Kuthibitishwa kwa sheria
(Warumi 3:31)
Kuhesabiwa haki ni kwa imani nasio matendo ya sheria. Sheria: ni faida kwao wanaoijua (mst. 1-2), uhalisi katika asili yake (mst. 3-8), haipindiki katika mamlaka yake (mst. 9-19), inakusudi la kipekee (mst. 20-30), haiepukiki bali imethibitishwa katika mioyo yetu (mst. 31).
Kuhesabiwa haki kwa imani huthibitisha sheria.
Kuhesabiwa haki sio kinyume cha sheria ya Musa. Wokovu kwa imani katika Kristo Yesu umekithi haja ya sheria ya Mungu. Yesu kwa ukamilifu amekamilisha au kuthibitisha uhitaji wa sheria. Kuna rejea pia hapa ya sheria ya maadili. Imani haipuki sheria ya maadili ya Mungu. Sheria ya sherehe imekamilishwa na Kristo. Hatuhitaji tena sadaka ya mbuzi na mafahalikumtolea Mungu, wala kushika sheria za sikukuu. Sheria ya maadili ya Mungu haibadiliki. Kuhesabiwa haki haikomeshi sheria ya maadili ya Mungu.
Sheria ya imani haifanyi sheria isitumike au kuepukika, bali huithibitisha. Imani haiondoi wala kuharibu sheria, bali kuiboresha.
Sheria huleta kuijuwa dhambi kwa mtu, na huyo mtu ambaye ameitambua hali yake awezekuhesabiwa haki kwa imani. Pasipo sheria mtu hangeweza kuijua dhambi, na kwa hiyo hangekuwa na hitaji kwa ajili ya kuhesabiwa haki, ukombozi au malipizi ya dhambi. Sheria ambayo kwa mara ya kwanza ilivunjwa imethibitishwa kwa njia ya imani katika kazi iliomalizika ya Kristo kwa maana kwa njia ya haki yake IMETOSHELEZA.
No Comments