Skip to main content

Wasifu wa mhubiri

Wasifu wa mhubiri

Kiwango cha uwezo wa mhubiri kinapimwa kwa akili, kwa maadili na kiroho. Mhubiri anapaswa kuwa amehitimu kiroho na anao upako wa kuhubiri. Mhubiri anapaswa kuwa amehitimu katika mafunzo yake ya Biblia. Mhubiri anapaswa pia kuwa msafi kimaadili na uwepo ushahidi wa Kikristo. Sasa tuangalie kwa makini wasifu bayana wa mhubiri.

Anapaswa kuwa Mkristo wa Kweli

Ili kumhubiri Kristo ni lazima umjue Kristo. Paulo alisali na kusema: ili niweze kumjua Yeye. Kama mhubiri unahitaji kumjua Kristo kama Mwokozi wako. Unalazimika kumjua Kristo ni nani ndio uweze kuwaeleza wengine Yeye ni nani. Ni wazi kwamba mhubiri ni lazima awe amezaliwa mara ya pili ingawa wengi siku hizi hata wale ambao bado hawajaokolewa hujiita wahubiri. Ni lazima uamini kabla ya kuwa mhubiri (II Wak. 4:13).

Charles Wesley, ndugu yake Yohana Wesley, alihubiri na kufundisha kwa miaka mingi kabla hajamkubali Kristo kama Mwokozi wake. Kama mdhambi, alianza masomo ya dini katika Kanisa ka Kristo huko Oxford mwaka 1726 lakini alipoteza nguvu zake nyingi akitafuta namna ya kujifurahisha. Alipata shahada yake ya uzamivu kwa kufaulu vizuri kama msomi mwaka 1733, na mwaka 1735 aliapishwa kuwa Mchungaji katika Kanisa la Anglikana. Mwaka 1738, Charles "alipata uamsho" aliokuwa anauhitaji sana. Mwishowe baada ya miaka 12 ya mafunzo marefu ya dini na hata mahubiri pia aliukubali ujumbe wa Agano Jipya kuhusu wokovu. Charles aliyekuwa hajapata matunda yoyote na wala hakuwa msaada katika miaka hiyo 12, baada ya kuokoka alikuwa sehemu muhimu ya uamsho mkubwa nchini Amerika na alifanya kazi pamoja na ndugu yake Yohana Wesley aliyekuwa mashuhuri sana. "Kazi yake kwa miaka iliyofuata iliweza kuandika nyimbo 6,500 kulieneza Agano Jipya kama alivyolielewa. Wakati alipofariki Machi 29, 1788 alijulikana kama mhubiri mwenye nguvu na hekima." ("Charles Wesley". 2005. http://www.bookrags.com/biography/charles-wesley)

Anapaswa kuwa na Wito

Kazi ya kuhubiri ni wito wa Mungu. Biblia inatueleza kwamba ni sharti mwanadamu atumwe ili akaihubiri Injili (Marko 3:14; War. 10:15). Ni Mungu ambaye hutuma. Mungu alimwita Yeremia kuwa Nabii kabla hata hajazaliwa. "Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa Nabii wa Mataifa" (Yeremia 1:5). Wito wa Mungu ni zaidi ya hisia na msisimko. Mungu wa mbinguni atauweka wito wake katika maisha ya mwanadamu akaihubiri Injili Yake.

Ni nini maana yake wito wa Mungu?

Ni ukubali wa ndani anaopewa mwanadamu na Roho Mtakatifu ambo huthibitishwa kwa Neno la Mungu na Mwili wa Kristo. Roho Mtakatifu ataongea na moyo wako. Paulo alizungumza kuhusu Roho Mtakatifu kushuhudia pamoja na dhamiri yake (Warumi 9:1). Mungu atawasha wito wake katika moyo wako. Neno la Mungu litaimarisha kukubali kwako. Mungu ataongea na wewe kwa Neno lake. Wakristo wengine waliojazwa Roho Mtakatifu watashuhudia wito wako. Roho Mtakatifu aliongea na kanisa la mwanzo kuwatenga Paulo na Barnaba kwa ajili ya kazi ambayo Mungu alikuwa amewaita waifanye (Matendo 13:1–3). Wito wa Mungu utathibitishwa kwa Mwili wa Kristo. Yakobo, Petro, na Yohana walitambua wito wa Mungu kwa maisha ya Paulo (Wagalatia 2:9).

Ni Mungu peke yake anaweza kumfanya mhubiri

Darasa hili halitakufanya uwe mhubiri. Darasa hili litakusaidia ujue namna ya kujifunza Biblia, kuandaa hotuba, na kuhubiri kile ulichojifunza. Vifaa hivi vyote havitakufanya uwe mhubiri. Mahubiri yenye maana siyo ya kuonyesha matukio tu na ukweli wa Neno la Mungu bali ni kazi ya Roho Mtakatifu kupitia katika chombo kilichoandaliwa.

Ni lazima awe Mwanafunzi wa Biblia

Ni lazima mhubiri ajue ni kitu gani anachohubiri. Ni lazima ulijue Neno kabla hujaanza kulihubiri Neno. Mtenda kazi atajifunza na kuelewa kazi ambayo anategemea kuifanya. Kwa mfano fundi magari atajifunza kuhusu magari, seremala atajufunza namna ya kufanya kazi kwa mbao, na mhubiri anapaswa kama yule mtenda kazi mwingine ajifunze Neno la Mungu ambalo anategemea kulihubiri.

Inabidi mhubiri ajenge tabia ya kujifunza Biblia kila siku. Iwapo mhubiri analishwa Neno la Mungu kila siku atakuwa na kianzio tajiri cha Mkate wa Maisha wa kuwalisha wengine. Mhubiri anapaswa kujiandaa kwa kujifunza andiko analotegemea kuhubiri kabla ya kuingia katika mimbari. Anapaswa kuwa na uelewa mzuri wa taarifa ya Injili ambayo itahubiriwa.

Ni lazima Awe Mtu wa Maombi

I Wathesalonike 5:17—Ombeni bila kukoma.

Waefeso 6:18—Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na mkidumu katika kuwaombea watakatifu wote;

Maombi ni ufunguo wa mafanikio ya mhubiri

Mafanikio ya mhubiri yanapimwa kwa Roho zinazookelewa na maisha ambayo yamebadilishwa kwa nguvu za Mungu, siyo kwa faida ya fedha au umashuhuri. Mhubiri anapaswa kuishi maisha ya maombi kama anategemea upendeleo wa Mungu uzifikie roho za wanadamu. Mhubiri ambaye hatajifunza kufanya maombi hatadumu katika kazi.

Utafundisha kwa kuwa mfano.

Watu unaowapatia mahubiri watakuona wewe kama mfano wao. Iwapo wataona kwamba mhubiri wao hathamini maombi basi na wao hawatafanya maombi pia.

Nguvu za Mungu huonekana kupitia katika maombi

Iwapo mhubiri atakuwa na nguvu za Mungu katika maisha yake ni lazima awe mtu wa maombi. Kama hakuna maombi hakutakuwepo nguvu, kama kuna kusali kidogo kutakuwepo na nguvu kidogo, na iwapo kuna kusali sana kutakuwepo na nguvu nyingi. Kila mtu wa Mungu aliyepewa nguvu na Mungu alikuwa ni mtu wa maombi. Hakuna njia fupi kwa Mungu. Iwapo unataka kuihubiri Injili kwa nguvu na mamlaka ni lazima usali na kusali na kusali.

Ni mtu Mnyoofu wa Maisha

Mhubiri anapawa kuishi maisha yaliyotengwa

Ni muhimu sana kwa mhubiri kuishi maisha yaliyo safi (II Wak. 6:17). Makuhani wa Agano la Kale waliwekwa wakfu kwa ajili ya kazi ya Bwana. Neno wakfu maana yake ni kutengwa au kuwekwa pembeni kwa ajili ya huduma ya Mungu. Mungu anahitaji mtu wa Mungu atenganishwe na dunia. Yesu alipakwa mafuta na Mungu juu yaw engine kwa sababu alikuwa myoofu wa Moyo na alichukia uovu (Waebrania 1:9). Moyo wa mhubiri unalazimika kuelekea mambo ya Mungu, na siyo mambo ya dunia. Nguvu ya Mungu huja katika maisha yaliyo safi.

Mhubiri anapaswa kuweka ushuhuda mzuri

Mh ubiri ambaye haishi kwa mfano wa Kimungu atashindwa kuwafanya wengine anaowahubiria waishi Kimungu. Neno la Mungu linatuambia kwamba sisi ni Nyaraka hai, husomwa na kujulikana kwa watu wote (II Wakorinto 3:2). Kwa mfano kama watu watamuona mhubiri wao akikasirika mara kwa mara na kuchukia hawatamsikiliza atakapowaambia wasikasirike. Watu hawatamuheshimu mtu ambaye haishi maisha yanayompendeza Mungu.

Anapaswa kuwa Tayari kwa Utumishi

Neno la Mungu linatuagiza kufanya kazi kwa uwezo wetu wote (Mhubiri 9:10), na hii ni pamoja na kuihubiri Injili. Mhubiri anapaswa kuishi kwa kuzingatia afya ili awe na nguvu kwa ajili ya huduma ya Mungu.

Mhubiri anapaswa kuwa na afya njema kwa ajili ya huduma

Ni muhimu kama mhubiri kujutunza mwenyewe. Unalazimika kujutahidi kula vizuri na kupata usingizi wa kutosha. Biblia inatuambia kwamba kuna faida katika kufanya mazoezi ya mwili. Ni vigumu kwa mhubiri wakati anahangaika, au anashindwa kupumua vizuri na anakosa pumzi wakati akijaribu kuhubiri. Inaweza kuwa vigumu pia kwa watu kupekea ujumbe wa mhubiri ambaye hushindwa kupumua mara kwa mara. Akili yako haitakuwa makini kama hutapata usingizi wa kutosha. Miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu. Mhubiri anapaswa kujitahidi kuutunza mwili wake.

Mhubiri anapaswa kuwa na akili timamu katika huduma

Hupaswi kuleta matatizo yako hadi katika mimbari. Watu watajisikia kwamba kama wewe umevunjika moyo na umelemewa.

  • Unapaswa kumpelekea mambo yako Yesu (I Petro 5:7)
  • Yesu ndiye anayebeba mizigo yetu (Mathayo 11:28)
  • Paulo alituonya tuache akili ya Kristo iwe ndani yetu (Wafilipi 2:5)

Mhubiri anapaswa kuwa na akili kama ya Kristo. Akili ya Kristo haina kukata tamaa, kuogopa, au kulemewa. Kuwa na mapumziko mazuri na chakula kutakufanya uwe na akili timamu kwa ajili ya huduma.