Hitimisho la kitabu cha warumi
Hitimisho la kitabu cha warumi (sura ya 16)
Utangulizi
Utata wa kifungu hiki
Utu wa kifungu hiki: ni wakibinafsi
Warumi sura ya kumi na sita inatunyesha upande binafsi wa Paulo kama anavyotuma salamu kwa waamini wanoishi Rumi. Anaongea kama mtu anayeongea na marafiki zake na sio kama kiongozi au mchungaji. Hii sura ya kumi sita mara nyingi huupuziwa na wengi. Ni kwa wale walio mbali zaidi, kwa siri, na umaaalumu wa barua ya Paulo yenye salamu (na ya pili ni Wakolosai 4). Hakuna atakaye athubutu kupoteza umwagikaji waajabu wa moyo wa mitume wetu kwa, watakatifu ambao aliwapenda sana, ambao ni kanisa la Mungu.
Roho ya kifungu hiki ni ya kipekee na maalumu unapofikiria kwamba Paulo hakukuta kanisa huko Rumi na hata alikuwa bado hajawahi kutembelea huko (barua hii inafanana na ile ya Wakolosai)! Licha ya kwamba Paulo anawataja kwa majina watu 26 katika kanisa hilo. Kila jina limeorodheshwa katika alama za Paulo za kufunga bila shaka alikuwa na historia yao ya kutia moyo, upendo na ibada kwa Bwana Yesu Kristo. Wengine zaidi ya majina yao, Paulo anawatambua hawa watu kama:
- Jamaa, dada, kaka, mama
- Watumishi wa kanisa
- Wafanya kazi, wasaidizi katika Kristo
- Wafungwa wenza
- watakatifu, makanisa ya Kristo
- wapendwa, waliopendwa katika Bwana
- Malimbuko katika Kristo
- Katika Kristo, katika Bwana
- aliyethibitishwa katika Kristo
- wateule katika Bwana
Amri ya Fibi (mst. 1–2)
[KUMBUKA: nukuu kadhaa katika sehemu zimechukuliwa kutoka fafanuzi za Alexander Maclaren ya maandiko matakatifu". Alexander MacClaren (February 11, 1826 - May 5, 1910) alikuwa mvuka salama na mhudumu wa injili kwa takribani miaka 65 aliyefanya kazi bila kuchoka katika kuhubiri na kuandika kuhusiana na maandiko matakatifu. Fafanuzi za MacClaren za maandiko matakatifu ni mkusanytiko wa zaidi ya hotuba 1,500]
Paulo anamwamru dada (sio dada katika mwili bali katika Bwana)
Cenchrea ilikuwa bandari ndogo katika Korinto
Lakini kama tutahesabu kutokuwa na maadili kwingi kuliko jificha kwa wakrinto, tutadhani labda ilikuwa hapa kulikuwa mji, wenye maji mengi, ilikuwa kama bandari nyingi, udongo ambamo wema kwa ulipandwa ilikukuwa, na kanisa lilikuwa na upinzani mwingi ambao walipaswa kupambana. Kuwa mkristo katika Cenchrea inawezekana haikuwa kazi rahisi. —MacClaren
Fibi alikuwa mmoja wa wanawake wema wengi walio msaidia Paulo katika kazi ya injili
Jina lake kwa wazi alikuwa mwabudu sanamu, na linamwelezea kama Mgriki, na kwa kuzaliwa labda alikuwa mwabudu wa Apolo.
—MacClaren
Kwa Fibi inaaminika aliipewa hii barua ili kuiwasilisha katika kanisa la Roma
Hapa ni Paulo myahudi, Fibi mgiriki, na wasomaji wa kirumi wa barua, wote waliungana kwa pamoja katika upendo wa kimungu ambao uliyeyusha mioyo yao, na imani ya kawaida ambayo iliounganisha maisha yao. Orodha ya majina katika sura hii, yanajumuishwa kama wanaume na wanawake wenye uraia mbalimbali, na baadhi ni watumwa kama watu huru.
—MacClaren
Wagalatia 3:28—Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.
Kwa ulimwengu ambao Paulo alikuwa anaishi ulikuwa ni wa kigeni, wazo jipya ambalo wanawake wangeshirikisha kwa wanaume katika msisimko yake ya kifahari. Kihistoria udhaifu wa nusu ya wanadamu ni matokeo ya moja kwa moja ya kanuni ya kikristo ambayo wote ni wamoja katika Kristo Yesu. —MacClaren
Maamukizi na salamu (mst. 3–15)
Paulo anayasalimia makundi 16 ya watu huko Rumi:
- Prisila na Akila, wasaidizi wangu katika Kristo (na kanisa la nyumbani mwa Prisila na Akila). Prisila na Akila walikuwa watengeneza hema kama Paulo alivyo kuwa. Kwa mapokeo hawa mishenari wawili wanajumuishwa katika orodha ya mitume 70 walioteuliwa na Yesu katika Luka 10. Wametajwa mara sita katika vitabu viine tofauti vya agano jipya. Maara zote hutajwa kama wenye ndoa na sio mtu moja moja. Kwenye rejea sita jina la Akila limetajwa mara tatu kwa mwanzoni na jina la Prisila limetajwa la kwanza katika mihula mitatu. Pirisila sio mali ya Akila bali zaidi ni wenzi katika huduma na ndoa. Pirisla na Akila walitajwa kwa mara ya mwisho katika maandiko kama walikuwa Efeso (Mdo 18:18–19). Pirisila na Akila walikuwa miongoni wayahudi waliokuwa wamefukuzwa toka Rumi na mtawala wa kirumi Kilaudio katika mwaka 49. Wanaishia kwa Wakoritho. Paulo aliishi na Prisila na Akila kwa makadirio ya miezi 18. Kisha wale wanandoa walianza kuondoka kumsindikiza Paulo alipoendelea kwenda Siria, lakini walisimama Efeso. Kama walivyotajwa katika Warumi 16, kwa wakati mwingine 56 au 57, walikuwa wamerudi Rumi. Kanisa la wamataifa walikuwa na shukurani kwa ajili ya Prisila na Akila kwa sababu walihatarisha shingo zao kwa ajili yao ("walilaza shingo zao chini").
- Epaineto, mpendwa wangu, malimbiko kwa Kristo ya Akaya.
- Mariamu, ambaye alijitoa sana kutuhudumia.
- Androniko na Yunia jamaa zangu, na waungwa wenzangu, wa mitume. Walikuwa ndani ya Kristo kabla ya Paulo. Ambao ni miongoni mwa watu ishirini na sita ambao Paulo anawatumia salamu maalumu, angalau sita kati yao ni wanawake, kuashiria nafasi na umuhimu wa wanawake miongoni wa kundi la wakristo huko Rumi. Utata juu ya msitari huu mfupi ni maswali "ni kwamba, Yunia ( ni jina la kike) au Yunias ni (la kiume?)" na je kifungu kinachofuata majina ni tafasiri nzuri ya ambayo iliobora miongoni mwa mitume au kilieleweka vinzuri kwa mitume'?"
- Ampliato, mpendwa wangu katika Bwana.
- Urbano, msaidizi katika Bwana.
- Stakisi, mpendwa.
- Apele, aliyethibitika katika Kristo.
- Wale wa nyumbani mwa Aristobulo.
- Herodioni, jamaa yangu.
- Watu wa nyumbani mwa Narkiso, walio katika Bwana.
- Trifaina na Trifosa, wenye bidii katika Bwana.
- Persisi, mpenzi aliyejitahidi sana katika Bwana.
- Rufo, mteule katika Bwana, na mamaye, aliye mama yangu pia.
- Asinkrito, Flegoni, Herme, Patroba, Herma, na ndugu walio pamoja nao.
- Filologo na Yulia, Nerea na dada yake, na Olimpa, na watakatifu wote walio pamoja nao.
Busu takatifu (mst. 16)
- "Busu takatifu" ni kitu cha mapokeo ya kiyahudi zamanni na salamu za Kikristo. Vile vile huitwa "busu la amani," "Busu la kindugu," au "busu la dada" miongoni mwa wanawake.
- Imetajwa mara 5 katika agano jipya: War 16:16; 1 Wakr 16:20 ; 2 Wakr 13:12 ; I Wathsl 5:26 ; 1 Petro 5:14. ("amani iwe nanyi", shaloomu"), "Shalom")
- Angalau kwa karine kadhaa za kwanza, busu hili halikuwa la mdomo kwenda kwenye shavu bali lilikuwa la mdomo kwa mdomo. Tokea tarehe za mwanzoni, busu hili lililindwa dhidi ya uharibifu wowote wa muundo huu wa salamu, wanawake na wanume walitakiwa kukaa kwa kutengena, na busu la amani lilitolewa tu kwa wanawake kwa wanawake na wanaume kwa wanaume.
- Makanisa mengi ya kiporostant yamechukuliana na busu takatifu kwa mfano (katika wale wanachama waliongozeka kama ukarimu safi wenye moto ambao hurejewa kama busu takatifu.
Onyo moja la mwisho (mst. 17-20)
Paulo anafuatana na baadhi miongozo ya kichungaji na maelekezo. Anasema na kuyatia "alama." Hili neno alama humaanisha "kuchukua lengo, kuwa mwangalifu." Ni neno lile lile lililotumika katika Wafilippo 3:17.
Kufungu (mst. 21-27)
Paulo anamalizia na HALELUYA!
No Comments