Skip to main content

KANUNI YA SITA

KANUNI YA SITA:SIKU ZOTE LINGANISHA MAANDIKO KWA MAANDIKO

Andiko siku zote hushikilia ufasiri wake lenyewe (II Pet. 1:20). Neno, maelezo, au wazo lazima lijifunzwe katika kitabu ambacho ndio limeandikwa, na kisha katika matumizi yake katika vifungu vingine. Endapo kifungu hakita kuwa wazi juu ya ukweli, hakuna hitimisho litakalo patikana kutokana nacho mpaka vifungu vyote vinavyo husiana vimejifunzwa. Maelezo ya mafundisho ya Kibiblia hayapaswi kufanywa kimsingi kwenye kifungu pekee, bali maelezo ya mafundisho lazima yapitie kile maandiko yote yanasema juu ya mada.

Andiko lita jieleza lenyewe kama mistari ya Biblia imelinganishwa yenyewe kwa yenyewe. Njia moja ya ufasiri sahihi ni kulinganisha mistari katika Biblia na mistari mingi tofauti ya Biblia. Biblia inatuagiza kulinganisha vitu vya kiroho kwa mambo ya rohoni (I Wak. 2:13). Kwa kulinganisha andiko kwa andiko Biblia itaeleweka vema. Neno la Mungu litakaa pamoja kama sehemu za fumbo au mkanganyiko. Andiko moja litafasiri andiko lingine. Biblia yenyewe iko katika umoja kamili. Hakuna mapingamano katika Biblia. Kile Mungu alicho andika katika Mwanzo kitakubaliana na kile Mungu alicho andika katika Ufunuo.

Linganisha vifungu vya maandiko kwenye somo hilohilo

Kulinganisha vifungu vya maandiko katika somo hilohilo itakusaidia kufahamu vema hilo somo. Itifaki ni kitabu cha orodha ya maneno katika Biblia na huonesha ni wapi yalipo ndani ya Biblia. Tumia itifaki kupata Injili zinazolihusu somo moja. Kwa mfano kama somo la kufunga limechaguliwa; utatafuta Maandiko yenye neno kufunga, funga au ufungaji na usome maandiko hayo ambayo yataelezea kuhusu mafungo. Hii itampatia mhubiri uelewa wa Biblia wa somo hilo na kumwonesha chanzo cha maneno ya kutumia awapo katika mimbari.

Linganisha jinsi Neno moja linavyotumika kwa Maandiko tofauti tofauti

Njia nzuri ya kufahamu maana ya neno ni kuona jinsi neno hilo limetumika katika mukitadha wa vifungu tofauti vya maandiko. Kutazama neno katika mukitadha wa vifungu mbalimbali vya maandiko itakusaidia kufahamu maana ya neno. Kwa mfano, angalia jinsi "Neno" linavyotumika katika Yohana 1:1 na 1:14 na utaelewa kwamba "Neno" ni kumhusu Yesu.

Mfano: Waefeso 1:22–23 wanaeleza kwamba kanisa ni mwili wa Kristo; na kwa kulinganisha aya hizi na I Wakorinto 12:13, tunaelewa kwamba "mwili" ni kuhusu "kanisa" katika aya zote mbili.

Unatakiwa kuhakikisha kuwa unalinganisha neno la lugha ileile ya asili katika msitari moja kwenda kwenye neno la lugha hiyohiyo ya asili katika msitari mwingine. Vilevile weka akilini mlinganisho wa Agano la Kale na Agano Jipya, lakini lazima ukumbuke kwamba unashughulika na lugha tofauti kwahiyo mlinganisho halisi wa neno la asili hautakuwa rahisi.