Skip to main content

Kufanya kazi kwa ajili ya umoja

Kufanya kazi kwa ajili ya umoja (sura ya 15)

Utangulizi

Waamini ni wakukaribishana wao kwa wao, kama Kristo alivyo wapokea mataifa—kwa utukufu wa Mungu. Sehemu ya kwanza ya sura hii inaelezea mahusiano ya Kikristo, Kristo akiwa kama mfano wao mkamilifu. Ujumbe binafsi wa Paulo kwa Warumi unaanza na katika msitari wa 14. Huduma ya Paulo ilikuwa kwa wote kwa wale waliokuwa ndani (wayahudi ambao makuu ya Mungu yalifanyika kwao na kwa wale ambao haikufanyika (wa mataifa). Kazi ya umoja kataika mwili wa Kristo ni kazi ya MUngu.

Tufanye kazi ya kukaribishana pamoj an Kristo kama mfano wetu (mst. 1–12)

Kuna tofauti kadhaa (mwanzo wa kihsitoria)

Kuna tofauti nyingi za kidini na kimila kati ya wayahudi na wamataifa kwa kufunguliwa injili kwa mataifa kulikuwa na ugumu mwingi wa kushinda. Paulo anaonya kwa ushupavu, tunatakiwa kufanya kazi ili kuwapokea wamataifa kama Mungu alivyo wapokea. Kiwango cha juu na kutawala kwa kile ambacho tabia zetu hupimwa "kama kristo alivyo tupokea sisi kwenye utukufu wa Mungu" (mst. 7).

Kuwa myahudi kwa shaka, makanisa ya kwanza yange jisikia "kuwa ya kiyahudi" (michanganyiko ya mila na ushawishi). Kulikuwa na ufukuzwaji kwa mara ya kwanza kutoka Roma kwa wayahudi wote na ni mageuzi ya kiasili na kimila yaliyo tokea katika makanisa ya kirumi. Mwishowe, Wayahudi walirudi katika mji wa Roma kupata vitu tofauti zaidi ya walivyokuwa wameacha. Ilikuepuka mgawanyiko, Kanisa la kwanza lilikuwa linafanya kazi kwa pamoja ilikushinda tofauti zao za kimila kwa kujifunza vile vitu ambavyo "vinahitaji sana" (Matendo 15:28; Waefeso 4:3, 13).

Kuna kanuni za kidunia

Wakristo waliitwa kuishi maisha ambayo sio ya kichoyo (mst. 1–2)

Warumi sura ya kumi tano inaongelea kuishi maisha yasiyo ya kichoyo. Wenye nguvu wanapaswa kuwasaidia wadhaifu. Tunapaswa kuishi sio kujipendeza wenyewe bali kumpendeza Mungu, kuwatanguliza wengine mbele yetu. Sura hii inaishia na safari za Paulo.

Sura ya kumi na tano ya Warumi inahisia nzito ya hitimisho. Kama ulivyo mtindo wa Paulo katika kitabu hiki, anarudia mawazo ambayo aliyawasilisha lakini ni kwa mwelekeo zaidi na kibinafsi. Anatoa maelezo ya maelekezo maelezo yaliyo fuata kwa wasomaji wake:

  • Wenye nguvu wanapaswa kuchukuliana na wadhaifu.
  • Kupendeza majirani zetu kwa wema wao na imani.
  • Kuchukuliana ni nia ya Kristo. Kwamba mwe na nia moja na kuwa na kauli moja ya kumtukuza Mungu.
  • Yesu ni mhudumu kwa wayahudi na kwa wa mataifa.
  • Wamataifa wanasababu ya kufurahi na wanaamriwa kufanya hivyo katika maandiko matakatifu.

Kristo ni mfano wa mkristo kwa ajili ya kuishi (mst. 3)

Kwa nini mkristo ni lazima kuhusika na wengine badala yake mwenyewe? Tunapaswa kumtumia Kristo kama mfano wetu, "hata Kristo hakujipendeza mwenyewe, kuhusika kwake ilikuwa ni kwa wengine alijionyesha kwa upendo, mafundisho yake na uponyaji wake."

Neno la Mungu ni chanzo cha Mkristo kuwa na faraja kwa ajili ya maisha (mst.4)

Tunaweza kuwa na faraja wakati mahitaji kwa kuyasoma maandiko. Tunaweza pia kuendelea mbele kwa tumaini.

Umoja katika mwili wa Kristo ni shabaha ya Mkristo (mst. 5-6)

Tunaswa kuunganika katika nia moja na kwa roho inayomtukuza Mungu ambaye ni lengo letu la maisha.

Kristo ni kiwango ambacho kwa hicho wakristo watakuja hukumiwa (mst. 7)

Mungu hulinda neno lake na yeye ni mwenye huruma (mst. 8–12)

Tunapaswa kufanya kazi ilikuwafikia wale ambao hawana neno la Mungu (mst. 13–21)

Ninyi ni ndugu zangu na mmejazwa na mema mengi (mst. 13–14)

Maoni ya Paulo yalikuwa nini kuhusu wakristo wa Rumi?

  • Paulo anamwamini Mungu kuelekea kuwasababisha kuwa na tumaini na nguvu (mst. 13).
  • Walikuwa wamejawa na wema.
  • Walijawa na ujuzi wote.
  • Waliweza kutangulizana.

Ijapokuwa Paulo hakuwahi kuwa Rumi, alijuwa na kufarijika kwa imani yao (1:8).

...Hata hivyo (mst. 15–21)

Kuna vitu vingi vya kutia moyo Paulo anaweza kusema na ameshasema (1:8), lakini wote tunakitu cha kufanya.

Paulo aliandika kwa ujasiri (mst. 15)

Katika hatari inaonekana ya kutotambuliwa kwa mfano wao na imani, Paulo kama mhudumu mwaminifu wa changamoto za injili ujasir wa kanisa na vitu vya lazima.

Paulo alikuwa na wito na jukumu (mst. 16a)

Je, Paulo anajirejea mwenyewe kama nini? Kama, mhudumu wa Yesu Kristo kwa mataifa. Akihubiri neno katika nguvu za Roho. Kwa ishara na maajabu kama uthibitisho. Utambulisho wa Paulo ulifunika wito wake. Paulo aliweka kipau mbele kwa wito wake na kuchelewesha matakwa na malengo binafsi. Sio kwamba kile anafanya hakina mzigo kwa ndugu zake, bali kile alichonacho ni wito ulikuwa unatangulia.

Paulo alikuwa na lengo (kujitoa sadaka kwa ajili ya mataifa) (mst. 16b)

Paulo alikuwa na wasikilizaji (Mungu alinipa) (mst. 17–21)

Kadiri Paulo alivyokuwa na ujasiri anaongea, haogopi kusema lakini kwa kile ambacho Kristo amemwezesha:

  • Mungu ametumia kwa nguvu, lakini sio yote ambayo Mungu ametenda katika uwanja huu ameyafanya kwa kunitumia.
  • Mimi sio mhudumu pekee kwa mataifa.
  • Kwa uangalifu: ruhusu wale walioponywa kutoa ushuhuda.
  • Kwa uangalifu usifiche kile ambacho Mungu anafanya popote-Paulo hakutaka kujenga juu ya msingi wa mwingine (kazi).
  • Hapa watedakazi wamezuiliwa.
  • Nina ujumbe kwa ajili wale ambao hawajasikia (Mungu ameahidi hiyo! mst. 21; Isa 52:15; 65:1).

Tunapaswa kufanya kazi katika kuwafikia wale ambao hawajafikiwa (mst. 22–33)

Sio kwa kwa bahati njema ya upendo, bali kwa ajili ya sababu kubwa nimezuiliwa (mst. 22–24)

Kifungu "hizi nyakati nyingi" inaonyesha jinsi ani wakisto wa Roma kwa kuendelea walivyokuwa katika moyo wake na shauku zake. Kifungu "muda mrefu unaokuja" inaonyesha kwamba yeye alikuwa shauku kubwa ya kuwatembelea watu.

Ratiba ya Paulo (mst. 25–28)

Paulo anaelezea tena shauku yake na kusudi lake la kutelea kanisa la Roma na ratiba yake. Alikuwa lazima kwanza aende Sipania na kukusanya sadaka kwa ajili ya watakatifu wa Yerusalemu. Yeye angeweza kuzileta Yerusalemu baada kile alichokusudia kutembelea Roma. Kwa jinsi gani wakristo wa Makedonia na Akaya walivyohusika na maskini miongoni wa wakristo walioko Yerusalemu? Walichangia kwa ajili ya maskini. Paulo mwenyewe pamoja na ndugu wengine walichukua hizi sadaka na kuzipeleka Yerusalemu, kupokea kwa mtu kile ambacho ni kanuni ya kiroho Paulo anawafundisha warumi kwa kuhusianisha hizi habari? Lilikuwa ni tendo la upendo juu ya sehemu ya watakatifu wa mataifa. Ilikuwa ni utimilizo wa maneno ya Bwana katika Yoh. 13:17, 35.

Hitimisho

Umoja wa utatu

Katika mstari wa 30 kwa mara ya kwanza tunaona utatu:

  • Kwa ajili ya Bwana Yesu Kristo mwenyewe.
  • Kwa ajili ya upendo wa Roho.
  • Maombi yenu kwa Mungu kwa ajili yangu.

Baraka (mst. 33)

"Mungu wa amani awe nanyi nyote," inaonyesha kwa jinsi gani moyo wa mtume ulikuwa umejawa na amani na kujawa mapensi ya Mungu! Inaonyesha pia upendo unaofurika kwa ajili ya watakatifu (mara mbili katika sura hii Paulo anaomba kwa ajili ya kanisa la Rumi. Angalia misitari ya 13 na 33). Kusudi na nguvu ilio nyuma ya umoja wa wakristo ni mfano wa upendo wa Kristo na huduma na dhabihu. Kuwa na msisimko kama huo miongoni mwa wakristo, tunahitaji kuomba kama Paulo alivyofanya uwezeshaji wa Bwana. Maana ya Paulo ya agizo kuu haikumfanya kuwa wakutegemewa na wakristo wenzake.