Skip to main content

Utangulizi

Utangulizi: Kuhubiri ni kufanya kitu gani?

Elimu ya mahubiri ni sanaa au sayansi ya majadiliano ya didini au kuhubiri. Katika darasa hili wanafunzi watapata msaada wa namna ya kuandaa hotuba na kuhubiri. Katika Biblia, tunaona mfano kwa mahubiri ya Kikristo. Ifuatayo ni orodha ya mambo ambayo tunajua kuhusu kuhubiri:

  1. Kufundisha na kuhubiri ni tofauti lakini nenda nayo vyote (Mat. 11:1)
  2. Yohana mpatizaji alihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya ondoleo la dhambi (Mark 1:4)
  3. Sababu kubwa kristo alikuja kuhubiri (Mar 1:38)
  4. Injili lazima ihubiriwe KILAMAHALI kwa KILA MTU pasipo udhuru (Marko 16:15; War. 1:15; II Cor. 10:16; Gal. 1:16; Ufu. 14:6; Mat. 10:7)
  5. Kristo lazima ahubiriwe (Mdo. 17:3; I Kor. 1:23; 2 Kor. 4:5; Waflp. 1:15–16)
  6. Kazi ya mhubiri na mzigo ni kuhubiri (I Kor. 9:16; Waef. 3:8)
  7. Injili ni ya kutolewa bure (I Kor. 9:18)
  8. Mhubiri huhubiri na kuacha matokeo na utukufu kwa Mungu (I Kor. 15:11)

Kuhubiri ni mawasiliano ya mazunguzmzo ya ukweli wa kimungu kwa lengo la kushawishi. Ufafanuzi huu unahusu njia tatu za kufanya mahubiri:

  1. Mambo ya Kuhubiri. "Ukweli wa Kimungu"—hutuambia nini cha kuhubiri
  2. Njia ya Kuhubiri. "mawasiliano ya mazunguzmzo"—hutuambia namma ya kuhubiri
  3. Malengo ya Kuhubiri. "kwa lengo la kushawishi"—hutuambia kwa nini tuhubiri

Mambo ya Kuhubiri

Kuhubiri ni kupeleka mbele ukweli (Gal. 1:8–9). Hii hutueleza ni nini tunachopaswa kuhubiri. Ukweli wa Kimungu unapaswa kuwa kiini cha mada ya somo. Katika msitari unaotangulia wa darasa hili (II Tim. 4:2), Paulo alimwambia Timoteo lihubiri Neno. Mhubiri anaitwa alitangaze Neno la Mungu. Neno la Mungu ndiyo mamlaka ya mwisho. Mhubiri anapaswa kujibu kila swali kwa kutumia Neno la Mungu; analazimika kutulia katika mamlaka kuu ya Maandiko. Kwa ufafanuzi mahubiri yanapaswa kuwa na ukomo katika:

  1. KUTANGAZA NA KUSIMAMIA NENO LA MUNGU
  2. KUFIKISHA UJUMBE TOKA KWA MUNGU KWA MWANDAMU
  3. KUHUBIRI KUNAWAHUSU VIUMBE WA MUNGU. Njia ya Wokovu ndio somo muhimu zaidi atakalofanya. Mwanadamu anahitaji kuwa na uhusiano na Mungu na siyo kuwa na uzito wa kidini au wa kifalsafa. Mhubiri atawaagiza waumini kuhusu wajibu wa Kikristo. Mhubiri anaitwa akaihubiri Injili ya Kristo, na siyo kufundisha fasihi au vitu ambavyo ni kinyume na masomo ya Biblia.
  4. MSINGI WA SOMO LA HOTUBA NI INJILI. Wakati mhubiri anapoongea kwa msisitizo, anapaswa kulipigia NENO LA MUNGU kelele. Upungufu wowote katika jambo hili haukubaliki kama mahubiri ya Kikristo.

Kiwango cha mafundisho ya Kikristo.

  • KUWA MAKINI—Usijaribu kuhubiri sana kwa wakati mmoja
  • KUWA SAHIHI—Inabidi uliweke somo katika wazo moja kuu
  • KUWA NA AKIBA—Unapaswa kubakiza cha kufundisha wakati unaofuata. Somo siyo lazima liwe la milele bali la Kimungu!

Mamlaka ya Mahubiri ya Kikristo

Unawakabidhi wanadamu Neno la Mungu na siyo taarifa ya kwenye gazeti. Hubiri kutokana na matokeo ya msukumo wa ushuhuda wa Kimungu wa Injili. Kuamini bila shaka yeyote msukumo wa Neno la Mungu ni muhimu kwa ajili ya kuukubali ukweli wake. Tunahubiri tunachohubiri kwa sababu ni sahihi na tunafahamu kwamba ni sahihi kwa sababu ni Mungu aliyesema hivyo. Iwapo msingi wako ni Shajara ya mwaka au Ensaiklopidia, ujumbe wako hata kama utakuwa na maelezo mazuri utakosa mamlaka. Msukumo wa Neno la Mungu katika Biblia ndio unaoyapa mahubiri ya Kikristo mamlaka yake.

Mamlaka ya mhubiri yanapatikana katika mamlaka ya Neno la Mungu. Mhubiri ni lazima aelewe kwamba Biblia siyo maneno ya wanadamu bali ni Neno la Mungu lenye nguvu. Neno lenye nguvu maana yake Mungu amelivuvia. Mungu aliwawezesha waandishi wa Biblia; ndio kusema kwamba, Mungu alipumua kupitia watu hao Neno la uhai. Biblia Haijahusisha Neno la Mungu peke yake bali ni Neno la Mungu.

Neno la Mungu lina nguvu za kuweza kubalisha maisha ya wanadamu na Neno la mahubiri linahitajika ili kupata mabadiliko hayo (War. 1:16). Mawazo ya mwanadamu hayatabadilisha maisha. Ni sharti muhubiri atumie Neno la Mungu kama msingi wa hotuba yake. Upo uhai katika Neno la Mungu.

LIJUE NENO!

Ni lazima ujifunze Neno la Mungu kwa sababu unapaswa kuelewa taarifa inayoenda kuhubiriwa (2 Tim. 2:15). Uelewa wa taarifa hiyo utampatia mhubiri mamlaka wakati wa kutoa ujumbe. Iwapo huna uhakika na unachosema au hujiamini katika uelewa wako wa ujumbe huo, uoneshaji wako wa somo utakuwa dhaifu. Kama huna uhakika kuhusu unachozungumzia watu hawatapokea ujumbe unaojaribu kuwahubiria.

Njia ya Kuhubiri

Njia ya kuhubiri ni "mawasiliano ya mazunguzmzo." Njia ya kuhubiri inatuambia namna ya kuhubiri. Mawasiliano yanahusu kuwaeleza watu wazo. Ni lazima wazo hilo lieleweke kwa watu ndio mawasiliano yaweze kufanyika. Mahitaji ya lazima kwa mawasiliano ni maneno sahihi na kauli zilizo wazi. Mhubiri anapaswa kuongea kwa njia ambayo watu wataelewa. Tuangalie mfano wa Nehemia katika Nehemia 8:8: "Nao wakasoma katika kitabu, katika torati ya Mungu kwa sauti ya kusikilika; wakaeleza maana yake, hata wakayafahamu yaliyosomwa." Neno la Mungu lilisomwa kwa usahihi au uwazi, likaelezwa kwa wale watu au wakawapa busara na watu hao wakafundishwa Neno na wakalielewa.

Ni vizuri mhubiri akihubiri na, akimaliza hotuba waumini watatawanyika wakisema, "mhubiri alisema hivi..."
—Martin Luther

Kazi nzuri na yenye nguvu ya mahubiri inahitaji:

  • Upako wa Roho Mtakatifu (I Yoh. 2:20)
  • Lugha iwe wazi na ya kawaida (Wahubiri wenye uwezo mkubwa kama D. L. Moody waliongea katika lugha ya mtu wa kawaida.)
  • ya kusisimua (sema unachomaanisha, na maanisha unachosema.)

Ushawishi unawezekana kutokana na uwezo mkubwa. Mwishowe uwezo wa mhubiri ni matokeo ya uweza wa Roho Mtakatifu. Uweza wa Roho Mtakatifu utamfanya mhubiri afundishe kwa hisia. Hubiri kama unayekwenda kinyume na majeshi yote ya motoni kama Daudi alivyopiga kelele katika ule mwamba, "hakuna kiini cha tatizo!" mhubiri anapaswa kuridhika na usahihi na nguvu za ujumbe wake ili kupata mafanikio. Fuata uongozi wa Roho Mtakatifu kwa sababu atakuelekeza vema na kutii uweza wake kwa sababu katika kukubali nguvu za Mungu zitaonekana wazi.

Waumini wanapaswa kushirikishwa katika mchakato mzima wa hotuba.

Akilini mwako waweke waumini wakati ukiandaa hotuba

Wafikirie na kuwaombea watu unaotegemea kuwapatia mahubiri. Mahubiri yenye manufaa yanamtaka mhubiri awe ni mtu anayejali na asiyekuwa mgumu wa moyo. Kuwakaribia baadhi ya watu kwa njia za uhakika huweza "kuwaweka kando". Mruhusu Roho Mtakatifu akuongoze katika maandalizi yako ya somo ili watu ambao watasikia wahisi nguvu za Mungu na kulipa nafasi somo lako. Mungu anafahamu ni akina nani watakaohudhuria na akili zao zitakuwaje na wewe pia unaweza kuona na kujifunza kitu kutokana na hali iliyopo mahali unapotoa mahubiri. Hata kama utakuwa unaongea katika ibada ya vijana wadogo, darasa la shule ya Jumapili, katika ibada ya watu wazima, katika kona ya barabara au katika hema lenye kikao cha wanauamsho; utulivu na hali ya hewa kwa ujumla ni lazima uvitilie maanani. Kwa kifupi, mhubiri ni mwanafunzi wa ubinadamu. "Mheshimiwa, siyo mambo ya kuhusu vitabu, ni wanadamu ndio tunaopaswa kuwaelewa"—Patrick Henry

Uweke waumini akilini mwako wakati unapoonesha

Utajifunza kufahamu kama wanalipokea Neno. Unaweza kuongeza mifano mingi zaidi na kuweka uzito kama watu wanaonekana kutoolewa ujumbe. Heshimu muda uliopewa.

Hotuba inapaswa kuwa ya kawaida, inayoweza kurudiwa na yenye maelezo makini

Njia ya kawaida hutumia Maandiko kama msingi wake kwa Neno la Mungu ni sahihi na halijatenganishwa na mahitaji ya wanadamu

Itaonekana ni jambo la kigeni (kwa usahihi kabisa) kwa waumini wa Kikristo kama Mchungaji wao atasimama na kutoa taarifa yake katika Kitabu cha Uchambuzi wa Msomaji (Reader's Digest). Pili, somo linapaswa kuwa linalozoeleka. Maneno yake na maana zake ziwe rahisi kueleweka. Michoro ya matukio ya kila siku inaweza kusaidia kuwafanya watu waioanishe na somo. Yesu aliweza kutumia vizuri kile ambacho kilikuwa kimezoeleka (Kondoo, kilimo n. k.) kwa mifano wa kile ambacho hawajakizoea (Ufalme wa Mbinguni). Mifano rahisi ya Maandiko haitawafanya washindwe kuelewa lakini, uhakikishe kwamba ni ukweli na unahusika.

Njia ya marudio ni tangazo rasmi la Neno

Mpango na ratiba nzuri itahakikisha kwamba wasikilizaji wako wataweza kufuata unachohubiri. Umoja na utulivu unapaswa kujibiwa kwa mahubiri mazuri yenye hisia ya Neno la Mungu. Umbile pekee yake halitoshi lakini ni mwanzo mzuri. Kurudia kinachofahamika ni mbinu inayomsaidia mhubiri lakini kuonyesha hisia na upako kutaamua uwezo wako wa kushawishi.

Matumizi ya matukio yanayoeleweka huonesha vizuri ukweli wa Neno la Mungu

Linganisha Injili na Injili nyingine na tasfiri kila taarifa kwa kutumia maandishi yake. Neno la Mungu ni Mamlaka ya Mwisho na kiwango cha kanuni za maisha. Wasiliana kwa busara na kwa njia iliyo wazi. Wewe unahitaji kuonekana una akili nzuri kwa sababu watu wanahitaji kuwa na uwezo wa kukufuata wakati unapohubiri. Waoneshe ukweli kwa njia rahisi na inayoelezeka. Washirikishe wasikilizaji wako ukweli hatua kwa hatua na jenga ujumbe huo kwa mpangilio kama somo linavyoendelea.

Malengo ya Kuhubiri

Ujumbe unatueleza sababu za kuhubiri. Somo limepangwa kwa mtazamo wa kushawishi. Kuhubiri kwa hakika siyo kuongea tu kuhusu Biblia, bali ni kupata uamuzi mioyoni mwa wanadamu. Lengo la kuhubiri ni malezi na maisha ya mabadiliko (Wakol. 1:28; Luka 4:18; 9:60; Mdo. 5:42; 10:42; 14:15; 15:21; War. 15:20). Malengo ambayo muhubiri anaweka mbele yake ni kama ifuatavyo:

Wokovu wa Roho za Watu

Wokovu wa Roho za watu ni moja ya malengo muhimu ya mahubiri. Mahubiri ni njia aliyochagua Mungu ya kuifikia mioyo ya wanadamu. Mungu amechagua kumtumia mwanadamu kumfikishia ujumbe wa Neno lake mwanadamu. Watenda dhambi hawatamuona Mungu kwa hekima ya mwanadamu, bali kwa kupitia mahubiri ya ujumbe wa Neno lake. Mungu alichagua upuzi wa kuhubiri kuokoa waliopotea (I Kor. 1:21).

Kukua Kiroho

Mungu alilipa Kanisa Wachungaji kwa lengo mahsusi la kukamilisha upatikanaji wa watakatifu (Efe. 4:11–14). Ni wajibu wa mchungaji kuwalisha kondoo kwa Neno la Mungu (Yoh. 21:15–17).

Kuzaliwa Imani

Kwa kuhubiri Neno la Mungu, mbegu za imani zinaweza kuoteshwa katika mioyo ya watu kwa kuponya na mahitaji mengine (War. 10:17). Mungu huhitaji imani (Ebr. 11:6) kuonekana kwa kila mmoja na wajibu wa mhubiri ni kuwafanya watu waliamini Neno la Mungu.

Liagize Kanisa

Wape Moyo Waumini

Mchungaji mwaminifu wa Injili hubeba mzigo ili kila aliyeusikia ujumbe wake apate moyo na msaada. Wakati wa mahubiri, mhubiri anawafikia watu hadi wa chini kabisa kwa nguvu za Roho Mtakatifu ambapo kwa njia yoyote ile mtu atapata msaada wa kumnyanyua na kumuondoa katika shimo la kutisha.

Unapaswa kuwa mwelekevu na mwenye kutia moyo ukiwa katika mimbari. Hata kukemea kunaweza kuhubiriwa kwa njia ya kuelekeza. Kumbuka kwamba unajaribu kunyanyua maisha ya watu na siyo kuwahamisha katika jamii yao. Iwapo utawahamisha kutoka katika mazoea ni kwa lengo la kuwajenga upya. Usimalizie somo lako kwa njia ambayo siyo endelevu bali elekeza njia rahisi. Dakitari akishatambua ugonjwa, haondoki akaondoka nyumbani bali hufuatia kwa dawa.

Waebrania 4:12—Maana neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

Wafanye Waumini wafikie Uamuzi

Usiridhike kama muhubiri kwa kuwapa watu moyo peke yake. Iwapo wasikilizaji hawatafikishwa katika hatua ya kufanya uamuzi, wataondoka kwa njia ile ile waliyokuja nayo. Siyo wajibu wa muhubiri na hawezi kuwalazimisha watu kuwa watii, lakini anaweza kuwaongoza moja kwa moja katika mahubiri yake hadi kwenye kisima na kuwatangazia kwa ushupavu kwa mamlaka ya Roho Mtakatifu, "Kunywa! Hiki ndicho kitu unachohitaji! Njoo kwa Kristo!" Muhubiri anapaswa kufanya kazi kwa kulenga "wito wa madhabahu" anapohubiri kwa sababu hapo ndipo kila mtu atapelekwa na kufikishwa katika hatua ya kuamua na ndipo wanalazimika kukubali au kuukataa ujumbe.