Skip to main content

Archived Textbook

MWAKA WA KWANZA

KITABU CHA KIADA

ELIMU YA MAHUBIRI 1

Maandalizi ya Hotuba na Mahubiri

CHUOCHA BIBLIA NA WOKOVU CHA MOSHI

Moshi, Kilimanjro, Tanzania

CHUO CHABIBLIA NA WOKOVU

Portland, Maine. Amerika

Utangulizi: Kuhubiri ni kufanya kitu gani?

Elimu ya mahubiri ni sanaa au sayansi ya majadiliano ya didini au kuhubiri. Katika darasa hili wanafunzi watapata msaada wa namna ya kuandaa hotuba na kuhubiri. Katika Biblia, tunaona mfano kwa mahubiri ya Kikristo. Ifuatayo ni orodha ya mambo ambayo tunajua kuhusu kuhubiri:

  1. Kufundisha na kuhubiri ni tofauti lakini nenda nayo vyote (Mat. 11:1)
  2. Yohana mpatizaji alihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya ondoleo la dhambi (Mark 1:4)
  3. Sababu kubwa kristo alikuja kuhubiri (Mar 1:38)
  4. Injili lazima ihubiriwe KILAMAHALI kwa KILA MTU pasipo udhuru (Marko 16:15; War. 1:15; II Cor. 10:16; Gal. 1:16; Ufu. 14:6; Mat. 10:7)
  5. Kristo lazima ahubiriwe (Mdo. 17:3; I Kor. 1:23; 2 Kor. 4:5; Waflp. 1:15–16)
  6. Kazi ya mhubiri na mzigo ni kuhubiri (I Kor. 9:16; Waef. 3:8)
  7. Injili ni ya kutolewa bure (I Kor. 9:18)
  8. Mhubiri huhubiri na kuacha matokeo na utukufu kwa Mungu (I Kor. 15:11)

Kuhubiri ni mawasiliano ya mazunguzmzo ya ukweli wa kimungu kwa lengo la kushawishi. Ufafanuzi huu unahusu njia tatu za kufanya mahubiri:

  1. Mambo ya Kuhubiri. "Ukweli wa Kimungu"—hutuambia nini cha kuhubiri
  2. Njia ya Kuhubiri. "mawasiliano ya mazunguzmzo"—hutuambia namma ya kuhubiri
  3. Malengo ya Kuhubiri. "kwa lengo la kushawishi"—hutuambia kwa nini tuhubiri

Mambo ya Kuhubiri

Kuhubiri ni kupeleka mbele ukweli (Gal. 1:8–9). Hii hutueleza ni nini tunachopaswa kuhubiri. Ukweli wa Kimungu unapaswa kuwa kiini cha mada ya somo. Katika msitari unaotangulia wa darasa hili (II Tim. 4:2), Paulo alimwambia Timoteo lihubiri Neno. Mhubiri anaitwa alitangaze Neno la Mungu. Neno la Mungu ndiyo mamlaka ya mwisho. Mhubiri anapaswa kujibu kila swali kwa kutumia Neno la Mungu; analazimika kutulia katika mamlaka kuu ya Maandiko. Kwa ufafanuzi mahubiri yanapaswa kuwa na ukomo katika:

  1. KUTANGAZA NA KUSIMAMIA NENO LA MUNGU
  2. KUFIKISHA UJUMBE TOKA KWA MUNGU KWA MWANDAMU
  3. KUHUBIRI KUNAWAHUSU VIUMBE WA MUNGU. Njia ya Wokovu ndio somo muhimu zaidi atakalofanya. Mwanadamu anahitaji kuwa na uhusiano na Mungu na siyo kuwa na uzito wa kidini au wa kifalsafa. Mhubiri atawaagiza waumini kuhusu wajibu wa Kikristo. Mhubiri anaitwa akaihubiri Injili ya Kristo, na siyo kufundisha fasihi au vitu ambavyo ni kinyume na masomo ya Biblia.
  4. MSINGI WA SOMO LA HOTUBA NI INJILI. Wakati mhubiri anapoongea kwa msisitizo, anapaswa kulipigia NENO LA MUNGU kelele. Upungufu wowote katika jambo hili haukubaliki kama mahubiri ya Kikristo.

Kiwango cha mafundisho ya Kikristo.

  • KUWA MAKINI—Usijaribu kuhubiri sana kwa wakati mmoja
  • KUWA SAHIHI—Inabidi uliweke somo katika wazo moja kuu
  • KUWA NA AKIBA—Unapaswa kubakiza cha kufundisha wakati unaofuata. Somo siyo lazima liwe la milele bali la Kimungu!

Mamlaka ya Mahubiri ya Kikristo

Unawakabidhi wanadamu Neno la Mungu na siyo taarifa ya kwenye gazeti. Hubiri kutokana na matokeo ya msukumo wa ushuhuda wa Kimungu wa Injili. Kuamini bila shaka yeyote msukumo wa Neno la Mungu ni muhimu kwa ajili ya kuukubali ukweli wake. Tunahubiri tunachohubiri kwa sababu ni sahihi na tunafahamu kwamba ni sahihi kwa sababu ni Mungu aliyesema hivyo. Iwapo msingi wako ni Shajara ya mwaka au Ensaiklopidia, ujumbe wako hata kama utakuwa na maelezo mazuri utakosa mamlaka. Msukumo wa Neno la Mungu katika Biblia ndio unaoyapa mahubiri ya Kikristo mamlaka yake.

Mamlaka ya mhubiri yanapatikana katika mamlaka ya Neno la Mungu. Mhubiri ni lazima aelewe kwamba Biblia siyo maneno ya wanadamu bali ni Neno la Mungu lenye nguvu. Neno lenye nguvu maana yake Mungu amelivuvia. Mungu aliwawezesha waandishi wa Biblia; ndio kusema kwamba, Mungu alipumua kupitia watu hao Neno la uhai. Biblia Haijahusisha Neno la Mungu peke yake bali ni Neno la Mungu.

Neno la Mungu lina nguvu za kuweza kubalisha maisha ya wanadamu na Neno la mahubiri linahitajika ili kupata mabadiliko hayo (War. 1:16). Mawazo ya mwanadamu hayatabadilisha maisha. Ni sharti muhubiri atumie Neno la Mungu kama msingi wa hotuba yake. Upo uhai katika Neno la Mungu.

LIJUE NENO!

Ni lazima ujifunze Neno la Mungu kwa sababu unapaswa kuelewa taarifa inayoenda kuhubiriwa (2 Tim. 2:15). Uelewa wa taarifa hiyo utampatia mhubiri mamlaka wakati wa kutoa ujumbe. Iwapo huna uhakika na unachosema au hujiamini katika uelewa wako wa ujumbe huo, uoneshaji wako wa somo utakuwa dhaifu. Kama huna uhakika kuhusu unachozungumzia watu hawatapokea ujumbe unaojaribu kuwahubiria.

Njia ya Kuhubiri

Njia ya kuhubiri ni "mawasiliano ya mazunguzmzo." Njia ya kuhubiri inatuambia namna ya kuhubiri. Mawasiliano yanahusu kuwaeleza watu wazo. Ni lazima wazo hilo lieleweke kwa watu ndio mawasiliano yaweze kufanyika. Mahitaji ya lazima kwa mawasiliano ni maneno sahihi na kauli zilizo wazi. Mhubiri anapaswa kuongea kwa njia ambayo watu wataelewa. Tuangalie mfano wa Nehemia katika Nehemia 8:8: "Nao wakasoma katika kitabu, katika torati ya Mungu kwa sauti ya kusikilika; wakaeleza maana yake, hata wakayafahamu yaliyosomwa." Neno la Mungu lilisomwa kwa usahihi au uwazi, likaelezwa kwa wale watu au wakawapa busara na watu hao wakafundishwa Neno na wakalielewa.

Ni vizuri mhubiri akihubiri na, akimaliza hotuba waumini watatawanyika wakisema, "mhubiri alisema hivi..."
—Martin Luther

Kazi nzuri na yenye nguvu ya mahubiri inahitaji:

  • Upako wa Roho Mtakatifu (I Yoh. 2:20)
  • Lugha iwe wazi na ya kawaida (Wahubiri wenye uwezo mkubwa kama D. L. Moody waliongea katika lugha ya mtu wa kawaida.)
  • ya kusisimua (sema unachomaanisha, na maanisha unachosema.)

Ushawishi unawezekana kutokana na uwezo mkubwa. Mwishowe uwezo wa mhubiri ni matokeo ya uweza wa Roho Mtakatifu. Uweza wa Roho Mtakatifu utamfanya mhubiri afundishe kwa hisia. Hubiri kama unayekwenda kinyume na majeshi yote ya motoni kama Daudi alivyopiga kelele katika ule mwamba, "hakuna kiini cha tatizo!" mhubiri anapaswa kuridhika na usahihi na nguvu za ujumbe wake ili kupata mafanikio. Fuata uongozi wa Roho Mtakatifu kwa sababu atakuelekeza vema na kutii uweza wake kwa sababu katika kukubali nguvu za Mungu zitaonekana wazi.

Waumini wanapaswa kushirikishwa katika mchakato mzima wa hotuba.

Akilini mwako waweke waumini wakati ukiandaa hotuba

Wafikirie na kuwaombea watu unaotegemea kuwapatia mahubiri. Mahubiri yenye manufaa yanamtaka mhubiri awe ni mtu anayejali na asiyekuwa mgumu wa moyo. Kuwakaribia baadhi ya watu kwa njia za uhakika huweza "kuwaweka kando". Mruhusu Roho Mtakatifu akuongoze katika maandalizi yako ya somo ili watu ambao watasikia wahisi nguvu za Mungu na kulipa nafasi somo lako. Mungu anafahamu ni akina nani watakaohudhuria na akili zao zitakuwaje na wewe pia unaweza kuona na kujifunza kitu kutokana na hali iliyopo mahali unapotoa mahubiri. Hata kama utakuwa unaongea katika ibada ya vijana wadogo, darasa la shule ya Jumapili, katika ibada ya watu wazima, katika kona ya barabara au katika hema lenye kikao cha wanauamsho; utulivu na hali ya hewa kwa ujumla ni lazima uvitilie maanani. Kwa kifupi, mhubiri ni mwanafunzi wa ubinadamu. "Mheshimiwa, siyo mambo ya kuhusu vitabu, ni wanadamu ndio tunaopaswa kuwaelewa"—Patrick Henry

Uweke waumini akilini mwako wakati unapoonesha

Utajifunza kufahamu kama wanalipokea Neno. Unaweza kuongeza mifano mingi zaidi na kuweka uzito kama watu wanaonekana kutoolewa ujumbe. Heshimu muda uliopewa.

Hotuba inapaswa kuwa ya kawaida, inayoweza kurudiwa na yenye maelezo makini

Njia ya kawaida hutumia Maandiko kama msingi wake kwa Neno la Mungu ni sahihi na halijatenganishwa na mahitaji ya wanadamu

Itaonekana ni jambo la kigeni (kwa usahihi kabisa) kwa waumini wa Kikristo kama Mchungaji wao atasimama na kutoa taarifa yake katika Kitabu cha Uchambuzi wa Msomaji (Reader's Digest). Pili, somo linapaswa kuwa linalozoeleka. Maneno yake na maana zake ziwe rahisi kueleweka. Michoro ya matukio ya kila siku inaweza kusaidia kuwafanya watu waioanishe na somo. Yesu aliweza kutumia vizuri kile ambacho kilikuwa kimezoeleka (Kondoo, kilimo n. k.) kwa mifano wa kile ambacho hawajakizoea (Ufalme wa Mbinguni). Mifano rahisi ya Maandiko haitawafanya washindwe kuelewa lakini, uhakikishe kwamba ni ukweli na unahusika.

Njia ya marudio ni tangazo rasmi la Neno

Mpango na ratiba nzuri itahakikisha kwamba wasikilizaji wako wataweza kufuata unachohubiri. Umoja na utulivu unapaswa kujibiwa kwa mahubiri mazuri yenye hisia ya Neno la Mungu. Umbile pekee yake halitoshi lakini ni mwanzo mzuri. Kurudia kinachofahamika ni mbinu inayomsaidia mhubiri lakini kuonyesha hisia na upako kutaamua uwezo wako wa kushawishi.

Matumizi ya matukio yanayoeleweka huonesha vizuri ukweli wa Neno la Mungu

Linganisha Injili na Injili nyingine na tasfiri kila taarifa kwa kutumia maandishi yake. Neno la Mungu ni Mamlaka ya Mwisho na kiwango cha kanuni za maisha. Wasiliana kwa busara na kwa njia iliyo wazi. Wewe unahitaji kuonekana una akili nzuri kwa sababu watu wanahitaji kuwa na uwezo wa kukufuata wakati unapohubiri. Waoneshe ukweli kwa njia rahisi na inayoelezeka. Washirikishe wasikilizaji wako ukweli hatua kwa hatua na jenga ujumbe huo kwa mpangilio kama somo linavyoendelea.

Malengo ya Kuhubiri

Ujumbe unatueleza sababu za kuhubiri. Somo limepangwa kwa mtazamo wa kushawishi. Kuhubiri kwa hakika siyo kuongea tu kuhusu Biblia, bali ni kupata uamuzi mioyoni mwa wanadamu. Lengo la kuhubiri ni malezi na maisha ya mabadiliko (Wakol. 1:28; Luka 4:18; 9:60; Mdo. 5:42; 10:42; 14:15; 15:21; War. 15:20). Malengo ambayo muhubiri anaweka mbele yake ni kama ifuatavyo:

Wokovu wa Roho za Watu

Wokovu wa Roho za watu ni moja ya malengo muhimu ya mahubiri. Mahubiri ni njia aliyochagua Mungu ya kuifikia mioyo ya wanadamu. Mungu amechagua kumtumia mwanadamu kumfikishia ujumbe wa Neno lake mwanadamu. Watenda dhambi hawatamuona Mungu kwa hekima ya mwanadamu, bali kwa kupitia mahubiri ya ujumbe wa Neno lake. Mungu alichagua upuzi wa kuhubiri kuokoa waliopotea (I Kor. 1:21).

Kukua Kiroho

Mungu alilipa Kanisa Wachungaji kwa lengo mahsusi la kukamilisha upatikanaji wa watakatifu (Efe. 4:11–14). Ni wajibu wa mchungaji kuwalisha kondoo kwa Neno la Mungu (Yoh. 21:15–17).

Kuzaliwa Imani

Kwa kuhubiri Neno la Mungu, mbegu za imani zinaweza kuoteshwa katika mioyo ya watu kwa kuponya na mahitaji mengine (War. 10:17). Mungu huhitaji imani (Ebr. 11:6) kuonekana kwa kila mmoja na wajibu wa mhubiri ni kuwafanya watu waliamini Neno la Mungu.

Liagize Kanisa

Wape Moyo Waumini

Mchungaji mwaminifu wa Injili hubeba mzigo ili kila aliyeusikia ujumbe wake apate moyo na msaada. Wakati wa mahubiri, mhubiri anawafikia watu hadi wa chini kabisa kwa nguvu za Roho Mtakatifu ambapo kwa njia yoyote ile mtu atapata msaada wa kumnyanyua na kumuondoa katika shimo la kutisha.

Unapaswa kuwa mwelekevu na mwenye kutia moyo ukiwa katika mimbari. Hata kukemea kunaweza kuhubiriwa kwa njia ya kuelekeza. Kumbuka kwamba unajaribu kunyanyua maisha ya watu na siyo kuwahamisha katika jamii yao. Iwapo utawahamisha kutoka katika mazoea ni kwa lengo la kuwajenga upya. Usimalizie somo lako kwa njia ambayo siyo endelevu bali elekeza njia rahisi. Dakitari akishatambua ugonjwa, haondoki akaondoka nyumbani bali hufuatia kwa dawa.

Waebrania 4:12—Maana neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

Wafanye Waumini wafikie Uamuzi

Usiridhike kama muhubiri kwa kuwapa watu moyo peke yake. Iwapo wasikilizaji hawatafikishwa katika hatua ya kufanya uamuzi, wataondoka kwa njia ile ile waliyokuja nayo. Siyo wajibu wa muhubiri na hawezi kuwalazimisha watu kuwa watii, lakini anaweza kuwaongoza moja kwa moja katika mahubiri yake hadi kwenye kisima na kuwatangazia kwa ushupavu kwa mamlaka ya Roho Mtakatifu, "Kunywa! Hiki ndicho kitu unachohitaji! Njoo kwa Kristo!" Muhubiri anapaswa kufanya kazi kwa kulenga "wito wa madhabahu" anapohubiri kwa sababu hapo ndipo kila mtu atapelekwa na kufikishwa katika hatua ya kuamua na ndipo wanalazimika kukubali au kuukataa ujumbe.

Wasifu wa mhubiri

Kiwango cha uwezo wa mhubiri kinapimwa kwa akili, kwa maadili na kiroho. Mhubiri anapaswa kuwa amehitimu kiroho na anao upako wa kuhubiri. Mhubiri anapaswa kuwa amehitimu katika mafunzo yake ya Biblia. Mhubiri anapaswa pia kuwa msafi kimaadili na uwepo ushahidi wa Kikristo. Sasa tuangalie kwa makini wasifu bayana wa mhubiri.

Anapaswa kuwa Mkristo wa Kweli

Ili kumhubiri Kristo ni lazima umjue Kristo. Paulo alisali na kusema: ili niweze kumjua Yeye. Kama mhubiri unahitaji kumjua Kristo kama Mwokozi wako. Unalazimika kumjua Kristo ni nani ndio uweze kuwaeleza wengine Yeye ni nani. Ni wazi kwamba mhubiri ni lazima awe amezaliwa mara ya pili ingawa wengi siku hizi hata wale ambao bado hawajaokolewa hujiita wahubiri. Ni lazima uamini kabla ya kuwa mhubiri (II Wak. 4:13).

Charles Wesley, ndugu yake Yohana Wesley, alihubiri na kufundisha kwa miaka mingi kabla hajamkubali Kristo kama Mwokozi wake. Kama mdhambi, alianza masomo ya dini katika Kanisa ka Kristo huko Oxford mwaka 1726 lakini alipoteza nguvu zake nyingi akitafuta namna ya kujifurahisha. Alipata shahada yake ya uzamivu kwa kufaulu vizuri kama msomi mwaka 1733, na mwaka 1735 aliapishwa kuwa Mchungaji katika Kanisa la Anglikana. Mwaka 1738, Charles "alipata uamsho" aliokuwa anauhitaji sana. Mwishowe baada ya miaka 12 ya mafunzo marefu ya dini na hata mahubiri pia aliukubali ujumbe wa Agano Jipya kuhusu wokovu. Charles aliyekuwa hajapata matunda yoyote na wala hakuwa msaada katika miaka hiyo 12, baada ya kuokoka alikuwa sehemu muhimu ya uamsho mkubwa nchini Amerika na alifanya kazi pamoja na ndugu yake Yohana Wesley aliyekuwa mashuhuri sana. "Kazi yake kwa miaka iliyofuata iliweza kuandika nyimbo 6,500 kulieneza Agano Jipya kama alivyolielewa. Wakati alipofariki Machi 29, 1788 alijulikana kama mhubiri mwenye nguvu na hekima." ("Charles Wesley". 2005. http://www.bookrags.com/biography/charles-wesley)

Anapaswa kuwa na Wito

Kazi ya kuhubiri ni wito wa Mungu. Biblia inatueleza kwamba ni sharti mwanadamu atumwe ili akaihubiri Injili (Marko 3:14; War. 10:15). Ni Mungu ambaye hutuma. Mungu alimwita Yeremia kuwa Nabii kabla hata hajazaliwa. "Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa Nabii wa Mataifa" (Yeremia 1:5). Wito wa Mungu ni zaidi ya hisia na msisimko. Mungu wa mbinguni atauweka wito wake katika maisha ya mwanadamu akaihubiri Injili Yake.

Ni nini maana yake wito wa Mungu?

Ni ukubali wa ndani anaopewa mwanadamu na Roho Mtakatifu ambo huthibitishwa kwa Neno la Mungu na Mwili wa Kristo. Roho Mtakatifu ataongea na moyo wako. Paulo alizungumza kuhusu Roho Mtakatifu kushuhudia pamoja na dhamiri yake (Warumi 9:1). Mungu atawasha wito wake katika moyo wako. Neno la Mungu litaimarisha kukubali kwako. Mungu ataongea na wewe kwa Neno lake. Wakristo wengine waliojazwa Roho Mtakatifu watashuhudia wito wako. Roho Mtakatifu aliongea na kanisa la mwanzo kuwatenga Paulo na Barnaba kwa ajili ya kazi ambayo Mungu alikuwa amewaita waifanye (Matendo 13:1–3). Wito wa Mungu utathibitishwa kwa Mwili wa Kristo. Yakobo, Petro, na Yohana walitambua wito wa Mungu kwa maisha ya Paulo (Wagalatia 2:9).

Ni Mungu peke yake anaweza kumfanya mhubiri

Darasa hili halitakufanya uwe mhubiri. Darasa hili litakusaidia ujue namna ya kujifunza Biblia, kuandaa hotuba, na kuhubiri kile ulichojifunza. Vifaa hivi vyote havitakufanya uwe mhubiri. Mahubiri yenye maana siyo ya kuonyesha matukio tu na ukweli wa Neno la Mungu bali ni kazi ya Roho Mtakatifu kupitia katika chombo kilichoandaliwa.

Ni lazima awe Mwanafunzi wa Biblia

Ni lazima mhubiri ajue ni kitu gani anachohubiri. Ni lazima ulijue Neno kabla hujaanza kulihubiri Neno. Mtenda kazi atajifunza na kuelewa kazi ambayo anategemea kuifanya. Kwa mfano fundi magari atajifunza kuhusu magari, seremala atajufunza namna ya kufanya kazi kwa mbao, na mhubiri anapaswa kama yule mtenda kazi mwingine ajifunze Neno la Mungu ambalo anategemea kulihubiri.

Inabidi mhubiri ajenge tabia ya kujifunza Biblia kila siku. Iwapo mhubiri analishwa Neno la Mungu kila siku atakuwa na kianzio tajiri cha Mkate wa Maisha wa kuwalisha wengine. Mhubiri anapaswa kujiandaa kwa kujifunza andiko analotegemea kuhubiri kabla ya kuingia katika mimbari. Anapaswa kuwa na uelewa mzuri wa taarifa ya Injili ambayo itahubiriwa.

Ni lazima Awe Mtu wa Maombi

I Wathesalonike 5:17—Ombeni bila kukoma.

Waefeso 6:18—Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na mkidumu katika kuwaombea watakatifu wote;

Maombi ni ufunguo wa mafanikio ya mhubiri

Mafanikio ya mhubiri yanapimwa kwa Roho zinazookelewa na maisha ambayo yamebadilishwa kwa nguvu za Mungu, siyo kwa faida ya fedha au umashuhuri. Mhubiri anapaswa kuishi maisha ya maombi kama anategemea upendeleo wa Mungu uzifikie roho za wanadamu. Mhubiri ambaye hatajifunza kufanya maombi hatadumu katika kazi.

Utafundisha kwa kuwa mfano.

Watu unaowapatia mahubiri watakuona wewe kama mfano wao. Iwapo wataona kwamba mhubiri wao hathamini maombi basi na wao hawatafanya maombi pia.

Nguvu za Mungu huonekana kupitia katika maombi

Iwapo mhubiri atakuwa na nguvu za Mungu katika maisha yake ni lazima awe mtu wa maombi. Kama hakuna maombi hakutakuwepo nguvu, kama kuna kusali kidogo kutakuwepo na nguvu kidogo, na iwapo kuna kusali sana kutakuwepo na nguvu nyingi. Kila mtu wa Mungu aliyepewa nguvu na Mungu alikuwa ni mtu wa maombi. Hakuna njia fupi kwa Mungu. Iwapo unataka kuihubiri Injili kwa nguvu na mamlaka ni lazima usali na kusali na kusali.

Ni mtu Mnyoofu wa Maisha

Mhubiri anapawa kuishi maisha yaliyotengwa

Ni muhimu sana kwa mhubiri kuishi maisha yaliyo safi (II Wak. 6:17). Makuhani wa Agano la Kale waliwekwa wakfu kwa ajili ya kazi ya Bwana. Neno wakfu maana yake ni kutengwa au kuwekwa pembeni kwa ajili ya huduma ya Mungu. Mungu anahitaji mtu wa Mungu atenganishwe na dunia. Yesu alipakwa mafuta na Mungu juu yaw engine kwa sababu alikuwa myoofu wa Moyo na alichukia uovu (Waebrania 1:9). Moyo wa mhubiri unalazimika kuelekea mambo ya Mungu, na siyo mambo ya dunia. Nguvu ya Mungu huja katika maisha yaliyo safi.

Mhubiri anapaswa kuweka ushuhuda mzuri

Mh ubiri ambaye haishi kwa mfano wa Kimungu atashindwa kuwafanya wengine anaowahubiria waishi Kimungu. Neno la Mungu linatuambia kwamba sisi ni Nyaraka hai, husomwa na kujulikana kwa watu wote (II Wakorinto 3:2). Kwa mfano kama watu watamuona mhubiri wao akikasirika mara kwa mara na kuchukia hawatamsikiliza atakapowaambia wasikasirike. Watu hawatamuheshimu mtu ambaye haishi maisha yanayompendeza Mungu.

Anapaswa kuwa Tayari kwa Utumishi

Neno la Mungu linatuagiza kufanya kazi kwa uwezo wetu wote (Mhubiri 9:10), na hii ni pamoja na kuihubiri Injili. Mhubiri anapaswa kuishi kwa kuzingatia afya ili awe na nguvu kwa ajili ya huduma ya Mungu.

Mhubiri anapaswa kuwa na afya njema kwa ajili ya huduma

Ni muhimu kama mhubiri kujutunza mwenyewe. Unalazimika kujutahidi kula vizuri na kupata usingizi wa kutosha. Biblia inatuambia kwamba kuna faida katika kufanya mazoezi ya mwili. Ni vigumu kwa mhubiri wakati anahangaika, au anashindwa kupumua vizuri na anakosa pumzi wakati akijaribu kuhubiri. Inaweza kuwa vigumu pia kwa watu kupekea ujumbe wa mhubiri ambaye hushindwa kupumua mara kwa mara. Akili yako haitakuwa makini kama hutapata usingizi wa kutosha. Miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu. Mhubiri anapaswa kujitahidi kuutunza mwili wake.

Mhubiri anapaswa kuwa na akili timamu katika huduma

Hupaswi kuleta matatizo yako hadi katika mimbari. Watu watajisikia kwamba kama wewe umevunjika moyo na umelemewa.

  • Unapaswa kumpelekea mambo yako Yesu (I Petro 5:7)
  • Yesu ndiye anayebeba mizigo yetu (Mathayo 11:28)
  • Paulo alituonya tuache akili ya Kristo iwe ndani yetu (Wafilipi 2:5)

Mhubiri anapaswa kuwa na akili kama ya Kristo. Akili ya Kristo haina kukata tamaa, kuogopa, au kulemewa. Kuwa na mapumziko mazuri na chakula kutakufanya uwe na akili timamu kwa ajili ya huduma.

Umuhimu wa Kuhubiri kwa Nguvu za Roho Mtakatifu

Popote na chochote tunacho hubiri lazima tuvuviwe na Roho Mtakatifu (Mdo. 16:6-10; I Kor. 1:17; II Kor. 2:12; Gal. 2:2; Yona 3:2; Isa. 61:1).

Mhubiri ni lazima ajazwe nguvu za Roho Mtakatifu

Mhubiri anahitaji kujazwa Roho Mtakatifu ili kuhubiri kwa nguvu. Mhubiri hawezi kulitoa Neno kwa nguvu na mamlaka bila msaada wa Roho wa Mungu.

Wafuasi wa kwanza wa kanisa waliambiwa na Yesu wasubiri katika mji wa Yerusalemu mpaka watakapopewa nguvu na Roho Mtakatifu (Mdo. 1:8; Luka 24:49). Baada ya Yesu kumwaga damu Yake msalabani kununua wokovu wa Mwanadamu, alipaa mbinguni na kuiacha kazi ya kuieneza Injili mikononi mwa mwanadamu. Yesu alifahamu kwamba mwanadamu hawezi kuhubiri Injili na kuzifikia Roho za watu zilizopotea bila kuwa na nguvu za Roho Mtakatifu. Aliwaambia wafuasi wake Roho Mtakatifu atawapatia nguvu ya kuieneza Injili kwa mataifa yote. Hakuna uhai wala nguvu katika maneno ya mhubiri bila upako wa Roho Mtakatifu.

Mhubiri ni cheche tu ya anachoweza kuwa bila upatanisho na Roho Mtakatifu

Mhubiri asiyekuwa na upatanisho ni karibu na kitu kisichokuwa na thamani. Wako wahubiri ambao wamekaukiwa na ni sawa na wafu kwa mafanikio yao kidogo au kushindwa kabisa kwa sababu ya kutokuwa na upatanisho na Roho Mtakatifu. Mbaya zaidi kuliko "kuwa na mafanikio kidogo" ni mizigo iliyooteshwa ndani ya maisha ya watu kwa unajisi wa wahubiri hao wanaoongozwa na matakwa yao wenyewe. Mhubiri anahitaji kujazwa na kuongozwa na Roho Mtakatifu.

Hakuna kilichombadala wa nguvu za Mungu katika maisha ya mhubiri

II Kor. 3:6—Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.

Kujifunza na kujiandaa bila kupakwa mafuta na Roho Mtakatifu hakutakamilisha kazi ya mhubiri katika madhabahu. Neno andiko katika andiko linamaanisha andishi la sheria bila kuwa na Roho wa Mungu. Neno peke yake bila Roho Mtakatifu halitakuwa na uhai. Lengo la darasa hili ni kuonesha umuhimu wa kujifunza na kufanya maandalizi pamoja na kupakwa mafuta na Roho Mtakatifu.

Mwanadamu hana uwezo wa kwake binafsi wa kuihubiri Injili

I Petro 4:11—Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina.

Mungu alikusudia mahubiri ya Injili yafanyike kwa nguvu.

I Yoh. 2:20—Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote.

Neno mmepakwa katika aya hii inahusu kupataniswa na Mungu. Neno hilo lina maana ya kile kinachotumiwa kufanya upako. Mito ya uhai inayomwagika kutoka kwa mhubiri itawafikia wanadamu wenye kuhitaji. Neno kupakwa maana yake ni kuloanisha. Kwa lugha ya asili ya Kiyunani; linaelezea kuenea kiasi cha kutosha kwa uwepo wa Mungu kunakomsaidia mwanadamu kuhubiri kwa nguvu na mamlaka.

Mungu huwapa uwezo wa kuhubiri wale anaowaita kuwa wahubiri wa Injili

Uwezo asilia peke yake hautoshi kuifikia mioyo ya wanadamu. Mbinu za kuongea na kupamba maneno hazitazaa uhai. Mhubiri anapaswa kuwa na upatanisho na Mungu ndipo aweze kutangaza Neno la Mungu.

Mtume Paulo alipewa nguvu na Roho Mtakatifu

Paulo alihubiri kwa nguvu za Mungu (I Kor: 2:4–5). Neno linatuambia kwamba nguvu hizo zilidhihirika wazi wazi. Kudhihirika ni kwa kitu kinachoonekana. Dunia inahitaji kuoneshwa zoezi la nguvu za Mungu. Paulo hakutegemea hekima ya mwanadamu kulihubiri neno la Mungu. Paulo alikuwa ni mtu mwenye elimu. Alikuwa ni Mfarisayo aliyefundishwa sheria ya Musa na Gamalieli ambaye alikuwa daktari wa sheria (Mdo. 5:34; 22:3). Hata hivyo Paulo pamoja na mafunzo aliyokuwa nayo alizihitaji nguvu za Roho Mtakatifu katika kazi ya kuhubiri Injili.

Upako wa Roho Mtakatifu: Maneno haya yana maana gani?

Mafuta ni alama ya Roho Mtakatifu

Katika Maandiko Matakatifu mafuta ni alama ya Roho Mtakatifu. Mafuta anayomiminiwa mtu ni alama ya Roho Mtakatifu anayemiminwa katika maisha ya mtu huyo.

Neno hili linahusu nguvu za Roho Mtakatifu zinazokuja juu yake na kuenea katika nafsi yake

Yesu alisema Roho Mtakatifu atamwagika kutoka ndani yake mwanadamu kama mito ya maji yenye uhai (Yoh. 7:38-39). Katika Agano Jipya kupakwa mafuta kunatumika kuonesha uhusiano wake na mahubiri ya Injili. Kupakwa mafuta ni kupewa nguvu za Mungu ili kumwezesha mwanadamu afundishe kwa nguvu na mamlaka.

Katika Agano la kale wafalme walipewa mamlaka yao kwa kupakwa mafuta

Wafalme walipakwa mafuta na manabii wa Mungu. Hii ilikuwa ni ishara kwamba wamepewa mamlaka na Mungu na kutengwa kwa ajili ya huduma yake. Mpango wa Mungu kwa wafalme hawa ni kuwapatia Roho Mtakatifu katika maisha yao. Baadhi ya wafalme hao hawakumtumikia Mungu kwa hiyo Roho Mtakatifu hakuwa pamoja nao.

Katika Agano la Kale manabii walipakwa mafuta

Katika I Wafalme 19:16 Elisha anaagizwa na Mungu ampake mafuta Yehu awe Mfalme naye Elisha apakwe mafuta ili awe Nabii mahali pake. Mafuta haya yalimwagwa juu ya Manabii kama alama ya Roho Mtakatifu akiwa amemwagwa katika maisha yao. Manabii waliongea kama kipaza sauti cha Mungu. Mungu aliongea kwa midomo ya Manabii; hawakusema mawazo yao wenyewe walipotabiri ila walifanya hivyo Mungu alipozungumza kupitia kwao. Biblia inatumia maneno: "Neno la Bwana," katika kuelezea Mungu alivyofikisha ujumbe kwa kuwatumia Manabii wake (Yeremia 44:24).

Katika Agano la kale Makuhani walipakwa mafuta

Makuhani hawa walipaswa kuwa Watakatifu katika Bwana. Walipakwa mafuta pia (Hes. 3:3). Hii inatuonesha kwamba wale ambao wanafanya kazi ya Bwana wanapaswa kumwagiwa Roho Mtakatifu.

Mungu alimpaka mafuta Yesu ndipo akaifundishe Injili

Luka 4:18, 19—Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru walioteswa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.

Waebrania 1:9—Umependa haki, umechukia maasi; kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, mafuta ya shangwe kupita wenzio.

Matendo 10:38—habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.

Mwana wa Mungu alipewa nguvu na Roho Mtakatifu kuihubiri Injili. Tunahitaji kuongezewa kupakwa mafuta kiasi gani ili tukaihubiri Injili?

Yesu aliongea kwa mamlaka (Mat. 7:29). Mungu hutoa mamlaka kwa mhubiri kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

Kupakwa mafuta huvunja vifungo vya dhambi

Kupakwa mafuta huharibu vikwazo vya kifungo (Isa. 10:27; 61:1). Watu wamefungwa kwa dhambi na ni nguvu ya Mungu peke yake inayoweza kuwaweka huru. Yesu alisema kupakwa mafuta kutawaletea mateka uhuru. Watu wengi wamefungwa kwa nguvu za shetani na kuwekwa katika gereza la dhambi. Neno la Mungu likihubiriwa na mpakwa mafuta na Roho Mtakatifu litavunja minyororo ya vifungo na kuwaweka watenda dhambi huru na nguvu za shetani.

Nguvu za Roho Mtakatifu huwepo wanapokusanyika waumini

Roho Mtakatifu anao uwezo wa kuvunja nguvu za dhambi wakati mhubiri anakihubiri. Kuhubiri hakuwezi peke yake kuvunja nguvu za dhambi. Upako wa Roho Mtakatifu ndio utakaovunja nguvu za dhambi katika maisha ya wanadamu. Upako ni zaidi ya nguvu za Mungu katika kumsadia mhubiri na ni nguvu za Mungu katika kulisaidia kusanyiko.

Roho Mtakatifu huleta ondoleo la dhambi

Roho Mtakatifu atawashawishi wanadamu wakubali dhambi zao kisha atawasogeza katika msalaba (Yoh. 16:8). Mahubiri ya mpakwa mafuta yataleta ondoleo la dhambi. Mwanadamu anaweza kulihubiri Neno, lakini ni Roho Mtakatifu peke yake anayeweza kuwafanya wanadamu watambue dhambi zao na kuwapeleka kwa Mungu.

Matumizi maalum ya kifungu (Vizibuo)

Utangalizi

II Tim. 2:15—Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.

Mhubiri anahitaji uelewa mzuri wa Neno yeye mwanyewe, ili waweze kuwatangazia wengine ukweli. Darasa hili litamwezesha mwanafunzi kufahamu namna ya kujifunza Neno la Mungu na kuelewa maana ya andiko. Nguvu ya hotuba ipo katika maandalizi. Mhubiri anahitaji ujumbe kutoka kwa Mungu. Maandishi ya andiko yanapaswa kuchaguliwa kwa maombi ya kina na kufikiri. Maandishi yakisha chaguliwa na mhubiri anapaswa kujifunza taarifa hizo za andiko. Lengo ni kufahamu unakoelekea kabla ya kufika katika madhabahu.

Kila mhubiri atajenga muondoko wake wa kuhubiri na wa kuandika dondoo. Baadhi ya wahubiri watahubiri bila kuwa na dondoo chache na wengine wataandika taarifa zote kuhusu hotuba yao yote. Darasa hili litapendekeza njia rahisi ya kuandika taarifa kwa ufupi kwa ajili ya matumizi ya mhubiri. Wahubiri wengine wanaweza kutumia maandishi hayo kwa ajili ya matumizi yao binafsi na wasiyatumie kabisa wakiwa Mimbari. Mhubiri anaweza kutumia njia yoyote lakini ni lazima ajifunze maandiko.

Maana ya vizibuo

Dikishenari ya Webster hufafanua vizibuo kama "sanaa ya kupata maana ya maneno ya mwandishi, ya kuielezea kwa wengine." Vizibuo vya kibiblia ni kujifunza ufafanuzi wa kibiblia. Vizibuo vya kibiblia ni kufanya harakati za kufafanua maandiko kwa usahihi. Vizibuo hushugulika na maswala kama vile:

  • Ni nini ufafanuzi wa kawaida wa kifungu hiki?
  • Ni nini ufafanuzi rasmi wa kifungu hiki?
  • Ni nini ambacho mwandishi anakusudia kusema?
  • Ujumbe gani ambao mwandishi anakusudia kuuwasilisha?
  • Je ni matumizi ya neno maalum, Uundaji wa kisarufi, wakati wa tendo, herufi, umuhimu katika mfano huu?
  • Nani waliokuwa wasomaji au wasikilizaji wa mwandishi, kwakupitia herufi?
  • Jinsi gani kifungu kimefasiriwa na watu wa siku za mwandishi?

Thamani ya vizibuo

Sio ujinga tu, bali ni hatari kupotosha Biblia Uvunjivu wa kipekee kuharibu maandiko kwa makusudi. Kuna kanuni husika za kufasiri zinazo tuongoza katika ufahamu na kufundisha maandiko Hizi kanuni huhudumia kama mistari ya mipaka ambayo hulinda maelezo yetu na uwasilishaji wa wazo la kiBiblia pamoja katika vifungo."

Tunarejelea maswala ya maandiko matakatifu kama kifungu kilicho patiwa mahali na baadhi ya wahubiri kwa kukosea hujaribu kuyafanya maandiko yakae mahali pa elimu yao ya filosofia. Biblia haihusiki na kile tunachotaka imaanishe, bali kujifunza kwetu maandiko sikuzote ingekuwa ni kungundua ujumbe wa Mungu Kufanya hivi lazima tutumie kanuni husika za vizibuo vizuri vya ufasiri na acha andiko lijisemee lenyewe (2 Pet. 1:16–21).

Kazi ya mhubiri ni kuwalisha watu ukweli wa Neno la Mungu (Yer. 3:15). Mhubiri anapaswa kuwafanya watu waweze kuielewa vema Biblia. Ni lazima mhubiri alielewe Neno yeye mwenyewe ndiyo aweze kuwahubiria watu wengine. Nehemia alisoma katika kitabu cha sheria, halafu akawaeleza watu maana yake ili waweze kuelewa Neno la Mungu kwa ajili matumizi yao wenyewe. Hii ndiyo maana ya mahubiri: kutangaza Neno la Mungu kwa njia ambayo watu watalipokea, watalielewa, watashawishika na kulifanyia kazi. Lengo la darasa hili ni kuwasaidia wanafunzi waweze kufahamu namna bora ya kujifunza Neno la Mungu. Hakuna njia maalumu iliyopangwa ya kujifunza; kila mhubiri ataweka utaratibu wake wa kujifunza Maandiko Matakatifu. Mhubiri anapaswa kujenga tabia ya kusoma Biblia kila siku. Mhubiri anapaswa kulijua Neno kabla ya kwenda kulihubiri.

Biblia ni ujumbe wa Mungu kwa mwanadamu, na Mungu anafahamu kwamba alikuwa na maana gani alipompatia mwanadamu Neno lake. Roho Mtakatifu atamwezesha mwanadamu kulielewa Neno (Yoh. 14:26; 16:7–13; I Wakr. 2:13). Mwanadamu hatapata uelewa mara moja wa Neno la Mungu. Mhubiri anaposali, na kujifunza Neno la Mungu, Mungu atamsaidia aweze kulielewa zaidi. Mhubiri ni sharti awe na uelewa angalao wa andiko anayokusudia kuihubiri.

Kanuni ya kwanza: kufasiri lazima kuwepo na msimamo na kutumika

Njia halali na ya heshima ya kufasiri kuwa na msimamo na pasipo mashindano au ubishi. Lazima usitawaliwe na yaliyokubaliwa kitheologia. Kama ufasiri wetu (vizibuo) vimetawaliwa na theolojia yetu, ndipo Biblia inaweza kufanywa iseme kile theolojia yetu inasema.

Lazima siku zote tumia kanuni sahihi za kufasiri ili kufahamu kipekee ukweli. Biblia imebeba aina mbali mbali za simlizi, kama vile mifano, mashairi, mithali, istiari, maombi, amri za wafalme, na nyaraka. Tusinge fasiri mashairi kama tafasiri Kwa mfano Nebkadreza alifanya amri ya kumkata vipande yeyote atakaye sema kinyume cha Mungu wa kweli Mhubiri anaweza kuwa amefanya vibaya kama atafuata ufasiri wa simlizi za siku za leo wa aina hii.

Kanuni ya pili: kuna maana sahihi moja tu ya kifungu cha Biblia

Kifungu cha kinabii cha weza kuwa na mikunjo miwili ya utimilifu, lakini kuna fasiri sahihi moja tu ya timilizo hizo.

Kanuni ya tatu: fasihi simlizi ni kwa kawaida huwa bora

Maandiko yote lazima ya chukuliwe katika simlizi yake na maana ya wazi kuruhusu tu kwa ajili ya mfano na mashauri ya vitabu. Kila kifungu lazima kichukuliwe katika thamani ya sura yake Maritini luther aliita hii kanuni "fasiri simlizi." Hii kanuni humanisha kwamba tunasoma na kutathimini maandiko pamoja na heshima hiyo hiyo na kufahamu kwamba tunasoma kitabu chochote.

Acha andiko lijizungumzie lenyewe. Ukweli ni kamili na hauhusiani na mpangilio wako wa matukio. Hii kanuni inauhusiano maalumu katika somo la unabii. Agano la kale linabeba karibu nabii 450 kuhusu ujio wa kwanza wa Kristo. Nabii nyingi zilikuwa nakala, angalau kweli sitini dhahiri za maisha ya Kristo na huduma ilio onyeshwa, na zote sitini, pasipo udhuru, zilikuwa unabii ulotimizwa kihalisi ambao ulikuwa hauja timizwa kihalisi na mimi sio unabii wa kweli.

Uliza swali: Mawazo gani KIHALISI hutiririka kutoka kifungu? Maana ya wazi kisome kwa njia iliondikiwa. Kuna hekima kuu katika urahisi.

Kanuni ya nne: soma kutoka pointi ya mwandishi ya upeo wa macho

Maandiko yote lazima ya chukuliwe kutoka pointi ya upeo wa mwandishi (2 Tim. 3:16). Fikiria habari kama, Nani waliokuwa shabaha ya mwandishi? Ni nani aliyeiandika? Paulo, Petro, Yohana aliependwa, Musa, au Marko? Watu hawa wote walikuwa na mitindo tofauti ya uandishi na madhumuni tofauti ya uandishi. Mazingira ya maandiko huhusisha nafsi na tabia za wandishi. Tunge hukumu habari ilioandikwa najicho la shahidi tofauti kutoka habari ilioandikwa na mtu fulani pamoja na habari za mkono wa pili.

Fikiria mpangilio wa kihistoria wa kifungu kwa kukata bima ya ufasiri sahihi

Mazingira ya maandiko huhusisha habari za kihistoria kwakushawishi kwenye wakati wa kifungu kilipokua kinaandikwa, na (Paulo aliwandikia waefeso, Wafilipi, Wakolosai, na Filimoni kutoka gerezani!Vilevile, Paulo alizaliwa Tariso mji mkuu wa kilikia na aliishi kwenye moja ya vyoo vikuu vitatu vya mababu wa ulimwengu wa waathene na Alexandrea ni wapili. Paulo alifundishwa katika Yerusalemu chini ya Gamaliel mwalimu mkuu wa sheria za kiyahudi. Paulo alipokea elimu bora iliowezakana katika siku zake. Yeye hakuwa mpumbavu asiye na elimu.)

Kwa mfano, Daniel 5 inafungua pamoja na sikukuu ya kusherehekea na kunywa. Mji wa babeli ulikuwa chini ya kuzingirwa na Wamedi na wajemi kwa kipindi cha miaka miwili hadi sherehe ya kufungua ya sura hii. Hii inatuambia kitu fulani cha kiburi na upuzi wa Wababeli ambao walijidhania kuwa hawata haribika. Njia pekee ya kujua kuhusu fikira za kihistoria ni kujifunza na kutafuta vifaa kama vile vitabu vya maoni. Neno la tahadhari si vitabu vyote ni sahihi kihistoria. Tahadhari maalum ingetumika kwa mfano unapo soma kitabu chochote kilichotolewa na Kanisa la Romani katholiki wamekuwa mara zote madhabahu ni sehemu yakuhesabia faida yao.

Fikiri kweli za kikiolojia kukusaidia kufahamu maana ya kifungu

Tena katika Daniel 5, kuta za mji wa Babeli zilikuwa nene ambayo jamii ya magari au vibandawazi vilikuwa vimeshikizwa juu ya kuta. Watu walifiri kuna ngome isiopita. Akiolojia au elimukale imejawa na kuungana na Biblia. Hii ndio sababu kujifunza na elimu ni vya muhimu sana kuweza kufahamu hizi kweli za kikiolojia ili kufahamu vema mpangilio wa mahesabu ya Kibiblia.

Fikiria kweli za kijeografia ambazo zingechangia katika ufahamu wa kifungu

Tuta bakia kwa Daniel 5 kukuonyensha jinsi fikira hizi zote zina chukuwa pamoja ilikupata maana yote ya kifungu Mto frati unapita katikati ya mji wa Babeli. Walikua na maji safi na walizalisha chakula chao; hii imeongeza katika hisia zao za kutokujihusisha na kuzingirwa kwa maana walifikiri hawangeweza kuondolewa milele. Muingilio wa mto ulikuwa unalidwa na milango mikubwa ya chuma. Habari hii ni msaada kwa kufahamu unabii wa Isaya kuhusu Babeli (Isaya 45:1). Historia hutuambia kwamba usiku wa karamu walinzi walilewa na kuacha milango wazi. Unabii wa Isaya ulikuwa umetimia wakati Koresh na Dario mumidiani alipochukua ufalme wa Babeli usiku huo wa karamu.

Fikiria matendo ya kisiasa ya wakati wa kifungu

Paulo anaonya mwanamke kunyamaza katika kanisa (1 Wak. 14:3). Tendo la kisiasa la siku hizo kwa ajili ya mwanamke kukaa upande moja na wanaume upande mwingine. Wanawake wasio elimika walikuwa wakisumbua ibada kwa kuuliza maswali toka upande baina ya njia ya viti kanisani. Muendelezo wa mukitadha wa msitari unatuambia wanawake kuuliza waume zao nyumbani. Au kutoa mfano kwa wengine, Paulo alikuwa akiwambia wanawake kusubiri mpaka waende nyumbani ndipo wawaulize waume zao maswali sio kuharibu ibada. Paulo sio kwamba alizuia mwanamke kuwa na nafasi ya kushuhudia na kushiriki huduma kanisani.

Ni aina gani ya maandiko yake?

Maana inategemeana na aina. Utafakari wa vifungu vingi vya kibiblia ni wa muhimu sana kumaanisha katika. Nyaraka, Injili, mambo ya kiyama, mambo ya kinabii, mambo ya kimafumbo, mambo ya kishairi, mambo ya kihisitoria hayawezi kufanywa katika kiwango kinacho tambulika kwasababu kila kitu kimetawaliwa na kusudi tofauti.

Kanuni ya tano: mazingira ni ufunguo mkuu kwa ufasiri

Kanuni hii ya tano hufikiriwa sana "majumuisho yote." Muktadha ni jinsi neno au sentesi imewekwa katika uhusiano kwenye kifungu kizima njia nzuri ya kufahamu maana ya neno ni kuona jinsi neno hilo limetumika katika sentesi. Mazingira huchukua katika yote sehemu moja moja ya kitu kizima. Mazingira ya maandiko huhusisha uwekaji wa msitari pamoja katika sura yake maalum na kitabu. Kila msitari wa maandiko ni wamuhimu kwa kina, lakini umuhimu wake unaweza tu kufahamika kwa kufiria madaraka yake katika aya, sura, kitabu, au hata Biblia nzima. Ufahamu mkamilifu wa kitabu kifungu huchukuliwa kutoka kilicho bora.

Hatuwezi kujifunza kipekee sehemu ndogo ya kitu chochote bila fikira za uangalifu maana yote ya sehemu zake.fikiria jinsi ufahamu wako usiokamilika kuhusu vyombo vya usafiri angani ingekuwaje kama huja elimishwa katika sheria za asili.masafa ya mruko wa ndege yeyote ingekuwa siri ya milele mpaka utakapokuwa umejifunza ndege katika "muktadha" wa asili ya upepo wa mazingira yake, mvutano, msukumo wa hewa, na kadhalika

MFANO: Tunajua Waebr 13:5 inasema kristo alituahidi, "sitawaacha kamwe, sitawaacha." Kwahiyo ni nini ambayo Yesu anamaanisha "Naenda zangu" katika Yohn 14:28? Kama yote tunayofanya ni kufikiri msitari wa 28 na kudharau muktadha wake, tutakuwa tumelazimisha kuhitimisha kuna upinzani ulio patikana hapa bali kama tunahitimisha kwa makini muktadha wake katika somo letu, tutagundua wazi rahisi kumaanisha katika. Kiwango katika kile Yesu alikuwa pamoja nao (katika uwepo wa kimwili) ilikuwa inaenda kubadilika kuwa (uwepo wa kiroho).

Kifungu kilichochukuliwa inje ya mazingira ni "hoja ya uwongo." Hoja ya uwongo imetumika kuficha sababu ya kweli na kusudi. Kutumia andiko kama hoja ya uwongo ni kutumia andiko liseme kile unacho taka liseme nasio kile Mungu amesema. Kifungu kilichochukuiwa inje ya muktadha ni kuharibu andiko.

Biblia imebeba hesabu ilovuviwa ya matukio yale yaliyo tokea na maelezo yaliyo fanywa Kwa mfano habari za kitabu cha Ayubu mazungumzo kati ya Ayubu na rafiki zake. Mazungumzo yaliyo andikwa kwa uangalifu kama yalivyo tukia, lakini ushauri wa wafariji wa Ayubu haukuwa ushauri mzuri hauwezi kuhusushwa kama ulivyo.

Majaribu ya Yesu yanapatikana katika Mathayo 4:1–11 inaandika Ibilis ananukuu maandiko kwa Yesu katika msitari wa 6. Iblis alipotosha maana ya Zaburi 91:11–12 kumjaribu Yesu ajirushe kutoka mnara wa hekalu Yesu alikanusha upotoshaji wa maaandiko wa shetani kwa kujibu kwa maandiko mengine: Usimjaribu Bwana Mungu wako (Kumb. 6:16).

Je, tunapaswa kufuata maneno ya mfalme katika Danieli 3:29?

Njia bora ya kufahamu maana ya neno ni kuona jinsi lile neno lilivyo tumika katika mukitadha wa sentensi.

KANUNI YA SITA:SIKU ZOTE LINGANISHA MAANDIKO KWA MAANDIKO

Andiko siku zote hushikilia ufasiri wake lenyewe (II Pet. 1:20). Neno, maelezo, au wazo lazima lijifunzwe katika kitabu ambacho ndio limeandikwa, na kisha katika matumizi yake katika vifungu vingine. Endapo kifungu hakita kuwa wazi juu ya ukweli, hakuna hitimisho litakalo patikana kutokana nacho mpaka vifungu vyote vinavyo husiana vimejifunzwa. Maelezo ya mafundisho ya Kibiblia hayapaswi kufanywa kimsingi kwenye kifungu pekee, bali maelezo ya mafundisho lazima yapitie kile maandiko yote yanasema juu ya mada.

Andiko lita jieleza lenyewe kama mistari ya Biblia imelinganishwa yenyewe kwa yenyewe. Njia moja ya ufasiri sahihi ni kulinganisha mistari katika Biblia na mistari mingi tofauti ya Biblia. Biblia inatuagiza kulinganisha vitu vya kiroho kwa mambo ya rohoni (I Wak. 2:13). Kwa kulinganisha andiko kwa andiko Biblia itaeleweka vema. Neno la Mungu litakaa pamoja kama sehemu za fumbo au mkanganyiko. Andiko moja litafasiri andiko lingine. Biblia yenyewe iko katika umoja kamili. Hakuna mapingamano katika Biblia. Kile Mungu alicho andika katika Mwanzo kitakubaliana na kile Mungu alicho andika katika Ufunuo.

Linganisha vifungu vya maandiko kwenye somo hilohilo

Kulinganisha vifungu vya maandiko katika somo hilohilo itakusaidia kufahamu vema hilo somo. Itifaki ni kitabu cha orodha ya maneno katika Biblia na huonesha ni wapi yalipo ndani ya Biblia. Tumia itifaki kupata Injili zinazolihusu somo moja. Kwa mfano kama somo la kufunga limechaguliwa; utatafuta Maandiko yenye neno kufunga, funga au ufungaji na usome maandiko hayo ambayo yataelezea kuhusu mafungo. Hii itampatia mhubiri uelewa wa Biblia wa somo hilo na kumwonesha chanzo cha maneno ya kutumia awapo katika mimbari.

Linganisha jinsi Neno moja linavyotumika kwa Maandiko tofauti tofauti

Njia nzuri ya kufahamu maana ya neno ni kuona jinsi neno hilo limetumika katika mukitadha wa vifungu tofauti vya maandiko. Kutazama neno katika mukitadha wa vifungu mbalimbali vya maandiko itakusaidia kufahamu maana ya neno. Kwa mfano, angalia jinsi "Neno" linavyotumika katika Yohana 1:1 na 1:14 na utaelewa kwamba "Neno" ni kumhusu Yesu.

Mfano: Waefeso 1:22–23 wanaeleza kwamba kanisa ni mwili wa Kristo; na kwa kulinganisha aya hizi na I Wakorinto 12:13, tunaelewa kwamba "mwili" ni kuhusu "kanisa" katika aya zote mbili.

Unatakiwa kuhakikisha kuwa unalinganisha neno la lugha ileile ya asili katika msitari moja kwenda kwenye neno la lugha hiyohiyo ya asili katika msitari mwingine. Vilevile weka akilini mlinganisho wa Agano la Kale na Agano Jipya, lakini lazima ukumbuke kwamba unashughulika na lugha tofauti kwahiyo mlinganisho halisi wa neno la asili hautakuwa rahisi.

KANUNI YA SABA:HAKUNA MABISHANO KATIKA BIBILIA.

Neno la Mungu halina makosa, haliwezi kupingana lenyewe. Mahali kumeonekana ubishi, ukweli bado hauja patikana endelea kutafuta. Kuna ukamilifu na umoja usio vunjika kuanzia Mwanzo hadi Ufunuo. Wakati unapofasiri sehemu ya andiko, nilazima tujifunze mukitadha wake. Sio mistari tu kabla na baada yake, bali ni andiko kuanza Mwanzo hadi Ufunuo. Ufasiri wangu wa sehemu ya andiko lazima usiharibu huu umoja mkamilifu na upatanifu wa andiko. Acha andiko liwe mfasiri wake lenyewe. Kumbuka, tunategemea toka Roho wa Mungu kufahamu neno lake (Yoh. 16:13; I Wak. 2:6–14). Muombe Mungu akuonyeshe ukweli wake (Yak. 1:5).

Wakati wakuthibitisha fundisho moja kutoka kifungu, lazima kamwe usiondoe fundisho lolote la maandiko matakatifu mahali pake.

KANUNI YA NANE: VIFUNGU VINAWEZA KUWA NAVYOTE VIWILI MATUMIZI YA KARIBU NA YA MBALI

Matumizi ni huonyeshwa kwenye kifungu. Maandiko mara nyingi yana matumizi ya karibu na ya mbali. Kwa ajili ya ufasiri halali pamoja na matumizi ya karibu na ya mbali, lazima uwazi uruhusiwe na kitabu cha mukitadha wa kifungu ambacho ni Biblia nzima. Vifungu walioandikiwa Waisrael vya weza kuwa na maana yenye thamani kuwakilisha kanisa la leo.

Katika mukitadha wenyewe tunajaribu kufunua 1) Maana ya asili ya kifungu; wakati katika, 2) Matumizi binafisi tunatafuta kupata umuhimu katika kifungu kwa ajili yetu leo. Juhudi hizi mbili kwa pamoja hutengeneza mzunguko wa kufasiri unaoitwa vizibuo mzunguko"(Grant R. Osborne). Ingawa tukio lililo andikwa katika maandiko lilitokea wakati wa mwanzo katika historia iliopita, kanuni za vifungu vyake havina muda na uhusiano binafsi.

Uhusiano kati ya maana na mihitasari mhimu ni kazi ya vizibuo. Mhubiri lazima aulize jinsi mwandishi wa kiBibilia alivyo fikisha kweli za habari za Mungu za kifungu kama alikuwa anazielezea kwa kusanyiko la siku za leo.

SOMO LINALOVUTIA ni wakati mwanafunzi wa Biblia anaporithiana na kifungu moja kwa moja kwenye muundo wa hitimisho zetu wenyewe.

SOMO LILILO PUNGUZWA ni wakati mwanafunzi Biblia anaporithiana na hitimisho za wasomi wengine na kufanyia kazi kanuni zetu. Kwa msaada katika kutuondoa kutoka maana zetu za siku hizi na mazoea binafsi. Ni muhimu kwamba tuna rithiana na vifaa vya kiufafanuzi kwa uhakiki si kuiga mawazo ya wengine pasipo uhakiki.

KANUNI YA TISA: KANUNI ZA LUGHA LAZIMA ZISIPUZIWE.

Lugha zote sio mbaya. Kama jambo la hakika, kila lugha ni ya kipekee pamoja na nguvu zake na udhaifu. Ufafanuzi wa kipekee wa kila lugha unafanya somo lake kukamilika, lakini kitu cha kusisimua!Kiyunani na Kiebrania ni za tofauti mno kutoka lugha zetu za sasa. Sifa za lugha za kiBiblia lazima kujifunza na kufahamu hata kufasiri andiko ambalo limetafasiriwa katika lugha zetu.

MFANO: Kristo anajieleza kwa Maria Yoh. 19:26 anatoa sauti ya ukali katika Kiswahili: "Mwanamke, tazama mwanao!" Kama jambo la hakika, ni sauti ya kushusha heshima sana. Tunafasiri kifungu hiki sio katika mwanga wa jinsi ya kutoa sauti katika Kiswahili, bali ni jinsi ya kutoa sauti katika kiyunani kwa sababu hiyo ni asili na lugha ilio vuviwa ya kitabu cha Yohn na Kiebrania au kiaramu kwa sababu ya mukini hiyo ndio lugha ambayo Yesu aliizungumza katika kiebrania, "mwanamke" inasauti kinyume kuliko ilivyo katika kiingereza; ni utaratibu wa heshima kama vile "mama."

Kutafuta maana ya maneno kwenye dikishenari inaweza kumsaidia muhubiri kupata ufahamu bora wa maandiko. Agano la kale kiasili lilikuwa limeandikwa kwa kiebrania na Agano jipya kiasili lilikuwa limeandikwa kwa kiyunani. Kuna vitabu vya rejea kama vile Concordance na dictionary ya Biblia. Vitabu hivi hutoa maana ya maneno katika lugha za kinadharia. Matumizi ya kamusi ya lugha ya kawaida kama Webster vilevile inaweza kusaidia katika kufahamu maana ya maneno katika kifungu cha maandiko.

MFANO: Neno "mtumishi" katika Warumi 1:1 ni doulos katika lugha ya asili ya kiyunani na ina maanisha mtumishi wa upendo au mtu ajichaguliaye kwa hiari yake kuwa mtumishi. Paulo hakulazimishwa kuwa mtumishi wa Yesu, bali alichagua kuwa mtumishi wa Yesu kwasababu ya upendo wake mkuu kwa ajili ya kutafuta maana ya neno mtumishi itakusaidia kufahamu maana sahihi ya kifungu.

KANUNI YA KUMI:VIFAA VYWA REJEA NI VYOMBO VYENYE NGUVU BALI MATUMIZI YAKE LAZIMA YATAWALIWE NA KANUNI ZA KIHABARI

Kamusi

Kamusi ni kifaa cha msaada kwa ufahamu bora wa maana ya maneno.

Concordence

Concordence ni ya thamani kupata wapi maandiko yaliko. Concordances hutoa neno la lugha ya asili katika kiebrania au kiyunani. Concordance ni kifaa kizuri kuonyesha mahali pa maandiko juu ya somo hilohilo. Hii ita kusadia kuwa na ufahamu bora wa somo linalo jifunzwa Kumbuka Biblia ni upatano mkamilifu yenyewe kwa yenyewe. Matumizi ya maandiko mengine yata kusaidia kupata taswira ya kiBiblia juu ya kifungu au somo unalo jifunza.

Siku zote fikiria maana ya neno pamoja na mukitadha wa andiko. Sehemu nyingi za fafanuzi za concordence hutoa orodha za maana zinazo wezekana na matumizi ya neno. Baadhi ya wahubiri wata chukua uchaguzi ambao bora kuyatia pasipo kujali mukitadha. Hii sio vizibuo vizuri. Tumia vifaa vya rejea kama chanzo, lakini sio kama mamlaka ya mwisho.

Maoni ya weza

Maoni ya weza pia kufaa kukusaidia kufahamu maana ya vifungu vya Biblia. Haya ni maoni ya watu juu ya Biblia. Maoni hutoa habari za kihistoria na kweli zingine zinazo faa kufahamu Biblia.

Wange paswa wasifikirie kamwe kama hayashindwi au mamlaka ya mwisho. Watu wengi wanajaribu kuhitimishia mawazo yao na maoni juu a Biblia. Maoni mengi ni makosa kuhusu unabii wa wakati wa mwisho. Maoni mengi ya kupendeza yalikuwa yameandikwa zaidi ya miaka miamoja iliopita. Mungu anaeleza katika neno lake kwamba yeye atafunua kweli za wakati wa mwisho katika wakati wa mwisho. Vitabu hivi vilikuwa vimeandikwa kabla ya wakati wa Mungu kuangazia ukweli wa wakati wa mwisho kwahiyo wao wasingeweza kuwa sahihi.

Mipango ya Computer

Hii mipangilio ya computer inaweka kuwepo na vifaa vingi vya rejea kwenye ubonyezaji wa kitovu. Unaweza pia kuleta vifaa na maandiko kwenye maandishi yako kwa haraka.

KANUNI YA KUMI NA MOJA: Lazima tufundishwe na Roho mtakatifu

Yeye ni mwalimu mkuu (I Wak. 2:13–14). Jihadhari na maneno ambayo hufundishwa kwa hekima za watu. Maoni ya weza kufaa hasahasa kwa kujifunza siasa na historia, bali sio mbadala wa mafundisho ya Roho mtakatifu.

Roho atakufundisha (Yoh. 14:26; 16:13). Hii ni ahadi ya Mungu. Omba kwa ajili ya neno unalo jifunza. Mungu ni mwaminifu atakufunulia neno lake.

Tafakari neno la Mungu (Yoshua 1:8).

HITIMISHO KWENYE VIZIBUO:

Mhubiri anapaswa kuandika kwa kifupi kitu alichojifunza

Andika maana ya maneno mapya au yasiozoeleka

Kila mmoja atajenga utaratibu wake mwenyewe wa kujifunza maneno mapya. Baadhi ya maneno ya Biblia yanayo maana tofauti katika lugha ya asili zaidi ya maana yake ya leo. Njia mojawapo ni kuwa na daftari ndogo ya maneno mapya na ufafanuzi wa maneno ya Biblia; hii itakusaidia kukumbuka maelezo yake. Jinsi muhubiri anavyoelewa zaidi kuhusu Neno la Mungu ndivyo Mungu anavyoweza kumtumia awpo katika mimbari.

Andiko unazojiandikia katika daftari ziwe katika lugha rahisi, wazi na zenye lengo

Sio lazima uandike kitabu ili kuwa na andiko nzuri. Panga andiko zako kwa mada na masomo. Weka orodha ya aya muhimu za maandiko zinazohusiana na somo lako. Iwapo utatumia maandishi katika mimbari hayapaswi kuwa na kila kitu ulichojifunza. andiko za somo zinapaswa kuwa fupi fupi na zenye mpangilio. Katika darasa hili tutajifunza namna ya kuandaa ratiba rahisi ya somo la kutumia katika mimbari.

Andika wazo au kichwa cha somo mapema utakavyoweza

Kama hutaandika kitu mara unapokipokea unaweza usikikumbuke baadaye. Mungu anaweza akakuonyesha kitu ukiwa katika maombi au unapolisoma Neno; mambo haya yanapaswa kuandikwa na kuhifadhiwa ili uweze kujifunza au kuyatumia baadaye.

Unaweza kupata faida kwa kuitenganisha Injili katika mawazo yake

Njia nzuri ya kusoma Injili ni kuitenga katika mafungu yake muhimu kama ilivyoandikwa. Unaweza kuendelea kujifunza wazo kuu la kilichoandikwa peke yake. Lengo la mhubiri ni kushirikisha wengine sehemu moja ya ukweli au tukio kwa wakati mmoja. Kuigawa Injili katika vipande kutakusaidia kuhubiri sehemu moja ya Injili halafu ukaendelea na sehemu nyingine kisha ukaijenga yote kwa wakati. Kwa mfano Yohana 3:16 inaweza kutenganishwa katika mawazo yake makuu kama ifuatavyo:

Sehemu ya Injili Mada ya Kujifunza
Kwa jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu upendo kubwa wa Mungu—anawapenda wote
hata akamtoa Mwanaye wa pekee gharama kubwa ya wokovu wetu—msalaba
ili kila amwaminiye mahitaji makubwa—imani
asipotee kutoroka kubwa—kutotiwa hatiani
bali awe na uzima wa milele zawadi kubwa—mbinguni

Ukiangalia sehemu ya aya hii na ukajifunza utaielewa vizuri zaidi aya yote. Hii itakusaidia pia kuihubiri kwa kipande kimoja baada ya kingine. Utajifunza maana ya kushirikisha wengine sehemu kwa sehemu na kujenga hatua moja kwa wakati mmoja.

Kutoa Hotuba

Sehemu hii itaangalia mbinu mbalimbali za kutoa hotuba. Hatupendi sote tuingie katika mtego wa kutoa hotuba (kuongea kwa werevu wa kisomi), lakini kuna mbinu fulani ambazo mhubiri anaweza kujenga ili zimsaidie katika mahubiri ya Injili. Kuhubiri ni jambo la kuongea hadharani na Mungu huwapatia zawadi na vipaji wanadamu ambao anaweza kuwatumia kueneza Injili.

Mhubiri anapaswa Kujitegemea

Usijaribu kumuiga mhubiri mwingine

Usijaribu kuwa mtu tofauti. Baadhi ya watu hujaribu kuiga matendo na miondoko ya wahubiri wengine au hujaribu kuiga sauti ya mhubiri mashuhuri kwa kudhania kwamba kufanya hivyo watakuwa na Roho sahihi na yenye kuvutia. Hii siyo njia sahihi ya kulihubiri Neno la Mungu. Njia sahihi ya kuhubiri ni kuuacha tabia na mazoea wako uwe kwa Roho Mtakatifu.

Unapaswa kuonekana asilia katika mimbari

Usijaribu kulazimisha kitu kisichokuwa asilia kionekana. Usirushe mkono wako ili kuonekana ukifanya chochote. Acha mikono yako ifanye mambo yanayoonekana ya asili, ikiwa imelegea na siyo migumu au iliyolazimishwa. Mhubiri anaweza kupiga kelele na kuruka ruka kuhusu kinachohubiriwa na upako utampatia nguvu na mamlaka pia yatakuwepo katika sauti lakini tumia sauti yako binafsi kila mara uwapo katika mimbari. (Unahubiri Injili siyo kwamba unafanya maigizo.)

Mungu atautumia tabia na mazoea wako

Tabia na mazoea ya mhubiri utakuwa dhahiri katika mimbari. Mungu atakutumia kama ulivyo kulitangaza Neno lake.

Epuka Tabia za Kuchanganyikiwa ambazo zitakupotezea ule ujumbe

Tutajadili mambo machache yanayofanywa na watu wengi ambayo huharibu kitu kinachosemwa ili upate kujua ni nini cha kuepuka unapohubiri. Ziko tabia nyingine zinazofanana na hiyo ambazo hata wahubiri wazoefu hujikuta zikiwasumbua:

Usiweke mikono yako mifukoni mwako

Watu wengine hufanya kitu kabla hawajatulia kwa sababu hawajafahamu vizuri ni nini cha kufanya. Baadhi ya wahubiri huchezea sarafu mifukoni mwao au funguo wakati wakiwa wanahubiri. Tabia za namna hiyo huwa zinasumbua sana na zinaweza kukuzuia kupokea kile Mungu anachotaka ukifikishe katika mioyo ya watu.

Usichezee vidole vyako

Kitu kidogo kama kuchezea vidole vyako kinaweza kukuharibia sana mahubiri.

C. Usiseme aah… au umm… unapohama kutoka wazo moja kwenda wazo lingine

Watu wengine wanayo tabia ya kujaza mianya kama hiyo kwa kuingiza ndani miguno isiyoeleweka wakati wanapoongea. Tabia za namna hii zinaweza kukuchukua muda mrefu kuziondoa, lakini ni muhimu kujitahidi kuziacha kabisa unapokuwa katika mimbari. Siyo vibaya kupumzika kidogo wakati unapohubiri. Wakati mwingine mapumziko ya namna hiyo yanaweza kuwafanya watu watulie zaidi. Ni bora kupumzika kuliko kujaribu kujaza nafasi hiyo kwa maneno ambayo hayana maana na wala usiongeze chochote katika ujumbe uliokuwa nao.

Usitembee tembee kwa kasi wakati unapohubiri

Siyo vibaya kutembea na kwenda hatua chache wakati unapohubiri na wakati mwingine mhubiri anaweza kuteremka kutoka katika jukwaa na kuchanganyika na watu huku akiwa anahubiri. Kunayo tofauti hata hivyo kati ya kutembea kama kawaida na kutembea kwa kasi. Mnyama aliyefungiwa kwenye kisanduku atakimbia huku na huko kwa lengo la kwenda mahali popote. Miondoko inayofanana na simba aliyefungiwa kwenye kisanduku wakati ukiwa unahubiri itahamisha akili za watu katika mahubiri yako.

Kuwaangalia watu machoni ni jambo zuri katika utoaji wa hotuba

Usiangalie chini unapohubiri

Baadhi ya wahubiri huwa na ujumbe mzuri lakini watu wanapata shida kuupokea kwa sababu mhubiri anaangalia chini kila wakati anapokuwa akiongea. Ni muhimu sana kwa mhubiri kutoonekana akidodosa alichoandika kwenye kijidaftari chake wakati akihubiri. Taarifa za namna hiyo zinapaswa kutupiwa jicho kwa haraka mara moja moja wakati wa hotuba. Unaangalia andiko lako halafu unawaangalia watu na kuwahubiria. Andiko lako linapaswa kuwa fupi tu kwa ajili ya kukusaidia kukumbuka kitu ulichojifunza na kuongezea Maandiko kuupa nguvu ujumbe wa hotuba yako.

Angalia watu machoni unapohubiri

Kuhubiri ni kuwafikishia watu ujumbe wa kweli. Mtu anayefanya mawasiliano kwa njia nzuri huangalia watu machoni anapoongea nao. Kukiwepo na mkusanyiko mkubwa haitawezekana kuangalia kila mmoja machoni, lakini bado mhubiri anahitaji kuangalia watu wakati akihubiri. Kukutana kwa macho hufanya anayesikiliza aone kwamba unaongea naye!

Kauli sahihi ni Muhimu kwa ajili ya ujumbe kueleweka

Usitafune maneno wakati unapoongea

Ni vema ukaongea vizuri na kutamka kila neno ili watu waweze kuelewa kitu unachosema. Fanya mazoezi ya kutotafuna maneno katika mazungumzo yako ya kila siku; hii itakufanya uwe na tabia ya kuongea sawasawa. Vilevile hii itawaondolea watu usumbufu wa kugeukiana na kuulizana mara kwa mara, "Amesema nini?"

Ongea kwa sauti kubwa na ya kutosha ili watu wasikie kitu unachosema

Hata kama utatumia kipaza sauti na vifaa vya namna hiyo unapaswa kuongea kwa sauti ya kueleweka. Wasemaji wazuri huweka sauti yao sambamba na sehemu ya kati ya kisehemu cha kuongelea. Fanya mazoezi ya kuelekeza sauti yako na ruhusu hewa itoke ndani ya mapafu yako.

Hubiri kwa moyo

Watu wanahitaji kuamini kwamba wewe unaamini unachohubiri

Unajaribu kuwashawishi watu kuamini kwamba Neno la Mungu ni ukweli na wao wanalihitaji katika maisha yao. Inapaswa kusiwepo na shaka au maswali katika akili ya mhubiri anapolitoa hadharani Neno la Mungu. Kusanyiko litachukulia kusita kwako kwa uzito na kutomwamini mhubiri. Kama unayo mashaka au maswali unahitaji kufanya maombi mpaka upate uthibitisho wa Mungu moyoni mwako kuhusu Neno unalotegemea kuhubiri.

Hubiri kwa hisia na msukumo

Ni vizuri ukisisimka kuhusu unachohubiri. Yesu alikuja kutupatia uhai. Mhubiri anapaswa kuwa amejaa uhai wa Yesu.

Kutupa Mikono na Kusogea

Ni sawa kutumia mikono wakati unapohubiri. Unahubiri Neno ambalo liko hai; huhitaji kukauka na kuonekana kama uliyekufa uwapo katika mimbari. Kama ulikuwa unaelezea hadithi ya Daudi na Goliati, ni vema ukiamua kuuzungusha mkono wako juu ya kichwa chako kama unayetupa jiwe. Kurusha mikono kunaweza kukusaidia unapowahubiria watoto lakini ni muhimu pia kwa mahubiri ya watu wazima.

Kupeleka mkono huku au kule kunaweza kukakuongezea uwezo wako wa kufikisha ujumbe

Mzungumzaji mzuri huonesha kwa mikono yake wakati anapoongea. Lengo letu katika kuhubiri ni kumzidi mhamasishaji yeyote, ijapokuwa tunataka kutumia kila njia iwezekanayo kuupeleka ukweli wa Neno la Mungu kwa watu. Iache mikono yako ifanye kile kitakachoweka uzito katika ujumbe. Hupendi kurusha rusha mikono bila kuwa na lengo au sababu. Kwa watu wengine matumizi ya vitendo vya kuonesha kwa mikono wanapoongea ni jambo la kawaida kwao wakati kwa wengine itaonekana wanajilazimisha kuchora chora kwa mikono yao. Unalazimika kukumbuka kwamba wewe utaendelea kuwa wewe, lakini siyo vibaya kujieleza kwa kupeleka peleka mikono.

Kufanya matendo fulani kunaweza kukasaidia kuchora wazo lako

Unaweza kutumia matendo kuonesha unachoshirikisha watu wengine. Kwa mfano unaweza kushikilia juu ngao ya imani au ukafanya matendo kama unaye zungusha upanga kuweka picha ya upanga wa Roho akilini mwa watu. Unajaribu kuwashawishi watu kuhusu mahitaji yao na unawashirikisha ukweli huo; unaweza kutumia njia yeyote ile kuweka uzito katika wazo ulilo nalo. Usingependa matendo ya namna hiyo yazidi kiwango hadi yakuhamishe kutoka katika kinachosemwa, lakini ni vyema kutia uhai na nguvu katika somo.