Skip to main content

Kwanini tujifunze Historia ya kanisa?

Kwanini tujifunze Historia ya kanisa?

Historia ya Kanisa inatusaidia kuelewa kile tunachoamini

Ukiingia kanisa la Kiprotestanti popote ulimwenguni, utasalimiwa na huduma inayofanana na nyingine yeyote uliyowahi kuhudhuria. Kutakuwa na tofauti za mtindo, lakini utatarajia sala ya ufunguzi, wakati wa kuimba, sadaka, na kuhubiri Mara nyingi hizi zitakuwa katika utaratibu sawa. Hakuna mahali popote katika Biblia hutolewa orodha ya jinsi ya kuongoza huduma ya kanisa, sasa imekuwaje wote tumekuwa na mfumo sawa?

Ni kwa sababu mengi ya yale tunayofanya na kuamini kama Wakristo yameumbwa na zaidi ya miaka elfu mbili ya mila, ingawa mara nyingi hatujagundua. Mila mara nyingi huonekana kuwa jambo baya katika makanisa ya Kiprotestanti. Tunapenda kuamini tunafanya mambo sawasawa na Paulo na mitume wengine walifanya katika Agano Jipya, lakini hakuna mahali pa Biblia tunaona kwamba Paulo alikuwa amevaa suti na tai siku ya Jumapili (kwa kweli, Jumapili kufanywa kama siku rasmi kwa wakristo kuabudu imetokana na mila na sio katika Biblia).

Mila ya kanisa inaweza kuwa jambo jema. Watu wengi wamejifunza Biblia, kuomba, na kujadili mafundisho na mawazo mengi kuhusu jinsi kanisa linapaswa kuishi. Hatupaswi "kurejesha gurudumu," na kujifunza masomo haya yote, lakini tunaweza kujifunza kutokana na kile ambacho watu hawa wamepitisha kwa njia ya mila. Hatuamini kwamba mila ni bora zaidi kuliko Maandiko, lakini tunaamini kwamba mila hutusaidia kuelewa Biblia.

Tukisoma historia ya kanisa, tutaelewa mengi kuhusu namna hii mila ilivyoingia. Tujifunze historia au la, tutaathiriwa na historia. Ushawishi utatoka kwenye utamaduni unaotuzunguka sisi, hitimisho tunayofikiria kwa siri, na hadithi ambazo tulisimuliwa. Hatari ni kwamba bila kujifunza kwa ufahamu wa jinsi tulivyokuwa, tunaweza kufikia hitimisho baya.

Kuijenga Imani yetu

Somo la historia ya kanisa linatuwezesha kuutambua urithi wetu. Wanaume wengi na wanawake walikwishajitoa mhanga maisha yao katika jitihada zaokueneza ujumbe wa neno la Mungu. Neno la Mungu limehubiriwa katika mazingira magumu sana na wakati mwingine yanayoogopesha.

Jifunze kuhusu uamsho wa ajabu uliofanyika katika Kanisa

Uwepo wa nguvu za Mungu umeonekana waziwazi katika historia yote ya Kanisa. Ni Roho Mtakatifu aliyewezesha uamsho ule uliopita na ndiye yeye anayefanya mambo yatendeke vizuri leo.

Unaweza kuuona mkono wa Mungu ukiwa juu ya Kanisa lake kila wakati

Historia hujirudiarudia

Mwandishi wa Mhubiri alisema "wala jambo jipya hakuna chini ya jua" (Mhubiri 1:9). Historia huja kwa mizunguko. Kwakuyasoma matukio yaliyokwishapita tunaweza kuelewa vizuri mambo yanayotokeahivi sasa. Tunaweza kujifunza kutokana na makosa yaliyofanywa na watu wengine. Mungu hachambui watu kwa ajili ya kuwaheshimu. Kila kitu alichokitendea kizazi kilichopita anaweza pia akatufanyia sisi iwapo tutamtii kama kizazi hicho cha zamani.

Warumi 2:11—Kwa maana kwa Mungu hakuna upendeleo.

Tunaweza kujifunza kutokana na mafanikio na makosa ya wale ambao wameishi mbele yetu.

Mungu habadili

Mungu huwataka watu wake watende kazi kwa usawa katika vipindi vyote. Mungu alivyowafanyia watu wa kale ni hivyo hivyo atawatendea watu wake leo. Mungu anataka watu waishi maisha matakatifu na hatabadilisha msimamo wake kabisa.

Mungu huwatumia wanadamu wa kawaida kufanya kazi zake

Mungu yule aliyewatumia akina Petro, Yakobo, na Yohane ni huyo atakayekutumia pia wewe. Mungu katika utendaji wake huwatumia watu wa kawaida tu kama wewe au mimi.

Uneemeshaji wa elimu ya mchungaji

Mchungaji wa Injili anapaswa asiwe mjinga, awe mjuzi kwa utajiri wa historia ya kanisa.