Uhalisia wa Sheria
(Warumi 3:3-8)
Uhalisia wa sheria (3:3-8)
Kuhesabiwa haki ni kwa imani pasipo matendo ya sheria. Sheria ni: faida kwa wale ambao wanaijua (mst. 1-2), ni halisi katika asili yake (mst. 3-8), kutopindika katika, mamlaka yake (mst. 9-19), inakusudi dhahiri (mst. 20-30), haikufanywa kwa ajili ya kuepukwa bali zaidi imethibitishwa katika mioyo yetu (mst. 31).
MFANO: Madireva wawili wa malori walikuwa wanasafiri kwa pamoja kwa kuburuza matrela ya urefu wa 12 na 4 walipofika eneo la alama ya kupita kwenye forodha alama ya 11 na 3. Wakwanza alimuuliza mwenzake, je unafikije? wa pili aliangalia pembeni ilikuona polisi hakuona mtu, ndipo alipendekeza kwamba twende tujaribu.
Kiwango ni Kristo asiyebadillika
Tumeshafanya udhahiri kati ya maagizo maalumu yaliyotolewa kwa njia ya Musa yaakijumuishwa na Kusudi la Mungu. Ni kosa kubwa kuifanya sheria ya Musa kuwa ni maagizo ya mwisho ya mapenzi ya Mungu. Ukamilifu wa mapenzi ya Mungu ni mkubwa sana kuliko sheria iliotolewa kwa njia ya Musa.
Iko katika Yesu, tunaona ukamilifu wa mapenzi ya Mungu. Bwana Yesu Kristo ni kiwango cha tarajio la Mungu (Waef. 4:11-16).
Kwa maana makusudi ya somo letu tumefafanua sheria ya Mungu kama:
Kiwango cha Mungu cha tarajio kwa ajili ya uumbaji wake.
Sheria ya Mungu inatawaliwa na asili yake. Kile kilicho ndani ya sheria ya Mungu kwasababu Mungu ndivyo alivyo. Mungu ni halisi na kwa hiyo sheria yake ni halisi--matarajio yake ya tabia ya mwanadamu ni halisi. (Muda mwingi, kujitawala kwa mwanadamu ni kitu chochote bali kiwe halisi.)
2 Samuel 22:31—Mungu njia yake ni kamilifu; Ahadi ya Bwana imehakikishwa; Yeye ndiye ngao yao Wote wanaomkimbilia. (linganisha na Zab. 101)
Kama baadhi hawaamini, je Mungu atavunja ahadi yake? (mst.3-4) Ameghairi Agano lake na Ibrahimu kwasababu baadhi ya wayahudi ni wabaya?kama baadhi yao hawa amini je itazuia mpango wa Mungu?
Je wasio amini hufuta mpango wa Mungu? Angali II Tim. 2:13.
Wayahudi hungangania urithi wao kama wana wa Ibrahimu kama haki yao (mst. 3)
Kizuizi chao kilikuwa hata baadhi yao hawakuamini; hakuna kitu kinacho weza kubatilisha ahadi zetu halisi tumekwisha pewa kwa kupitia Abrahamu. Walikuwa katika tokeo la kusema hakuna haja zaidi kile tulivyo, sisi ni wa uzao wa Abrahamu na hiyo itatufikisha mbinguni.
Jibu kwa halisi: ni sio! (mst. 4)
Mst. 4—Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo…
II Tim. 2:13—Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.
Hii sio sababu, ya baadhi ya wayahudi ambayo hawakuwa waaminifu na ikahitajika imani katika kumwemini Yesu Kristo. Hii ni kwasababu ya ukamilifu wa mpango wa Mungu ambao muda wote uko katika Kristo.
Uf. 13:8—Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.
Ilielezewa toka maisha ya Daudi
Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu (mst. 4).
Zaburi ya Daudi ilinakiliwa kuonyesha kuwa Mungu ni mwenye haki hata ijapokuwa Daudi alikuwa amehukumiwa kwa ajili ya dhambi yake. Kulingana na Zab. 51:4, Mungu ni mwenye haki anapozungumza na kuwa wazi wakati anapohukumu. Hii imetumika hapa kuonyesha kwamba Mungu anahaki ya kuhukumu wayahudi kwasababu wao walimkataa masiha ambaye alikuja kwa njia ya uzao wa Ibrahimu kulingana na ahadi. Hizi ahadi ambazo wao walizidai zingewahalalishia uhakika ulioleta hukumu kwa wayahudi kwasababu ya kumtaa kwao Yesu Kristo.
Ikiwa dhambi zetu zinaitukuza haki ya Mungu, je yeye atatuhukumuje? (mst. 5-7)
Hebu tufahamu maana ya swali
Sifu - ni kuwakilisha sitahili ya maandishi, kujali, au wema; kuongea kwa kupendelea; kutukuza neno la Kigiriki la Webster. Neno linabeba maana ya kutumia yote (kama tabia yenye kuonekana), au kutambulisha, au kusimama na, au kuja katika uwepo.
Lazima tutegemee kwenye mukitadha kutusaidia kufahamu maana ya swali hili. Hii imetolewa kama maswali mawili katika kifungu na kimerahisishwa kwa ajili ya kujifunza. Swali kwa halisi huuliza:kama kutokuwa haki kwetu kumetukuzwa au kulela usikivu kwenye haki ya Mungu na huruma; je Mungu atakuwa hana haki anapotuhukumu?
Hii bado iko upande wetu kufahamu. Kukumbuka kwamba Mungu anashughulika na vizuizi halisi vya wayahudi. Kizuizi ni sawa na vizuizi vya wengi leo. Tungeuliza kwa njia hii: Ikiwa Mungu ni mwenye haki kwanini anihukumu kwa ajili ya dhambi yangu na kunitupa jehanamu? (Hasahasa tukiwa watoto wa Ibrahimu.)
Mungu amepinga: kwahiyo basi jinsi gani atauhukumu ulimwengu?
Jibu ni: kwa hakika sio. Kama kanuni hii imetumika kisha itakkuwaje Mungu kuipitia hukumu juu y a ulimwengu? Ulimwengu hapa unarelewa kama mataifa. Wayahudi walikuwa bado wanajaribu kujitolea udhuru kutoka kwenye hukumu. Ni kitu maalumu kwa Mungu mwenye haki kuhukumu wasio haki wenye dhambi haijalishi ni Wayahudi ama Wamataifa.
Ukweli ni, Mungu anaweza kuuhukumu ulimwengu kwasababu yeye ni mwenye haki.
Je tutende uovu ili wema uweze kuja? (mst. 8)
Baadhi ya watu huharibu ukweli wa huruma ya Mungu na kujivuna kwamba hali yao ya dhambi huishi na kibali cha Mungu kisicho na mashariti, kinaielezea huruma kuu ya Mungu. Paulo hakuwa anahubiri mafundisho haya potofu, lakini alikuwa ameshitakiwa kwa kufanya hivyo pia.
Hili lilikuwa ni shambulio juu ya mahubiri ya Paulo ya kuhesabiwa haki kwa njia ya imani. Wayahudi walikuwa wanasema: wewe unatuambia Mungu anawahesabia haki watu waovu, kwanini wasiendelee kuwa waovu ili wema uweze kuja kutoka kwenye uovu?
Maelezo ya Paulo kwa hawa aliowahubiria yalikuwa ni: wale ambao hukumu ni haki yao. Kwakuwa shitaka halikuwa kweli Paulo hakwenda ndani zaidi kwenye jibu hili; yeye anathibitisha tu kwamba hukumu ya Mungu juu yao ni sahihi.
No Comments