Skip to main content

Mamlaka yasiyopindika ya sheria

(Warumi 3:9-19)

Kuhesabiwa haki ni kwa imani pasipo matendo ya sheria. Sheria ni: faida kwa wale ambao wanaijua (mst. 20-30), haijafanywa kama kitu cha kuepuka bali inathibitishwa kwa imani yetu. (mst. 31)

Dunia yote iko chini ya hukumu.

Shitaka limetozwa dhidi ya mwenye dhambi (mst. 9)

Mwenye dhambi ni nani? Tumeshathibitisha kuwa wote wayahudi na wamataifa wako chini ya dhambi kwahivyo wote wanahatia ya kuvunja sheria.

Ushahidi hutolewa mbele ya mshitakiwa

Ushahidi wa uumbaji (1:20)

Ushahidi wa dhamira (2:15)

Ushahidi wa amri (3:19)

Shitaka lililo somwa toka Maandiko (mst. 10-18)

Kulingana na sheria za kimahakama shitaka rasimi lazima liwe limeandikwa

Shitaka rasmi ni shitaka lililoandikwa au shitaka la kawaida la mhalifu au mkosaji, hurejelewa kama baraza la wazee wa mahakama chini ya kiapo cha mahakama. —Webster

Hakimu mkuu haachi udhuru kwa ajili binadamu na Paulo ametumia neno lililoandikwa kuonyesha mshitakiwa.

Paulo alitumia maandishi yao matakatifu ya kuwahukumu Wayahudi

Myahudi alitamka kwamba alikuwa na Maandiko; sasa Mungu anatumia Neno lile lile kufungua dhambi zao. Mungu anawafanya kuwajibika kwa Neno Lake.

Ingawa wamataifa hawakuwa na neno lilioandikwa; lakini bado wanakanuni ileile ikiwa pamoja na neno lililoandikwa katika mioyo yao

Ulinzi wa mshitakiwa (mst. 19)

Ulinzi wa mshitakiwa ni nini?

Mshitakiwa hana la kusema; kila kinywa kimefungwa.

Siku ya hukumu itakuwa ni siku ya kunyamaza kimya.

Uamuzi (mst. 20)

HATIA KAMA ILIVYO SHITAKIWA!

Hakuna mwenye mweili atakaye hesabiwa haki kwa matendo sheria

Sheria inarejea zaidi ya sheria ya Musa; vilevile pia kwenye sheria ya maadili na sheria ya dhamiri. Watu wamataifa hawakuimiliki sheria ya Musa, lakini kila mtu anasheria ya maadili ya Mungu ilioandikwa katika moyo wake na kuthibitishwa na dhamiri yake.

Malipo ya kifo yameshatolewa dhidi ya mhukumiwa (War. 6:23)