Skip to main content

Dhabihu iliyohai

Dhabihu iliyohai (sura ya 12)

Utangulizi

Warumi sura ya 12-16 kamilisha mwisho wa sehemu ya kitabu hiki. Hii sehemu ni ya vitendo zaidi katika maelezo yake. Tunaona Haki ya Mungu inatumika katika maisha ya kila siku ya Muumini.

Warumi sura ya kumi na mbili inahusiana na majukumu ya Wakristo, ambapo mwishowe inapelekea maisha ya kushindwa. Kanisa linafananishwa na mwili wa binadamu. Lazima kuwepo na umoja kwenye mwili, kama hakuna umoja, mwili hautafanya kazi vizuri. Sura hii inahusiana na majukumu mbali mbali ya kanisa. Hii sura inahitimisha na roho ya mkristo. Hatupaswi kushinda kwa mabaya bali kushinda kwa mema.

Dhabihu ilio hai (mst. 1-2)

Maneno maalumu na vifungu katika mistari

Maneno yaliyotumika mara nyingi hupoteza thamani yake kwetu kwa kutumika mara nyingi. Hebu tuangalie kwa karibu kwenye misamiati ya mistari miwili ya mwanzo ambapo tunaweza kupata uelewa zaidi:

  • Kusihi — Hii ina dhana ya kuita karibu na kufanyia. Hili ni ombi katika kujipatia.
  • Kwahiyo — hii ni KWA AJILI YA? Yote ya sura ya kumi na moja inaeleza ni kivipi rehema imetolewa. Aliyetengwa alijumuishwa. Kwahiyo lazima tufanye...
  • Ndugu — Anaongea kwa wale ambao wamekwisha kununuliwa kwa damu na kuzaliwa mara ya pili, Israeli wa Isaka, bali ni Waisraeli wa kiroho.
  • Huruma za Mungu — Ni kwa huruma za Mungu kwamba tungeweza kusikia ombi kama hilo. Haikuwa kwa ajili ya huruma za Mungu iliyoonyeshwa kwenye barabara ya kuelekea Daneski, Paulo hangeweza kufanya ombi kama hilo. Hafanyi ombi hilo kwa sababu yeye ni bora zaidi ya Mtu yeyote, lakini kwa sababu ya huruma za Mungu alipata sifa ya kufanya ombi hilo.
  • Miili — Katika mwili wa nyama lazima kumtukuza Mungu. Sio kwa siku fulani na kwa sasa tufanye vizuri zaidi kadri tuwezavyo tunapaswa kuishi kwa busara, kwa haki, kwa utauwa, katika ulimwengu huu wa sasas (Tito 2:12).
  • Dhabihu ilio hai — Mwili lazima usulbiwe. Mapenzi yetu lazima yasulubiwe. Tunatoa maisha yetu kuwa sadaka, lakini Mungu atatusafisha kadiri tunavyobakia katika madhabahu.
  • Utakatifu — Maisha yetu lazima yawe nuru kwa wale ambao huzurura gizani.
  • Aliyekubalika kwa Mungu — mwenye kukubali kikamilifu; kupendeza vizuri katika enzi hizi mpendeza watu, lazima tutafute ubora wetu kwa Mungu. Je yeye hufikiria nini katika mwelekeo unaochukuwa? kukubalika katika ulimwengu huu ni kumkataa yeye. Hatuwezi kukubalika kimwili katika ulimwengu huu na wakati huo huo tukubalike kwa Mungu. Lazima uwepo mstari wa wazi wa ushirikiano uliofafanuliwa. Utaambatana na nani?
  • Huduma ya kurithisha — Nira yake ni laini, lakini kigezo chochote ambacho Mungu angefanya kwa ajili yetu ingechangia katika ukuu kwa kile ambacho ameshatoa kwa ajili yetu.
  • Iliothibitishwa — Thibitisha mfano ule ule; mtindo wenyewe kulingana na;
  • Aliyegeuzwa — Badiliko; toka udogo kwenda ukubwa;hii ni kazi ya miujiza ya Mungu.
  • Kufanywa upya nia yako — Nia zetu hufanywa upya kwa Neno la Mungu. Kuwa mbadala wa mawazo ya kimwili kwa kile kilichosemwa na Bwana.
  • Mwema, aliyekubalika, na mapenzi makamilifu ya Mungu — Haya sio mapenzi matatu ya Mungu, bali sifa tatu za moja ya mapenzi yatawalayo ya Mungu. Yeye hana nia mbili (au kuwa wapande tatu kwa ajili ya jambo hilo).

Mapenzi makamilifu ya Mungu

Hii ni ombi kuu la Paulo kwa ajili ya utakaso binafsi kwa Mungu. Paulo anafundisha kwamba kila muumini anapaswa kutamani mapenzi makamilifu ya Mungu. Maelekezo yanatolewa kwaajili muumini kuyafuata.

Dhabihu

Katika mstari wa 1 anatuambia kutoa miili yenu, "hii inamaanisha kutoa sio nafsi tu," bali na miili yetu vile vile. Ni sadaka ya hiari, na kutakugharimu kitu fulani. Ni dhabihu iliohai. Tunapswa kujipeleka wenyewe kwa Mungu tukiwa hai!

Ni huruma zipi za Mungu ambazo Paulo anarejea?

  1. Kuhesabiwa — pamoja na msamaha, kuondolewa toka dhambi maovu hayatakumbukwa kamwe, haki inasimama katika Kristo-kufanywa mwenye haki wa Mungu katika yeye.
  2. Utambulisho — ulliotolewa kwa Adamu kwa kufa pamoja na Kristo—mfu katika dhambi na sheria—na sasa tunatambulika katika Kristo.
  3. Chini ya neema — kumzalia Mungu matunda — kwenye utakaso, na kufanya uwezekano.
  4. Kukaa katika Roho — ushahidi wa Roho ya uwana na mrithi.
  5. Msaada katika udhaifu — katika mateso yote ya sasa, katika njia yetu ya kushirikiana utukufu na Kristo.
  6. Chaguo la kimungu — mabadiliko yetu ya mwisho kuwa sura ya kristo—Kusudi lenye kukaa la Mungu.
  7. Utukufu ujao — ni mbali na mlinganisho wa mateso.
  8. Hakuna utenganisho unaowezekana — Mungu anatupenda katika Kristo.
  9. Ujasiri katika uaminifu wa Mungu — uliothitishwa kwa mipango iliofunuliwa kw ajili ya Israel.

Huduma ya kurithisha

Mungu ametoa sana kwa watu wake. ametoa neema, yeye ametoa kwa kila mtu kipimo cha imani, amefanya mwili moja katika Kristo, naye ametoa karama za unabii, huduma na ufundishaji.

Watu wa Mungu wanapaswa kutenda kwa usahihi tunapaswa kufikiri kwa busara, kutoa kwa urahisi, kutawala kwa akili, kuonyesha huruma na uchangamfu, upendo usio na mfarakano, chuki ambayo ni uovu, kuambatana na lililojema, kuwa mwema kwa upendo, kuonyesha upendo wa kidugu, kupendana, sio wa kujipachika katika shughuli nyingi, kuwa mwenye juhudi katika Roho, mtumikie bwana, furahahi katika tumaini, kuwa mvumilivu katika dhiki, kuendelea katika maombi, kugawia mahitaji ya lazima kwa watakatifu, kutoa kwa ukarimu, kuwabariki wale wanao kutesa, kufurahi na wanao furahi kulia na wanao lia, kuwa na nia inayo fanana.

Kutojifananisha na dunia

Muumini na mtindo wake wa maisha lazima yawe tofauti zaidi kuliko ulimwengu. Ulimwengu unatumia kanuni za Mungu kwa ajili ya mafanikio yao katika kujipatia mapato. Tuzitumie kanuni za Mungu kwa ajili ya mafanikio sio kwa ajili yetu bali kwa ajili yake na ufalme wake. Kwanini nataka kuwa mkristo mwenye mafaniko?mafanikio ni kujifunza jinsi ya kuongoza wengine kwa Kristo. Maisha yetu yawe mfano wa Kristo.

Kuwa aliyegezwa

Kazi ya Roho mtakatifu kwanza anza na ufahamu, unaobebwa kwenye mapenzi, upendo na mazungumzo, hadi kuwa na badiliko la mtu mzima kwenda kuwa mfano wa Mungu, katika ujuzi, haki, na utakatifu wa kweli. Kwa wale wamchao Mungu tunapaswa kujitoa kwa Mungu.
—Maoni ya Matayo Henery

Kufanywa upya katika nia

Kufanywa upya kwa ufahamu hutokea kwa Neno la Mungu (Zab. 119:9, 105). Ni kazi ya Roho. Ufahamau mzima lazima uje chini ya uongozi wa Roho (Waefeso 5:17-20—17). Ufahamu uliofanywa upya ni ufahamu wa Kristo. Sio kwamba ni ufahamu tofauti au mwingine, bali ni kazi ya Mungu ndani inayo zalisha ufahamu wa Kristo (Waflp. 2:5; 1 Cor. 2:14-16; Luka 19:10; 2 Tim. 1:7; Yohn 8:50).

Msimamo wa mkristo kwa wengine (mst. 3-8)

Tu mwili mmoja katika Kristo, wenye karama mbali mbali. Kila moja ni kiungo cha mwenzake. Mtu anapo miliki karama atapaswa kuitumiaje? Karama mbali mbali hutolewa na Roho. Kazi za karama ni unabii, huduma, kufundisha na kutia moyo, nk. Umiliki wa karama sio bila matumizi. Ni mazoezi mazima ya karama, wakati imetolewa na kusihiwa na mitume. Karama zimetolewa moja kwa moja na Roho. Imani ni ya lazima kwa kupokea na kutumia hizi karama.

Amri kwa muumini (mst. 9-21)

Penda kikwelii (mst. 9a)

Kutokuiga humaanisha "kutochukua wazo la mtu, hisia, au tabia; kujifanya." Upendo usioshindwa umeshuhudiwa kwa wema (2 Wakor 6:6).

Kupenda wema na kuchukia uovu (mst. 9b)

Zaburi 34:14—Uache mabaya ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie.

"Uovu" ni kile kinacho umiza, kuzuia uzalianaji katika asili, ya shetani, anasa au ubaya. Tunahitaji kukimbia uovu na kukimbilia mema. Hii sio hofu ya uovu kama ilivyo kwa ushirikina,lakini ni utakaso au mgawanyiko wa mwenendo wetu na maisha ya mawazo kutoka kwa vitu hivyo ambavyo ni kinyume na utakatifu wa Mungu. Je, tunawezaje "kuchukia" na "kuachana" na uovu? (Zab. 37:27; Is. 1:16)

Hitimisho la War 12

Kuwa mkristo inajumuisha kila eneo la maisha ya mtu. Nia na mwili hutolewa kwa Mungu kwa kujikabithi kimaadili kama sadaka ya kiroho. Kwa msimamo wake na matendo mbele ya Wakristo wengine yeye ni wakuonyesha ukweli kwamba yeye ni mfuasi na wengine katika mwili wa Kristo. Katika uhusiano wake na mwenye dhambi, yeye hufanya katika upendo na kumwachia Mungu ulipizaji kisasi kwa ajili ya uovu.