Skip to main content

Imani, Neema, na kuhesabiwa haki

Imani, Neema, na kuhesabiwa haki (sura ya 4)

Utangulizi

Kazi ya sheria katika kuhesabiwa haki ni ile inayoleta kuijua dhambi. Mtu haihesabiwa haki kwa njia ya matendo sheria. Kwasababu kuhesabiwa haki inachukua nafasi katika muumini "kwa neema kwa njia ya imani." Kwa Neema zawadi ya uzima wa milele imetolewa bure kwa ulimwengu wote ni kwa njia ya imani ambayo zawadi hupokelewa. Mungu amefanya ya kwanza kuondoka kwenye ukombozi na kwa ajili ya ule mpango kuwa wamanufaa kwangu, lazima nichague kupokea zawadi kwa imani. (Neema ya Mungu husaidiana na asili ya mapenzi huru ya Mungu aliyoyatoa kwa mwanadamu.) Angalia pia Waefeso 2:8 na Warumi 4:16. Kuhesabiwa haki kwa njia ya imani imeonyeshwa katika maisha ya Ibrahimu.

Abrahimu alihesabiwa haki kwa njia ya imani na sio kwa matendo (mst. 1-8)

War. 4:3—...Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki.

Kwa nini Paulo anaongelea kuhusu Ibrahimu? Paulo anaelezea swali la Wayahhudi. Wayahudi walihusiana na Ibrahimu kwa undani. Abrahamu alirejewa kama baba yetu katika mistri ya 1, 12, na 17. Abrahamu alikuwa baba yetu kama alivyofungamana katika mwili, baba wa tohara, baba wa imani yetu, baba wa mataifa (hii ilikuwa ni ahadi ya Mungu kwake).

Wayahudi walikuwa wameshikiliwa katika uhusiano wao na Abrahamu ("wana wa Abrahamu kimwili") kama dhamana yao kwa uzima wa milele. Wayahudi waliweka faraja kubwa kwa Abrahimu baba wa taifa lao hii ni swali la kiyahudi, Paulo analielezea:

  • Ni nini kuhusu Ibrahimu Baba yetu?
  • Ni agano gani la tohara lililotolewa kwa Abrahimu, lisilo tufanya sisi kuwa haki?

War sura ya 4 inashughulika na "haki ya Ibrahimu." Ibrahimu ni mfano wa kuhesabiwa kwa neema kupitia ya imani. Paulo anatumia maisha ya Ibrahimu kama YALIVYOONYESHWA KATIKA MAANDIKO MATAKATIFU kuelezea fundisho la haki kwa njia ya imani. Katika sura sura zote mbili ya 3 na ya4 Paulo anautoa ukweli kwamba yeye hahubiri injili ya kushindanisha maandiko ya (Agano la kale), bali za ni injili ambayo mwendelezo wa kusudi la Mungu la milele.

  1. katika sura ya 3, Paulo anathibitisha kwamba imani haipuki sheria bali zaidi ya hapo inaithibitisha.
  2. Katika sura ya 4 ahadi iliotolewa kwa Ibrahimu haikuwa kwa njia ya sheria (tohara) bali kwa njia ya haki ya imani.

Kabla ya Torati kutolewa, Ibrahimu alihesabiwa kama mweye haki (mst. 4)

Mwanzo 15:6—Akamwamini BWANA, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki.

Kabla ya torati kwa Musa na kwa mda mrefu hata kabla hata musa kuzaliwa, Ibrahimu alikuwa amekwisha hesabiwa haki kwa imani kama ilivyo kwa wakristo wa leo. Mungu alimpa Ibrahimu ahadi; yeye alimwamini Mungu ikahesabiwa kwake kuwa haki (War. 4:4).

Mungu humhesabia haki mtu asiye mcha (mst. 5)

Wale wasio zaliwa mara ya pili ni wenye dhambi na wapagani. Mwenye kutubu hutangazwa kuwa mwenye haki na Mungu kupitia damu ya Yesu. Wapagani hawana lolote la kufanya kwa ajili ya kuupata wokovu. Watahesabiwa haki kwa neema tu kwa njia ya imani.

KUMBUKA: Mungu anadai imani na haghairi neema ya Mungu. Mashariti ya kuhesabiwa haki kwa matendo iko katika ushindani pamoja na neema ya Mungu ambao ni wema wake ambao ulikusudiwa tu kwasababu ya wema wa Mungu. Sharti la kuhesabiwa haki ni itikio la imani. Imani kikwelii inahitajika na kuhesabiwa haki kwetu bado ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu kama yeye alivyotupa karama ya imani ambayo kwa hiyo twaweza kuitikia neema yake. Kuhesabiwa haki ni kwa neema na pia ni shariti: kwa neema kwa njia ya imani.

Ushuhuda wa Daudi (mst. 6-8)

Paulo anatoa ushuhuda kutoka kwa Daudi unaosaidia ujumbe wa kuhesabiwa haki kwa imani. Daudi alienziwa na wayahudi kama mfalme wao mkuu. Nukuu hii kutoka Zaburi huthibitisha kwamba watu huhesabiwa haki kwa imani tu na sio kwa matendo (Zab. 32:1-2).

Daudi alikuwa anamshukuru Mungu kwamba dhambi zake zilikuwa zimesamehewa na hakuhesabiwa dhambi tena. Ikiwa dhambi haikuwa ndani yake na kusamehewa hii humaaniisha yeye akihifadhiwa katika uhusiano sahihi na Mungu.

Abrahamu alikuwa amehesabiwa haki kwa neema nasio kwa tohara (mst. 9-17)

Wayahudi walitazamia tohara na sheria kama chanzo cha haki yao. Ibrahimu alihesabiwa haki kabla ya agano la tohara. Alihesabiwa kuwa mwenye haki katika sura 15 na alikuwa na umri miaka 86 katika sura ya 16 wakati Ishimaili alipozaliwa. Mwanzo 17:24 inatoa habari ya kutahiriwa Ibrahimu akiwa umri wa miaka 99. Inaweka wazi kwamba yeyealihesabiwa kabla ya kutahiriwa. Kifungu hiki kinawaambia wayahudi kwamba Ibrahimu alihesabiwa haki kabla ya kupokea agano la tohara.

Tohara haikumhesabia Ibrahimu haki. Tohara ilikuwa imetolewa kama ishara ya ahadi. Ilikuwa imetolewa kama mhuri wa haki ya imani. Ni alama ya kuindoa sehemu ya mwili. Hakuna nguvu ya haki katika tendo la kimwili. Hii kwa uhalisi ni kazi ya Mungu mara nyingi katika njia hiyo hiyo ubatizo ni alama ya kazi kamili.

Sheria inaleta kuitambua dhambi (mst. 15). Inasema mahali ambapo hakuna sheria hakuna uasi inarejea kwenye ukweli kwamba ikiwa hakuna sheria basi hakuna kuivunja sheria. Hii pia lazima inarejea kwenye sheria ya maadili kama ilivyo kwa sheria Musa. Ibrahimu alikuwa amehesabiwa kwa imani kwa njia ya neema (mst. 16). Hakujipatia haki kwa uwezo wake mwenyewe;Itolewa pasipo kusitahili kwasababu ya imani yake.