Skip to main content

Hatua za simulizi hadithi

Hatua za simulizi hadithi

Chagua hadithi

Hadithi ni magali popote. Waweza kusikia kwenye redio, kwa kusoma vitabu, na kusikia kwenye mazungumzo. Unaweza kupata hadithi kutoka kwenye matukio yaliotokea katika maisha yako. Kwa mazoezi katika darasa hili; unaweza kuchagua hadithi kutoka kwenye Biblia, lakini njia hizi unaweza kutumia katika hadithi yeyote. Kama unatafuta hadithi katika biblia, usitumie hadithi iliyozoeleka kama Daudi na Goliati au safina ya Nuhu. Kuna hadithi nyingi katika biblia ambayo watu kanisani hawjawahi kuzisikia. Hizi ni baadhi ya simulizi za hadithi kwenye Biblia, lakini zipo nyingi zinazoweza kupatikana:

  • Adamu na Eva
  • Kaini na Abeli
  • Gharika
  • Kuitwa kwa Ibrahim
  • Lutu kuepuka Sodoma na Gomora
  • Yakobo na Essau
  • Yusufu na ndugu zake
  • Ndama wa dhahabu
  • Yethro anamsaidia Musa
  • Kora
  • Baalam na punda
  • Joshua na Yeriko
  • Hukumu ya Ehudi
  • Debora na Baraka
  • Gidioni
  • Ahadi ya Yefta
  • Samsoni
  • Maisha ya Mfalme Sauli
  • Jinsi Daudi alivyo kutana na Abigaeli
  • Busara ya Sulemani
  • Ruthu
  • Yosia Mfalme kijana
  • Elia na manabii wa Baali
  • Naamani mkoma
  • Hekalu kujengwa tena
  • Esta
  • Yona katika Samaki
  • Kuzaliwa kwa Yesu
  • Yohana Mbatizaji
  • Majaribu ya Yesu
  • Kulisha watu elfu tano
  • Mwanamke kisimani
  • Msamaria mwema
  • Mtu aliye jenga nyumba yake juu ya mwamba
  • Mwana mpotevu
  • Tajiri na Lazaro
  • Utukufu wa Mungu
  • Lazaro anaishi tena
  • Yuda anamsaliti Yesu
  • Ufufuko wa Yesu
  • Siku ya Pentekoste
  • Kifo cha Stefano
  • Petro na Yohana wakamponya kiwete
  • Anania na Safira
  • Kubadilika kwa Paulo
  • Huduma ya Filipo
  • Petro na Kornelio
  • Paulo na Sila wanaimba gerezani
  • Onesmo na Filimoni

Hakikisha hadithi ni nzuri kwa wasikilizaji unao zungumza nayo. Hadithi katika Biblia zinafaa kwa watu wote, lakini baadhi zaweza zisiwe nzuri kwa watoto, kama vile Juda na Tamari.

Zoezi: Chagua hadithi kutoka kwenye Biblia ambayo unaweza kuisema darasani. Unaweza kutumia zilizo tajwa hapo juu, lakini pia waweza kuchagua nyingine tofauti.

Jaribu hadithi

Sasa ile hadithi uliyoichagua, unahitaji uilewe. Isome mara kadhaa ili kujua wahusika wakuu na mazingira yake. Baada ya kuhisi umeelewa wazo kuu la hadithi, waweza kumsimulia mtu yeyote kuhakikisha kuwa ni hadithi inayofurahisha na kujua sehemu muhimu katika hadithi. Si lazima kukaririsha kila sehemu na hutakiwi kuogopa wakati unatoa hadithi yako kwa wasikilizaji wako kwa wakati huu.

Zoezi: Chagua mtu yeyoye darasani na awaambie hadithi bila kuangalia kwenye Biblia. Hutakiwi kuwa na mashaka kuhusiana na habari zote, lakini jaribu kulenga kupata sehemu muhimu kwa usahihi wa hadithi. Bada ya kusema hadithi yako, sikiliza hadithi kwa marafiki zako.

##Ubunifu hadithi zinazo husiana na miguso ya siku hizi

Kama unaenda kusimulia hadithi ambayo imeunganisha na wasikilizaji, tena unataka kuhusisha na wahusika na hali zao. Chukua muda wa kukaa kimya, fumba macho yako, na fikiri kuhusu hadithi. Kuna hisia gani kifungu kinasema muhusika alivyo? ana hasira, huzuni, furaha, au kitu kingine? Biblia mara zote haisemi wazi hisia za mtu katika hadithi, lakini tunaweza kufikiri baadhi ya hisia zao kama sisi wenyewe tutafanya mazingira hayo. Kama hali hii ikitokea katika hadithi yako, utajisikiaje? kwa mfano, mzazi yeyote lazima ajisikie maumivu makubwa kama akipoteza mmoja wa watoto wake, kwa hiyo kama unasimulia hadithi ya Ayubu, hakikisha unahusisha huzuni hii katika uwasilishaji. Vitu vingi vinabadilishwa kwa tamaduni na hadithi, lakini misisimuko lazima ibaki palepale, na unaweza kutumia haya kufanya hadithi idumu miaka elfu mbili zaidi kukumbukwa, lakini hasira iliyo mshinda Daudi kuhusu mtu mmoja aliyemtania Mungu wake bado ni kitu tunacho kihisi hadi leo, kama imani yake Mungu hufanya kisicho wezekana. Jaribu kuchora mwenyewe katika mazingira ya hadithina ujibu maswli yafuatayo:

  • Unaona nini?
  • Uko mjini, mkulima, mfugaji, mtu wa baharini, au sehemu nyinginezo?
  • Una sifa gani za uvaaji?
  • Unaonekaneje?
  • Una harufu yeyote au sauti?
  • Una muda wa siku ngapi?
  • Una penda hali gani ya hewa
  • Kuna sifa yeyote ambayo unataka kuwa nayo ambazo sio muhimu kuzitaja katika hadithi, kama vile washirika wa kundi, watumishi, au wanafamilia?

Zoezi: Fumba macho yako na uifikiri mwenyewe hadithi. Waambie marafiki zako mnaona nini. Waache wenyewe wajiulize maswali wanaona nini.

Tafuta uwanja wa hadithi

Eneo la hadithi unayeweza kuweka hadithi hubadilika, hasa pale wahusika wanahama kwend sehemu nyingine. Wakati mwingine, uwanja mpya waweza kuwa katika eneo hilohilo, lakini kwa siku tofauti. Waweza kuangalia hadithi na kuiweka katika maeneo tofauti. Mara nyingine kutoa kwa maeneo tofauti husaidia hadithi. Kwa mfano, Ikulu ambalo Daudi alilipata mwenyewe alipokuwa anapiga kinubi chake kwa ajili ya Daudi ilikuwa ni tofauti sana kutoka eneo wanalokuuzia kondoo. Mara nyingine kipindi cha muda mrefu kinatokea katika maeneo ya hadithi. Jaribu kufikiri nini ingetikea kwa kipindi hicho.

Zoezi: Soma hadithi uliyoichagua na utafute maeneo tofauti na uiandike. Fikiri kuhusu vitu vinavyo weza kubadilika kati ya maeneo na kuiwekea alama yeyote ambayo itasaidia hadithi kuendelea.

Chagua mbinu ya kutoa hadithi

Hadithi inaweza kuzungumzwa kwa mwonekano tofauti.

Mtu wa kwanza

Hii ni wakati unatoa hadithi kama wewe ni mti wa hadithi. Utakuwa mhusika mkuu, lakini pia awepo kwenye hadithi. Uwe mbunifu kwa hili. Waweza kusimulia hadithi ya Yesu kupitia machoni pa Yuda, simulia hadithi ya Daudi kupitia machoni pa Sauli, au simulia hadithi ya safina ya Nuhu kama vile alikuwa ni moja ya wanyama.

Wakati unatoa hadithi kwa mtu wa kwanza, lazima ukumbuke kuwa msimuliaji, lazima uwe na maarifa ya kujua wahusika. Unatakiwa kujua vitu ambavyo mtu anayo yaona au kuyasikia.

Mtu wa tatu ajue yote

Hii ni wakati unasimulia hadithi kama mtu ambaye hakuwa katika hadithi. Wewe ni mhadithiaji anayejua yote kila mtu asemavyo au awazavyo. Kamwe usiwekewe kikomo kufuatilia mhusika mmoja, unaweza kujua sifa zote za wahusika wavyoendelea hata kama wapo sehemu tofauti. Katika hadithi ya Yusufu katika Mwanzo, mwandishi anatuambia yote mawili nni ilitokea katika Misri kwa Yusufu na ni kipi kitakacho tokea kanani katika familia yake.

Mtu wa tatu atakuwa na maarifa

Hii ni kama chagua la kwanza. Endelea kuongea kama mtu aliye nje ya hadithi, kumbe unamkaribia mtu kwa ukaribu zaidi. Unaweza kujizuia na mawazo ya watu tuu.

Zoezi: Chagua njia nzuri ya kutumia kusimulia hadithi yako. Ukitaka kujaribu kusimulia hadithi kwa njia tofauti kabla ya kuchagua moja. Hakikisha unapo chagua njia ambayo utaitumia ni kwa hadithi yote ili usije kuchanganya wasikilizaji.

Anzisha ukweli wa hadithi

Hadithi nyingi zina sababu ya kusimuliwa. Zinajaribu kuwasilisha ukweli fulani. Waweza usiuseme mara zote ukweli huu kwa wasikilizaji, lakini bado watakiwa kuuja. Huu ukweli utakusaidia kusistiza vyanzo fulani vya hadithi ambavyo vinahusisha ukweki.

Zoezi: Andika ukweli mkuu wa hadithi yako.

##Tafuta ndoana ya kumbukumbu

Unapo simulia hadithi, ni vizuri uwe na kitu fulani ambayo utakirudia mara nyingi kwenye hadithi ili kusaidia watu kukumbuka hadithi. Laweza kuwa neno, kifungu, au hata wimbo mfupi.

Angalia hadithi yako yote kama kuna kifungu fulani ambacho unaenda nacho na ukiwasilishe katika hadithi yote. Yaweza kuwa ni kifungu a\kinachoroka kwenye Biblia moja kwa moja. Pia waweza kuja kuja na wimbo rahisi ambayo wakilizaji wataweza kuimba pamoja na wewe.

Zoezi: Chagua ndoana ya kumbukumbu kuitumia katika hadithi yako na fanya mazoezi ya simulizi hadithi uliyo nayo.

Buni maneno yako ya kwanza

Huwezi kukaririrsha hadithi yote neno kwa neno. Kwamba itakupa ugumu wa kuisema haraka na unaweza kuifanya hadithi yako ionekane nzito. Lakini kuna sehemu mbili ambayo unatakiwa kuzijua sawasawa kuwa zinasemaje. Hizi ni mwanzoni na mwishoni.

Usicheleweshe muda kwa kuanza. Baadhi ya watu wanapenda kuzungumza kabla ya kuanza hadithi halisi, lakini vitu vichache vya kwanza waweza kuzungumza ili kuwapa wasikilizaji umakini. Kama ukipoteza umakini wa watu mwanzoni, itakuwa ni vigumu kuwarudisha kuwapata tena. Usianze kwa kusema, "Moja kwa moja" au "Nataka kuwaambia hadithi." Watu husikia maneno kama haya mara nyingi na siyo mapya na mazuri, na hayawapi watu umakini.

Zoezi: Pata muda kufikiri kuhusu namna ya kuanza hadithi yako kwa njia ambayo watu watakupa umakini. Kiandike ulichokifikiri. Kikariri na kiruhusu kukifanyia mazoezi kukisema.

Jua hadithi inaishia vipi

Watu wengi hawajui hadithi inaisha vipi. Kama wewe hufikirii kwa undani kuhusu hili, hautafanya vizuri. Mwisho lazima ufunge pamoja sehemu zote za hadithi usiwaache wasikilizaji wakushangae. Usiendeleze hadithi iwe ndefu sana.

Zoezi: Amua hadithi yako utaimaliza vipi.

Pitia ukweli

Kama hadithi yako inachukua nafasi kwa vipindi tofauti, tamaduni, au Nchi zaidi ya unayoishi sasaivi,ndipo kunaweza kuwa na vitu unavyo weza kujifunza kutafiti ambayo vitakusaidia wewe.

Zoezi: Fanya tafiti kadhaa kuhusu habari ya kitamaduni na kihistoria ya hadithi yako.

Ondoa habari zisizo hitajika

Si kila kitu lazima kiwepo kwenye hadithi yako. Mara nyingi isitumie Biblia katika habari, ukihusisha tarehe na baadhi ya majina ya wahusika, katika hadithi kama si muhimu. Baadhi ya watu wanapenda kutoa kila habari wakati wanasimulia hadithi, lakini waweza kujiuliza mwenyewe kuhusu kila sehemu, "Kama nikitoa hiki, hadithi bado yaweza kueleweka?" Kama jibu ni ndio, ndipo usihusishe sehemu ile katika hadithi yako.

Watu watakuwa na wakati mugumu kukumbuka mjina maalumu kama vile watu na mahali. Unaweza kutimia majina maalumu machache katika hadithi zako. Kuna sababu ambazo mara nyingi zinasemwa katika Biblia tuu "wanafunzi" Badala ya kutaja kila jina mojamoja. Ila tuu kama unasema mwanafunzi momja au kuna kitu maalumu tunaweza kuona majina yao maalumu.

Huhitaji kumwambia kila mtu historia ya maisha yako yoye, lakini waweza kumwambia kwa sehemu. Kuna sura nyingi katika Biblia ambazo zinazungumzia wahusika fulani kama vile Yusufu, Musa,na Yesu. Waweza kuchagua sehemu fulani ya maisha yao na ukazungumzia badala ya kwenda kuanza kuzaliwa na kufa kwa wahusika hawa.

Zoezi: Fikiri juu ya hadithi yako na angalia kama kuna sehemu yeyote au habari ambayo umeiacha itakayo fanya hadithi iwe nzuri.

Ongeza maelezo

Hadithi nzuri si lazima utaje vitendo na matukio, lakini iwafanye wasikilizaji wawe kama wapo katika sehemu ya hadithi. Waweza kuhusisha baadhi ya maelezo ya vitu (lakini iszidi) na pia ongeza baadhi za hisia kuleta hadithi katika maisha.

Zoezi: Tumia utafiti wa kihistoria na kiutamaduni ulioufanya na kufikiri kwako, ongeza baadhi ya maelezo kwa hadithi yako.

Pata msikilizaji wa mazoezi

Mara ya kwanza unapo simulia hadithi, haita kuwa nzuri sana. Kadiri unavyo zidi kusimulia hadithi ndivyo utakavyo kuaw mzuri. Hii ni kwanini tunafanyia mazoezi yetu mbele ya watu halisi.

Zoezi: Tafuta watu baadhi useme hadithi yako kwao. Waache wakuulize maswali baadae na kuongeza mawzo vitu gani vitaifanya iwe nzuri