Ukataaji wa wanaisrael na jukumu la mwanadamu
Ukataaji wa wanaisrael na jukumu la mwanadamu (9:30-10:21)
Kujikwaa na kushinda: Hitimisho la sura 9 (9:30-33)
Haki kwa njia ya imani (9:30)
Mataifa hawafuati haki (haki kwa sheria), hupatikana kwa imani. Imani imetofautishwa katika kifungu kwa njia hii: Kutafuta haki kwa shika sheria dhidi ya kutafuta haki kwa njia imani katika Kristo Yesu.
Hakuna haki kwa njia ya sheria (9:31)
Israeli alifuatasheria ya haki, lakini hakujipatia (hangeweza kuitunza sheria). Israeli anafuata sheria, lakini alijikwa njiani.
Lazima kutafuta haki kwa njia ya imani (9:32)
Israeli hakutafuta kwa imani.
Jiwe likwazalo limewekwa (9:33)
Walijikwaa kwenye mwamba uchukizao. Walijikwaa kwa Yesu. KUMBUKA: Njia pekee ya kuwa na Yesu katika maisha yako ni kumwamini. Vinginevyo yeye ni "mwamba uchukizao." Alichukiza viongozi wa Israeli kwa kukemea dhambi.
Ni ujumbe gani wa injili uliofunuliwa kwa wote? "Na yeyote aminiye hata aibika." Huruma Mungu imeonyeshwa kwa kazi zake kwa wayahudi na wamataifa. Unyenyekevu na uchaji ni misimamo maalum kwa ajili yao wote ambao wanaipokea huruma na wema wa Mungu. Iwe mtu ni myahudi au wamataifa, wokovu wake hutegemea zaidi au kidogo kuliko vile anavyofikiri na kufanya pamoja na Yesu. Kujishusha chini ya njia ya Mungu kwaq ukiri binafsi wa Yesu kama Bwana mfufuka, na kumleta mwanadamu katika "haki na kusimama pamoja na Mungu."
Wokovu kwa ajilli ya wayahudi (10:1-21)
HAWAJA OKOLEWA (10:1)
Injili ni kwa ajili ya Wayahudi (War. 1:16; 2:9-10. Wayahudi wengi walikataa Injili (Mdo. 2:22-23). Mateso ya kwanza ya wakristo yaliandaliwa na serikali ya kirumi chini ya utawala Nero mnamo 64 AD baada ya moto mkuu wa Rumi. Kwa hiyo mateso ya kwanza ya wakristo kwa ukubwa yalitokea kwa Wayahudi (Mdo. 9:1-2).
Uzembe wakijinga wa wayahudi (10:2)
Mafarisayo: Maagizo madogomadogo yaliongezwa katika sheria (Mdo. 23:6; 26:5; Fil. 3:5-6). Paulo hadharau juhudi zao. Anashuhudia kwenye ari yao "kwa Mungu."
Dharau ya Wayahudi (10:3-11)
Walikuwa na ari ya Mungu, lakini walipoteza ukweli wa muhimu: Haki ya Mungu ambayo ni kwa imani. Na lengo la imani hii ni Yesu Kristo mwana pekee wa Mungu ni mwisho wa sheria kwa njia ya Imani. Imani hii huja kwa neno la Mungu haihitaji mpaka ufike mbinguni au jehanamu kwanza, bali ni sasa hivi.
Njia ya Wayahudi kwenda kwa Mungu (10:12-15)
Kukataa injili kwa Wayahudi (10:16-21)
Soma Isaya 65:1-10. Mungu atuma mhubiri -> mhubiri ahubiri -> wasikiaji wanasikia -> wasikiaji wanaamini -> muumini analiita jina la Bwana -> Bwana ana mwokoa. KUTOKUUNGANIKA kuko wapi? "Hawaja itii injili au kuisikiliza."
- Je Mungu alituma mhubiri? (NDIO (mst. 19, 20, Musa, Isaya, n.k.)
- Mhubiri alihuri? NDIO (mst. 16, taarifa ya KUHUBIRI katika)
- Kusanyiko lilisikia? NDIO (Musa alisimulia na Isaya pia alisimulia, n.k.)
Wasikiaji walikataa kuamini. TUNAJUKUMU KATIKA MPANGO WA MUNGU KWA AJILI YA UKOMBOZI. Mungu anawatumia wa mataifa kuwaachokoza Wayahudi kwenye wivu (10:19).
No Comments