Skip to main content

Maoni tofauti miongoni wa Wakristo

Maoni tofauti miongoni wa Wakristo (sura ya 14)

Utangulizi

Warumi sura ya kumi na nne inaongelea kuhusu jinsi ya kumtendea ndugu mdhaifu.tunapaswa kuwasaidia wale ambao ni wadhaifu katika imani yao. Tunaona hitaji la kuwa na upendo. Tunapaswa kumishia Mungu, na yote tunayohitaji kwa Mungu. Hatupaswi kuhukumiana, kwa kuwa siku moja kila mmoja atatoa hesabu ya maisha yake mwenyewe.

Tunawatendeaje wakristo wenye maoni tofauti (mst. 1)

Kunatofauti katika afya za imani zetu vile vile kunatofauti za maoni (madhaifu na yenye nguvu). Kunamaelekezo yaliyo wazi yaliyotolewa katika maandiko matakatifu:

  • "Hutafanya" katika amri 10 (Kutoka 20:1-17)
  • Wokovu ni kwanjia ya Yesu (Yoh 8:24; 14:6; Matendo 4:12)
  • Huwezi kumtumikia Mungu na mali (Mith 28:22; Waefeso 4:19; 1 Tim. 6:10; Mat 6:24)

Lakini pia kuna maoni mengi na ufasiri na matumizi ambayo hujazwa kati ya mistari. Wakristo wengi hugawanyika juu ya mambo kama vile:

  • Wanasiasa (je unaweza kuwa mkristo na wakati huo huo kuwa mwanademokrasia?)
  • Mwanamke katika huduma (Je mwanamke anaweza kuwa mchungaji?)
  • Internet (je mkristo anaweza kubakia mtakatifu wakati anatumia vitu ambavyo sio vitakatifu?)
  • Damu ya Yesu
  • Mamlaka ya neno la Mungu
  • Ubatizo wa Roho mtakatifu
  • Majadiliano juu ya Jumamosi/Jumapili

Mpokee aliyemdhaifu wa imani, lakini sio kuhojiana naye

Mara nyingi maoni huvuviwa na maandiko matakatifu, lakini tunafanya kujaza sehemu ya kijivu (isio elezwa) maeneo ya maandiko kwa maoni yetu. Tofauti za maoni zisingekuwa sababu za migawanyiko au kisngizio kwa ungomvi.

Kila mtu angekuwa kama mimi?

Ndugu dhaifu ni nini katika mazingira haya? (mst. 2-4)

Uthafu Paulo ameutaja hapa unabeba dhana ya ugonjwa na hali ya kushindwa kuzaa hanithi. Wale walio wadhaifu katika imani wanafanana na kilema anayehitaji kujikokota, kipofu anayehitaji kuongozwa, au mwenye kupooza anayehitaji msaada kwenye mambo ya lazima katika maisha ya kila siku. Magonjwa hukatisha maisha na kuyaondoa kama hayatatibiwa. Huu udhaifu wa imani ni sawa na ugonjwa ambao ni lazima ufahamike na kushughulikiwa kwa neema, lakini pia uwe ni uponyaji ulio hudumiwa. Wadhaifu lazima wasiachwe wapweke, lakini watiwe nguvu (Yak. 5:16).

Udhaifu katika vyakula Weakness in eating

Katika Wakor wa kwanza sura ya 8 Paulo alipaswa kushughulika na swala lile lile na Kanisa la Wakoritho. Hili linaweza kusikika kama kitu kisicho na maana na sio cha kidini na mabishano kwa mkristo wa sasa, lakini Biblia ya maoni ya Layman inatupatia mwanga kwenye ubishi huu:

Ilikuwa ni aina tofauti ya swali la kidini katika utawala wa kirumi. Uhakika ni katika soko la kirumi ungeweza kwa ugumu kupata nyama nzuri au ya kuokwa au aina yeyote ya nyama ambayo haikutokana na wanyama waliochinjwa ndani hekalu. Mnyama angeweza kuchinjwa kwa ajili ya sadaka ya kutekezwa;kisha kuhani (amabo walikuwa hawana idadi ingawa walikuwepo lakini haingwezekana kula wanyama wote walioletwa kama sadaka) wangeweza kuwauza kwa reja reja kwenye vituo. Hii ilikuwa chanzo kikuu cha nyama katika masoko, Mkristo mnunuzi angekumbana na shida: katika kununua na kuila nyama hii, nifanye au nisitoe msaada kwa ibada ya kipagani?

Watumishi — wewe ni nani hata umuhukumu mtumishi wa mwingine?

Hukumu — Kila mtu atatoa hesabu kwa Mungu na sio kwa mwingine

Siku Days

Roho ya sheria haiulizi "uliikumbuka siku?" bali huuliza kwamba je ulifanya kama kwa Bwana?" waliabudu kwa siku kadhaa, na walikuwa wanaweka umuhimu juu ya siku na sio kwa Kristo.

Sisi ni ndugu na sio mahaki (mst. 5–12)

Msitari wa sita kwa wazi unaelezea pande zote mbili za hoja ya kumjua Bwana.

Ni nini tunayodhani kuwafanyia wengine:

  • Onyesha heshima na shukurani (12:10; 15:7)
  • Shaurianeni (15:14; Wakol. 3:16) tunapenda mioyo ya watu, na kuifikia mioyo ya watu. Tunaweka mioyo yetu kwa watu wengine kwa kuwapenda. Tunaonyesha huruma kwa kuwatia moyo wengine. Upendo husahihisha, hutia moyo, na hufundisha. Ili tumfundishe mwingine tofauti kati ya haki na uovu, Kwanza tunapswa kujijua tofauti zetu wenyewe.
  • Sameheaneni (Wakol. 3:13)
  • Acha kuhukumu (Warumi 14:13)
  • Tunapaswa kubebeana mizigo (Wagl. 6:2)

Usiweke kikwazo katika njia ya ndugu (mst. 13–17)

Tunaambiwa kudumisha amani katika tofauti zetu (mst. 18–20)

Baraka ya kuwa huru (mst. 22–23)

Ni baraka zaidi kuwa na uhuru mbele ya Mungu ambayo hatutumii udhaifu wa ndugu, zaidi ya kusisitiza uhuru, ingawa umetolewa kwa utofauti.