Kusudi la kweli la sheria
(Warumi 3:20-30)
WARUMI 3: Kuhesabiwa ni kwa njia ya imani sio kwa matendo sheria. Sheria ni: faida kwa wale wanaoijua (mst. 1-2), ni halisi katika asili yake (mst. 3-8), haipindiki katika mamlaka yake (mst. 9-19), inayokusudi la pekee (mst. 20-30), sio kitu cha kuepuka bali zaidi imethibitishwa ndani ya mioyo yetu (mst. 31).
Sheria haijawahi kumhesabia haki mtu yeyote (mst. 20)
Sheria ni shitaka kwa asili dhidi ya wanadamu wote. Kusudi la kweli la sheria sio kumhesabia mtu haki, bali ni kuleta kuijua dhambi. Kipekee, sheria haiwezi kuzalisha wokovu au haki katika macho ya Mungu. Wokovu ni kwa neema kwa njia ya imani katika Yesu Kristo.
Kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakaye hesabiwa haki
Mwenye mwili: ni mwili (ni kama kinyume cha nafsi (au roho)) ni ishara ya kile kitokacho inje, au asili ya mwanadamu pamoja na madhaifu yake (kimwili na kimaadili), hali ya kuwa na mwili.
Kujua dhambi ina umuhimu wa namna gani?
haki ya Mungu imedhihirishwa kwa wanadamu (mst. 21-23)
Kudhihirisha ni kuonyesha au kutangaza (mst. 21)
Mwenye haki aliyetangazwa
Maana ya "kuhesabiwa" haki ni kutangazwa kuwa mwenye haki. Kuhesabiwa ni kuwekwa mahali penye uhusiano sahihi pamoja na Mungu. Paulo anaongea na watu jinsi gani wataweza kuhesabiwa haki au kutangazwa haki; kwa njia Yesu Kristo.
Kuhesabiwa haki: kurudisha (kuonyesha au kujali) mwenye haki au asiye na hatia: —uhuru, kuhesabiwa haki.
Umuhimu mkubwa, kuhesabiwa haki haimaanishi kwamba Mungu hutufanya haki, bali hututangaza kuwa wenye haki. Kuhesabiwa haki ni jambo la kisheria. Mungu huweka ya Kristo kwenye hesabu yetu ya wenye dhambi. —Wiersbe, W. W. (1996). The Bible Exposition Commentary
Bado, Wokkovu haujakamilika katika maelezo haya. Kwa kuwa katika tangazo la Mungu la kuhesabiwa haki, kwa kutupa haki yake ametufanya wenye haki.
War. 5:19—Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki.
Haki hurejea usafi wa maadili
Kirahisi humaanisha kuwa haki ni kuwa kinyume cha ubaya. Dhambi ni ubaya na Mungu ni haki. Ilivyotumika kwa Mungu inarejea kuwa kamili au utakatifu wa asili yake; Mungu muda wote ni mwenye haki. Maneno haki na kuhesabiwa yako karibu sana na yametokana na neno lilelile la kigriki. Mzizi ni dika. Kuhesabiwa haki ni--dikaio, haki ni--dikaiosune.
haki hii hutoka kwa Mungu
Hii sio haki ya kuifanyia kazi au hata matendo ya haki. Kuhesabiwa haki ni haki ya Mungu kuwekwa kwenye hesabu ya mtu; Hiyo ni Mungu kumhesabia mtu haki kwa njia ya haki ya Kristo. Kifungu hiki humwonyesha mtu kuwa chanzo pekee cha haki ni kutoka kwa Mungu.
Njia ya Mungu kumhesabia mtu haki (mst. 24)
Imetolewa kwa neema ya Mungu
Mwenye dhambi hasitahili kupata haki. Mtu anasitahili kwa ajili ya dhambi. Mungu kwa uhuru huwahesabia haki wale ambao wanapokea utoaji ya Kristo kwa imani. Wokovu ni zawadi ya Mungu kwa wale wanao pokea utoaji wa Kristo kwa imani.
Kwa njia ya ukombozi katika Kristo Yesu
Ukombozi humaanisha kununuliwa, kuwekwa huru kwa malipo ya fidia. Yesu alilipa gharama kwa ajili ya wokovu wetu katika damu yake. Mtu anatangazwa kuwa haki kipekee kwenye stahili ya Yesu Kristo.
Matakwa ya sheria yametimizwa (mst. 25)
Mungu bado anadai haki
Kuhesabiwa haki sio tu Mungu kuonyesha huruma juu ya mwenye dhambi na kumwacha huru bila malipizi kulipwa. Neno uheri limetumika katika rejea kwa Kristo kukidhi matakwa ya sheria. Uheri sio sababu utekelezaji wa hukumu iliositahili. Huelezewa kwenye neno la kiebrania kumaanisha kiti ccha rehema ambacho kilikuwa kikiwekwa damu ya malipizi na kunyunyizwa ili kukidhi hukumu ya Mungu. Hii damu ya kunyunyiza ilifunika vibao vya sheria ikiwa nipamoja na sanduku la agano. Huu ni mfano wake yeye ambaye angekuja kumwaga damu ya kiungu kukidhi sheria. Damu ya Yesu ni sababu ya hukumu kutotekelezwa kuhusu mwenye kutubu.
KIPATANISHO
Kipatanisho kihalisi humaanisha kuonyesha uondoaji wa ghadhabu kwa utoaji zawadi. Katika Angano la kale huelezwa kwa tendo la kukausha samaki (MALIPO). Jambo la kipanisho huinuka kwa ukubwa wa jambo kutoka kwenye dhana nzima ya ghadhabu ya Mungu, ambao watetezi wa mtazamo huu huwakilisha jamii na msemo wa kale. Wanahisi watu wa sasa hawawezi kushikilia dhana hii. Lakini watu wa Agano wa la kale hawakuwa na makatazo kama hayo. Kwa wao Mungu hukasirishwa na uovu kila siku (Zab. 7:11). Wao hawakuwa na shaka kwamba dhambi kwa kutoepuka huamsha mwitikio wenye nguvu kutoka kwa Mungu. Yeye kwa ujasiri yuko kinyume uovu katika kila muonekano na mundo wakati yeye huo huo yeey anaweza kuwa mpole wa hasira. -Kamusi mpya ya Biblia
Hebu tuangalie kifungu kwa ajili ya ondoleo la dhambi zile zilizotangulia kufanywa
Katika kipindi cha Agano la kale, damu ya wanyama haikuweza kuondoa dhambi (Waebr. 10:4). Damu ya wanyama ni kivuli cha damu ya Yesu, ilikuwa ni kitu cha muda mfupi hadi pale Yesu alipokuwa amekuja na kujitoa mwenyewe kama dhabihu ya kiwango cha juu kwa ajili ya dhambi. Tafasiri halisi ya fungu hiki ni kwamba Mungu alizipitia juu dhambi ambazo zilitangulia kufanywa. Yeye akijua kwamba Yesu angekuja kulipa gharama yote hapo msalabani. Damu ya wanayama ilikuwa kama hati ya malipo hadi gharama yote iishe kulipwa. Hapakuwa na mtu aliyekuwa ameokolewa kwa wanyama Watu wote wanaokolewa kwa damu ya Yesu Agano la kale na jipya.
Mtu anahesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria (mst. 28)
Imani ni kigezo cha kupokea kutoka kwa Mungu
Imani na haki - nenda sawa kwa sawa ukimwona mtu mwenye haki, umeona mtu mwenye imani. Kumbuka imani mbali na haki sio ya kimaandiko. Haki kwa halisi inafaa haki (Marko 11:22). Haki: ni uwezo wa kufikiri na kutenda kama Mungu. Kuna haki za aina mbili: 1. ya kuwekewa - tendo la neema (Mungu anaweka katika hesabu yetu) 2. ya kugawiwa-neema ya kushirikisha au kutoa. 1:17 - "maana kuna haki ya Mungu iliofunuliwa toka imani hadi imani." Hatua: I Wakr. 1:30 kuna viwango vya imani. Tunabadilishwa toka kuamini hadi kuamini, imani hadi imani, utukufu hadi utukufu. "Metron" - Kigiriki - kipimo cha imani, kiwango, sehemu. Kipimo cha imani imani iokoayo. Ikiwa wewe una imani wewe una imani katika moyo wako.
No Comments