Skip to main content

Sheia ni taswira sahihi

(Warumi 3:1-2)

Sheia ni taswira sahihi (sura ya 3)

Kuhesabiwi haki ni kwa imani pasipo matendo ya sheria. Sheria ni: faida kwao wanaoijua (mst. 1-2), kwa uhalisi katika asili yake (mst. 3-8), pasipo kupinda katika mamlaka yake (mst. 9-19), kuna kusudi tofauti (mst. 20-30), hakufaywa kwakkuepuka, bali zaidi huthibitishwa kwa imani yetu, (mst. 31).

Utangulizi

Katika sura ya 3, tuna kanuni tano kuhusiana na sheria:

Katika sura ya 1

Paulo anajitambulisha mwenyewe na shauku yake kutembelea kanisa huko Rumi na kisha kutambulisha somo lake la Injili ya Yesu Kristo. Katika hii Injili, haki ya Mungu imefunuliwa kutoka imani hadi imani na ghadhabu ya Mungu imefuliwa dhidi ya wale wanao kataa Injili.

Katika sura ya 2

Paulo anathibisha kwamba ujuzi wa sheria hauwezi kuokoa (sio wasikiaji bali watendaji ndio wanao hesabiwa haki) na kusalia au kujivuna katika kujua sheria ni ujinga. Wote wanahatia chini ya sheria; wale ambao wanasheria watahukumiwa kwa ile sheria na wale wasio kuwa nayo watapotea pasipo sheria.

Paulo anaweka wazi kwamba kuhesabiwa sio kwa wale wanao hifathi herufi ya sheria, bali kwa wale ambao ni wayahudi kwa ndani (2:29). Sheria ya tohara ambao inafaa ni utaratibu wa moyo na roho.

Katika sura ya 3

Paulo anaiweka sheria katika taswira yake ilio sahihi. Myahudi wa kidini anatoa sauti ya mgongano katika ujuzi wake wa sheria ya Musa kana kwamba ilikuwa kitu cha kuwahesabia haki mbele za Mungu. Wao walikuwa wamefunika taswira ya kile ambacho sheria hufanya. Yesu hakuitoa wala Paulo hakuitoa sheria kama kitu kisicho faa, bali anakiweka katika nafasi sahihi katika taswira iliotolewa na ufunuo wa msalaba. Katika uyahudi sheria ni mfalme, bali kulingana na Injili kuna haki na kuhesabiwa haki pasipo matendo ya sheria.

Ushawishi katika ukuu wa pili wa sheria ni kile ambacho kililisha upinzani wa wayahudi kwa Kristo. Roho mtakatifu alijuwa wayahudi walikuwa wanashikiliwa katika ukubwa wao na kjaribu kuhalalisha ukataaji wao kwa Injili. Katika War. 3, tunakuna na ukanushi wa udhuru wa wayahudi kwa kuendelea kuonyesha kwamba wako chini ya hukumu na wanamhitaji Yesu.

  • Faida ya kweli ya kuwa na sheria (mst. 1-2)
  • Uhalisi wa sheria (mst. 3-8)
  • Mamlaka yasiyo pinda sheria (mst. 9-19)
  • Kusudi la kweli la sheria (mst. 20-30)
  • Kuthibitishwa kwa sheria (mst. 31)

Sheeria ni nini?

Neno "sheria" kwa ujumla humaanisha kanuni "maandishi ya maelekezo." Ingawa ilikuwa imetolewa kwa wayahudi na Mungu kwa kupitia Musa, wote wayahudi na wamataifa walikuwa na sheria ya Mungu katika dhamiri zao (Iwe isiwe wanachagua kuipokea ilikuwa chaguo lao).

Kote katika Warumi, Paulo anaelezea udhaifu wa sheria iliotolea na Musa na bado kwa wakati huo huo anathibitisha thamani yake ya ukweli. Sheria iliotolewa kwa Musa kwakweli ni mapenzi ya Mungu, lakini haikuwa jumla ya maelekezo yake. Kosa la wayahudi lilikuwa kwamba walifanya zile kanuni pamoja na sherehe zake na kuambatanisha mapokeo kwenye jumla ya kusudi la Mungu mbele ya ubinadamu.

Ingawa tunaweza kupata neno lilelile "sheria" limetumika katika mistr 52 katika Warumi, Paulo mda wote hajadili kanuni zilezile au maelekezo.

  • War. 2:12-13, 17, 18, 20, 23, 25, 26: Wayahudi walikuwa na sheria ya Musa na wamataifa hawakuwa nayo. Wayahudi walijivuna na kubakia katika sheria ilioletwa kwa njia ya Musa na kwasababu ya kushika matendo ya sheria.
  • War. 2:14-15: Wamataifa walikuwa na sheria katika mioyo yao ama katika dhamiri zao
  • War. 3:27: Sheria ya imani
  • War. 7:2: Sheria ya mme wake
  • War. 7:22: Sheria ya Mungu
  • War. 7:23: Sheria ya dhambi
  • War. 8:2: Sheria ya Roho wa uzima katika Kristo Yesu
  • War. 9:31: Sheria ya haki

Musa alikuwa ametumiwa kama mwaaguzi wa Mungu, lakini yeye hakuwa mjumbe pekee na wa mwisho kwa wajumbe wa Mungu. Hatimaye, yeye alikuwa tu sehemu ya alama ya neno la uzima! Sheria katika dhamiri zetu au sheria iliotolewa kupitia Musa zote ni dhana za sheria ya Mungu. Mungu ametoa kanuni zake za milele kwa Musa na Mungu anatamani mapenzi yake, sheria yake, na maandishi yake kuhifadhiwa ndani ya moyo wa kila mtu na kuelewweka katika maisha yao.

War. 3:28—Basi, twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria.

Mtu anaweza kuhesabiwa haki mbele za macho ya Mungu pasipo matendo ya sheria ya Musa (mwizi msalabani). Mtu hawezi kamwe kuhesabiwa ikiwa anakinzana na mawazo ya Mungu.

War. 7:22—Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani,

Faida ya kweli ya kuwa na sheria (mst. 1-2)

Kuwa na sheria iliopokelewa mara kwanza, je wayahudi wana faida gani? (mst. 1-2)

Faida SIO ILE ambayo wao kwakurithi ni kuu kwa mataifa

Kuhesabiwa haki kwa imani ni fundisho la usawa wa watu wote ambao wayahudi walidharau kutokana na msisitizo wao wa kuwa na ukuu kwa mataifa. Wayahudi walitaka kuringia ukuu wao juu ya mataifa. Wayahudi wengi waliendelea kukataa injili na kushikilia ukuu wao na sehemu ya kujitukuza katika Yehova kirahisi kwa sababu msitari wao kwa Ibrahimu. Wayahudi wengi walitishwa na dhana ya mataifa kuwa sawa na wao kwa njia ya imani kwa njia ya Yesu.

Faida ni kwamba wao walipokea kwanza mambo ya Mungu.

"Ndio myahudi anafaida, lakini sio ile unayofikiri!" Uaguzi kihalisi humaanisha usemi na uliotumika hapa unarejea kama maneno ya usemi wa Mungu uliotangazwa kwa njia ya manabii na kuhifadhiwa katika Maandiko matakatifu. Wayahudi walikuwa wamepokea unabii wa masiha na kwa hiyo walikuwa na faida ya kuongeza ufunuo wa masiha ambawo mataifa hawakuwa nao. Faida waliokuwa nao wayahudi ilikuwa ni kitu ambacho kiliwahukumu kwa wengi ambawo waliendelea kumkataa Yesu kama masiha (Yoh. 1:11).

Faida ya kuijua sheria sio kile ambacho hutuhesabia sisi haki, bali ile kusikia kwetu neno la Mungu linalo funua furusa ya kupokea imani kutoka kwa Mungu. Tunaweza kkujua zaidi na kutamani kumpendeza Mungu.

Maaombi

2 Petro 2:21—Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa.

Swali: Je ni faida kutojua mapenzi ya Mungu?

Jibu: Hapana. Nibaraka kuwa na furusa ya kujua mapenzi ya Mungu. Petro anaelezea ukuu wa kiwango cha hukumu ya watu wanaorudi nyuma wamehukumiwa.