Skip to main content

Utii wa Mkristo

Utii wa Mkristo (sura ya 13)

Pitio la sura ya 13

Warumi sura ya 13 inaelezea kazi yetu katika amri na sheria, vilevile kazi za kiraia. Ndani yake tunaona kwamba upendo ni utimilifu wa sheria na kwamba hatuhitaji utoaji wowote kwa ajili ya mwili (mst.14).

Kwa kuwa sisi tunapokea ahadi ilioko kwenye Zaburi 47:3 (yeye atawashusha watu chini yetu na mataifa chini ya miguu yetu.) sasa tunaenda kujiunza kwenda kuwa watiifu sisi wenyewe kwa Mungu kwenye mamlaka yake. Hebu tuchunguze "utii wa Mkristo" (utii kwa watawala kama walivyo agizwa na Mungu) katika War sura ya kumi na tatu.

Vifungo vya utiifu wetu (mst. 1)

Sura ya 12 husisitiza hitaji letu la kukabithi miili yetu kama dhabihu iliohai, na sura ya 13 inafundisha juu ya umuhimu wa utii kwa wenye mamlaka.

Sehemu ya pili ya mstari wa 2 hutuambia kwamba mamlaka yote hutoka kwa Mungu. Mamlaka yote ni ya Mungu (Zab. 62:10–11; 29:10; Mat. 19:26). Mamlaka ya kidunia lazima yapokee msukumo toka kwa Mungu mtawala (Kol. 1:16–17; Dan. 2:21). Tunainamishwa na Mungu kuwa katika utii wa mamlaka. Amri hii hutoka kwa Mungu.

Jaribu la utii wetu (mst. 2)

Kwa kuwa mamlaka yote ni ya Mungu, wakati tunapojitiisha wenyewe kwa watu, kwa uhallisi tunajitiisha wenyewe kwa Mungu. Kuwa kinyume cha Mungu ni kuwa kinyume chetu wenyewe. Hatumuumizi Mungu kadiri tunavyokuwwa sio watii kwa Mungu tunajiumiza wenyewe.

Sababu ya utii wetu (mst. 3–5)

Tunajitiisha ilikuipisha ghadhabu (mst. 3–4)

Uasi unagharama kubwa. Hukumu ndio ile ambayo Paulo anaiwasilisha kama gharama ya uasi. Hakuna hofu kwa jambo la watawala wanaoagizwa na Mungu kama wenye hofu kwa ajili ya kazi njema bali kwa maovu. Kuepuka ghadhabu ya upanga wao (War. 12:18; Waebr. 12:2).

Tuna jinyenyekeza kwa sababu ya dhamiri zetu (mst. 5)

Mungu anaagiza mamlaka kwa ajili ya kusudi la kulinda wema na kuadilisha uovu. Mamlaka yamebuniwa kwa ajili ya wema wetu na ulinzi. Pasipo uongozi hapatakuwa na utaratibu na machafuko yaweza kutokea.

Tunapaswa kuwa wa watiifu sio kwa sababu ya kuepuka adhabu, bali pia kwa kuhifadhi dhamiri zetu safi. Kwa Wakristo Mungu anatuagiza kuwa katika unyenyekevu.

Tunajinyenyekeza kwa namna gani? (mst. 6–10)

Tunajinyenyekeza kwa kulipa kodi (mst. 6–7)

Mathayo 22:21—Wakamwambia, Ni ya Kaisari. Akawaambia, Basi, mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu.

Kanuni inayohusiana na maandiko matakatiu ni ndefu kiasi kwamba "Kaisari" haihitaji zaidi ya kile ambacho Mungu anataka sisi kubakia katika utiifu. Kwa kadiri iwezekanavyo, tunapaswa kuishi kwa amani. Labda miaka kama 4 au 5 kabula paulo hajaandika barua hii kwa Warumi, kulikuwa na amri iliotolewa na serikali ya Kirumi ambayo ilikuwa inazuia wayahudi (kwa kuongezeka, Wakristo) kubakia katika mji wa Rumi. Na haki kwa ajili ya amri hii iliozuia mnongono ulioenea wa Wayahudi waliokuwa waleta matatizo. Paulo haelezei "haki za kiraia" za wayahudi na wakristo katika sura hii, badala yake anasisitiza majukumu yao wenyewe.

Katika mistari ya 6 na 7 tunaona mifano ya utii kwa mamlaka ya kiraia:

  1. Toa kodi kwa anayesitahili kodi
  2. Toa ushuru kwa anayetoza ushuru
  3. Hofu kwa anaye sitahili hofu
  4. Heshima kwa anayesitahili heshima

Tunatii kwa kuheshimu sheria ya upendo (mst. 8–10)

Upendo hutimiza sheria. Kujihusisha na upendo ni kuitimiza sheria. Katika Yohana 14:15 Yesu anasema, "Mkinipenda, mtazishika amri zangu." Muumini yuko katika "uumbaji mpya," na kuenenda katika madarka ya "juu ya maisha" (Wagal. 6:15–16) sio kwa sheria. Katika kupenda yeye ametimiza sheia ya kiwango cha chini.

Uwakala wa utiifu (mst. 11–12)

Bwana anaahidi kurudi, lakini wakati wakurudi ataikuta imani duniani? (Luk. 18:8)

Sifa ya utii wetu (mst. 13–14)

Kutembea kwetu

Kila mwanafunzi wa kikristo, lazima awe na kusudi, au maono, vinginevyo tutashindwa. Hili ni jambo ambalo Kristo atatupa.

Je, tunafanya kazi ya Mungu au kazi zetu?

Hii sio kazi yetu. Kazi yetu ni kuyafanya mapenzi yake yeye aliye tuita. Ni kuifanya kazi yake (Yoh. 4:34). Ikiwa tumeitwa, tuna kusudi lililo funuliwa katika maisha yetu. Ufunuo huu wa kusudi la Mungu kwa ajili ya maisha yetu hupokelewa kwa maombi.

Kama wahudumu mnahitajiwa kuwaleta wengine kwenye kumjua Kristo; Iliwalitafute neno la Mungu wao wenyewe (mwanamke kisimani aliamini kwa sababu ya kile ambacho neno linasema).

Wasaa wetu

furusa ni haki iliopatikana popote ulipo. Unapokuwa mtiifu na kuwa na hiari kwenye mapenzi ya Mungu, tunakuwa vifaa katika mikono ya Bwana.

Hitimisho la sura ya 13

Amri za sura hii huelekezwa kwetu leo kama zilivyoelekezwa katika siku za Paulo. Mkristo anapaswa kuchukuliana na kila hali kulingana na Mungu alivyo na kile Mungu afanyacho. Matazamio ya mkristo yameelekezwa kwa mtazamo wa Mungu wa dunia na kusudi la Mungu katika dunia.