Skip to main content

Dhamira ya Paulo: Injili

(Warumi 1:16-17)

Dhamira ya Paulo: Injili (1:16-17)

Mistr ya 16 na 17 ni mistr ya ufunguo wa waraka huu na vifupusho vingi vya waraka.

Injili ni uwezo wa Mungu kwa ajili ya wokovu

Wote waminio wanaweza kubadilishwa na nguvu ya Mungu

Maandiko matakatifu hutangaza kwamba Injili ya Kristo ni kwa kila mtu aminiye. Baadhi ya watu kwa uwongo hufundisha kwamba Mungu huchagua baadhi ya watu tu kwa ajili ya kuwaokoa. Injili sio kwa ajili ya wachache walioteuliwa, bali kwa yeyote atakayekuja kunywa maji ya uzima. Kwa yeyote amwaminiye Yesu atakuwa na uzima wa milele (Yoh. 3:16). Watu wote wanauwezo wa kuamini, bali watu hawachagui kumwamini Yesu na kukubali utoaji wake wa ukombozi kwa njia ya damu yake.

Wokovu ni kazi ya Mungu

Mtu hawezi kufanya chochote kwa ajili ya kujiokoa. Alizaliwa katika dhambi pamoja na njia zisizo na matumaini za mwanadamu. Mtu hana wema wakutosha kukidhi matakwa ya sheria ya Mungu. Yeye ana hatia na amehukumiwa kwenda jehanamu. Hakuna gharama ambayo mtu anaweza kulipa ilikununua wokovu wake. Wokovu ni kazi ya Mungu iliotolewa kwa neema na kupokelewa kwa njia ya imani katika kumwamini Yesu Kristo. Wengi huchanganywa na urahisi wa injili na hawezi kukubali mwenye dhambi anaweza kufanywa upya na kubadilishwa kwa nguvu za Mungu kadiri anavyoifikisha imani katika mikono ya Yesu iliopigwa misumari.

Injili hufunua haki ya Mungu toka imani hata imani

Haki hutoka kwa Mungu

Mtu hana haki yake mwenyewe (Isa. 64:6). Haki ya Kristo inawekwa katika hesabu ya mwenye dhambi. Hii ndio inayomaanishwa kuwekewa haki. Kuwekewa ni neno la toleo KJV kuweka hesabu ya. MAELEZO YA MFANO: mtu ambaye hana fedha katika akaunti ya benk anahitaji mtu wa kumwanzishia akaunti yake. Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu (Yakobo 2:23). Ibrahimu alikuwa na haki ya Mungu iliowekwa katika hesabu yake (War. 4:3). Mungu humwangalia mwenye kutubu kupitia damu ya Kristo.

Haki hupokelewa kwa imani kwenye wokovu. Kuna tofauti kati ya haki iliowekwa na haki ya kupewa. Kupewa humaanisha kuweka kwenye. Mungu huweka haki yake ndani ya mtu kwenye wokovu. Kuna badiliko la asili ambalo huambatana na kuzaliwa upya (Wafl 3:9).

Maelezo kutoka imani hata imani hurejea kwenye ongezeko la imani; kuonyesho ukuaji kutoka imani ya mwanzo ya wokovu kwenda imani kubwa katika Mungu ambayo huja pamoja na ukuaji wa mkristo. Maandiko hutuambia kwamba kila mtu amegawiwa kipimo cha imani (War. 12:3). Watu wote wana uwezo wa kuamini, lakini bado hawafanyii kazi imani yao kumwamini Yesu Kristo. Mitume waliuliza Bwana tuongezee imani (Luka 17:5). Imani huongezeka kwa kadir inavyo fanyiwa kazi. Kwa ukomavu wa mkristo huja ongezeko la imani. Haki ya mungu hufunuliwa toka imani hata imani kwa njia ya Injili.

Haki ya Mungu ni endelevu kwa maisha ya wakristo

Ufunuo wa tabia ya Mungu na asili sio kitu cha kutenga mbali na Injili, bali yamefungana katika Injili kwamba sisi kama wasikiaji tuweze KUISHI. Uzima huu na haki sio vitu vinavyopokelewa kwa mara moja, bali hufunuliwa kwetu toka imani hata imani, kadiri tunavyotii na kufanyia kazi yale tuliyo ya pokea, Mungu hutupa zaidi na mchakato wake endelevu katika haki ni njia ya mwenye HAKI. Ufunguo wa kudumisha uzoevu wetu na Mungu ni mchakato endelevu. Paulo anatangaza katika Waebr 6:1, "tukaze mwendo ili tuufikilie utimilifu."

Mwenye haki ataishi kwa imani

Paulo anajenga dhamira ya waraka kwenye msingi wa maandiko. "Kama ilivyo andikwa" iko kwenye rejea ya Habakuki 2:4 kutoka ambako taarifa hii imechukuliwa.

Wenye haki ni wale ambao wamehasabiwa haki na Mungu kwa njia ya imani

Wenye haki hurejelea kwa wale ambao wamewekwa katika uhusiano sahihi pamoja na Mungu kwa njia ya malipo yaliyotolewa na yesu Kristo. Wale waliokoka ni wenye haki au wamekwisha hesabiwa haki.

Mkristo hulindwa na nguvu ya Mungu

Mwenye haki hubakia kwa kulindwa na nguvu za Mungu. Katika ulimwengu huu wa dhambi, mkristo anahitaji kutunza nguvu ya Mungu ilikumlinda kwenye njia nyoofu ambayo humwoongoza kwwenda uzimani. Yesu alisema kwamba hakuna mtu anayeweza kumpokonya kondoo toka kwenye mkono wake (Yoh. 10:28). Hii haimanishi kwamba Mungu ataliondoa mbali chaguo la mtu. Wakristo lazima wachague kumtumikia Mungu, kuishi ni uzoevu wa kila siku (mkristo ataishi) hiyo hudai upokeaji endelevu wa nguvu ya Mungu kwa imani.

Njia ya mweye haki huongoza kwenye ukomavu katika Kristo

Nuru huwakilisha ukweli ambao humwongoza mkristo kwenye safari yake (Mith. 4:18; Zab. 119:105). Na zaidi tunatembea katika njia ambao ukweli zaidi hupokelewa. Mungu hufunua zaidi ukweli kadir tunavyo tii ukweli ambao tayari tulisha upokea. Maisha ya ukamilifu wa urithi wetu kama waamini.

Mkristo huishi maisha yake kwa imani katika Kristo

Wagal. 2:20—Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.