Utangulizi wa Paulo kwa Warumi
(Warumi 1:1-7)
Salamu za Paulo 1:1-7
Mtume ni mtu ALIYETUMWA KWENDA kama mjumbe au mwakilishi wa mamlaka halisi ya mtumaji; mjumbe au balozi (Mdo. 9:3-9, 15-22, 28). Wito wa kitume wa Paulo haukuwa wa kidunia. Wala hakuwa mgombea kwa wale waliopigiwa kura katika Mdo. 1 bali wito wakitume wa Paulo ni kwenda mbele kama mtume aliyekuja toka kwa Kristo (1:5). Paulo anasisitiza kuwa yeye alikuwa ameitwa kuwa mtume; na wito huu ulikuwa wa kimungu na sio wa kibinadamu.
Paulo alikuwa mhubiri wa injili yeye alikuwa mjumbe aliye tengwa mwenye ujumbe maalumu. Injili ni siri (Marko 4:11; I Tim. 3:9, 16; Kol. 2:2; 4:3; Waef. 1:9) ufunuo wa kimungu (Mdo. 9).
Uwekwaji wakifu kamili umezungumzwa katika maneno haya. Paulo alitengwa kuhubiri ujumbe moja na wa pekee. Paulo hakutangaza kwamba ujumbe huo ungemtukuza yeye wala hakufanya zaidi ya nafasi yake mbele ya macho ya watu. Paulo alitangaza kwamba kusudi lake katika maisha llilikuwa ni Injili ya Mungu, na kwahiyo hili lingepaswa kuwa kusudi letu kama wa hudumu Injili.
Ujumbe wake (mst. 1-5)
Ujumbe wa Paulo ni injili. Injili haikutokana na Paulo injili yote inamhusu Yesu Kristo: Bwana wetu, uzao wa daudi, mwana wa Mungu, aliyefufuka.
Wasomaji wake (mst. 6-7)
Wale waliounganishwa na Yesu wameungwa pamoja naye katika wito wake. Walioitwa ambao Paulo anaandika haimanishi waalikwa, bali humaanisha wale walioalikwa ambao wamekuja tayari.
Haina shaka kwamba waandikiwa wa waraka huu walikuwa ni wakristo Warumi (mst. 7, 15). Andiko linaonyesha kwa kanisa la kirumi lililo athiriwa na wamataifa kama Paulo anavyolielezea kanisa akiliacha kwa ugumu na shaka ambayo anawaaandikia wa mataifa. Katika sura ya kwanza, anazugumza habari ya utume kwa ajili ya utii wa imani kati ya mataifa (1:5). Hurejea kwa waandikiwa kama wamataifa mengine na kutoa kama sababu yake kuwa tayari kuhubiri injili kwao kana kwamba yeye anadaiwa kwa Wagriki na kwa wayunani (1:14), kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia (1:16).
Wakati nafasi na matumaini ya taifa la kiyahudi yako chini ya uangalizi na Paulo anakuja kuwaasa, hii ni kwa waumini wa mataifa ambao anaelezea (1:13; 11:13; 15:15-16).
Familia ya Mungu hujumuisha watakatifu walioitwa kwa neema ya Mungu kutoka duniani kuwa watu wake (1 Kor. 1:2). Watakatifu waliotengwa kwa ajili ya ibada na sifa. Ufunguo mwingine wa kufahamu maana ya neno watakatifu; ni waliotakaswa, watakatifu moja kwa moja wako kinyume cha dhambi. Watakatifu ni wale ambao hurusu utakatifu kuwa uhalisia wa maisha yao. Haki ya kweli ni tukio la mapenzi. Haki ya kweli sikuzote huzalisha tendo la inje na matokeo ya ndani. Kila muundo wa dhambi lazima uwekwe inje ya moyo. Kama mawakili wa maadili lazima akili zetu zisikubaliane na dhambi.
Neema kwenu na amani zitoka kwa Mungu Baba yetu, na bwana wetu Yesu Kristo
Hii ni salamu ya kawaida kwa Paulo katika nyaraka zake. Jina Yesu Kristo au Bwana au Bwana Yesu Kristo limetajwa mara kumi katika Warumi. Yesu ni jina binafsi kama mwokozi (Mat. 1:21). Kristo ni mpakwa mafuta wa Mungu Bwana anadokeza kusema kuwa yeye ni Bwana wa vyote vya mbinguni na duniani (Mdo. 10:36). Yesu kristo ni bwana wetu wa kila hali!
Utayari wa Paulo (kutembelea, kupasha, & kuhubiri) (1:8-15)
Mstari ya 8-15 inaelezea hisia binafisi za Paulo kwa ajili ya watakatifu wa Rumi.
Paulo anatoa shukurani kwa ajili imani ya watakatifu wa Rumi na kuwaombea (mst. 8-9)
Dunia yote ni rejea kwa umiliki wa utawala wa kirumi ambao siku zote hujirelea kama dunia yote. Ilikuwa ni Augustino alitoa amri wakati wa kuzaliwa Kristo ambao dunia yote ingetoa ushuru, ambayo ilikuwa ni rejea ya utawala wa Kirumi.
Imani ya watakatifu wa Rumi katika utawala wote. Hawa wakridto wa kirumi walikuwa ni "wapendwa wa Mungu," "walioitwa kuwa watakatifu," wapokeaji wa neema na amani "kutoka kwa Mungu Baba yetu, na Bwana Yesu Kristo." Ushuhuda wao ulitoka kwamba walikuwa wametengwa kwa ajili ya Mungu na kumwakilishi mfalme wa utukufu. Hazina nzuri ya ushuhuda ni Paulo anasimama juu ya uwanja vita katika maombi ambaye imani yao na ushuhuda wao ungeendelea.
Yeye amekuwa na shauku ya kutembelea watakatifu wa Rumi na kuwatakia karama za roho kwa kusudi lake kuliona kanisa likiwa limethibitika (mst. 10-12)
Roma ilikuwa ya kimkakati, lakini Paulo anaongozwa na Roho na sio takwimu. Inawezekana kwamba Paulo alitambua thamani ya kimkakati ya kujenga kanisa katika mji mkuu wa Dola la Kirumi, lakini Paulo alikuwa aina ya mhubiri ambayo ingewekeza sana katika jiji ambalo hakuna mtu aliyewahi kusikia. Alibarikiwa kusikia kwamba kulikuwa na watakatifu kule Roma na alitamani kuwatembelea ili kufanya sehemu yake kuimarisha kanisa huko. Ni mantiki kwamba uamsho katika mji wa Roma ungeathiri Dola yote, lakini ukweli ni, Mungu angechagua mahali popote kuwa mwanzo wa uamsho ambao ungeugeuza ulimwengu (Mdo. 17:6).
Paulo alikuwa amezuiliwa kwenda Roma (mst. 13-15)
Alikuwa anataka na hata alipanga kwenda, lakini alikuwa amezuiliwa. Paulo siku moja angeenda Roma kama mfungwa kusimama mbele ya viongozi wa Warumi na kutangaza Injili ya Yesu Kristo. Kitabu cha Matendo kinatuambia kwamba Paulo alikaa miaka miwili huko Roma. Inaaminika kwamba alikuwa chini ya kukamatwa kwa nyumba wakati huu wa kuwa Roma. Alikatwa kichwa huko Roma mnamo 67 BK.
Paulo alikuwa na hamu kubwa ya kuhubiri Injili huko Roma. Yeye hutumia neno "mdaiwa" akimaanisha mwenyewe kuonyesha kuwa amejitolea kuwahubiria watu wote (mst. 14). Alikuwa na deni kwa mwenye dhambi kumwambia juu ya Kristo. "Wayunani" hutumiwa kurejelea Mataifa wenye busara ambao wameelimishwa kwa tamaduni na falsafa ya Uigiriki. "Wasio Wayunani" hutumiwa kurejelea wale walio nje ya tamaduni ya Uigiriki, ambayo isingeelimishwa. Paulo yuko tayari kuhubiria kila mtu.
No Comments