Subiri kwa uvumilivu kutwaliwa
Subiri kwa uvumilivu kutwaliwa (mst. 17-25)
Muumini ana vitu vikuu vya kuangalia mbele kwa Mungu. Mungu amefanya mambo makuu na atafanya kwa waumini na bado ametupa ukombozi tulio usubiri kwa uvumilivu katika tumaini au imani! Kitu gani muumini anaweza kukiangalia mbele?
Urithi wa Mungu (mst. 17a)
Muumini atapokea marupurupu na urithi wa mwana kwa sababu atashirikishwa katika uhusiano pamoja na Baba.
Mateso katika utukufu (mst. 17b-18)
Majaribu huhakikisha sifa ya kweli ya Mkristo. Ingawa kuteswa sio kutukuzwa, Paulo ameleta uangalifu wa kutukuzwa kwetu. Mkristo ana tumaini katika mateso, kwa kuteswa, pia tutatawala. Kristo ni mfano wetu wa mateso (I Petr. 2:21; Waebr. 2:10; 5:8-9; I Petr. 4:1; Yak. 5:10).
Muumba husubiri kwa udhihirisho wa mwana wa Mungu (mst. 19-22)
Mungu ana mpango mkubwa na Tumaini lililo liweka mbele kwa uumaji. Ni utumwa kwasababu dhambi iko ulimwenguni, bali kule tutakuwa tumefunguliwa!
No Comments