Skip to main content

Kutoa Hotuba

Kutoa Hotuba

Sehemu hii itaangalia mbinu mbalimbali za kutoa hotuba. Hatupendi sote tuingie katika mtego wa kutoa hotuba (kuongea kwa werevu wa kisomi), lakini kuna mbinu fulani ambazo mhubiri anaweza kujenga ili zimsaidie katika mahubiri ya Injili. Kuhubiri ni jambo la kuongea hadharani na Mungu huwapatia zawadi na vipaji wanadamu ambao anaweza kuwatumia kueneza Injili.

Mhubiri anapaswa Kujitegemea

Usijaribu kumuiga mhubiri mwingine

Usijaribu kuwa mtu tofauti. Baadhi ya watu hujaribu kuiga matendo na miondoko ya wahubiri wengine au hujaribu kuiga sauti ya mhubiri mashuhuri kwa kudhania kwamba kufanya hivyo watakuwa na Roho sahihi na yenye kuvutia. Hii siyo njia sahihi ya kulihubiri Neno la Mungu. Njia sahihi ya kuhubiri ni kuuacha tabia na mazoea wako uwe kwa Roho Mtakatifu.

Unapaswa kuonekana asilia katika mimbari

Usijaribu kulazimisha kitu kisichokuwa asilia kionekana. Usirushe mkono wako ili kuonekana ukifanya chochote. Acha mikono yako ifanye mambo yanayoonekana ya asili, ikiwa imelegea na siyo migumu au iliyolazimishwa. Mhubiri anaweza kupiga kelele na kuruka ruka kuhusu kinachohubiriwa na upako utampatia nguvu na mamlaka pia yatakuwepo katika sauti lakini tumia sauti yako binafsi kila mara uwapo katika mimbari. (Unahubiri Injili siyo kwamba unafanya maigizo.)

Mungu atautumia tabia na mazoea wako

Tabia na mazoea ya mhubiri utakuwa dhahiri katika mimbari. Mungu atakutumia kama ulivyo kulitangaza Neno lake.

Epuka Tabia za Kuchanganyikiwa ambazo zitakupotezea ule ujumbe

Tutajadili mambo machache yanayofanywa na watu wengi ambayo huharibu kitu kinachosemwa ili upate kujua ni nini cha kuepuka unapohubiri. Ziko tabia nyingine zinazofanana na hiyo ambazo hata wahubiri wazoefu hujikuta zikiwasumbua:

Usiweke mikono yako mifukoni mwako

Watu wengine hufanya kitu kabla hawajatulia kwa sababu hawajafahamu vizuri ni nini cha kufanya. Baadhi ya wahubiri huchezea sarafu mifukoni mwao au funguo wakati wakiwa wanahubiri. Tabia za namna hiyo huwa zinasumbua sana na zinaweza kukuzuia kupokea kile Mungu anachotaka ukifikishe katika mioyo ya watu.

Usichezee vidole vyako

Kitu kidogo kama kuchezea vidole vyako kinaweza kukuharibia sana mahubiri.

C. Usiseme aah… au umm… unapohama kutoka wazo moja kwenda wazo lingine

Watu wengine wanayo tabia ya kujaza mianya kama hiyo kwa kuingiza ndani miguno isiyoeleweka wakati wanapoongea. Tabia za namna hii zinaweza kukuchukua muda mrefu kuziondoa, lakini ni muhimu kujitahidi kuziacha kabisa unapokuwa katika mimbari. Siyo vibaya kupumzika kidogo wakati unapohubiri. Wakati mwingine mapumziko ya namna hiyo yanaweza kuwafanya watu watulie zaidi. Ni bora kupumzika kuliko kujaribu kujaza nafasi hiyo kwa maneno ambayo hayana maana na wala usiongeze chochote katika ujumbe uliokuwa nao.

Usitembee tembee kwa kasi wakati unapohubiri

Siyo vibaya kutembea na kwenda hatua chache wakati unapohubiri na wakati mwingine mhubiri anaweza kuteremka kutoka katika jukwaa na kuchanganyika na watu huku akiwa anahubiri. Kunayo tofauti hata hivyo kati ya kutembea kama kawaida na kutembea kwa kasi. Mnyama aliyefungiwa kwenye kisanduku atakimbia huku na huko kwa lengo la kwenda mahali popote. Miondoko inayofanana na simba aliyefungiwa kwenye kisanduku wakati ukiwa unahubiri itahamisha akili za watu katika mahubiri yako.

Kuwaangalia watu machoni ni jambo zuri katika utoaji wa hotuba

Usiangalie chini unapohubiri

Baadhi ya wahubiri huwa na ujumbe mzuri lakini watu wanapata shida kuupokea kwa sababu mhubiri anaangalia chini kila wakati anapokuwa akiongea. Ni muhimu sana kwa mhubiri kutoonekana akidodosa alichoandika kwenye kijidaftari chake wakati akihubiri. Taarifa za namna hiyo zinapaswa kutupiwa jicho kwa haraka mara moja moja wakati wa hotuba. Unaangalia andiko lako halafu unawaangalia watu na kuwahubiria. Andiko lako linapaswa kuwa fupi tu kwa ajili ya kukusaidia kukumbuka kitu ulichojifunza na kuongezea Maandiko kuupa nguvu ujumbe wa hotuba yako.

Angalia watu machoni unapohubiri

Kuhubiri ni kuwafikishia watu ujumbe wa kweli. Mtu anayefanya mawasiliano kwa njia nzuri huangalia watu machoni anapoongea nao. Kukiwepo na mkusanyiko mkubwa haitawezekana kuangalia kila mmoja machoni, lakini bado mhubiri anahitaji kuangalia watu wakati akihubiri. Kukutana kwa macho hufanya anayesikiliza aone kwamba unaongea naye!

Kauli sahihi ni Muhimu kwa ajili ya ujumbe kueleweka

Usitafune maneno wakati unapoongea

Ni vema ukaongea vizuri na kutamka kila neno ili watu waweze kuelewa kitu unachosema. Fanya mazoezi ya kutotafuna maneno katika mazungumzo yako ya kila siku; hii itakufanya uwe na tabia ya kuongea sawasawa. Vilevile hii itawaondolea watu usumbufu wa kugeukiana na kuulizana mara kwa mara, "Amesema nini?"

Ongea kwa sauti kubwa na ya kutosha ili watu wasikie kitu unachosema

Hata kama utatumia kipaza sauti na vifaa vya namna hiyo unapaswa kuongea kwa sauti ya kueleweka. Wasemaji wazuri huweka sauti yao sambamba na sehemu ya kati ya kisehemu cha kuongelea. Fanya mazoezi ya kuelekeza sauti yako na ruhusu hewa itoke ndani ya mapafu yako.

Hubiri kwa moyo

Watu wanahitaji kuamini kwamba wewe unaamini unachohubiri

Unajaribu kuwashawishi watu kuamini kwamba Neno la Mungu ni ukweli na wao wanalihitaji katika maisha yao. Inapaswa kusiwepo na shaka au maswali katika akili ya mhubiri anapolitoa hadharani Neno la Mungu. Kusanyiko litachukulia kusita kwako kwa uzito na kutomwamini mhubiri. Kama unayo mashaka au maswali unahitaji kufanya maombi mpaka upate uthibitisho wa Mungu moyoni mwako kuhusu Neno unalotegemea kuhubiri.

Hubiri kwa hisia na msukumo

Ni vizuri ukisisimka kuhusu unachohubiri. Yesu alikuja kutupatia uhai. Mhubiri anapaswa kuwa amejaa uhai wa Yesu.

Kutupa Mikono na Kusogea

Ni sawa kutumia mikono wakati unapohubiri. Unahubiri Neno ambalo liko hai; huhitaji kukauka na kuonekana kama uliyekufa uwapo katika mimbari. Kama ulikuwa unaelezea hadithi ya Daudi na Goliati, ni vema ukiamua kuuzungusha mkono wako juu ya kichwa chako kama unayetupa jiwe. Kurusha mikono kunaweza kukusaidia unapowahubiria watoto lakini ni muhimu pia kwa mahubiri ya watu wazima.

Kupeleka mkono huku au kule kunaweza kukakuongezea uwezo wako wa kufikisha ujumbe

Mzungumzaji mzuri huonesha kwa mikono yake wakati anapoongea. Lengo letu katika kuhubiri ni kumzidi mhamasishaji yeyote, ijapokuwa tunataka kutumia kila njia iwezekanayo kuupeleka ukweli wa Neno la Mungu kwa watu. Iache mikono yako ifanye kile kitakachoweka uzito katika ujumbe. Hupendi kurusha rusha mikono bila kuwa na lengo au sababu. Kwa watu wengine matumizi ya vitendo vya kuonesha kwa mikono wanapoongea ni jambo la kawaida kwao wakati kwa wengine itaonekana wanajilazimisha kuchora chora kwa mikono yao. Unalazimika kukumbuka kwamba wewe utaendelea kuwa wewe, lakini siyo vibaya kujieleza kwa kupeleka peleka mikono.

Kufanya matendo fulani kunaweza kukasaidia kuchora wazo lako

Unaweza kutumia matendo kuonesha unachoshirikisha watu wengine. Kwa mfano unaweza kushikilia juu ngao ya imani au ukafanya matendo kama unaye zungusha upanga kuweka picha ya upanga wa Roho akilini mwa watu. Unajaribu kuwashawishi watu kuhusu mahitaji yao na unawashirikisha ukweli huo; unaweza kutumia njia yeyote ile kuweka uzito katika wazo ulilo nalo. Usingependa matendo ya namna hiyo yazidi kiwango hadi yakuhamishe kutoka katika kinachosemwa, lakini ni vyema kutia uhai na nguvu katika somo.