Skip to main content

Ufafanuzi wa Historia ya Kanisa

Ufafanuzi wa Historia ya Kanisa

Kanisa

Neno la Kigiriki la kanisa ni ekklesia lenye maana "wale walioitwa pamoja au wale walioitwa mbele."

Darasa hili litasoma kuhusu kanisa la Yesu Kristo. Neno kanisa kama linavyotumika siku hizi humaanisha majengo ambamo watakatifu walikusanyika ndani yake kwa ajili ya kuabudu lakini nisahihi zaidi kuhusisha watu. Maandiko hutumia neno kanisa kumaanisha kusanyiko katika nyumba mahali au mji fulani (Warumi 16:5; 1 Kor. 16:19; Kol. 4:15). Kanisa ni zaidi ya nyumba au jengo ila ni watakatifu ambao ndio mwili wa Kristo.

Bwana akalizidisha kanisa

Matendo 2:47…Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa walewaliokuwa wakiokolewa.

Baada ya kupata ubatizo mkuu wa Roho Mtakatifu katika chumbacha ghorofani, wanafunzi wake walikuwa na ushawishi mkubwa katika kumshuhudia Kristo. Siku ile roho 3,000 ziliokolewa na kuongezwa katika kusanyiko la mahalipale. Kila siku wengi zaidi walizidi kuongezwa!

Kuna kanisa moja tu la Mungu, na Mungu peke yake anaweza kuongeza wanachama kwa hilo. Wanadamu wana mashirika ya kidini na wanaweza kudhibiti wanachama wao, lakini hakuna mwanadamu anayeweza kusema nani au si mwanachama wa kanisa la Mungu.

Yesu ni kichwa cha kanisa

Waefeso 1:22–23—akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo ndilo mwili wake…

Kanisa katika andiko hili linaelezwa kama mwili wa Kristo. Yesu ni kichwa cha Mwili wake. Katika hali ya kawaida kichwa huuagiza mwili kufanya mambo inayotakiwa na kazi nyinginezo. Katika mwili wa Kristo, Yesu ni Kamanda anayeamrisha Kanisa lake kufanya kazi ya Mungu.

Kanisa lilizaliwa na Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste. Darasa hili litajumlisha somo la kanisa la mwanzo la Matendo hadi Kanisa letu la kipindi hiki cha sasa.

Historia

Neno hili historia linatokana na neno "linalomaanisha kujifunza kwa kufanya uchunguzi."

Kamusi ya Webster inafafanua historia kama "lile tawi la elimu linalohusu matukio fulani katika hii dunia yetu. Somo au uchunguzi wa mambo ya wakati uliokwishapita."

Mwandishi mmoja alisema kwamba "Zamani ni nchi ya kigeni: wanafanya mambo tofauti huko." [1]

Ukristo

Tunajifunza historia ya kanisa la Kikristo. Neno Mkristo lina maana "ya kuwa kama Kristo au mmoja wa Wafuasi" wa Kristo ambapo lilitumika kwa mara ya kwanza huko Antiokia kwenye mwaka wa 40 BK (Matendo 11:26).

Kuzaliwa, maisha, kifo, na ufufuko wake Kristo ndio kiini cha historia ya dunia. Historia imeandikwa kumzunguka Kristo; tarehe huandikwa katika KK (Kabla ya Kristo) na BK (Baada ya Kristo). Historia yote imemweka Kristo katikati yake.

[1] L. P. Hartley, The Go-Between (1953)