Mungu atatimiza ahadi yake
Mungu atatimiza ahadi yake (4:18-25)
Ahadi kwa Ibrahimu (mst. 18-22)
Abrahamu alipewa ahadi ya Mungu. Mungu alimwahidi kuwa atakuwa na mwana. Pia Mesiha angekuwa mwana wa Ibrahimu. Yesu alitimiza unabii na aliziwa kulingana na ukoo wa mababu wa Abrahamu.
Ahadi ya kkuhesabiwa haki (mst. 23-24)
Shariti la kuhesabiwa haki (mst. 24)
Mtu hupokea kuhesabiwa haki kutoka kwa Mungu kwa imani—"kama tunaamini..."
Ujasiri wa imani na kitendo cha kimungu cha kuhesabiwa
Abrahamu aliamini ahadi ya Mungu. Dhidi ya tumaini aliamini katika tumaini. Abrahamu aliamini ahadi ya Mungu bila kujali hali. Sara alikuwa na miaka karibia 90 na Ibrahimu alikuwa ni miaka zaidi ya 100. Hapakuwa na njia ya asili ya wao kujipatia mtoto. Abrahimu alikuwa hajakata tamaa kwa ahadi ya Mungu (mst. 20).
Kuhesabiwa haki ni kazi ya kimungu. Mtu hawezi kujihesabia haki mwenyewe zaidi ya kule Ibrahimu kupata mwana. Kuhesabiwa haki ni kazi ya Mungu inayotolewa kwa neema katika kuitikia kwa imani.
IKIWA TUTAMWAMINI
War. 4:24—bali na kwa ajili yetu sisi mtakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu katika wafu;
Hitimisho
Zifuatazo ni hoja zilizo tolewa:
- Kuhessabiwa haki/haki ni kwa imani.
- Kuhessabiwa haki/haki haipatikani kwa matendo.
- Kuhessabiwa haki/haki haihitaji tohara.
- Huwezi kujipatia kuhesabiwa haki/kwa njia ya ufuasi wa sheria (4:13-17).
- Imani ya Abrahimu inatuonyesha mfano ambao lazima tuufuate.
- Paulo alitoa hoja kwamba kuhesabiwa haki/haki kwa imani ndio njia pekee ya kumpendeza Mungu.
No Comments