Skip to main content

Umuhimu wa Kuhubiri kwa Nguvu za Roho Mtakatifu

Umuhimu wa Kuhubiri kwa Nguvu za Roho Mtakatifu

Popote na chochote tunacho hubiri lazima tuvuviwe na Roho Mtakatifu (Mdo. 16:6-10; I Kor. 1:17; II Kor. 2:12; Gal. 2:2; Yona 3:2; Isa. 61:1).

Mhubiri ni lazima ajazwe nguvu za Roho Mtakatifu

Mhubiri anahitaji kujazwa Roho Mtakatifu ili kuhubiri kwa nguvu. Mhubiri hawezi kulitoa Neno kwa nguvu na mamlaka bila msaada wa Roho wa Mungu.

Wafuasi wa kwanza wa kanisa waliambiwa na Yesu wasubiri katika mji wa Yerusalemu mpaka watakapopewa nguvu na Roho Mtakatifu (Mdo. 1:8; Luka 24:49). Baada ya Yesu kumwaga damu Yake msalabani kununua wokovu wa Mwanadamu, alipaa mbinguni na kuiacha kazi ya kuieneza Injili mikononi mwa mwanadamu. Yesu alifahamu kwamba mwanadamu hawezi kuhubiri Injili na kuzifikia Roho za watu zilizopotea bila kuwa na nguvu za Roho Mtakatifu. Aliwaambia wafuasi wake Roho Mtakatifu atawapatia nguvu ya kuieneza Injili kwa mataifa yote. Hakuna uhai wala nguvu katika maneno ya mhubiri bila upako wa Roho Mtakatifu.

Mhubiri ni cheche tu ya anachoweza kuwa bila upatanisho na Roho Mtakatifu

Mhubiri asiyekuwa na upatanisho ni karibu na kitu kisichokuwa na thamani. Wako wahubiri ambao wamekaukiwa na ni sawa na wafu kwa mafanikio yao kidogo au kushindwa kabisa kwa sababu ya kutokuwa na upatanisho na Roho Mtakatifu. Mbaya zaidi kuliko "kuwa na mafanikio kidogo" ni mizigo iliyooteshwa ndani ya maisha ya watu kwa unajisi wa wahubiri hao wanaoongozwa na matakwa yao wenyewe. Mhubiri anahitaji kujazwa na kuongozwa na Roho Mtakatifu.

Hakuna kilichombadala wa nguvu za Mungu katika maisha ya mhubiri

II Kor. 3:6—Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.

Kujifunza na kujiandaa bila kupakwa mafuta na Roho Mtakatifu hakutakamilisha kazi ya mhubiri katika madhabahu. Neno andiko katika andiko linamaanisha andishi la sheria bila kuwa na Roho wa Mungu. Neno peke yake bila Roho Mtakatifu halitakuwa na uhai. Lengo la darasa hili ni kuonesha umuhimu wa kujifunza na kufanya maandalizi pamoja na kupakwa mafuta na Roho Mtakatifu.

Mwanadamu hana uwezo wa kwake binafsi wa kuihubiri Injili

I Petro 4:11—Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina.

Mungu alikusudia mahubiri ya Injili yafanyike kwa nguvu.

I Yoh. 2:20—Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote.

Neno mmepakwa katika aya hii inahusu kupataniswa na Mungu. Neno hilo lina maana ya kile kinachotumiwa kufanya upako. Mito ya uhai inayomwagika kutoka kwa mhubiri itawafikia wanadamu wenye kuhitaji. Neno kupakwa maana yake ni kuloanisha. Kwa lugha ya asili ya Kiyunani; linaelezea kuenea kiasi cha kutosha kwa uwepo wa Mungu kunakomsaidia mwanadamu kuhubiri kwa nguvu na mamlaka.

Mungu huwapa uwezo wa kuhubiri wale anaowaita kuwa wahubiri wa Injili

Uwezo asilia peke yake hautoshi kuifikia mioyo ya wanadamu. Mbinu za kuongea na kupamba maneno hazitazaa uhai. Mhubiri anapaswa kuwa na upatanisho na Mungu ndipo aweze kutangaza Neno la Mungu.

Mtume Paulo alipewa nguvu na Roho Mtakatifu

Paulo alihubiri kwa nguvu za Mungu (I Kor: 2:4–5). Neno linatuambia kwamba nguvu hizo zilidhihirika wazi wazi. Kudhihirika ni kwa kitu kinachoonekana. Dunia inahitaji kuoneshwa zoezi la nguvu za Mungu. Paulo hakutegemea hekima ya mwanadamu kulihubiri neno la Mungu. Paulo alikuwa ni mtu mwenye elimu. Alikuwa ni Mfarisayo aliyefundishwa sheria ya Musa na Gamalieli ambaye alikuwa daktari wa sheria (Mdo. 5:34; 22:3). Hata hivyo Paulo pamoja na mafunzo aliyokuwa nayo alizihitaji nguvu za Roho Mtakatifu katika kazi ya kuhubiri Injili.

Upako wa Roho Mtakatifu: Maneno haya yana maana gani?

Mafuta ni alama ya Roho Mtakatifu

Katika Maandiko Matakatifu mafuta ni alama ya Roho Mtakatifu. Mafuta anayomiminiwa mtu ni alama ya Roho Mtakatifu anayemiminwa katika maisha ya mtu huyo.

Neno hili linahusu nguvu za Roho Mtakatifu zinazokuja juu yake na kuenea katika nafsi yake

Yesu alisema Roho Mtakatifu atamwagika kutoka ndani yake mwanadamu kama mito ya maji yenye uhai (Yoh. 7:38-39). Katika Agano Jipya kupakwa mafuta kunatumika kuonesha uhusiano wake na mahubiri ya Injili. Kupakwa mafuta ni kupewa nguvu za Mungu ili kumwezesha mwanadamu afundishe kwa nguvu na mamlaka.

Katika Agano la kale wafalme walipewa mamlaka yao kwa kupakwa mafuta

Wafalme walipakwa mafuta na manabii wa Mungu. Hii ilikuwa ni ishara kwamba wamepewa mamlaka na Mungu na kutengwa kwa ajili ya huduma yake. Mpango wa Mungu kwa wafalme hawa ni kuwapatia Roho Mtakatifu katika maisha yao. Baadhi ya wafalme hao hawakumtumikia Mungu kwa hiyo Roho Mtakatifu hakuwa pamoja nao.

Katika Agano la Kale manabii walipakwa mafuta

Katika I Wafalme 19:16 Elisha anaagizwa na Mungu ampake mafuta Yehu awe Mfalme naye Elisha apakwe mafuta ili awe Nabii mahali pake. Mafuta haya yalimwagwa juu ya Manabii kama alama ya Roho Mtakatifu akiwa amemwagwa katika maisha yao. Manabii waliongea kama kipaza sauti cha Mungu. Mungu aliongea kwa midomo ya Manabii; hawakusema mawazo yao wenyewe walipotabiri ila walifanya hivyo Mungu alipozungumza kupitia kwao. Biblia inatumia maneno: "Neno la Bwana," katika kuelezea Mungu alivyofikisha ujumbe kwa kuwatumia Manabii wake (Yeremia 44:24).

Katika Agano la kale Makuhani walipakwa mafuta

Makuhani hawa walipaswa kuwa Watakatifu katika Bwana. Walipakwa mafuta pia (Hes. 3:3). Hii inatuonesha kwamba wale ambao wanafanya kazi ya Bwana wanapaswa kumwagiwa Roho Mtakatifu.

Mungu alimpaka mafuta Yesu ndipo akaifundishe Injili

Luka 4:18, 19—Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru walioteswa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.

Waebrania 1:9—Umependa haki, umechukia maasi; kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, mafuta ya shangwe kupita wenzio.

Matendo 10:38—habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.

Mwana wa Mungu alipewa nguvu na Roho Mtakatifu kuihubiri Injili. Tunahitaji kuongezewa kupakwa mafuta kiasi gani ili tukaihubiri Injili?

Yesu aliongea kwa mamlaka (Mat. 7:29). Mungu hutoa mamlaka kwa mhubiri kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

Kupakwa mafuta huvunja vifungo vya dhambi

Kupakwa mafuta huharibu vikwazo vya kifungo (Isa. 10:27; 61:1). Watu wamefungwa kwa dhambi na ni nguvu ya Mungu peke yake inayoweza kuwaweka huru. Yesu alisema kupakwa mafuta kutawaletea mateka uhuru. Watu wengi wamefungwa kwa nguvu za shetani na kuwekwa katika gereza la dhambi. Neno la Mungu likihubiriwa na mpakwa mafuta na Roho Mtakatifu litavunja minyororo ya vifungo na kuwaweka watenda dhambi huru na nguvu za shetani.

Nguvu za Roho Mtakatifu huwepo wanapokusanyika waumini

Roho Mtakatifu anao uwezo wa kuvunja nguvu za dhambi wakati mhubiri anakihubiri. Kuhubiri hakuwezi peke yake kuvunja nguvu za dhambi. Upako wa Roho Mtakatifu ndio utakaovunja nguvu za dhambi katika maisha ya wanadamu. Upako ni zaidi ya nguvu za Mungu katika kumsadia mhubiri na ni nguvu za Mungu katika kulisaidia kusanyiko.

Roho Mtakatifu huleta ondoleo la dhambi

Roho Mtakatifu atawashawishi wanadamu wakubali dhambi zao kisha atawasogeza katika msalaba (Yoh. 16:8). Mahubiri ya mpakwa mafuta yataleta ondoleo la dhambi. Mwanadamu anaweza kulihubiri Neno, lakini ni Roho Mtakatifu peke yake anayeweza kuwafanya wanadamu watambue dhambi zao na kuwapeleka kwa Mungu.