Skip to main content

Dhambi imekufa na tuko huru kuoa mwingine

Dhambi imekufa na tuko huru kuoa mwingine (mst. 1-6)

Maana ya mfano

Afanyaye dhambi yuko katika kifungo cha mahusiano ya dhambi yake, kama vile mke aliyefungwa na mme wake. Kama wataendelea kuwa hai wote wawili, mme na mke wamefungana kila mmoja chini ya Mungu.

Paulo alitangaza kifo! ni kifo cha binafsi. Kama mke atakuwa huru kutoka kwenye torati ya mme wake ni kwa kifo, hivyo wenye dhambi watakuwa huru kutoka kwenye sheria ya dhambi kwa njia ya kushiriki kifo cha Kristo. Kifo hiki ni kuusulibisha utu wa zamani pamoja na Kristo (Mdo. 13:38-39; War. 3:25; 5:21; 6:6; 7:4; II Kor. 5:15; Gal. 1:4; 2:20; 5:24; 6:14; Efes. 4:22; 5:2; Col. 2:11; 3:5, 9; Tit. 2:14; Ebr. 9:15; I Petr. 1:21; 4:2; I Yoh. 2:2; 4:10). Basi alimfufua katika ufufuo, tunashiriki katika maisha ya Kristo ambayo kwa nguvu za Mungu tunaweza kuwa mwanandoa wa ndoa nyingine. Katika ndoa hii ya pili, Tumeungana pamoja na Kristo.

Nguvu ya sheria imeondolewa

Kadiri mtu anavyo ishi katika dhambi yuko chini ya sheria, na njia pekee ya kuepuka ni kuifia dhambi zake. Atendaye dhambni hana chaguo bali kuwa chuni ya sheria. Kifo huvunja wajibu wa sheria ya wa ndoa. Mtenda dhambi anaweza kuwa huru kutoka kwenye nguvu ya dhambi na adhabu ya kuvunja torati (7:4; 6:14).

Paulo alirudia maneno "hamjui" mara tatu wakati akizungumzia hili somo:

  1. "Hamfahamu" utu wa kale ulibatizwa katika mauti yake (6:3).
  2. "Hamfahamu" utumishi wa zamani umekatwa, umeharibiwa kupitia Kristo (6:16).
  3. "Hamfahamu" umoja wa zamani hauwezekani na umoja mpya Kristo (7:1).

Huduma ya umoja pamoja na Kristo Yesu

Kutokana na umoja huu wa Kristo utumishi wa Kristo utakuwa wetu (mst. 6).

  • Utumishi pamoja na uzima mpya (6:4)
  • utumishi katika upya wa Roho (7:6)
  • Utumishi kwa nguvu mpya (1:16; 8:11; IKor. 6:14; II Kor. 13:4; II Thes. 1:11)
  • Utumishi wa kiumbe kipya (II Kor. 5:17; Gal. 6:15)

Matunda ya umoja huu The fruitfulness of this union

Umoja wetu pamoja na dhambi huzalisha mauti (7:5; 1:32; 6:21; 7:5; Gal. 5:19-21), bali umoja pamoja na Kristo unatuwezesha sisi kuzaa matunda ya haki katiak utakatifu (1:13; 5:3-5; 6:22; Yoh. 15:2, 4, 5, 8, 16; I Kor. 1:6; Gal. 5:22-23; Efes. 5:9; Filp. 1:11; 4:17; Kol. 1:6, 10; Tit. 3:14; Ebr. 12:11; 13:15; Yak. 3:18; 5:7; II Pet. 1:3-9).