Skip to main content

Walioko katika Kristo hawako kwenye hukumu ya adhbu

Walioko katika Kristo hawako kwenye hukumu ya adhbu (mst. 1-9)

Wanatembea katika uhuru pasipo hukumu (mst. 1)

Paulo alipiga kelele juu ya ukombozi katika 7:24 na kutangaza katika 8:1. Ubora wa maisha mbele ya vizazi vya kidini ni baadhi ya vitu vya kutisha, bali mtu mpya katika Kristo ana uzoefu mkubwa wa uhuru. Hakuna hukumu tena ya kifo kama mtu aliyefungwa kwa maiti, Kwa maana hiyo sasa hakuna hukumu kwao kwa wale walio kwa Kristo Yesu. Dhambi huleta kifungo, bali sheria ya Roho ya uzima katika Kristo Yesu ilikuwa kazi kubwa ya uhuru! Nafasi yetu kwa Kristo ikiwemo uhuru kutoka kwenye hukumu.

Hatutembei kwa mwili bali kwa Roho

Matendo mema ya sheria yamekamilishwa kwetu kupitia kumfuata Kristo kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu. Kuna njia mbili kutembelea njia ya uzima: 1) Kwa kuufuata mwili 2) Kwa kumfuata Roho wa Mungu. Mapenzi yangu mara zote yanafanya kinyume cha mapenzi ya Mungu, lakini ukiutanguliza mwili juu ya mapenzi ya Roho wa Mungu utashindwa kabisa. Akili ya kimwili au akili ambayo inaongozwa na ile iliyo ya mwilini ni ufafanuzi mkubwa wa uasi juu ya Mungu (mst. 7). Kutembea katika matendo ya mwilini sio kumtumaini Kristo kama Mwokozi na sio kumfuata Yeye kama Bwana wa wote. Kutembea kimwili mtindo wa maisha anayeuzingatia mtu mwenyewe. Kutembea katika Roho, kwa kuongozwa. Hii unaweza kujikana mwenyewe kwa mahitaji binafsi na kujihusisha katika hatua za kukua (kukomaa). Katika Wagalatia 5:16-26, "tunda la Roho" linalinganishwa na "kazi ya mwili."

Tunatembea kulingana na sheria mpya (mst. 2-3)

Kuna sheria tatu zilizotajwa hapa

  1. Sheria ya dhambi na kifo. Ilikuwa ni kama sheria ya mvutano daima ikikuvuta chini. Inapinga ile ambaye ni ya njema na ya Kimungu. Inatuleta katika kifungo na hukumu. Kufungwa kwenye dhambi hutufanya tuwe watumishi wa shetani. Kuitumikia sheria ya dhambi huleta mauti. (7:22-23)
  2. Sheria ya Mungu (aliyopewa kupitia Musa). Ni haki, nzuri, na takatifu. Inapinga dhambi na kazi za mwili. Inakuletea kushawishika na uamuzi. Sheria ikiwa dhaifu haiwezi kuokoa lakini inaelekeza kwa Kristo.
  3. Sheria ya uzima wa Roho. Sheria hii ni kuliko sheria ya dhambi na kifo. Ni maisha ya Yesu yalitolewa kwa waamini wa imani. Uhuru ni hali ya kuzaliwa kwa mtu upya, uhuru wa kumtumikia Yesu Kristo. Kumtumikia Bwana huleta wingi wa uzima. Kila muumini lazima adhihirishe maisha ya Yesu zaidi na zaidi.

Asili ya "sheria ya Roho wa uzima"

Huleta kuhesabia haki pale katika sheria ya zamani ilipokua inatufunga. Sheria hii inafanya kazi njema kwa muumini, bali sheria ya zamani inaweza kutambua tu uovu. Uzima huu ni somo la shreia ya Mungu, ambapo mwili hautaweza na hauwezi kuwa adui wa Mungu.

Utimilifu wa "sheria ya Roho wa uzima" (mst.4)

Ilitimilizwa kati ya mmoja ambaye alitembea si kwa mwili, bali kwa Roho. Kama Roho wa Mungu akikaa ndani yako ndipo uzima wake utakamilika kwako. Usijaribu kumtumikia Mungu katika hali ya mwilini, bali unaye Roho wa Kristo atakye kuvuvia na kuhakikishia uzima. Huu uzima si wako mwenyewe, bali ni uzima wa Kristo (Gal.2:20). Huu uzima haudaiwi kwenye mwili, bali kwa kumtumikia Mungu na kumtii Yeye (mst. 12). Huu uzima ulitimilika kwa kupoteza matendo ya mwili (mst. 13).

Tembea katika akili mpya (mst. 5-6)

Walio katika Kristo wanafanya vitu vya tofauti vyotye viwili kutenda na kufikiri. Tutembee kwa kufuata Roho wa Mungu. Roho wa Mungu atatuongoza kwenye uzima, bali mwili utatuongoza kwenye kifo na uharibifu.

Ninyi ni wa Roho, kama roho yu ndani yenu (mst. 9)