Skip to main content

Sheria ya Roho ya uzima ni Kristo Yesu

Sheria ya Roho ya uzima ni Kristo Yesu (sura ya 8)

Utangulizi wa Warumi sura ya nane

Dondoo

  • Wale walio kwa Kristo hawako kwenye hukumu (mst. 1-9 )
  • Wale walio kwa Kristo wamepokea Roho ya kutwaliwa (mst. 10-16)
  • Wale alio katika Kristo wanasaburi ya kusubiri kutwaliwa (mst. 17-25)
  • Wale walio katika Kristo waatatukuzwa kupitia huduma ya Roho Mtakatifu (mst. 26-30)
  • Wale walio katika Kristo wanao Mungu akiwa mtetezi wao (mst. 31-39)

Muhtasari

Warumi sura ya nane inazungumzia ushawishi wa "Sheria ya Roho wa Uzima" juu ya Mwamini. Matokeo ya mwisho ya wokovu kupitia Yesu Kristo ni ukombozi wa maisha ambayo zamani yalikuwa yamehukumiwa na Mungu kwa maisha yaliyotukuzwa na Mungu. Kusudi la Mungu kwa Mkristo ni kuwatukuza pamoja na Kristo. Roho Mtakatifu anafanya kazi katika maisha ya mwamini akizalisha matokeo ya Mungu. Wale walio ndani ya Kristo hawalaaniwi tena, lakini wako kwenye njia na mchakato wa utukufu wa Mungu.

Kristo ndani yetu na Sisi ndani ya Kristo

Ina maana gani kuwa ndani yua Kristo?

  • Walio kwa Kristo wanatembea sio kwa mwili, bali wanatembea katika Roho (mst. 1)
  • Walio katika Kristo hawahukumiwi tena na dhambi wanayo uzima (mst. 1)
  • Wale walio katika Kristo hawawezi kutengwa na upendo wa Mungu (mst. 39)
  • Wale walio katika Kristo wako katika mwili mmoja na kila mmoja yuko ndani ya mwingine (12:5; IKor. 16:24)
  • Wale walio katika Kristo wanakua kama watoto wachanga hadi utu uzima (I Kor. 3:1)
  • Wale walio katika Kristo na watakaye kufa (lala) wana tumaini la Ufufuo (I Kor. 15:17-20)
  • Wale walio katika Kristo wanao ushindi katika Mungu (II Kor. 2:14)
  • Wale walio katika Kristo ni viumbe vipya (II Kor. 5:17; Gal. 6:15)
  • Wale walio katika Kristo wamepatanishwa na Mungu (II Kor. 5:19)
  • Wale walio katika Kristo wanao uhuru (Gal. 2:4)
  • Wale walio katika Kristo ni wana wa Mungu (Gal. 3:26)
  • Wale walio katika Kristo wote ni wamoja si Myunani wala Myahudi (Gal. 3:28)
  • Wale walio katika Kristo wamebarikikwa (Efes. 1:3)
  • Wale walio katika Kristo wataketi pamoja katika mahali pa Mbinguni (Efes. 2:6)
  • Wale walio katika Kristo waliumbwa kwa kazi njema (Efes. 2:10)

Kuwepo kwa Kristo ni kushirikishwa katika Mzabibu wa keli. Maisha yake aliyaweka kwetu na kile kilicho chake kimekuwa chetu. Mungu Baba ametuonyesha vile vilivyoko kwa Mwanawe wa pekee ambaye tumekuwa warithi wa Mungu. Kwa Kristo, hatushindani na mwili bali dhambi pekee, na wala hatupati ondoleo la dhambi pekee, bali tumempokea Kristo Mwenyewe. Waumini wako kwa Kristo na Kristo yuko kwa waumini (11:16-18).