguvu siku Roho Mtakatifu alipowashukia (Mdo. 1:8)

Makazi asilia ya Kanisa

Kanisa lilianzia katika mji wa Yerusalemu lakini mateso yalilitawanyia nchi nyingine (Matendo 8:1).

Uanachama katika Kanisa

Wanachama wa mwanzo katika Kanisa walikuwa wote ni Wayahudi. Walikuwa hawajafahamu kwamba injili ni kwa ajiliya mataifa pia.

Serikali ya Kanisa

Wale Mitume kumi nawawili waliongoza kanisa.

Kanuni za Kanisa

Yesu alikuwa ndiye Masia (Mdo. 2:36)

Ufufuko wa Kristo (Mdo. 2:30–32)

Kuja tena kwake Kristo (1 The. 4:15–17)

Wakuu wa Kanisa

Mtume Petro

Katika kanisa la Yerusalemu Mtume alikuwa ndiye msemaji wa mitume wote na msaidizi wake alikuwa ni Yakobo. Historia inasema kwamba Petro alikufa shahidi huko Roma mwaka wa 67 BK.

Stefano

Alikuwa nimmoja kati ya watu saba walioteuliwa kwa ajili ya kutunza mahitaji ya kanisa (Mdo. 6:8) Anasimuliwa kama mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu. Alitumiwa na Mungu kufanya mambo makubwa ya ajabu na miujiza katikati ya watu. Stefano alikufa shahidi wa kwanza (Mdo. 7:55–60).

Philipo

Alianzisha kanisa katika Samaria. Kanisa hili lilitambuliwa na Mitume. Hili lilikuwa kanisa la kwanza nje ya dhehebu la Yuda. Alianzisha pia makanisa huko Gaza, Joppa na Kaesaria (Mdo. 8:40).

Mtume Paulo

Mateso ya Sauli

Sauli aliongoza askari waliowatesa sana Wakristo (Mdo. 8:3). Sauli ndiyea liyeidhinisha Stefano auawe. Mateso hayo yalisaidia kulieneza kwa upana zaidi kanisa (Mdo. 8:4).

Kubadilika kwa Sauli

Yesu alikutana na Sauli katika barabara iendayo Dameski. Akiwa njiani alianguka na akageuka mara akawa mhubiri shupavu kwa Wayahudi na Mataifa mengine (Mdo. 9:19–22). Jina la Sauli lilibadilishwa likawa Paulo. Huyu Paulo akawa mtume mmoja mkakamavu sana kwa mataifa.

Safari za umishonari za Paulo

Paulo alifanya safari nyingi za kueneza injili na alianzisha makanisa huko Filipi, Tesaloniki, Berea, Athene, na Korinto. Aliyaunda yale makanisa saba ya Asia moja kwa moja au kwa njia iliokuwa rasmi (Mdo. 19:10). Makanisa hayo yalianzishwa katika mateso makubwa (2 Kor. 11:23–28).

Alifundisha katika masinagogi na alipokea toka kwa Roho Mtakatifu ujumbe mwingi wa Agano Jipya. Alipokuwa kifungoni Roma aliandika waraka kwa Waefeso, Wafilipi, Wakolosai na kwa Filemoni. Historia inaonesha kwamba Paulo alikufa shahidi mwaka 67 BK.

Yakobo

Yakobo alikuwa mdogo wake Yesu. Huyu anatakiwa asichanganywe na mtume Yakobo ambaye aliuawa na Herode katika Matendo 12. "Na akamuua Yakobo nduguye Yohana kwa upanga" (Mdo. 12:2). Yakobo alikuwa mzee kiongozi au mchungaji wa kanisa la Yerusalemu. Yeye alitambua mataifa mengine kama sehemu ya mwili wa Kristo. Historia inaonesha kwamba Yakobo alikufa shahidi mwaka 62 BK.

Mtume Yohana

Huyu mtume Yohana alikuwa ndiye kijana mdogo kuliko mitume wengine wote. Alinyanyuka baada ya mitume wengine kufa. Alimfundisha injili Inyasi na Polikarpi ambao baadaye waliliongoza kanisa.

Kanisa katika Mataifa

Petro na Kornelio (Mdo. 10)

Petro alihubiri injili katika nyumba ya Kornelio na hapo ndipo Mataifa mengine yalipompokea Roho Mtakatifu (Mdo. 10:44–48).

Taarifa ya Petro kwa wazee (Mdo. 11:1–18)

Baraza la Yerusalemu katika mwaka wa 48 BK (Mdo. 15:5–20)

Mitume waliitisha baraza la wakuu wa watu wakae pamoja kuamua iwapo mataifa mengine walipaswa kufuata sheria ya itifaki ya Musa. Baadhi yao walikuwa wakisisitiza kwamba ni lazima watu wa mataifa watahiriwe (mst. 5). Baraza iliamua kwamba Mataifa hawana haja ya kufuata sheria ya ibada ya Kiyahudi.

Paulo anamkemea Petro (Wagal. 2:11–14)

Anguko la Yerusalemu mwaka wa 70 BK

Wayahudi waliasi dhidi ya utawala wa Warumi mwaka wa 66 BK

Jemadari wa Yerusalemu aliyejulikana kama Tito aliubomoa kabisa mji wa Yerusalem

Mji huo uliwaka moto mkubwa uliosababisha dhahabu iyeyukie katikati ya matofali yaliyoujenga. Askari walilivunja hekalu vipandevipande, tofali kwa tofali kwa lengo la kuondoa ile dhahabu iliyokuwa imeyeyukia katikati. Hili lilitimiza utabiri wa Yesu kuhusu hekalu hilo.

Marko 13:2—Yesu akajibu, akamwambia, Wayaona majengo haya makubwa? Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomolewa.

Sadaka za kuteketeza wanyama zilikoma hekalu lilipobomolewa

Wakati huo Mungu alihitimisha mambo yake na dhehebu la Yuda